Tuesday, December 15, 2015

UONGOZI WA WIZARA YENYE DHAMANA NA SANAA WAKUTANA NA VIONGOZI WA MASHIRIKISHO YA SANAA KUJADILI NAMNA YA KUBORESHA TASNIA YA SANAA NCHINI

E51
: Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akizungumza na viongozi wa mashirikisho ya sanaa wakati wa kikao cha kuchanganua changamoto zilizopo katika tasnia ya sanaa jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Bibi. Leah Kihimbi na kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo
E52
Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonyesho Bibi. Agnes Lukanga (wapili kulia) akichangia mada wakati wa kikao kilichoandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuchanganua changamoto zilizopo katika tasnia ya sanaa jana Jijini Dar es Salaam.
E53
Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifamba (wapili kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao kilichoandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuchanganua changamoto zilizopo katika tasnia ya sanaa jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni msemaji wa Shirikisho la Filamu Bw. John Kallage.
E54
Baadhi ya viongozi wa mashirikisho ya sanaa wakifuatilia kwa makini mada zilizokua zikiendelea wakati wa kikao kilichoandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuchanganua changamoto zilizopo katika tasnia ya sanaa jana Jijini Dar es Salaam.
E55
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (watatu kulia waliokaa) katika picha ya pamoja na viongozi wa mashirikisho ya sanaa baada ya kumaliza kikao cha kuchanganua changamoto zilizopo katika tasnia ya sanaa jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Bibi. Leah Kihimbi, wapili kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo na watatu kushoto ni Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifamba
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo
Post a Comment