Thursday, March 28, 2019

NHC YAKABIDHIWA ENEO LA VINGUNGUTI KWA AJILI YA KUANZA UJENZI WA MACHINJIO YA KISASA

 Hili ndilo jengo la machinjio la sasa ambalo linatumia kuchinjia mifugo takribani 500 kwa siku wakati lilijengwa kwa ajili ya kuchinjia mifugo 25 tu eneo la Vingunguti Dar es Salaam. Eneo hili limekabidhiwa kwa Shirika la Nyumba la Taifa kama Mkandarasi kwa ajili ya kuliendeleza.
 Eneo la nyuma ya machinjio hayo kama linavyoonekana kwa sasa.
 Viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala na wa Machinjio wakilitembelea eneo hilo linalotarajiwa kujengwa machinjio ya kisasa.
 Viongozi wakishuhudia miundombinu ya upitishaji maji taka na masalia ya mifugo katika eneo la sasa la machinjio hayo,
 Msanifu wa Majengo kutoka Kampuni ya Cons Africa Limited, Joseph Mandwa akionyesha mchoro wa jengo jipya la machinjio litakavyokuwa.
 Viongozi hao wakiangalia kwa pamoja wakiangalia kwa pamoja mchoro huo.

Kaimu Mkurugenzi wa Ubunifu, Margareth Ezekiel akimkabidhi Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto mchoro wenye ramani ya machinjio hayo 

Monday, February 25, 2019

MIKOA YATAMBA MATEMBEZI YA MWISHO WA MWEZI, MAKAO MAKUU WACHACHE WAJITOKEZA

Utaratibu wa Matembezi ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kwaajili ya kuimarisha afya, kuunga mkono agizo la Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na kisha kuunga mkono agizo la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa mwisho mwa wiki hii yalifanyika huku  mikoa ya NHC ikiongoza kwa kujitokeza kwa wingi kufanya mazoezi na makao makuu kujitokeza wachache katika matembezi yaliyoanzia jengo la makao makuu ya NHC Kambarage House kuelekea Barabara ya Barack Obama hadi Palm Beach na kuingia Barabara za Ali Hassan Mwinyi, Ohio, Kivukoni Front, Luthuli na baadaye kuelekea kwenye eneo kutakakokuwa na mazoezi ya viungo katika eneo la Sea View Beach (Dengu Beach). Matembezi haya hufanyika kila mwisho wa mwezi na kwa mikoa yote ya NHC ili kuimarisha afya za wafanyakazi na kujenga mshikamano. Matembezi haya yatafanyika tena mwishoni mwa mwezi huu. Pichani ni wafanyakazi wa NHC Tabora.
 NHC Singida  walijitokeza kufanya matembezi hayo, yakiongozwa na Meneja wa Singida, Nistas Mvungi katika matembezi hayo ya mwisho wa Mwezi.

NHC Musoma walijitokeza kufanya matembezi hayo.
 NHC Tanga walijitokeza kufanya matembezi hayo.


 NHC Musoma walijitokeza kufanya matembezi hayo.



 

 NHC Mtwara walijitokeza kufanya matembezi hayo. Matembezi hayo kwa mkoa wa Mtwara yaliongozwa na Meneja wa NHC Mtwara, Angela Magazi.



  NHC Kilimanjaro walijitokeza kufanya matembezi hayo.


 NHC Kilimanjaro walijitokeza kufanya matembezi hayo. Matembezi hayo yaliongozwa na Kaimu Meneja Stanley Msoffe.


 NHC Mbeya  walijitokeza kufanya matembezi hayo, yakiongozwa na Meneja wa Mbeya Saidi Bungara na Mama Sinda naye alikuwapo katika matembezi hayo ya mwisho wa Mwezi.

 NHC Makao makuu  walijitokeza kufanya matembezi yaliyoanzia jengo la makao makuu ya NHC Kambarage House kuelekea Barabara ya Barack Obama hadi Palm Beach na kuingia Barabara za Ali Hassan Mwinyi, Ohio, Kivukoni Front, Luthuli na baadaye kuelekea kwenye eneo kutakakokuwa na mazoezi ya viungo katika eneo la Sea View Beach (Dengu Beach).

 Pichani mmoja wa washiriki Arden Kitomari akiwa anafurahia mazoezi.

 Matembezi hayo yakiendelea eneo la Beach




 NHC Tanga  walijitokeza kufanya matembezi hayo, yakiongozwa na Meneja wa Tanga, Ramadhani Macha katika matembezi hayo ya mwisho wa Mwezi.





  NHC Tabora  walijitokeza kufanya matembezi hayo, yakiongozwa na Meneja wa Tabora, Dickson Ngonde katika matembezi hayo ya mwisho wa Mwezi.



  

 NHC Singida  walijitokeza kufanya matembezi hayo, yakiongozwa na Meneja wa Singida, Nistas Mvungi katika matembezi hayo ya mwisho wa Mwezi.
 NHC Singida  walijitokeza kufanya matembezi hayo, yakiongozwa na Meneja wa Singida, Nistas Mvungi katika matembezi hayo ya mwisho wa Mwezi.

 NHC Singida  walijitokeza kufanya matembezi hayo, yakiongozwa na Meneja wa Singida, Nistas Mvungi katika matembezi hayo ya mwisho wa Mwezi.

Thursday, February 21, 2019

HALMASHAURI YA CHATO/NHC WAZINDUA RASMI MAUZO YA VIWANJA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani akisisitiza jambo katika mkutano huo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara, William Genya akijadiliana jambo na Meneja wa Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) mkoa wa Geita, Glagys Jeffta wanaoshuhudia ni maafisa uendelezaji biashara, Clara Lumbanga, Olivia Musanga Zoka na Phoibe Keu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Eliud Mwaiteleke akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani leo jioni.
Eneo lililopimwa la Rubambangwe linavyoonekana kwa picha ya Drone,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Eliud Mwaiteleke, Mkuu wa Wilaya ya Chato Mtemi Simioni na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani wakijadiliana jambo jioni ya leo baada ya uzinduzi wa mauzo ya viwanja Chato.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Eliud Mwaiteleke akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Geita Josephat Maganga.
 Mazungumzo yakiendelea baada ya uzinduzi wa mauzo ya viwanja.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Eliud Mwaiteleke akijadiliana jambo na  na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa NHC, Itandula Gambalagi.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani akizungumza kutoa neno la shukurani katika uzinduzi huo kulia kwake ni Mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Chato Injinia Msafiri Mtemi Simioni na kushoto kwake ni Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani.
Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani kwa mchango wake katika upimaji wa viwanja hivyo vilivyozinduliwa mauzo.


 Hadhira ikifuatilia hafla hiyo ya uzinduzi.
 Hadhira ikifuatilia hafla hiyo ya uzinduzi.
Mkuu wa Wilaya ya Chato Injinia Msafiri Mtemi Simioni  akizunguma katika uzinduzi huo kushoto kwake ni  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani na Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya hiyo, Philip Shoni.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani akijadiliana jambo na Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani.

Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani akizungumza katika hafla hiyo na kulia kwake ni  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani.


Mkuu wa Wilaya ya Chato Injinia Msafiri Mtemi Simioni akijadiliana jambo na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani na Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani.
 Wakifuatilia hafla hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Chato Injinia Msafiri Mtemi Simioni akijadiliana jambo na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani na Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani.
Wakiagana mara baada ya kuhitimisha hafla ya uzinduzi wa mauzo ya viwanja.


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UUZAJI WA VIWANJA KATIKA ENEO LA RUBAMBANGWE HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO

Halmashauri ya Wilaya ya Chato ikishirikiana na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) inautangazia umma juu ya uuzaji wa viwanja 1,035 vilivyopimwa na kuwekewa barabara katika eneo la Mlimani na Rubambangwe kata ya Muungano. Mauzo ya viwanja yanaanza wiki ijayo.

Wananchi wote mnakaribishwa kununua viwanja vyenye matumizi mbalimbali kama vile makazi, makazi na biashara, viwanja vya biashara, maeneo ya kumpumzikia, viwanja vya michezo na huduma mbalimbali za kijamii kama zahanati, Shule, Vituo vya Mafuta kwa bei ya kuanzia Tsh 1,300 kwa mita ya mraba.

Viwanja vipo mita chache kutoka katikati ya mji wa Chato. Vipo mkabala na barabara kuu iendayo Bukoba. Pembezoni mwa Ziwa Victoria.

Viwanja vilivyopimwa na kupangwa kwa ajili ya makazi vina ukubwa kama ifuatavyo:
1. Ujazo wa juu (High density)
2. Ujazo wa kati (Medium density)
 3. Ujazo wa chini (Low density) 

VIWANGO VYA GHARAMA YA VIWANJA KWA MATUMIZI MBALIMBALI

1. Makazi –Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 1,300/=
2. Makazi na biashara- Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 1,700/=
3. Biashara (Hotel, Vituo vya mafuta, maduka makubwa)- Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 2,200/=
4. Huduma za jamii (Zahanati, shule ya awali, sekondari) Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 2,200/=
5. Ibada/kuabudu- Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 2,200/=

UTARATIBU WA KUNUNUA KIWANJA

Chukua fomu ya maombi kutoka o­fisi za Halmashauri ya Wilaya ya Chato au Ofi­si ya NHC iliyo karibu nawe.
Lipia angalau asilimia 30 ya thamani ya kiwanja unachonunua na kiasi kinachobaki kilipwe ndani ya siku 90.
Malipo yote yafanyike kwenye akaunti ya benki ifuatayo: Jina la Akaunti : MRADI WA VIWANJA CHATO Nambari ya akaunti : 327 100 116 07 Benki: NMB Tawi la Chato
Rejesha fomu ya maombi uliyojaza kwa usahihi ukiambatanisha pamoja na vielelezo vinavyohitajika ikiwemo nakala ya malipo (deposit slip) kutoka benki.
Utapatiwa barua ya uthibitisho (Offer Letter) mara tu ombi lako litakapokubaliwa, pamoja na masharti ya kukamilisha malipo ya kiwanja unachochagua.
Kwa maelezo zaidi tembelea ofisi za Idara ya ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Chato.

Au KAMBARAGE House, 1 Mtaa wa Ufukoni, Dar es Salaam, Tanzania. Kwa Mawasiliano piga namba  +255 282 228 007/ +255 754 444 333.

PHILIP SHONI
KWA NIABA YA MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO
21/02/2019