Thursday, January 31, 2008

Cardilac la BushNgoma hii ndo atatinga nayo huyu George Kichaka Februari 16 mwaka huu, gari hii ni miongoni mwa magari ya kifahari sana duniani tunatarajia litakanyaka lami iliyopigwa deki na lazima wakuu wetu wannuswe sana na mbwa.

Balozi wa Marekani atoa somo kwa viongoziNa Andrew Msechu

BALOZI wa Marekani nchini Mark Green amewataka viongozi na wanasiasa nchi kukubali mabadiliko na kuwa tayari kukosolewa, kwa kuwa ni jukumiu lao kutoa na kupokea kutoka kwa wananchi.

Green, akizungumza katika hafla maalum ya kukabidhi tuzo ya ‘Drum Major for Justice’ kwa Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa Vyombo vya habari nchini Reginald Mengi iliyofanyika ubalozi wa Marekani jana alisema ni lazima viongozi wawajibike kwa wananchi.

Alisema katika kuwawajibisha watendaji, viongozi wa serikali na wanasiasa, vyombo vya habari vimekuwa vikikutana na hila kadhaa za watu wasiopenda kuwajibika kwa wananchi, akitoa mfano wa matukio ya hivi karibuni baada ya Mhariri wa gazeti la Mwana Halisi kumwagiwa kemikali usoni na mshauri wa taaluma wa gazeti hilo Ndimara Tegambwage kukatwa kwa panga kichwani.

“Katika hili ni wazi kiuwa linapoibuka suala lolote linaloleta mjadala kwa jamii ni lazima milango iachwe wazi, kuwepo na uhuru kwa kila mtu kupata fursa ya kushiriki. Nafasi hiyo inayowapa wananchi fursa ya kushiriki na kutoa mawazo yao haiwezi kufika popote ila kwa kutumia vyombo vya habari,” alisema.

Aliongeza kuwa pamoja na umuimu wa vyombo vya habari katika kuonyesha njia na kupambana na rushwa na ufisadi vimekuwa vikikabiliana na vitisho vinavyoingilia uhuru wa watu kujieleza na uwazi katika serikali.

Balozi Green alisema nchi yake iko tayari kuendeleza juhudi za kuhakikihsa vyombo vya habari vinawajibika kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi na kuendelea kuwa nyenzo ya wananchi kufikisha kilio chao na kuwawajibisha viongozi wa serikali na taasisi za umma.

Alisisitiza kuwa ipo haja kwa wanahabari kuendelkea kupigania mabadiliko bila kuchoka, kama ilivyokuwa kwa Marin Luther King Junior ambaye pamoja na kukutana na vitisho aliendelea kupigania mabadiliko nchini Marekani akitaka kuwepo kwa usawa na haki, nia ambayo ilisukuma mabadiliko hayo hata baada ya kuuawa kwake mwaka 1968.

Akielezea tuzo hiyo, Greena alisema Mengi amekuwa nguzo muhimu katika kiuwezesha uandishi wa habari za uchunguzi na kuwasilisha kilio cha wananchi ambao hawana sehemu nyingine ya kusemea mambo yanayowakera.

“Kupitia vyombo vyake vya habari na kupitia nagasi yake kama Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari Mengi amekuwa akitoa nafasi kwa wananchi wasiotendewa haki na kuwasaidia kutoa mawazo na malalamiko yao kwa vyombo husika,” alisema.

Tuesday, January 29, 2008

Reginald alipokwenda kuchukua jiko


Kamanda wetu aliyekuwapo Kenya hivi karibuni, danny mwakiteleko akiwajibika huku mzee wa sumo akingoja zamu yake kwa nyuma. Sijui humo ndani ya vyupa kuna karubisi au ni bia.

Ukweni hakuna cha bosi wala nini. wote kubeba mzigo kichwaniMzee wa Kisima cha Fikra, Reginald Simon akitambulishwa kwa wakweze hakika alionyesha heshima ya ajabu.Kazi ya ushenga ni kazi kubwa hebu cheki jamaa hapa mtu mzima kapiga magoti akiomba idhini ya wazee.

Polisi Kenya waua MbungeMambo sasa Kenya ni mabaya na ripoti za asubuhi hii zinaeleza kuwa mbunge wa chama cha upinzani cha Orange Democratic Movement (ODM) wa Embakassy bwana Mugabe Were ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi.

Mugabe Were, mwanachama wa ODM anadaiwa kushambuliwa nje ya nyumba yake, Polisi wanasema.

Msemaji wa ODM ametaka kuwepo kwa hali ya utulivu hasa katika kipindi hiki kigumu baada ya mbunge huyo kupoteza maisha.

Wakati huo huo ande zinazovutana katika mgogoro wa kisiasa ulioibuka baada ya kutangazwa matokeo nchini Kenya baada ya Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo (ECK) kumtangaza Mwai Kibaki kuwa mshindi, ushindi ambao unapingwa hadi leo na Rail Odinga wa ODM anaedai kuwa yeye ndiyo mshindi. bonyeza hapa
http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/7214558.stm

Kenya hakukaliki tena

Askari wa kuzuia ghasia wakiwazuia Wakikuyu baada ya kuzuka mapambano baina ya Wajaluo na Wakikuyu mjini Naivasha.

Mmoja wa wakazi wa Naivasha kutoka kabila la Wajaluo akimtoa motto kutoka katika gari la polisi katika eneo la Naivasha Club, mjini Naivasha.

Wakazi wa mji wa Naivasha, Kenya kutoka kabila la Kikuyu wakichoma mali za wenzao wa kabila la Wajaluo baada ya kuzuka katika mji wa Naivasha uliopo kilomita 60 nje ya jiji la Nairobi jana. Mapambano kadhaa yaliripotiwa kuibuka Magharibi mwa Kenya na makundi ya watu wenye silaha za kijadi kama mapanga na marungu walifanya vurugu katika mkoa wa Rift Valley baada ya wenzao kadhaa kupoteza maisha katika maambano ya kikabila na hivyo kurudisha nyuma juhudi za upatanishi zinazoongozwa na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa mataifa Kofi Annan. REUTERS.Wakikuyu wakinyanyua silaha zao za kijadi juu nje ya klabu ya Naivasha mjini Naivasha.


Saturday, January 26, 2008

Msiba huko Houston, Texas


Wananchi,
On behalf of the family and Tanzanians living in Houston, I sadly announce the death of our brother Felix Chambi (aka Felix Makene) pictured above.

Felix passed away on Thursday morning (24/1/08) after having a stroke on Monday night (21/1/08). Felix leaves behind his wife Maryam and young son Baraka. Condolences can be offered to Felix’s family at their home on8618 Rose Garden, Houston, TX, 77083.

You can also call: Maryam (wife) on 832 865 3366 or 314 369 2338
Alfred (brother) on 314 584 9708
Mchuma (sister) on 314 489 3248
The community of Tanzanians living in Houston is making plans to transport Felix from Houston to Tanzania next week.

CONTRIBUTIONS:
As we all know, the costs of transporting Felix’s body from Houston to Tanzania will be high.We have estimated the total cost of this process to be $22,400. While any amount you donate will be greatly appreciated, we are recommending that Tanzanians living in Houston contribute around $100 each.
The Tanzanian Community in Houston will conduct a fund raiser on Saturday (1/26/08).
The fundraiser will begin at 4pm and will be held at:Safari Party Hall (Kwa Inno) 8951 Bissonnett, Houston TX 77036. Like always, men should bring drinks and women food to the fundraiser. Ladies can get in touch with Nuru Mazola and gentlemen with Alex Tibaigana for further information on our needs.

If all goes well, we plan to pay our last respects to Felix on Sunday (1/27/08).
You will receive more information on this as it becomesavailable.
If you have any questions please feel free to contact thepeople below.

BANK: Washington Mutual Bank

NAME: Jadi malumbo

ACCT #: 4213965100

ROUTING#: 111993776
BANK ADDRESS

10850 Bellaire BlvdHouston,

TX, 77072281.498.2233

Miraji Malewa 713 373 6525
Nuru Mazola 832 630 8090
Anita Massawe 832 721 3832
Rosemary Mlekwa 832 867 2140
Muddy Chamshama 713 203 4629
Jadi Malumbo 713 419 6803
Karim Faraji 713 702 9050

Bush kuja bongo


THE WHITE HOUSE Office of the Press SecretaryJanuary 25, 2008,
STATEMENT BY THE PRESS SECRETARY.President and Mrs. Bush will travel to Africa from February 15-21, 2008. They will visit Benin, Tanzania, Rwanda, Ghana, and Liberia.
This trip will be an opportunity for the President to review firsthand the significant progress since his last visit in 2003 in efforts to increase economic development and fight HIV/AIDS, malaria, and other treatable diseases, as a result of the United States robust programs in these areas.
The President will meet with President Yayi, President Kikwete, President Kagame, President Kufuor, and President Johnson-Sirleaf to discuss how the United States can continue to partner with African countries to support continued democratic reform, respect for human rights, free trade, open investment regimes, and economic opportunity across the continent.

Annan ana kazi kubwa sana Kenya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan anayo kazi ngumu sana kuweza kurudisha hali kama ilivyo Kenya sababu wanasasa wanalia machozi ya mambo wanakula Wakenya huku machozi yanawatoka hebu cheki hapa chini Hili jamaa siyo kwamba linalenga wanyama linakung'uta risasi live kwa watu.
Watoto wakiwa wamegeuka machokoraa kwa kulala mitaani , hapa wamejifunika blanketi.
Askari Polisi sijui kama ni kweli lakini nadhani ni wanajeshi wakiwa mitaani nakuru kupambana na raia hii ni noma.
Njemba hiii imeumizwa inawasilishwa hositalini leo asubuhi
Huyu naye makubwa yalimkumba, amekatwa mapanga kapigwa hadi anatisha.
Huyu kadungwa mshale. Picha zote za Reuters

Friday, January 25, 2008

cheki Gado mambo yake


eti hapa hawa wakulu wanakutana mbele ya msuluhishi wa kimataifa.

mabundi


Wanafunzi wa shule ya Secondari ya Bugamba iliyopo Kigoma vijijini wakila kitabu katika ghetto lao walilopanga kutokana na shule yao kutokuwa na mabweni na wao wanaishi mbali na shule. Shule hiyo ina mwalimu 1 tu wa kuaajiliwa na 6 walio katika majaribio . Picha na Edwin Mjwahuzi.

Vongozi wa taifa la keshoTunawatayarisha kuwa viongozi wetu wa baadaye, wanafunzi wa shule ya msingi Mwamgongo, Kigoma vijijini wakitoka shule

kweli safari ni ngumu


Mmoja kati ya Madiwani wa Mkoa wa Kigoma akishuka katika usafiri kwenda kufanya ukaguzi katika mashule ya msingi ya vijijini picha na Edwin Mjwahuzi.

kweli safari ni ngumu


Mmoja kati ya Madiwani wa Mkoa wa Kigoma akishuka katika usafiri kwenda kufanya ukaguzi katika mashule ya msingi ya vijijini picha na Edwin Mjwahuzi.

safari na muzikiDaraja la Mpakani mwa Kagera na Kigoma, picha ya Edwin Mjwahuzi.

Kikwete akutana na Nkurunziza

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi katika uwanja wa ndege Mwanza jana mchana. Baadaye viongozi hao walifanya mazungumzo Ikulu ndogo Mwanza

Thursday, January 24, 2008

Mwai Kibaki , Raila Uso kwa uso


Jamaaa hatimaye wamekutana leo mchana na tabasamu la bandia. hebu waangalie vizuri hawatazaani wala nini. Sijui kama kitaendelea kitu. Hebu Bonyeza hapaupate habari zaidi. Navyo vyombo vya Kenya vilikuwa kimbelembele vikasema hivi hapaupate habari zaidi.

Wednesday, January 23, 2008

Tabora Boys wa enzi hizo mpoooooo

Hapa washikaji unaweza kuwaona kutoka kulia Danny Lyimo, Luwaga Kizoka, James Kapaya, Daudi Masoli na Mzee Gombo mvua ilikuwa imenyesha kinoma.

Yahya Charahani, Danny Lyimo na Luwaga Kizoka


Jopo zima la wanafunzi wa kidato cha sita miaka hiyo hapo naweza kumuona kamanda Albert Ballati aliyepo karibu na mwalimu mwenye koti namkumbuka akiitwa mwalimu Nyanda wa Baioloji. Na huyu mbele kabisa hapa anaitwa afande Warioba alikuwa mnoko huyo sijui yuko wapi sasa?

Hapa ni langoni mwa Tabora boys high school, ukiwa unaingia hapa lazima uingien kikakamavu.

Tuesday, January 22, 2008

Tume ya Rais ya kuchunguza ufisadi yaanza kazi

Na Tausi Mbowe

TIMU iliyoteuliwa kufuatilia taarifa ya ukaguzi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuhusu upotevu wa fedha za akaunti ya Malipo ya Kigeni (EPA) imeanza kazi yake rasmi na tayari timu hiyo imeshaanza kukusanya maoni kutoka kwa wananchi.
Time hiyo iliyoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kufutia kampuni ya Ernest & Young kubaini kuwa kulikuwa na upotevu wa zaidi ya Sh133 bilioni katika mazingira ya kutatanisha ndani ya benki hiyo na hatimaye Rais Kikwete kutengua wadhifa wa aliyekuwa Gavana Mkuu, Daud Balali.
Timu hiyo yenye wajumbe kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo za polisi ilipewa muda wa miezi sita kumaliza ukaguzi huo.
Taarifa ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ni Mwenyekiti wa Timu hiyo, Johnson Mwanyika ilisema tayari timu hiyo imeshaanza kazi yake na wamekuwa wakipata ushirikiano mkubwa wa wananchi.
Mwanyika alisema wananchi wote ambao mpaka sasa wamejitokeza wamejitokeza kwa ridhaa yao na kutoa taarifa muhimu zianzoendelea kusaidia kazi yao.
Timu hiyo imesema kuwa itakuwa makini kwa nia ya kuhakisha kuwa ukweli unajulikana na kuweka wazi hadharani ili kulinda heshima ya Taifa kwa kila chembe ya habari itakayopatikana itafuatiliwa kwa makini.
Kwa mujibu wa Mwanyika nia ya timu ni kufanya kazi yake kwa uhakika na kuwaomba wananchi kuwa na subira na kutoa kila ushirikiao utakaoiwezesha timu hiyo kukamilisha majukumu yake.
Alisema timu hiyo itaweza kufanikisha majukumu yake kama wananchi wote popote walipo wataendelea kuisaidia kwa kutoa taarifa zozote mbazo wataona ni muhimu na zinahusiana na kazi hii.
Alisema kwa sasa Timu hiyo imeweka utaratibu wa kupokea tarifa hizo kupitia Jeshi la Polisi na Taasisi ya upambana na kuzuia rushwa na kutoa namba za simu za mikononi kwa wajumbe wa timu hiyo.
Wajumbe wengine katika timu hiyo ni pamoja na Mkuuwa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali, Saidi Mwema, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini, Robert Manumba, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Lilian Mashaka. Wakati timu hiyo ikitangaza kuanza kazi yake rasmi tayari serikali kupitia Waziri wa Fedha, Zakhia Meghji imesema ufisadi wa mabilioni ya shilingi uliobainika katika Akaunti hiyo ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), umepoteza imani ya wananchi kama chombo thabiti na makini katika utekelezaji wa majukumu yake.
Tayari serikali imeshatangaza bodi mpya ya benki hiyo ambayo inaongozwa na Gavana mpya wa BoT, Profesa Benno Ndulu, Mbali na Profesa Ndulu ambaye ni mwenyekiti, wajumbe wengine wa bodi hiyo ni pamoja na Manaibu Gavana, Dk Enos Bukuku, Juma Reli na Lila Mkila.
Kutokana na hali hiyo, Waziri Meghji aliitaka bodi kuhakikisha inachukua hatua madhubuti kurejesha imani miongoni mwa wananchi kutokana na taarifa za kuhusika kwa BoT katika malipo haramu au ambayo uhalali wake unatia shaka, ikiwa ni moja ya mikakati ya bodi hiyo ya kukabiliana na changamoto kubwa zinazoikabili.
Pamoja na mambo mengine bodi hiyo imepewa jukumu la kuchukua hatua zinazostahili dhidi ya maofisa watakaodhihirika kuhusika na upotevu wa fedha za umma chini ya EPA kama ilivyoelekezwa na Rais Jakaya Kikwete na kuweka taratibu madhubuti ili kuepuka upotevu kama huo kutokea tena katika siku zijazo.
Vilevile, bodi hiyo imepewa jukumu la kuimarisha mfumo wa usimamizi wa mabenki na taasisi za fedha, kuhakikisha usalama na umadhubuti katika mfumo mzima wa sekta ya fedha, kuimarisha masoko ya fedha na mkakati wa kuweka mazingira bora ya kisheria ili kuwezesha upatikanaji zaidi wa mikopo ya muda wa kati na mrefu kwa ajili ya sekta ya uzalishaji.

Museveni, Graca arrive for talksStory by ODHIAMBO ORLALE

Uganda’s President Yoweri Museveni and Mozambique’s Graca Machel have arrived in Nairobi as part of international mediation efforts to resolve political disputes over the Kenyan presidential election.


President Kibaki receives Ugandan President Museveni at JKIA earlier today.
Former UN chief Kofi Annan is due in Nairobi later this evening to lead the talks. The other mediator is retired Tanzanian president Benjamin Mkapa who has been in Nairobi.

President Museveni, who doubles as the chairman of the East African Community and of the Commonwealth, was received at the Jomo Kenyatta International Airport by President Kibaki.

The mediation talks have been embraced by the main protagonists - President Kibaki and the Orange Democratic Movement leader Raila Odinga.

Several international and local election observers have declared that the tallying of the December 27 presidential poll results were flawed. Mr Odinga believes that the flaws included manipulation of results to favour President Kibaki.

President Kibaki has already named 10 Cabinet ministers led by Vice-President Kalonzo Musyoka as his negotiation team, but ODM is yet to name its side.

The Ugandan leader’s trip coincided with the release of a paid up half page advertisement in local dailies by his Foreign Affairs ministry on the current situation in Kenya, where they denied reports that he had sent troops to assist President Kibaki deal with the opposition demonstrators.

In the statement, the ministry said: "It is in the interest of Uganda that a peaceful solution is found to the situation in Kenya. Uganda cannot therefore engage in any activity that would go against the spirit, as has been stated in some dailies in Kenya."

The statement further said President Museveni had been in close telephone contacts with President Kibaki and the ODM leader since the outbreak of violence on December 30 when the disputed results were announced.

The Ugandan leader was the first to arrive for the talks, at 1.30pm and was followed at 3pm by Ms Machel while Mr Annan is expected at 8pm.

Meghji: Wanannchi hawana imani na BoT

* Asema ni kutokana na ufisadi uliobainika
* Asema itachukua muda mrefu kuisafisha
* Aagiza Bodi mpya kurejesha hadhi yake
* Asifu mafanikio kiduchu yaliyopatikanaNa Muhibu Said wa Mwananchi

SERIKALI imesema ufisadi wa mabilioni ya shilingi uliobainika katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), umepoteza imani ya wananchi kama chombo thabiti na makini katika utekelezaji wa majukumu yake.

Kauli hiyo ambayo ni ya kwanza kutolewa na serikali tangu ufisadi huo ubainishwe na kampuni ya nje ya ukaguzi ya Ernst & Young, ilitolewa na Waziri wa Fedha, Zakhia Meghji alipokuwa akizindua bodi mpya ya BoT, jijini Dar es Salaam jana.

Alisema bodi hiyo ambayo inaongozwa na Gavana mpya wa BoT, Profesa Benno Ndulu, inaanza kazi katika mazingira ambayo wananchi wamepoteza imani juu ya BoT kama chombo thabiti na makini katika utekelezaji wa majukumu yake kutokana na matukio ya hivi karibuni yanayohusiana na upotevu wa fedha nyingi za umma chini ya EPA.

"Matukio haya yametia doa kubwa katika sifa za taasisi hii muhimu na itachukua muda na juhudi kubwa kurudisha imani ya wananchi kwa chombo hiki," alisema Waziri Meghji.

Kutokana na hali hiyo, Waziri Meghji aliitaka bodi kuhakikisha inachukua hatua madhubuti kurejesha imani miongoni mwa wananchi kutokana na taarifa za kuhusika kwa BoT katika malipo haramu au ambayo uhalali wake unatia shaka, ikiwa ni moja ya mikakati ya bodi hiyo ya kukabiliana na changamoto kubwa zinazoikabili.

Watuhumiwa wa kumshambulia Kubenea hawa hapa

WATU watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kujibu tuhuma za kuvamia ofisi za gazeti la MwanaHalisi na kummwagia kemilikali inayodhaniwa kuwa tindikali Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo Saed Kubenea na kumjeruhi kwa sime Mhariri wake wa habari, Ndimara Tegambwage.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Polisi, Charles Kenyela aliwataja washtakiwa hao mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Addy Lyamuya kuwa ni Alex Mwandemele (28) maarufu kwa jina la Chusa wa Kigogo na Hashim Mndoe (32) maarufu kwa jina la Madilu wa Tegeta.

Wengine ni Augustino Joseph (30) maarufu kwa jina la Cheusi wa Mwananyamala, Hamis Ramadhani (25) wa Mwananyamala na mkazi wa Kinondoni Alfred Moshi (64), maarufu kwa jina Chambya.

Kenyela alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na makosa ya kula njama ya kujeruhi, kummwagia tindikali Kubenea na kumjeruhi Ndimara Tegambwage.

Saturday, January 19, 2008
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi ya bweni ya KEMEBOS iliyopo Ijuganyondo katika manispaa ya Bukoba muda mfupi baada ya Rais Kuifungua shule hiyo.
Rais Kikwete akiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Orthodox Tanzania Jeronymos Muzeeyi muda mfupi baada ya Rais kuweka jiwe la msingi katika hospitali hiyo huko Kitendaguro, katika manispaa ya Bukoba, inayojengwa na kanisa hilo eneo la Kitendaguro katika manispaa ya Bukoba jana mchana.

Rais aliushukuru uongozi wa kanisa hilo kwa uamuzi wa kujenga hospitali hiyo Bukoba akisema kuwa itakapokamilika itawapunguzia wakazi wa mji wa Bukoba na maeneo mengine mkoani Kagera adha ya kwenda hospitali ya Rufaa Bugando kwa matibabu ya magonjwa makubwa.

Ufisadi Air Tanzania Corp. Ltd Jk iokoe kampuniKuna hawa Watanzania wenzetu waliopo ndani na nje ya ATCL wameona hawawezi kukaa kimya wakiangalia jinsi inavyoangamia kwa ufisadi wa kisayansi.

Wanasema kuna Ufisadi wa kisayansi kwa sababu wanaofanya ufisadi huo ni uongozi wa kampuni kwa kutumia nafasi zao za madaraka na kujifanya huo ndio uongozi.

Wametaja watu kibao wanaodai ni mafisadi na pia wametaja mianya kibao inayowahusisha washirika hao. Hebu Bonyeza
hapaupate habari zaidi.

Ile pangua pangu ilimkumba huyu jamaaIle panga pangua ya BoT ilimkumba kigogo Amatus Liyumba, ambaye inasemekana ndiye alikuwa akikaimu ugavana wakati Ballali alipokuwa nje kwa kipindi kirefu kipindi kile ambacho Naibu Gavana Mbaye alipoondoka na kabla Naibu Gavana Reli hajateuliwa.

Kanumba ndani ya HollywoodMcheza sinema maarufu wa Tanzania, Steven Kanumba aka. Denzel wa Tanzania, yuko ziarani Marekani. Kwa sasa yuko Hollywood. Ametembelea Warner Brothers na Universal Studios.

Juzi juzi kapewa tuzo ya Best Tanzania Hollywood Achievement, kutoka Kampuni ya Universal Hollywood ya nchini humo.
Hii ni tuzo ya pili kwa msanii huyo kutunikiwa kutoka Marekani ambapo ya kwanza ni ya Johnwyne International Award.

Kanumba yuko nchini Marekani kwa takriban miezi mitatu sasa kwa mwaliko wa Kampuni ya Johnwyne ya Hollywood.

Bonyeza hapatu upate habari zaidi.

Thursday, January 17, 2008

Mishahara ya maana kwa masikini ndoto

Circular
To: All members
From: Executive Director
Ref: CTI/8/3861/2008
Date: 16th January 2008
Subject: Minimum Wage for the Industrial Sector

You would recall that when the Government increased the minimum wage from TZS 48,000/- to TZS 150,000/- per month, CTI interceded on behalf of its members. As a result of CTI’s intervention, the minimum wage was reduced from TZS 150,000/- to TZS 80,000/- for industries employing 300 workers and over and those exporting at least 25 per cent of their production. Schedule Part B of GN 223/2007 relating to fringe benefits was scrapped for all industries.

Please tick the box(es) below that describes your company’s status following CTI’s intervention:

1. Benefitted from the scrapping of Schedule Part B relating to fringe benefits.

2. Benefitted, my company employs 300 or more workers.

3. Benefitted, my company exports at least 25 per cent of its production.

4. Did not benefit, my company does not meet the criteria for exemption.

Please reply by 5 p.m. on Friday, 18th January 2008 as we need the information for further follow up.

We will appreciate other comments that will assist our follow up.

Kind regards.

Christine Kilindu

BoT wafanya mabadiliko


KATIKA harakati za kusafisha uozo ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Gavana Profesa Benno Ndulu, amefanya mabadiliko makubwa ndani ya taasisi hiyo nyeti ya fedha nchini kwa kupangua safu ya wakurugenzi wa Idara mbalimbali.

Mabadiliko hayo ambayo ni ya kwanza kufanywa na GAvana Ndulu tangu ateuliwe kushika wadhifa huo wiki iliyopita, yamemng'oa mmoja wa vigogo wa benki hiyo Amatus Liyumba ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi (DPA).

Gavana Profesa Ndulu, alimweleza mwandishi wa gazeti hili ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana kuhusu mabadiliko hayo ambaye lengo lake ni kuboresha utendaji ndani ya BoT.

Awali taarifa zilizofikia gazeti hili kutoka vyanzo habari ndani ya serikali, zilisema taarifa za mabadiliko hayo zimetangazwa juzi jioni.

Profesa Ndulu alimtaja Leornad Kasalika kutoka BoT tawi la Arusha kuchukua nafasi ya Liyumba.

Kwa mujibu wa Profesa Ndulu, Liyumba atapangiwa kazi nyingine na kuongeza kwamba mabadiliko hayo yameangalia mambo matatu ya msingi.

Alisema mabadiliko hayo yanalenga kuboresha mazingira ya utendaji ili kuleta tija na ufanisi ndani ya benki.

Alifafanua kwamba, mabadiliko hayo yamegusa idara karibu zote isipokuwa Idara ya Uchumi, Fedha na Masoko.

Gavana huyo ambaye amekuwa akiangaliwa kama mwenye kuweza kuleta mabadiliko ndani ya BoT kutokana na uzoefu wake wa kufanya kazi Benki ya Dunia (WB) alifahamisha kwamba mabadiliko hayo yamegusa idara za makao makuu na matawi yote ya benki hiyo, isipokuwa Mwanza.

Matawi ya BoT nchini ukiacha Mwanza ni pamoja na Zanzibar, Mbeya na Arusha ambayo yamekuwa yakiongozwa na wakurugenzi huku.

Alizitaja idara nyingine zilizohusika na mabadiliko hayo kuwa ni Fedha, Benki, Idara inayoshughulikia Deni la Taifa na inayoshughulikia Zabuni.

Profesa Ndulu aliongeza kwamba katika mabadiliko hayo, baadhi ya wakurugenzi wamepandishwa, wengine kuondolewa na baadhi kuhamishwa idara.

Hata hivyo, Profesa Ndulu alisema taarifa zaidi kuhusu idara na majina ya watu walioteuliwa zitatangazwa wakati wowote kuanzia sasa.

Ingawa hakutaja majina zaidi, alisema wakurugenzi watano ni wapya ambao wamepandishwa.

Alisema mabadiliko hayo pia yameondoa watu ambao walikaa muda mrefu katika idara zao, kupandisha vijana na kuleta uwiano wa rika la uongozi kwa kuzingatia sifa zinazostahili.

Mabadiliko hayo ya wakurugenzi yamefanywa siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kumfukuza kazi Ballali na kuagiza kuwa watu wote waliohusika katika ufisadi wa Sh133 bilioni katika Akaunti ya Mabdeni ya Nje (EPA) katika ya benki hiyo washughulikiwe mara moja.

Hatua hiyo pia imekuja huku Kikosi Kazi (Task Force) kinachoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Johnson Mwanyika, kikiwa kimepewa miezi sita kuhakikisha wote waliohusika kuanzia ndani ya BoT na wamiliki wa makampuni 22 wanachunguzwa na kukamatwa kisha kufikishwa katika vyombo vya sheria na fedha zirejesheshwe. Habari hii imeandikwa na Ramadhan Semtawa wa Mwananchi

Wednesday, January 16, 2008

Mhariri Kubenea arejea nchini

Picha zote na Felix Fidelis

KAMANDA Saed Kubenea, Mkurugenzi Mtendaji wa magazeti ya MwanaHalisi na Mseto, aliyekuwa amelazwa hospitali nchini India akipatiwa matibabu ya macho, amerejea nchini na kudai kuwa baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi, wakiwamo vigogo wa serikali kwamba, ndio waliohusika na kushambuliwa kwake.

Kubenea (37)amesema anaamini hivyo kwa kuwa tukio la kushambuliwa kwake lilitokea katika mazingira ya kazi yake na pia baada ya moja ya magazeti yake kuyaweka majina na picha za watuhumiwa hao hadharani.

Alisema hayo alipozungumza na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya nchi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam jana.

"Suala, hapa kuna mkono wa mtu. Wanaweza kuwa viongozi wa serikali kwa kuwa wapo baadhi yao walituhumiwa kuhusika na ufisadi na gazeti langu likaweka hadharani majina yao na pia wanaweza kuwa watu wengine," alisema Kubenea.