Sunday, December 13, 2015

MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KICHWA KIKUBWA NA MGONGO WAZI DUNIANI 2015 YAFANYIKA MOI MUHIMBILI


 Meneja Ustawi wa Jamii na Mahusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Jumaa Almasi akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo  Dk, Othman Kiloloma wakati wa  Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo wazi Duniani 2015.  Maadhimisho hayo yamefanyika Moi katika hospitali ya Muhimbili  jijini Dar es salaam na kaulimbiu ya mwaka hu inasema “PAMOJA TUZUIE  ULEMAVU WA KUZALIWA” (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) WA UJIJIRAHAA BLOG
Mwenyekiti na Mjumbe wa Kamati ya kusaidia watoto wenye ulemavu wa vichwa vikubwa na mgongo wazi wakishirikiana na   Wafanya Biashara wa Soko la Kariakoo Mtaa wa Raha Sweya  na Mhonda Jijini Dar es Salaam,  Ludovick Mmasi  akizungumza kwa niaba ya wenzake katika Maadhimisho hayo baada ya kuguswa na watoto wenye ugonjwa huo.
 Mtoto Selemani Joseph (14) kushoto ambae ni mwanafunzi wa Darasa la Tatu katika Shule ya Mother Telesia iliyopo  Kisiwani, Kigamboni Dar es Salaam  akipozi na mwenzake katika ofisi za  Chama hicho.
 Wakifanya matembezi ya kuadhimisha maadhimisho hayo yaliyofanyika jijini dar es salaam.
Post a Comment