Saturday, July 28, 2018

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA RASMI NYUMBA 14 ZA MAKAZI ZA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUSOKELO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan sambamba na Mkuu wa Mkoa Wa Mbeya Amos Makalla, Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Julius Challya na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo jioni. Nyumba hizo 14 zimejengwa katika Kata ya Lwangwa. Mradi huo umegharimu kiasi cha Shilingi bilioni 1.1 ikiwa ni wastani wa sh. milioni 79 kwa kila nyumba. mradi huu wa Busokelo ulianza rasmi mwaka 2014 na na ulikakamilika mwaka 2015 kisha kukabidhiwa Machi 24, 2017. Hadi kukamilika mradi huu umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.1 na pesa hii imelipwa kwa awamu tatu zikiwemo baada ya kuweka sahihi katika mkataba, mwaka mmoja baada ya malipo ya awali na malipo ya mwisho ndani ya miaka minne. Makamu wa Rais amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya pamoja na Mkuu wa Wilaya kuharakisha mazungumzo ili maombi ya kujengewa nyumba 11 za watumishi wa Halmashauri hiyo yatimie.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan sambamba na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo jioni. Wengine ni Mkuu wa Mkoa Wa Mbeya Amos Makala na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Julius Challya pamoja na Mbunge wa Jimbo la Busokelo, Freddy Mwakibete wakishuhudia uzinduzi huo.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi wakati akimpa maelezo kuhusu mradi huo wakati Makamu wa Rais alipokuwa akizindua nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo jioni
Mojawapo ya nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo jioni.

 Umati wa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Watumishi wa Halmashauri hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan sambamba na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo jioni. Wengine ni Mkuu wa Mkoa Wa Mbeya Amos Makala na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Julius Challya pamoja na Mbunge wa Jimbo la Busokelo, Freddy Mwakibete wakishuhudia uzinduzi huo.
 Mojawapo ya nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo jioni.
Jiwe la msingi mbele ya Mojawapo ya nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo jioni.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akitoa maelezo ya mradi wa nyumba za makazi za Watumishi wa Halmashauri ya Busokelo kwa mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan

  Umati wa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Watumishi wa Halmashauri hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika uzinduzi huo.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akisalimiana na mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan baada ya uzinduzi huo leo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akisalimiana na mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan baada ya uzinduzi huo leo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akisalimiana na Profesa Mark James Mwandosya mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan baada ya uzinduzi huo leo.

NHC YASAINI MKATABA NA HALMASHAURI MPYA YA WANGING'OMBE ILIYOPO MKOANI NJOMBE

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akitiliana saini mkataba wa ujenzi wa jengo la Utawala na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Athony Emmanuel Mawata huku wakishuhudiwa Mkuu wa Huduma za Sheria wa Shirika la Nyumba laTaifa, Martin Mdoe  Utiaji saini makubaliano hayo umefanyika leo asubuhi katika Ofisi za Halmauri hiyo na kuhudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Emmanuel Kirundo na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Athony Emmanuel Mawata na watumishi waandamizi wa Halmashauri hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akitiliana saini mkataba wa ujenzi wa jengo la Utawala na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Athony Emmanuel Mawata huku wakishuhudiwa Mkuu wa Huduma za Sheria wa Shirika la Nyumba laTaifa, Martin Mdoe  Utiaji saini makubaliano hayo umefanyika leo asubuhi katika Ofisi za Halmauri hiyo na kuhudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Emmanuel Kirundo na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Athony Emmanuel Mawata na watumishi waandamizi wa Halmashauri hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akitiliana saini mkataba wa ujenzi wa jengo la Utawala na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Athony Emmanuel Mawata huku wakishuhudiwa Mkuu wa Huduma za Sheria wa Shirika la Nyumba laTaifa, Martin Mdoe  Utiaji saini makubaliano hayo umefanyika leo asubuhi katika Ofisi za Halmauri hiyo na kuhudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Emmanuel Kirundo na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Athony Emmanuel Mawata na watumishi waandamizi wa Halmashauri hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akipeana mkono na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Athony Emmanuel Mawata baada ya kusaini mkataba huo.
Picha ya pamoja ya viongozi hao.

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&


SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) leo limesaini mkataba na Halmashauri ya Wilaya Mpya ya Wangingómbe iliyopo Mkoani Njombe ya Ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri hiyo wenye thamani ya shilingi bilioni 2.7.

Utiaji saini makubaliano hayo umefanyika leo asubuhi katika Ofisi za Halmauri hiyo na kuhudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Emmanuel Kirundo na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Athony Emmanuel Mawata na watumishi waandamizi wa Halmashauri hiyo.
Akizungumza wakati wa utiaji saini huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi alisema ujenzi wa jengo hilo unaotarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja utaanza ndani ya wiki mbili kuanzia sasa.
“Ni jengo litakalokuwa na ofisi nyingi za viongozi na wataalamu wa Halmashauri na pande zote mbili tuko tayari kutekeleza majukumu ya kimkataba,”alisema.
Akizungumza wakati wa utiaji saini huo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Emmanuel Kirundo alisema wameamua kulikabidhi Shirika hilo dhamana ya ujenzi wa jengo hilo kubwa lenye nafasi ya kutosha kutokana na uwezo lililo nao Shirika hilo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Athony Emmanuel Mawata
 alisema wamepitia michakato mingi katika kumtafuta mkandarasi bora atakayejenga jengo hilo na hatimaye wakafikia hatua ya kukabidhi ujenzi wa jengo hilo kwa NHC kutokana na ubora wa kazi zilizokwishawahi kufanywa na Shirika hilo.

Thursday, July 26, 2018

WAWEKEZAJI KUTOKA KOREA KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA NYUMBA NCHINI

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akijadiliana na  Ujumbe wa Wataalamu wa Sekta ya Ujenzi na Nyumba waliokuwa katika ujumbe wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak-yon kuhusu fursa za uwekezaji katika Sekta ya Nyumba zilizopo nchini na namna nchi ya Korea inavyoweza kuwekeza katika sekta hiyo nchini. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara, William Genya. Katika mazungumzo hayo wataalamu hao wameahidi kurejea nchini baadaye mwaka huu kuja na mkakati kamambe wa kuwekeza na Shirika la Nyumba la Taifa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akijadiliana na  Ujumbe wa Wataalamu wa Sekta ya Ujenzi na Nyumba waliokuwa katika ujumbe wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak-yon kuhusu fursa za uwekezaji katika Sekta ya Nyumba zilizopo nchini na namna nchi ya Korea inavyoweza kuwekeza katika sekta hiyo nchini.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wataalamu wa Sekta ya Ujenzi na Nyumba waliokuwa katika ujumbe wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak-yon. Wa pili kushoto ni Joo Chang -Kon na Meneja Mkuu wa anayeshughulikia Biashara za Kimataifa Shirika la Nyumba la Korea, wengine ni Maafisa wa Uendelezaji Biashara wa NHC, Clara Lumbanga na Patrick Mwakasungungula Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara, William Genya.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wataalamu wa Sekta ya Ujenzi na Nyumba waliokuwa katika ujumbe wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak-yon. Wa pili kushoto ni Joo Chang -Kon na Meneja Mkuu wa anayeshughulikia Biashara za Kimataifa Shirika la Nyumba la Korea, wengine ni Maafisa wa Uendelezaji Biashara wa NHC, Clara Lumbanga na Patrick Mwakasungungula Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara, William Genya..
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akijadiliana na  Ujumbe wa Wataalamu wa Sekta ya Ujenzi na Nyumba waliokuwa katika ujumbe wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak-yon kuhusu fursa za uwekezaji katika Sekta ya Nyumba zilizopo nchini na namna nchi ya Korea inavyoweza kuwekeza katika sekta hiyo nchini. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara, William Genya.

Tuesday, July 24, 2018

TANZANIA YATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA MKUTANO WA 37 WA SHIRIKA LA MAKAZI AFRIKA 2018

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi ambaye alikuwa Mwenyekiti akiwa na wenyeviti wenza wa Mkutano wa 37 wa Shelter Afrique wakiongoza ajenda mbalimbali zilizowasilishwa katika Mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Windsor jijini Nairobi Kenya.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi ambaye alikuwa Mwenyekiti akiwa na wenyeviti wenza wa Mkutano wa 37 wa Shelter Afrique wakiongoza ajenda mbalimbali zilizowasilishwa katika Mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Windsor jijini Nairobi Kenya.
  
Kaimu Mkurugenzi wa Nyumba wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Pius Tesha, akipitia na kusikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zinajadiliwa na Wajumbe kutoka nchi 44 za Afrika waliohudhuria Mkutano huo uliofanyika katika Jiji la Nairobi nchini Kenya.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi, akifuatilia ajenda mbalimbali zilizowasilishwa katika Mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Windsor jijini Nairobi Kenya.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi, akifuatilia ajenda mbalimbali zilizowasilishwa katika Mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Windsor jijini Nairobi Kenya.

Tanzania imeteuliwa kwa kauli moja na wajumbe wa Mkutano wa 37 wa Makazi Afrika (Shelter Afrique) kuwa Mwenyekiti wa Mkutano wa 37 wadhifa ambao atautumikia kwa mwaka mmoja na kukabidhi madaraka katika mkutano utakaofanyika mwezi Julai 2019 Jijini Rabat, Morocco. Mkutano huo ambao una wanachama kutoka nchi 44 za Afrika walikutana katika jiji la Nairobi nchini Kenya ili kujadili changamoto za hali ya makazi kwa watu wa nchi hizo ili kuona namna ya kutatua changamoto hizo kwa kutumia uzoefu wa kila nchi mwanachama. 

Aidha, katika Mkutano huo ambapo Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi, iliteuliwa kuwa Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo wa 37. 

Tanzania ilijiunga na Shelter Afrique mwaka 2003 na Mkutano wa 32 wa Shelter - Afrique uliofanyika N’djamena, Chad mwaka 2013 ulipitisha Azimio Namba GM/2013/005 la kuongeza Hisa kwa kila nchi mwanachama kwa lengo la kukuza mtaji wa kampuni hiyo na kuiwezesha kuweka nguvu zaidi katika masuala ya uendelezaji nyumba barani Afrika.

Shirika la Nyumba la Taifa limenufaika na mtaji huo ambapo mwaka 2002 lilikopeshwa Dola za Kimarekani 1.5 milioni na kuzitumia kujenga nyumba 212 eneo la Boko Jijini Dar es Salaam na mwaka 2011 lilikopeshwa fedha kiasi cha Dola za Kimarekani 14.5 milioni mkopo uliotakiwa kurejeshwa katika kipindi cha miaka 10 na mkopo huo ulitumika kujenga nyumba za gharama nafuu zipatazo 558 katika maeneo mbalimbali nchini. Pamoja na kuikopesha NHC, Shelter Afrique imewekeza kiasi cha Dola za Kimarekani 27,500,000/= katika miradi mbalimbali ya ujenzi wa nyumba nchini Tanzania.Monday, July 23, 2018

RAIS DK. MAGUFULI APOKEA GAWIO LA SERIKALI LA SH. BILIONI 1.2 KUTOKA NHC

Rais Dk. John Pombe Magufuli na Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango wakipokea mfano wa hundi ya gawio la shilingi Bilioni 1.2 kwa serikali  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi kwenye hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2018.

Leo Jumatatu (23/07/2018) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekabidhiwa Hundi za fedha zenye Thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 717.6 kutoka kwa wakala, kampuni , Taaisis na mashirika 47 ambayo Serikali inayamiliki, NHC ikiwamo.

Serikali imefanikiwa kupata bilioni 717.6 kutoka Katika baadhi ya Mashirika , kampuni na taasisi chache tu ambazo Ziko nyingi ambazo zinapaswa kutoa Gawio kwa Serikali kama mwana Hisa.

 Rais Dk. John Pombe Magufuli na Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango wakipokea mfano wa hundi ya gawio la shilingi Bilioni 1.2 kwa serikali  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi kwenye hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2018.
Rais Dk. John Pombe Magufuli na Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango wakipokea mfano wa hundi ya gawio la shilingi Bilioni 1.2 kwa serikali  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi kwenye hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2018.
Rais Magufulia akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa taasisi mbalimbali za umma 47 bambazo zilifika kuwasilisha hundi zao za gawio kwa Serikali ikiwa ni faida waliyoipata kutokana na biashara na ama kuchangia.
 Rais Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa taasisi mbalimbali za umma 47 bambazo zilifika kuwasilisha hundi zao za gawio kwa Serikali ikiwa ni faida waliyoipata kutokana na biashara na ama kuchangia
 Wageni waalikwa wakiwasili katika eneo la tukio kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere JINCC.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akijadilia jambo na mmoja wa wadau kwenye hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2018.

***************************

Wakati huo huo huo, Rais John Magufuli amemwagiza Msajili wa Hazina, Dk Athuman Mbuttuka kubadilisha uongozi au kufuta kampuni, wakala, taasisi na mashirika ya umma ambayo yatashindwa kutoa gawio kwa Serikali.
Ameyasema hayo leo Julai 23, 2018 katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akipokea gawio la Sh736.36 bilioni kwa mwaka 2017/18 kutoka kwa kampuni 43 kati ya 90 ambazo zinastahili kulipa gawio serikalini.
“Halipendwi shirika, inapendwa pesa tunachotaka ni gawio na si vinginevyo. Hatutaki kuwa na kitu ambacho hakishiriki kujenga uchumi wa nchi hii, nakuagiza msajili wa Hazina (Mbuttuka) hakikisha mashirika na taasisi zote zenye kutoa gawio kwa Serikali zinafanya hivyo,” amesema Rais Magufuli
Aidha ameyapongeza mashirika ambayo hayakuwahi kutoa gawio awali na mwaka huu yamejitokeza na kuchangia katika pato la Serikali yakiwemo yale ya UTT, DSE na Kadico.
Hata hivyo, ameonya kuwa bado kuna kampuni nyingi zinazalisha kiasi kidogo ikilinganishwa na kile kilichowekezwa na Serikali, hivyo kuwataka viongozi wa kampuni hizo kujitathmini.
Pia, Rais Magufuli ametoa wito kwa kampuni za Serikali kuhakikisha zinatekeleza majukumu ipasavyo ili kuondoa mianya ya rushwa na upotevu.
“Wakati mwingine tunaliwa kutokana na uzembe wa watendaji wetu, wanakaa pale wanakuwa sehemu ya kuwaumiza Watanzania badala ya kutekeleza majukumu yao. Nawaagiza wenyeviti wa bodi na watendaji wa Serikali mkalisimamie hili. Nataka kuona matrilioni na si mabilioni kama nilivyoona mwaka huu,” amesema Rais Magufuli.

Thursday, July 19, 2018

WAZIRI LUKUVI AONGOZA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA SHELTER AFRIQUE- KENYA


Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Vangimembe  Lukuvi ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa 37 wa Makazi Afrika (Shelter Afrique) ulioanza leo jijini Nairobi akizungumza na wanachama wa mkutano huo (hawapo pichani). Mkutano huo ambao una wanachama kutoka nchi 44 za Afrika wanakutana katika nchini humo ili kujadili changamoto za hali ya makazi kwa watu wa nchi hizo ili kuona namna ya kutatua changamoto hizo kwa kutumia uzoefu wa kila nchi mwanachama.

 Mambo mbalimbali yanajadiliwa katika mkutano huo ikiwa ni pamoja na kuondoa changamoto ya Rasilimali Fedha inayozikabili nchi nyingi wanachama wa Umoja huo na kushindwa kuwapatia wananchi wa Afrika makazi bora na nafuu. 

Kwa ujumla changamoto za nchi za kiafrika katika kuwapatia wananchi wa kawaida makazi nafuu zinafanana na kilio kikubwa katika nchi wanachama, ambazo ni  kuwepo makazi holela hata baada ya nchi hizo kujikomboa kutoka ukoloni mkongwe.

Tanzania ni nchi mojawapo Mwanachama wa Shelter Afrique kati ya nchi 44 za barani Afrika ilijiunga na Shelter Afrique mwaka 2003 na Mkutano wa 32  ambao ulifanyika N’djamena, Chad 2013, uliopitishwa na Azimio Namba GM/ 2013/005 la kuongeza Hisa kwa kila nchi mwanachama kwa lengo la kukuza mtaji wa Kampuni hiyo na kuiwezesha kuweka nguvu zaidi katika masuala ya uendelezaji nyumba barani Afrika. Mkutano wa mwaka huu unafanyika Jijini Nairobi katika hoteli ya Windsor.

Aidha, katika Mkutano huo ambapo Tanzania iliwakilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi, Mkurugenzi wa Nyumba wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Pius Tesha, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Utoaji Mikopo kwa Benki na Taasisi za fedha kwa ajili ya mikopo wa nyumba Tanzania (TMRC), Oscar Mgaya Pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Maendeleo ya Biashara wa NHC William Genya.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Nyumba wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Pius Tesha huku wajumbe wengine wakishuhudia.
Ujumbe wa Tanzania Mkutano wa 37 wa Makazi Afrika (Shelter Afrique) ukifuatilia mkutano huo wa leo wa kwanza kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Utoaji Mikopo kwa Benki na Taasisi za fedha kwa ajili ya mikopo wa nyumba Tanzania (TMRC), Oscar Mgaya, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi, Mkurugenzi wa Nyumba wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Pius Tesha na Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Maendeleo ya Biashara wa NHC William Genya. Ujumbe wa Tanzania Mkutano wa 37 wa Makazi Afrika (Shelter Afrique) ukifuatilia mkutano huo wa leo wa kwanza kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Utoaji Mikopo kwa Benki na Taasisi za fedha kwa ajili ya mikopo wa nyumba Tanzania (TMRC), Oscar Mgaya, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi, Mkurugenzi wa Nyumba wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Pius Tesha na Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Maendeleo ya Biashara wa NHC William Genya.


 Ujumbe wa Tanzania Mkutano wa 37 wa Makazi Afrika (Shelter Afrique) ukifuatilia mkutano huo wa leo.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Vangimembe  Lukuvi akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi nchini Kenya jana.
Waziri wa Ardhi na Upimaji wa Kenya, Mama Farida Karoney akijadiliana masuala mbalimbali na ujumbe wa Tanzania kwenye makao makuu ya wizara hiyo nchini Kenya. Mheshimiwa Waziri Lukuvi alifanya ziara ya kikazi katika Wizara ya Ardhi na Upimaji nchini Kenya jana tarehe 18 Julai, 2018 ambapo pamoja na mambo mengine Waziri alitaka  kujua mifumo ya upimaji, ugawaji, umiliki na utawala wa ardhi wa nchini Kenya.

Waziri wa Ardhi na Upimaji wa Kenya, Mama Farida Karoney akijadiliana jambo na Waziri Lukuvi kwenye makao makuu ya wizara hiyo nchini Kenya.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Vangimembe  Lukuvi akizungumza kwenye mkutano wa alipofanya ziara ya kikazi katika Wizara ya Ardhi na Upimaji nchini Kenya jana (18 Julai, 2018) ambapo pamoja na mambo mengine Waziri alitaka  kujua mifumo ya upimaji, ugawaji, umiliki na utawala wa ardhi wa nchini Kenya.
Monday, July 09, 2018

WAZIRI LUKUVI ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI MIRADI MTWARA

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , William Vangimembe Lukuvi akisikiliza maelezo ya Renald Kazoba wa Shirika la Nyumba Mtwara juu ya maendeleo ya ukamilishwaji wa ujenzi wa Jengo la Biashara la RahaLeo Commercial Complex lililopo eneo la Rahaleo Mtwara, akiwa huko Waziri Lukuvi amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa kwa kukamilisha miradi mikubwa mitatu mkoani Mtwara kwa wakati na akalitaka Shirika kuendelea na kasi hiyo bila kuathiri rasilimali za Shirika. Kushoto anayeshuhudia ni Meneja wa NHC Mtwara, Angela Magazi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , William Vangimembe Lukuvi akisikiliza maelezo ya Renald Kazoba wa Shirika la Nyumba Mtwara juu ya maendeleo ya ukamilishwaji wa ujenzi wa Jengo la Makazi eneo la Shangani Mtwara, akiwa huko Waziri Lukuvi amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa kwa kukamilisha miradi mikubwa mitatu mkoani Mtwara kwa wakati na akalitaka Shirika kuendelea na kasi hiyo bila kuathiri rasilimali za Shirika. Kulia anayeshuhudia ni Meneja wa NHC Mtwara, Angela Magazi.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , William Vangimembe Lukuvi akikagua makabati ya nyumba za makazi za Shangani.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , William Vangimembe Lukuvi akisikiliza maelezo ya Renald Kazoba wa Shirika la Nyumba Mtwara juu ya maendeleo ya ukamilishwaji wa ujenzi wa Jengo la Biashara la RahaLeo Commercial Complex lililopo eneo la Rahaleo Mtwara, . Kushoto anayeshuhudia ni Meneja wa NHC Mtwara, Angela Magazi.
 Jengo la Biashara la RahaLeo Commercial Complex lililopo eneo la Rahaleo Mtwara.

  Jengo la Biashara la RahaLeo Commercial Complex lililopo eneo la Rahaleo Mtwara.
  Jengo la Biashara la RahaLeo Commercial Complex lililopo eneo la Rahaleo Mtwara.
  Jengo la Biashara la RahaLeo Commercial Complex lililopo eneo la Rahaleo Mtwara.
  Jengo la Biashara la RahaLeo Commercial Complex lililopo eneo la Rahaleo Mtwara.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , William Vangimembe Lukuvi akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa NHC Mtwara. akiwa huko Waziri Lukuvi amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa kwa kukamilisha miradi mikubwa mitatu mkoani Mtwara kwa wakati na akalitaka Shirika kuendelea na kasi hiyo bila kuathiri rasilimali za Shirika. 
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , William Vangimembe Lukuvi akikaribishwa na Meneja wa NHC Mtwara, Angela Magazi. akiwa huko Waziri Lukuvi amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa kwa kukamilisha miradi mikubwa mitatu mkoani Mtwara kwa wakati na akalitaka Shirika kuendelea na kasi hiyo bila kuathiri rasilimali za Shirika.