Wednesday, July 31, 2013

TCRA YAZITAMBUA RASMI BLOGS, NA KUZINDUA KAMPENI MPYA YA KUPINGA MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO YA KIJAMII


 Msanii wa muziki wa asili Tanzania ambaye pia ni msanii wa maigizo na filamu, Mrisho Mpoto akizungumza jambo mbele ya waaandishi wa habari na wamiliki wa blogs mbalimbali katika uzinduzi wa matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii. Mrisho alisimama kuzungumza dakika chache baada ya wimbo alioimba na Banana Zoro kuzinduliwa, unaojulikana kama 'Futa, Delete Kabisa'. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),John Nkomo katika uzinduzi huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkomo, akizungumza mbele ya wamiliki wa blogs mbalimbali Tanzania, waandishi wa habari katika warsha ya kampeni ya kuzindua matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuhamasisha suala zima la maendeleo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), waandishi mbalimbali wa habari pamoja na wamiliki wa mitandao ya kijamii, Blogs, wakisikiliza maneno mazuri kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Tanzania, Profesa John Nkoma, hayupo pichani. Hii ni sehemu maalumu ya kuonyesha kuwa TCRA wanatambua mchango wa mitandao ya kijamii, hususan blogs na wamiliki wao kwa ujumla.
Afisa Uhusiano wa TCRA,Innocent Mungi akiwakaribisha wadau mbalimbali wa mambo ya habari za kwenye mitandao,kuhusiana na uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha matumizi mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano,Warsha hiyo imefanyika leo Makao makuu ya Ofisi hizo,zilizopo barabara ya Sam Nujoma jijini Dar.
 Wadau wa mawasiliano wa mitandao ya kijamii, blogs, wakisikiliza hoja mbalimbali zilizotolewa na viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA katika uzinduzi wao wa matumizi mazuri ya mitandao kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo ya Taifa.

Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu Mwaka wa Masomo 2013/2014 Haya Hapa


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dr Shukuru kawambwa. 
---
Serikali imetangaza majina ya wanafunzi 18,754 waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya ualimu vilivyo chini yake ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 1,659 ikilinganishwa na 17,095 waliochaguliwa mwaka jana.

Kati ya wanafunzi hao, 11,806 wamechaguliwa kusomea ngazi ya cheti (Grade A) na 6,948 watasoma katika ngazi ya stashahada.Wanafunzi 363 wamechaguliwa kusoma elimu maalumu kwa ngazi ya cheti huku 57 wakisoma elimu hiyo kwa ngazi ya stashahada.
---

MAELEKEZO MUHIMU:

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu mwaka wa masomo 2013/2014 wanatakiwa kuripoti katika Vyuo walivyopangiwa tarehe 15/08/2013.

Fomu ya maelekezo (joining instruction) itatumwa kwa mhusika kupitia anuani yake. Aidha, fomu hizi zinapatikana pia kwenyetovuti hii  kwa kubofya katika link ya Chuo husika.
Wanafunzi wanatakiwa kufika Vyuoni wakiwa na mahitaji yafuatayo:
  1. Vyeti halisi vya Baraza la Mitihani la Tanzania kidato cha NNE na SITA kulingana na kozi husika;
  2. Ada ya muhula wa kwanza sh.100,000/= au ya mwaka sh. 200,000/=;
  3. Sare ya Chuo kulingana na maelekezo ya Chuo husika; na
  4. Fedha za tahadhari chuoni na matumizi binafsi.

Mkuu wa Chuo anatakiwa kuhakikisha wanafunzi wanaosajiliwa Chuoni ni wale waliopo kwenye orodha hii tu na SI vinginevyo.

Usajili wa waliochaguliwa kujiunga na Vyuo utafungwa tarehe 25/08/2013 saa 12.00 jioni.

*Bofya namba 1 au 2 hapa chini ili kupakua nakala yenye orodha ya majina


 
  1.  WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI 2013/2014 (1.64 MB)
  2.  WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA 2013/2014 (997.5 kB)

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete Ashiriki Mkutano Wa Siku Mbili Wa “High Level Group” Nchini Botswana


 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea ua mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa  Sir Seretse Khama jijini Gaberone nchini Botswana kutoka kwa binti Jessica Kissasi, anayesoma darasa la pili, Baobab International School  t arehe 29.7.2013
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Bwana Christopher Castle,Mkuu wa Idara ya HIV and Health Education kutoka Makao Makuu ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni  (UNESCO) yaliyoko Paris nchini Ufaransa wakati Mama Salma alipowasiri kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sir Seretse Khama huko Botswana tarehe  29.7.2013.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipewa maelezo mafupi na Dr. Patricia Machawira, Mshauri Mkuu wa HIV and AIDS wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika muda mfipi kabla ya kuanza kwa  mkutano wa  “High Level Group-Action on comprehensive sexuality education and health services for adolescents and young people in Eastern and Southern Africa “ unaofanyika Gaberone nchini Botswana tarehe 30-31.7.2013.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia wajumbe wa mkutano wa  sikuk mbili wa  “High Level Group”  kutoka  Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika unaofanyika katika hoteli ya Lansmore Masa Square jijini Gaberone nchini Botswana.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia wajumbe wa mkutano wa  sikuk mbili wa  “High Level Group”  kutoka  Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika unaofanyika katika hoteli ya Lansmore Masa Square jijini Gaberone nchini Botswana.
Baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania  ( kulia kwenda kushoto) Dr. Kadija Mwamtemi, Mwanahamisi Kitogo, Mshauri wa Rais kuhusu masuala ya huduma za jamii, Ndugu Daud Nassib, Katibu wa WAMA foundation na Balozi wa Tanzania nchini Botswana mwenye makao yake makuu nchini Afrika Kusini Mheshimiwa  Radhia Msuya Mtengeti wakisikiliza kwa makini hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Mama Salma tarehe 30.7.2013.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa High Level Group wakisikiliza hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Mama Salma Kikwete .
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akichangia baadhi ya mambo wakati wa mkutano wa  “High Level Group” kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika unaofanyika nchini Botswana  tarehe 30.7.2013

  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipongezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki Mheshimiwa Jesca Eriyo baada ya kufungua mkutano wa “High Level Group” huko Gaberone nchini Botswana terehe 30.7.2013.Picha na John Lukuwi

Rais Jakaya Kikwete ampokea Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini.
 Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  akikagua gwaride maalum la heshima lililoandaliwa kwaajili yake mara baada ya kuwasili nchini
  Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra na Mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete wakikagua ngoma. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini.
 Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  akisalimiana na baadhi ya raia wa Thailkand wanaoishi nchini alipowasili katika hoteli ya Kilimanjaro Regency Hyatt jijini Dar es salaam jana Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuonesha mandhari ya bandari ya salama Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  alipowasili jijini Dar es salaam jana Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiingia Ikulu nwa mgeni wake  Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  alipowasili jana  Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo rasmi na Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  alipowasili na ujumbe wake jijini Dar es salaam jana Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo rasmi na Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  alipowasili na ujumbe wake jijini Dar es salaam jana Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini.Picha na IKULU

Tuesday, July 30, 2013

AIRTEL TANZANIA YALA FUTARI NA WATEJA WAKE DAR ES SALAAM MWISHONI MWA WIKI‏

Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso 
(wa pili kushoto) akiwakaribisha baadhi  ya wateja wao
 katika hafla ya futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini
 Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano
 wa Airtel, Beatrice Singano Mallya.
Baadhi ya wateja wa kampuni ya simu za mkononi ya 
Airtel Tanzania wakichukua mlo wa futari iliyoandaliwa
 na kampuni hiyo jijini Dar es Salaamu juzi.
Wateja wa Airtel Tanzania wakichukua mlo wa futari 
iliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Dar se Salaam juzi.
Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications, 
Bakari Machumu (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji 
wa Airtel Tanzania, Sunil  Kolaso (kulia kwake) 
wakichukua mlo wa futari iliyoandaliwa na Airtel kwa 
wateja wake jijini Dar es Salaam juzi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Azam, Said Salim Bakhresa
 (wa pili kushoto),  akichukua mlo wa futari pamoja na
 baadhi ya wateja wa Airtel katika hafla iliyoandaliwa
 na kampuni hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam juzi.
Baadhi ya wateja wa kampuni ya simu za mkononi ya 
Airtel Tanzania wakifuturu katika hafla iiliyoandaliwa 
na kampuni hiyo jijini Dar es Salaamu juzi.

VODACOM ELIMU EXPO YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo (katikati) Mkurugenzi 
Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama (kulia) na  Mkuu wa Idara ya 
Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa, wakigonganisha glasi, 
kama ishara ya uzinduzi wa maonyesho hayo, wakati wa mkutano 
na waandishi wa habari uliofanyika Hoteli ya Serena jijini 
Dar es Salaam, jana.
 Mkurugenzi Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama (kulia) akizungumza 
na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo , Katikati ni   
Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo, na Mkuu wa Idara ya Masoko 
na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin
 Twissa, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa 
mkutano huo , Katikati ni   Naibu Waziri wa Elimu, 
Phillip Mulugo, na Mkurugenzi Mkuu 
wa Elimu Expo, Joel Njama.
 Sehemu ya waandishi wa habari, waliohudhuria mkutano huo.PICHA NA SUFIANIMAFOTO.

Rais Jakaya Kikwete Atawazwa Rasmi Kuwa Chief wa Missenyi (Omukama)


 Omukama Kikwete akihutubia wananchi Missenyi
  Rais Jakaya Kikwete baada ya kutawazwa kuwa Omukama (Chifu) wa Missenyi wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani Kagera akiwa na  kiongozi wa wazee wa Missenyi, Mzee Ernest Babeiya.
 Rais Jakaya Kikwete akitawazwa kuwa Omukama (Chifu) wa Missenyi wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani Kagera. Anayemsimika ni kiongozi wa wazee wa Missenyi, Mzee Ernest Babeiya.
 Rais Jakaya Kikwete akitawazwa kuwa Omukama  (Chifu) wa Missenyi wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani Kagera.  Anayemsimika ni kiongozi wa wazee wa Missenyi, Mzee Ernest Babeiya.
Rais Jakaya  Mrisho Kikwete akihutubia maelefu ya wananchi wa mkoa wa Kagera  waliofurika katika uwanja wa michezo wa Kaitaba kumsikiliza siku ya  mwisho ya ziara yake ya siku sita mkoani humo.Picha na IKULU

MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA KUPITIA MDAU AKABIDHI VIFAA KWA AL - MADRASSATUL MUNAUWARATUL ISLAMIYA CHA MSASANI BONDE LA MPUNGA


IMG_1336
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza na uongozi wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya iliyopo Msasani Bonde la Mpunga Ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Spika mbili, Vipaza sauti viwili (Microphones) pamoja na Amplifaya ambavyo vitatumika kuendeshea shughuli mbalimbali za kueneza mafunzo ya dini kwa jamii na watoto wanaosoma chuoni hapo. Vifaa hivyo vimetolewa na mdau mpenda maendeleo kupitia kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
IMG_1345
Pichani juu na chini ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa pamoja na Bw. Abdulmalik Ibrahim (kulia) aliyemwakilishi mdau aliyetoa vifaa hivyo (jina kapuni) wakikabidhi Spika tatu, vipaza sauti viwili na Mixer kwa Katibu wa Madrasa hiyo Bw. Salim Amri (wa pili kushoto) aliyeambatana na Ustaadh Nurdin Nassor Abdallah (katikati). Kushoto ni mmoja wa walimu wa madrassatul Munauwaratul Islamiya kilichopo Msasani Bonde la Mpunga Ustaadh Mohamed Kassim.
IMG_1339
IMG_1344
Mstahiki Meya Jerry Silaa akikagua moja vifaa hivyo alivyokabidhi leo ofisini kwake .
IMG_1360
Ustaadh Nurdin Nassor Abdallah wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya ya Msasani Bonde la Mpunga akitoa shukrani kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa pamoja na mdau alijitolea baada ya kupokea vifaa hivyo ambavyo amesema vitawasaidia katika kazi zao za kueneza neno la Mungu hasa kipindi hichi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwemo kuhubiri Amani nchini.
IMG_1372
Uongozi wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya kilichopo Msasani Bonde la Mpunga wakiomba dua za baraka kwa msaada waliopokea leo ofisini kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa.