Monday, July 31, 2017

TAMASHA LA ‘KOMAA CONCERT 2017’ LATIKISA DAR


Msanii wa Hip Hop, Chemical, akiwaburudisha mashabiki.
Ruby akifanya yake stejini
Mwana- FA naye akiwarusha vilivyo mashabiki wake.
Young D akifanya yake.
Dogo Aslay akikamua stejini.

TAMASHA la “KOMAA CONCERT 2017, la kituo cha redio cha Efm na TV-E jana lilifunika vilivyo katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, ambapo lilitawaliwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya.
Komaa Concert’ linafanyika mara ya pili sasa baada ya kutikisa jijini Mwanza wiki zilizopita ambapo Mkoa wa Dar es Salaam lilifanyika jana.
Tamasha hilo lilitawaliwa na wasanii kama Dog Aslay, Mr. Blue,Young D, Msaga SumuShalo Mwamba na wengineo waliotoa burudani za kutosha kwa mashabiki wa muziki.
Vile vile, kulikuwa na mchezo wa bahati nasibu uliochezeshwa na kampuni ya BIKO ambao walikuwa wadhamini wakubwa wa tamasha hilo ambapo mshindi katika mchezo huo aliondoka na zawadi ya shilingi ya milioni kumikwa kutumia elfu moja tu kuchezea bahati nasibu hiyo.
Efm redio imekuwa ikifanya tamasha hilo kwa lengo la kuwashukuru wasikilizaji wake pamoja na kuendelea kuongeza masafa ya redio katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.
NA HILALY DAUDI/GPL

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MHANDISI RAMO MAKANI, AMUAGIZA MKUU WA WILAYA YA MUHEZA KUSHUGHULIKIA MGOGORO WA HIFADHI YA MSITU WA DEREMA WILAYANI HUMO

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati), akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msasa IBC wilaya ya Muheza mkoani Tanga jana wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kwa ajili kutatua mgogoro wa hifadhi ya msitu wa Derema. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanaisha Tumbo. 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati), akimuonesha mwenyekiti wa kamati ya wakulima wa vijiji vitano vya tarafa ya Amani, Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mohammed Ramadhani Shesha viwango halali vya serikali vya kulipia fidia za mazao kwa wananchi waliondolewa katika eneo la hifadhi ya msitu wa Derema wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo jana kwa ajili ya kutatua migogoro wa hifadhi hiyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanaisha Tumbo.  
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia), akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msasa IBC wilaya ya Muheza mkoani Tanga jana wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kwa ajili kutatua mgogoro wa hifadhi ya msitu wa Derema.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani, (wa tatu kushoto), akiangalia eneo la Msitu wa hifadhi ya Derema na viongozi wa wilaya ya Muheza Muheza wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo jana kwa ajili ya kutatua mgogoro wa hifadhi hiyo. 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia), akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Msasa IBC wilaya ya Muheza Mkoani Tanga jana wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kwa ajili ya kutatua mgogoro ya hifadhi ya msitu wa Derema. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kushoto), akimuonesha mwenyekiti wa kamati ya wakulima wa vijiji vitano vya tarafa ya Amani, Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mohammed Ramadhani Shesha (kulia) viwango halali vya serikali vya kulipia fidia za mazao kwa wananchi waliondolewa katika eneo la hifadhi ya msitu wa Derema wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo jana kwa ajili ya kutatua migogoro wa hifadhi hiyo. 

Na Hamza Temba - WMU - Muheza, Tanga
.............................................................................

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga kukutana na wakulima 879 wa vijiji vitano katika Tarafa ya Amani Wilayani humo kwa ajili kufanya uhakiki wa malipo ya fidia ya mazao waliyolipwa na Serikali ili kupisha eneo la hifadhi ya msitu wa Derema.

Mhandisi Makani ametoa agizo hilo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Msasa IBC, Tarafa ya Amani, Wilayani Muheza kufuatia malalamiko ya wananchi hao kupunjwa malipo yao wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kwa ajili kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 15 baina Serikali na wananchi wa vijiji hivyo vya Kisiwani, Kwemdim, Msasa IBC, Antakae na Kambi.

Akisoma risala ya wakulima hao mbele ya Naibu Waziri Makani, Mwenyekiti wa Kamati ya wakulima hao, Mohammed Rama Shesha alidai kuwa jumla ya wakulima 1,128 wa vijiji hivyo wanailalamikia Serikali kwa kuwalipa viwango pungufu vya malipo ya fidia ya mazao yao tofauti na viwango vilivyolipwa na Serikali mwaka 2002 kupitia mradi wa FINIDA. Aidha, alidai kuwa kuna baadhi ya mazao pia hayakulipiwa kabisa fidia hizo.

Akizungumzia viwango vya fidia hizo Shesha alisema wananchi walilipwa Shilingi 28,800 kwa mche mmoja wa iliki na Shilingi 11,000 kwa mche mmoja wa mgomba. Alidai viwango hivyo vilibadilika kuanzia mwaka 2005 ambapo walilipwa Shilingi 3,315 kwa kila mche mmoja badala ya Shilingi 5,100 kama ilivyoainishwa kwenye viwango vya Serikali hivyo akaomba walipwe kiasi kilichobakia cha shilingi 1,785.

Akitolea ufafanuzi wa malalamiko hayo, Naibu Waziri Makani alisema idadi kamili ya wananchi waliohakikiwa katika eneo hilo ni 879 na sio 1,128 kama alivyodai mwenyekiti huyo. Aidha, alisema viwango vilivyotumiwa kuwalipa wananchi hao mwaka 2002 sio vya Serikali na kwamba vilitumiwa na mradi wa FINIDA uliofadhiliwa na Serikali ya Finland kwa ajili ya kulipa fidia wananchi wa mpakani na hifadhi hiyo ili kufanikisha zoezi la kuanisha mpaka wa hifadhi hiyo na kusaidia Serikali kutimiza azma ya kuhifadhi eneo hilo.

Alisema viwango halali vya Serikali vilivyopo kisheria kwa ajili ya kulipa fidia ya mimea hiyo ni kuanzia Shilingi 5,100 kwa kiwango cha juu kwa mmea uliokoma kufikia kiwango cha uzalishaji, Shilingi 3,315 kwa mmea wenye mwaka mmoja na Shilingi 2,040 kwa mmea wenye mwezi mmoja. Alisema viwango vingine vya malipo kwa kiwango cha chini ni Shilingi 204, Shilingi 102 na Shilingi 51.

Alisema Serikali iliamua kulipa kiwango cha Shilingi 3,315 kwa mazao yote ikiwemo yale yaliyostahili kulipwa kiwango cha chini kabisa cha Shilingi 51 ili kuweka uwiano na kurahisha zoezi hilo la malipo. Alihoji kama kuna mwananchi yeyote aliyelipwa chini ya kiwango hicho japokuwa kulikuwepo na wengine mazao yao yalistahili kulipiwa viwango hivyo, hakuna aliyejitokeza.

Kufuatia ufafanuzi huo aliuagiza uongozi wa Wilaya ya Muheza kutumia kipindi cha mwezi mmoja kuanzia leo Jumatatu kuonana na wakulima hao ili kuhakiki malipo yao na hatua zaidi ziweze kuchukuliwa kama kuna yeyote aliyezulumiwa apewe haki yake. 

"Kwa wale ambao tayari wana kumbukumbu zao vizuri wazilete mbele ya Serikali, kupitia wao pengine tunaweza kupata picha ya jumla pengine kulikua na mapungufu kwenye malipo. Kuanzia jumatatu ijayo Mhe. DC tulitekeleze hilo la kukusanya nyaraka kwa wale walizonazo tuweze kuzilinganisha na zile tulizokua nazo Serikalini tujadiliane nao kwamba ni kitu gani kimebaki tofauti katika maeneo yale yale mliyofanyiwa uhakiki", alisema Mhandisi Makani.

Alisema kwa wale ambao wamepoteza nyaraka zao za malipo wataandaliwa utaratibu maalum wa uhakiki kwa kuwa kumbukumbu zote za malipo zipo kwenye Kompyuta za halmashauri ya Wilaya ya Muheza.

Alisema lengo la Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inamaliza kabisa migogoro ya ardhi nchini. “Tutahakikisha tunaboresha zaidi usimamizi wa uhifadhi wa rasilimali zetu za misitu, wanyamapori na nyinginezo kuhakikisha migogoro hiyo inapungua kwa kasi kuelekea kwenye sifuri, zero rate", alisema Makani.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanaisha Tumbo alisema, Serikali ya Wilaya imepokea maelekezo hayo na itayafanyia kazi na kwamba maafisa wa Halmashauri watafika katika kila kijiji siku ya Jumatatu na Jumatano kwa ajili ya kuendesha zoezi hilo la uhakiki.

Akizungumzia zoezi la fidia Mkuu huyo wa Wilaya alisema pamoja na wananchi hao kulipwa fidia za mazao yao ambayo yalilipwa kwa awamu tatu, asilimia 50 mwaka 2005, asilimia 25 mwaka 2006 na asilimia 25 mwaka 2008, pamoja na asilimia 23 kama fidia ya ucheleweshaji wa deni, Serikali pia itawapa maeneo ya fidia ambapo kila mwananchi aliyeathirika eneo lake atapewa ekari tatu.

Alisema eneo ambalo limeanishwa kwa ajili ya kuwagawia wananchi hao ni lililokuwa shamba la mkonge Kibaranga ambalo lina ukubwa wa hekta 1370 sawa na ekari 3425 na lilikua likimilikiwa na Bodi ya Mkonge, eneo hilo lilitolewa tamko ya kufutiwa umiliki wake na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli mwezi Julai, 2016.

JAFO AWAJIA JUU WATAALAM WA AFYA NA AFISA MANUNUZI WILAYA YA UKEREWE


Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua chumba cha upasuaji kilichopo katika moja ya kituo cha Afya wilayani Ukerewe.
jf (2)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi katika hospitali ya wilaya ya Ukerewe.
jf (3)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua majengo ya kutolea huduma katika Hospitali ya Ukerewe.
jf (4)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki katika hospitali ya wilaya ya Ukerewe.
jf (5)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Frank Bahati katika ukaguzi wa miradi ya Afya.
jf (6)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Afya wilayani Ukerewe.
…………………………………………………….
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amewajia juu Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya(DMO), Afisa Manunuzi, na mwakilishi wa Mweka hazina wa halmashauri ya wilaya ya ukerewe baada ya kushindwa kutoa ufafanuzi sahihi juu ya ununuzi wa dawa chini ya mfuko wa Afya wa pamoja (Busket Fund).

 Akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo, Jafo amefika kwenye hospitali ya wilaya ya ukerewe na kuwaomba wananchi waliokuwepo hospitalini hapo kueleza changamoto wanazozipata wanapofika hospitalini hapo.

 Kufuatia changamoto walizoeleza wananchi, Jafo alionyesha kukerwa kutokana na maafisa hao kushindwa kujibu hoja ya wananchi waliokuwa wakilalamika kwamba wanapofika kwenye hospitali hiyo mara nyingi wataalam wamekuwa na kauli mbaya sambasamba na kukosa dawa. 
 Jafo aliwageukia wataalam hao kwa kuwauliza ni kiasi gani cha fedha za basket fund wamepokea kwa mwaka Fedha 2016/2017 na kiasi gani kilitumika kununua dawa na vifaa tiba.

 Kutokana na Jafo kuhoji fedha hizo, wataalam hao wote walishindwa kufahamu, jambo lililomkera Naibu Waziri Jafo.

 Alisema ameshangazwa na kitendo cha wataalam wahusika kushindwa kutambua mambo ya msingi ambayo wanapaswa kuyasimamia ili kutatua kero ya afya kwa wananchi.

 Jafo aliwajulisha wananchi kuwa halmashauri yao imepokea jumla ya sh.milioni 727.4 ambapo 33% ilipaswa kununulia dawa na vifaa tiba.
 Naibu Waziri Jafo amewataka watumishi wote kusimamia mipango ya serikali ili kutatua kero za  wananchi ili kuleta maendeleo katika jamii.

WAZIRI MKUU AWAASA WATUMISHI WANAOFANYAKAZI VIWANDANI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa umma wa wilaya ya Rungwe Julai 30, 2017. Kulia ni Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa kiwanda cha gesi cha TOL Gasese Limited kilichopo katika kijiji cha Ikama wilayani Rungwe Baada ya kuwasili kiwandani hapo Julai 30, 2017 Kushoto ni Naiobu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana viongozi wa kiwanda cha chai cha Katumba wilayani Rung wakati alipowasili kiwandani hapo kukagua shuguli za kiwanda hicho Julai 30, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha chai cha Katumba wilayani Rungwe Julai 30, 2017. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla na kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Ramadhani Kampasili. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitazama chai iliyosindikwa na kufungashwa tayari kwa kuuzwa wakati alipotembelea kwianda cha chai cha Katumba wilayani Rungwe Julai 30, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri ) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Rungwe baada ya kutembelea kiwanda cha Chai cha Katumba Julai 30, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezokutoka kwa Mkutugenzi wa Ufundi, Bw. McJohn Mbiri (kulia Kwake) kuhusu mitambo ya kuzaisha gesi ya hewa ya ukaa wakati alipotembelea kiwanda cha TOL Limited kilichopo katika kijiji cha Ikama wilayani Rungwe Julai 30, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wazee wa Busokelo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa michezo wa Kandete katika jimbo la Busokelo kuhutubia mkutano wa hadhara Julai 30, 2017. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifuhia ngoma ya asili baada ya kuwasili kwenye uwanja wa michezo wa Kandete katika jimbo la Busokelo mkoani Mbeya kuhutubia mkutano wa hadhara Julai 30, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Baadhi ya watumishi wa umma wa wilaya ya Rungwe wakati alipozungumza nao leo Julai 30, 2017. 

………………………………………………………………….. 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasihi Watanzania wanaofanya kazi katika viwanda mbalimbali nchini kufanya kazi kwa bidii na kuwa waaminifu. 

Amesema Tanzania imedhamiria kukuza uchumi wake kupitia sekta ya viwanda hivyo ni vema watakaopata fursa ya ajira katika viwanda hivyo kuwa waadilifu. 

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 30, 2017) wakati akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha gesi cha Ikama kilichoko wilayani Rungwe. 

Waziri Mkuu amesema wakati Serikali ikiendelea kuwakaribisha wawekezaji nchini, wananchi walioajiriwa kwenye maeneo hayo wawe waaminifu. 

“Mnatakiwa muwe waaminifu, msibebe kitu chochote ndani ya kiwanda bila ya ridhaa ya wamiliki kwa kuwa mtaonyesha taswira mbaya kwa wawekezaji.” 

Amesema uaminifu wao ndio utawezesha Watanzania wengi kupata ajira kwenye viwanda hivyo ambavyo vimejengwa katika maeneo yao. 

Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na kampuni ya TOL Gases, Mhandisi Harold Temu alisema kiwanda kinauwezo wa kuzalisha tani 46 kwa siku. 

Alisema gesi inayozalishwa kiwandani hapo ni ya Carbon Dioxide ambayo inauzwa nchini na nchi jirani za Zambia, Malawi, Zimbabwe na Congo. 

Mhandisi Temu alisema wateja wakubwa wa gesi hiyo ni viwanda vya kutengenezea soda, bia na pia hutumika katika kuhifadhia chakula na kwenye vifaa vya kuzimia moto. 

Mapema Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kuchakata majani ya chai cha Katumba, ambapo alisema Serikali inaimarisha Ushirika wa zao hili ili wakulima waweze kupata tija. 

Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ Yaibuka Kidedea Katika Mwajiri Bora Katika Ushirikishwaji na Chama cha Wafanyakazi ZAFICOW.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi ZAFICAW Bi. Rihii Haji Ali, akimkabidhi Cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Ameir Khafidh cha Mwajiri Bora Katika Ushirikiano na ZAFICOW kwa mwaka 2017. wakati wa hafla ya Bonaza la Wafanyakazi wa PBZ lililofanyika katika ufukwe wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi ZAFICAW Bi. Rihii Haji Ali, akimkabidhi Cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Ameir Khafidh cha Mwajiri Bora Katika Ushirikiano na ZAFICOW, wakati wa hafla ya Bonaza la Wafanyakazi wa PBZ lililofanyika katika ufukwe wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja. 
 Viongozi wa PBZ na wa ZAFICOW wakiimbi wimbo wa ushirikiano wa Wafanyakazi wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa Cheti zilizofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Zanzibar. 
Wafanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar wakiimbi wimbo wa Wafanyakazi wa Mshikamano wakati wa mkutano wao na Mwenyekiti wa ZAFICOW wakati wa hafla ya bonaza la Michezo lililowashirikisha Wafanyakazi wa PBZ, 
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar ZAFICOW Bi. Rihii Haji Ali akitzungumza wakati wa mkutano huo na wafanyakazi wa PBZ kujuwa wajibu wao katika kazi na kuwataka kujiunga na Chama hicho kwa faida yao na maslahi kwa muajiri wao.Pia alikabidhi Kadi kwa Wanachama wapya ya PBZ 10 waliojiunga na kuwakabidhi Kadi za Uwanachama. 
Watendaji wa PBZ wakifuatilia mkutano huo na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar Bi Rihii Haji Ali alipokuwa akizungumza na wafanyakazi hao wakati wa Tamasha la Bonaza la Wafanyakazi wa PBZ lililofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.
Wafanyakazi wa PBZ wakifuatilia mkutano huo na Uongozi wa PBZ na ZAFICOW uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Visiter Inn Jambiani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Ameir Khafidh akimkabidhi Kadi ya Mwanachama mpya wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar ZAFICOW Ndg. Suleiman Abdi, baada ya kujiunga na Chama hicho wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Ameir Khafidh akimkabidhi Kadi ya Mwanachama mpya wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar ZAFICOW Ndg. Bakari Hussein, baada ya kujiunga na Chama hicho wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Ameir Khafidh akimkabidhi Kadi ya Mwanachama mpya wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar ZAFICOW Bi. Fatima Ali Denge, baada ya kujiunga na Chama hicho wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Ameir Khafidh akimkabidhi Kadi ya Mwanachama mpya wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar ZAFICOW Bi. Mkunga Mohammed Saleh, baada ya kujiunga na Chama hicho wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkurugenzi Mtendajio wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ngd Juma Ameir Khafidh akimkabidhi zawada ya fedha shilingi miliono moja kwa kuibuka Mfanyakazi Bora wa Benki ya Watu wa Zanzibar kwa mwaka 2017  Ndg. Juma Ameir Makame (kulia) akishuhudia Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar (ZAFICOW) Bi. Rihii Haji Ali hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja. 
Mfanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg.Haji Masoud, akikisoma Cheti cha Mwajiri Bora Katika Ushirikishwaji katika Chama  cha Wafanyakazi cha ZAFICOW, wakati wa kukabidhi na Uongozi wa ZAFICOW.  
Afisa Muandamizi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ Ndg. Anasi Rashid akizungumza na kutowa maelekezo wakati wa Mkutano huo wa Wafanyakazi na Uongozi wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar Wafanyakazi Zanzibar (ZAFICOW)  
Mkurugenzi Rasilimali Watu PBZ Ndg. Mohammed Omar (kulia) akimkabidhi zawadi maalum iliyotolewa na Wafanyakazi wa PBZ kwa Boss wao wakati wa Mkutano huo na Wafanyakazi wa PBZ Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Zanzibar. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Ndg Juma Ameir Khafidh akitowa nasaha zake kwa Wafanyakazi wakati wa mkutano huo ulioambatana na michezo mbalimbali iliowashirikishwa Wafanyakazi kujumuika pamoja na kubadilishana mawazo Bonaza hilo limefanyika katika ufukwe wa Hoteli ya Visiter Inn Jambani.Mkoa wa Kusini Unguja.  
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Ameir Khafidh akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo na Wafanyakazi uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Visiter Inn Jambiani Zanzibar.
Wafanyakazi wa PBZ wakipata viburudisho ya maji ya madafu baada ya mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.

Imeandaliwa na Othmanmapara.blog.
Zanzinews.com
othmanmaulid@gmail.com
Mobile.0777424152.