Wednesday, April 30, 2008

Masikini mtoto azikwa


Mtoto aliyechinjwa alipewa sumu ya panya


WAKATI mwili wa mtoto, Salome Yohana (3) aliyefariki dunia kwa kutenganishwa kichwa na kiwiliwili, umezikwa jana katika makaburi ya Tabata/Segerea kwa Bibi, Kaimu Kamishina wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Liberatus Barlow, amesema mtoto huyo alipewa sumu ya panya kabla ya kuchinjwa kichwa chake.

Kamishna Barlow alisema inasadikiwa mtoto huyo aliuawa kwa sumu kabla ya kutenganishwa kichwa na kiwiliwili na Ramadhani Mussa (18) ambaye anadaiwa aliondoka nyumbani kwao Tabata akiwa na kisu, panga na sumu ya panya.

Alisema baada ya Ramadhani kufanya tukio hilo hakurudi tena nyumbani hadi alipokamatwa na polisi akiwa na kichwa cha mtoto.

Barlow alisema mtuhumiwa Ramadhani aliendelea kutozungumza, lakini alionyesha eneo alilofanya mauaji hayo, mita chache kutoka katika nyumba aliokuwa marehemu siku hiyo ya tikio.

Aliongeza kutokana na kauli ya mama mzazi wa mtuhumiwa, Khadija Ally na utata uliopo juu ya kifo cha mtoto huyo, vipimo zaidi vimechukuliwa na ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi wa kina. Habari hii ya Festo Polea.

Tuesday, April 29, 2008

bongo noma kichizi




Mambo ya bongo kiboko kila kitu kwa foleni, magari foleni shuleni folleni hadi nyumbani foleni hebu nambieni picha hii ya mdau Deus Mhagale inaonyesha msongamano mkubwa katika mitaa ya Jamhuri

Habari Njema



Habari za leo wadau,
Ule wakati tulio usubiria sasa umefika, Website ya pekee itakayo jishughulishaktk kuutangaza muziki wa Tanzania ipo jikoni na ina karibia kuiva.

Unataka kusikiliza muziki wa nyumbani? Basi watembelee wajuzi wa fani hiikupitia
www.mkmusicgalaxy.com kwa miziki mipya na ya kizamani uburudike na roho yako.

Kumbuka, hawa ndio walewale wakiokupaga raha siku za nyuma na mambo ya mahusiano.com. sasa wamekuja upya!!

Nawatakia siku njema.


Kind Regards,

Support Department

MK MUSIC GALAXY - Exploring the Tanzanian Music.

Part of MK GROUP OF COMPANIES (T) LTD - http://www.mkgroupltd.com
Tel: +44 - 752 - 792 - 9234

Uchaguzi Chuo Kikuu UDSM wadorora



Jackson Odoyo na Christopher Maregesi wa Mwananchi

KUTOKUWEPO kwa jina la mgombea urais wa serikali ya wanafunzi (DARUSO) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Odong’ Odwar raia wa Uganda aliyekuwa akikubalika na wanachuo walio wengi, baada ya jina lake kuondolewa katika kinyang’anyiro hicho kwa madai kuwa hakuwa na sifa ya kuwa chuoni hapo kimesababisha wanafunzi wengi kususia uchaguzi huo.

Pamoja na wanafunzi wengi kususia uchaguzi ila wachache waliojitokeza kupiga kura waliongozwa na wasichana, huku wavulana wengi wakionekana kuvinjari sehemu mbalimbali katika vituo vya kupigia kura chuoni hapo bila kupiga kura.

Hata hivyo ilielezwa kuwa sababu kubwa iliyofanya wavinjari katika vituo hivyo ni kuwabainisha wenzao ambao walidhaniwa kuwa wangekaidi na kusaliti msimamo wao.

Mwitikio wa uchaguzi haukuwa mkubwa baada ya wapiga kura wengi kukataa kupiga kura kwa kile walichodai kuwa mgombea waliyekuwa wanamtaka hakuwepo hivyo hawakuwa na sababu ya kupiga kura kumchagua mtu asiye chaguo lao.

Hata hivyo kulikuwa na kampeni ya chinichini chuoni hapo iliyolenga kuzua wanafunzi kutopiga kura ingawa baadhi yao walionekana wakivinjari katika vituo vya kupigia kura bila kupiga kura. Kwa habari zaidi soma Mwananchi kesho.

Sunday, April 27, 2008

Mshindi wa kisura wa Tanzania


emmy melau toka a-taun mshindi wa shindano la face of tanzania lililofanyika usiku huu hoteli ya moevenpick, dar, akifurahia baada ya kutwa taji

tano bora ya face of tanzania kabla ya kupanda jukwaani. hapo aliyeshinda ni emmy (pili shoto)

shindi wa pili yvonne ramomi toka zenj (kulia) na mshindi wa tatu edna makanzo wa dar (shoto)

Friday, April 25, 2008

Tabata Dampo mambo yao tambarare



TUME iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro, kuhakiki uhalali wa viwanja vya waathirika wa bomoabomoa ya Tabata Dampo kabla ya kulipwa fidia, imeanza kazi jana.

Akizungumza na wahanga hao jana, Mwenyekiti wa tume hiyo Michael Ole Mungaya alisema, utekelezaji wa zoezi hilo unakwenda sanjari na kupiga picha waathirika hao wakiwa wamesimama kwenye viwanja vyao.

Ole Mungaya alisema, Wanatarajia kazi hiyo itamalizika ndani ya siku mbili na waathirika watapatiwa barua maalum, zikiainisha uhalali wa umiliki wa nyumba kwa kuzingatia namba ya leseni za makazi na picha ya mmiliki halali wa kiwanja husika.

"Fedha zao zitakapoanza kutolewa, walipaji watakuwa na nakala za walipwaji... hivyo wakifika ofisini, fomu zao zitalinganishwa na zilizopo kwenye kumbukumbu zetu, kama kutakuwa hakuna shida watapatiwa hundi zao,"alisema Ole Mungaya.

Waliotimuliwa Chuo kikuu Warejeshwa


Waliotimuliwa Chuo Kikuu warejeshwa

Na Tausi Mbowe wa Mwananchi

BAADHI ya wanafunzi waliofutiwa udahili na kufukuzwa masomo kutokana na kufanya vurugu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamerudishwa chuoni hapo baada ya uongozi wa chuo hicho kumuomba Waziri wa Elimu kubatilisha uamuzi wake wa awali.

Awali serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, mwishoni mwa wiki ilitangaza kuwafutia udahili wanafunzi 38 na kutangaza kuwa hawataruhusiwa kujiunga na chuo chochote nchini pia alitangaza kutimuliwa kwa wengine 300.

Uamuzi huo uliotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, katika kikao cha Bunge kilichokuwa kikiketi mjini Dodoma.

Wanafunzi 38 wa chuo hicho ambao walidaiwa kuongoza vurugu, walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na shitaka ya kula njama na kusababisha fujo.

Taarifa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, iliyosainiwa na Makamu Mkuu wa Chuo, Professa Rwekaza Mukandala ilisema kuwa uongozi wa chuo umefikia hatua hiyo kutokana na hali halisi inayoendelea chuoni hapo ambapo mpaka sasa kumeshindikana kupatikana kwa hali ya amani.

Professa Mkandala alisema kutokana na hali hiyo uongozi wa chuo umeamua kumuomba Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi kubatilisha uamuzi wake wa awali na badala yake wanafunzi hao washughulikiwe kutokana na sheria za chuo kama zinazoonyesha.

Kwa mujibu wa Professa Mukandala, Waziri Maghembe amekubaliana na ombi la uongozi wa chuo hicho na kwamba wanafunzi hao watashughulikiwa kulingana na sheria za chuo na wale wasio na hatia wataruhusiwa kuendelea na masomo kama kawaida. kwa taarifa za kina soma Mwananchi la kesho.

Akudo Impact








Muziki wa dansi hapa nchini hivi sasa umeonekana kuvaa sura mpya kutokana na kupendwa zaidi na watu tofauti na awali. Kumekuwa na bendi kadhaa hapa nchini ambazo zimekuwa zikivuma sana huku zikijipatia mashabiki lukuki.

Bendi hiyo hivi sasa inaitwa Akudo Impact ambayo ina muda wa mwaka mmoja lakini imeweza kujipatia umaarufu mkubwa kutokana na vipaji vilivyo jaa katika bendi hiyo.

Bendi inaongozwa na Taksis Masela ambaye ni makamu kiongozi mkuu aliyewahi kuimba katika bendi ya Felix Wazekwa anasema bendi ina jumla ya wanamuziki 19. pia wapo Taxis Masela Jqoto ambaye nilikuwa BCBG, Zegre Butamu ambaye alikuwa BCBG, Alan Kabasele ambaye alikuwa Empire Bakuba ( ya Lofombo) nao waliungana kuunda Akudo. Nwijac alimkuta kwa Fere gola, Canal Top aliyekuwa kwenye bendi ya Wenge BCBG ya JB Mpiana,

Yupo mpiga gitaa la solo Mechant imbwa mukali kutoka katika bendi ya Wenge El Paris , De Kanto mpiga gitaa la bass kutoka Extra Muzika. Buffalo Maziwi aliyetokea BCBG ambaye anapiga ngoma".

Wanenguaji wake ni kiboko wacheki Nasi ambaye alikuwa mnenguaji kutoka katika bendi ya Koffie Olomide, Shushuu nae kutoka kwa Coffie na Faally. Josline aliyetoka kwa Empire Bakuba ya Djuna Mumbafu, Karen kwa Redy Amis.
Kiongozi mukulu kabisa ni Christian Bella maarufu kama 'Tajiri ya Masauti'' Bendi hiyo hivi sasa inajiandaa na uzinduzi wa albamu yake ya kwanza. Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Mei 16 mwaka huu, katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Hebu pata burudani hii kutoka Harieth Makweta wa Mwananchi usome kwa kina.

Thursday, April 24, 2008

Waliofanya vurugu Chuo Kikuu Dar watimuliwa



Na Waandishi wa Mwananchi

SERIKALI imetangaza kuwafutia udahili na kuwafukuza masomo wanafunzi waliofanya vurugu katika huo Kikuu cha Dar es Salaam.

Taarifa ya serikali iliyosomwa bungeni jana vioni mjini hapa na Waziri wa Elimu na na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, ilieleza kwa kifupi kuwa wanafunzi hao wapatao 39 na wengine 300 walioshiriki maandamano wa chuo hicho wamefutiwa udahili na hawataruhusiwa kujiunga na chuo chochote nchini.

“Waliofanya vujo leo (jana) wamefutiwa udahili na kufukuzwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na hawataruhusiwa kujiunga na chuo chochote,” alisema Profesa Maghembe katika taarifa hiyo bungeni saa 11.30.

Profesa Maghembe alisisitiza msimamo wa serikali kuwa haitawavumilia watu wanaofanya uhalifu na vurugu badala ya kusoma.

Adhabu hiyo imewakumba wanafunzi 39 waliodaiwa kuwa vinara mgomo ulianza Jamatatu wiki hii ili kuushinikiza uongozi wa chuo hicho kuwarudisha chuoni wenzao 15 waliofukuzwa awali kwa tuhuma kama hizo.

Mgomo huo ulifuatwa na vurugu zilizozuka juzi chuoni na kusababisha uongozi wa chuo kutoa taarifa polisi ambao waliwadhibiti wanafunzi hao na kuwakamata baadhi yao huku wengine wakiumizwa vibaya kwenye mapambano hayo. Pichani wanafunzi wa Chuo Kikuu wakigangamala wakitaka wenzao warejeshwe. Picha ya mdau Faraja Jube.

Wednesday, April 23, 2008

Kwaheri Ditopile





Kikwete aongoza mazishi ya Ditopile

RAIS Jakaya Kikwete jana aliongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Marehemu Ukiwaona Ditopile Mzuzuri (60) yaliyofanyika kwenye makaburi ya familia yao huko Kinyerezi, jijini Dar es Salaam.

Marehemu Ditopile alifariki dunia ghafla Aprili 20 katika Hoteli ya Hilux, iliyopo mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akimwelezea marehemu, msemaji wa famili ambaye ni mdogo wa marehemu, Abdallah Ramadhani Ditopile alisema kaka alikuwa ni nguzo ya familia yao kwa kipindi chote cha uhai wake hivyo kifo chake kimeacha pengo kubwa lisiloweza kuzibwa.

Akitoa salamu za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Katibu wa chama hicho ambaye pia ni Waziri wa Michezo na Utamaduni, Kapteni George Mkuchika alisema mbali na kumfahamu marehemu wakiwa shuleni, alimfahamu zaidi kutokana na uadilifu wake kazini katika nyadhifa mbalimbali alizoshika.

Katika uhai wake, Ditopile aliwahi kuwa mbunge wa Ilala kwa miaka 10, Katibu Mwenezi wa CCM, Mkuu wa Mkoa Dar es salaam, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mkuu wa Mkoa Pwani, Naibu wa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Wakati wa dua ya kumuombea marehemu inasomwa nyumbani kwake, viongozi mbalimbali wa serikali walihudhuria wakiongozwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete.

Hata hivyo, msiba huo ulitawaliwa na utani wa hapa na pale kati ya kabila la Wandengereko ambalo ni kabila la marehemu na kabila la Wanyamwezi na wasukuma ambao ni watani wa kabila hilo.

Katika hali hiyo ya utani, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya na aliyekuwa Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge waliombwa kwenda kula chakula cha watani ulioandaliwa kwa niaba yao msibani.

Baada ya hapo mwili wa marehemu ulipeleka katika Msikiti wa Tambaza kwa ajili ya kumuombea kuswaliwa na ilipomalizika swala hilo, ulipelekwa hadi katika makaburi Kinyerezi kwa kupitia barabara ya Umoja wa Mataifa, Morogoro, Mandela na Tabata Segerea.

Wakiwa katika makaburi hayo, mamia ya waombolezaji waliongozwa na Rais Kikwete waliweka mchanga katika kaburi la marehemu. Pichani Rais Jikwete, Bilionea Chenge na waombelezaji wengine wakijumuika.

FFU watembeza mkongoto UDSM




Pichani baadhi ya wanafunzi walioshiriki mgomo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana wakiwa mikononi mwa polisi, picha za mdau Salhim Shao

Na Pius Rugonzibwa wa Citizen

ASKARI polosi wa Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia (FFU) wametembeza mkong'oto kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliodaiwa kuchochea fujo na kuwahimiza wenzao kugomea masomo chuoni hapo.
Wanafunzi hao walipata kipigo hicho jana mchana na kusababisha baadhi yao kuumia na wengine kukamatwa kwa kusababisha fujo chuoni.
Kuitwa kwa askari hao kulitokana na wanafunzi hao kuendesha mgomo siku mbili kwa madai ya kutaka wenzao waliosimamishwa masomo warejee chuoni bila masharti.
Juhudi za uongozi wa chuo kuwataka wanafunzi hao warejee madarasani zalishindikana hiyo kuulazimu utawala kutoa taarifa Jeshi la Polisi kuomba msaada ndipo FFU walifika na kutembeza mkong'oto wa nguvu.
Kabla ya kipigo hicho kuanza, wanafunzi hao waliogoma walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali kushinikiza wenzao waachiwe ikiwa ni pamoja na wimbo wa taifa na kutoa hotuba za kuhamasisha
“Hatuwezi kuendelea na mosomo wakati wenzetu wako nje, huu utakuwa usaliti. Tukubaliane pamoja na tuungane kuwarudisha wenzetu vinginevyo hakieleweki hapa,” walisikika baadhi ya wanafunzi wakisema.
Rais wa Serikali ya wanafunzi chuoni hapo (Daruso), Deo Daudi, alisema wanafunzi wengi hawataki kufuata utaratibu katika kudai haki zao, hivyo kusababisha hali hiyo.

Tuesday, April 22, 2008

Bongo Dar es Salaam


Dar kila mtu yuko bize na mambo yake na kila mmoja anasaka kile anachokitaka wakati mwingine vitu humfuata mtu badala ya mtu kufuata vitu, hebu cheki wabongo hapa wanavyochangamkia viwalo.
Kilio cha samaki machozi yanakwenda na maji, hapa pichani mkazi wa jiji la Dar es salaam anaonekana akiwaandaa samaki tayari kwa kuwauza, picha zote kwa niaba ya mdau wa blogu hii.

Monday, April 21, 2008

Utupaji taka hovyo


Hebu angalia uchafuzi wa mazingira ulivyo ndani ya miji yetu, watu wanatupa vitu popote wanapotaka, hali hii haipendezi na ndiyo inayorudisha maendeleo ya afya ya jamii yetu nyuma.

Sunday, April 20, 2008

Chenge ajiuzulu


SIKU chache baada ya kuandamwa na tuhuma za kumiliki mabilioni ya shilingi katika akaunti yake ya nje katika kisiwa cha Jersey, Uingereza Mbunge wa Bariadi Magharibi na Waziri wa Miundo Mbinu, Andrew Chenge amejiuzulu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia Mwananchi usiku jana, Waziri Chenge aliwasilisha barua ya kujiuzulu kwa Rais Jakaya Kikwete muda mfupi baada ya Rais kuwasili nchini.

Kujiuzulu kwa Waziri Chenge kulithibitishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu ambaye alisema kuwa rais amekwishaipokea barua ya kujiuzulu kwa Chenge na amemkubalia na akasema huo ndiyo uamuzi wa busara na ndiyo aliokuwa akusubiria.

"Rais amepokea barua ya Waziri Chenge na ameshamjibu akisema uamuzi huo ndiyo alikuwa akiusubiri,"alisema Rweyemamu alipozungumza na Mwananchi.

Taarifa za kujiuzulu kwa Waziri Chenge zilianza kusikika tangua subuhi ya jana, lakini zikawa hazijathibitishwa hadi zilipopatikana jana jioni.

Uamuzi huo unakuja siku chache baada ya Waziri Chenge kukataa kujibu tuhuma zinazomkabili za kumiliki mabilioni ya fedha nje ya nchi na kuwakimbia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, huku taarifa zingine zikidai kuwa aliomba radhi kwa Watanzania akidai kutojua kiswahili.

Chenge ambaye anatuhumiwa kumiliki dola za Marekani 1 milioni (Sh1.2 bilioni) katika mazingira tata, alifikia hatua hiyo baada ya kukataa kujibu maswali ya waandishi wa muda mfupi baada ya kufunga Mkutano wa Kimatiafa nchi 19 duniani kuhusu Udhibiti wa Vitendo vya Uharamia na Uvamizi dhidi ya Meli zinazopita katika Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi, uliofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, jijini Dar es Salaam, Aprili 14-18, mwaka huu.

Mara baada ya kufunga mkutano huo, alitoka nje ya ukumbi wa mkutano na mwandishi wa gazeti hili alimfuata na kumwomba kufanya naye mahojiano lakini alimkatalia.

Tuhuma dhidi ya Chenge za kujilimbikizia fedha hizo, ziliibuliwa na gazeti la The Guardian linalochapishwa nchini Uingereza katika toleo lake la Jumamosi wiki iliyopita ambalo lilieleza kuanza kwa uchunguzi dhidi yake, kutokana na akaunti yake kukutwa na zaidi ya dola za Marekani 1 milioni.

Ditopile afariki dunia

Hii ya Braza Dito ilipigwa sioku nyingi zilizopita na Faza Kidevu.

Taarifa zilizotufikia hivi sasa zinasema kuwa Mwanasiasa machachari Ukiwaona Ramadhani Mwishehe Ditopile Mzuzuri amefariki dunia huko Morogoro akiwa anaangalia Televisheni katika hoteli akisumbuliwa na maradhi ya kisukari pichani mwili wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa tabora,Ditopile Mzuzuri ukipakiwa katika gari tayari kupelekwa katika chumba cha kuifadhia maiti cha hospitali ya mkoa wa Morogoro. Picha na Juma Ahmedi, Morogoro) taarifa zaidi mtaendelea kuzipata kadri tunavyozipata.

Friday, April 18, 2008

Zitto huyooo Marekani




U.S. Ambassador to Tanzania Mark Green wishes Hon. MP Zitto Kabwe a
"safari njema" following their meeting at the U.S. Mission in Dar es
Salaam, on Thursday, April 17, 2008. MP Kabwe is traveling to the U.S.
on the prestigious International Visitor Program: Leadership Development
for Young Political Leaders.

Thursday, April 17, 2008

Bilionea Chenge ndani ya Dar


Akiondoka n akurejea VIP baada ya kumalizana na waandishi.


Baadae huyoo akatimua zake kuendelea na mpambano wa shutuma hizo zilizosisimua watu nchini. Picha hizi ni za mdau Mpoki Bukuku.

WAZIRI wa Miundombinu, Andrew Chenge amerejea nchini jana akitokea China na kusema kuwa mambo yote anaachia vyombo vya uchunguzi ili kuthibitisha tuhuma za rushwa dhidi yake.

Alisema katika Uwanja wa ndege wa Dare s Salaam leo alasiri kuwa akiwa mwanasheria hawezi kuzungumzia shutuma ambazo bado ziko katika hatua ya uchunguzi.

"Unapotuhumiwa, uchunguzi unafanyika, kwa kanuni na taratibu za uchunguzi, siruhusiwi kuzungumza. Kwa sasa ni mapema mno, tuvipe nafasi vyombo vya uchunguzi vifanye kazi yake,"

"Hoja ya msingi hapa ni kwamba, nimelipwa fedha na Kampuni ya BAE System (ya Uingereza) katika ununuzi wa rada. Tuhuma hiyo ni nzito kweli kweli na siyo ya kuropoka,"

“wakimaliza uchunguzi wao then wakuliza Bw. Chenge hivi vijisenti ulivipateje ndipo ntaeleza,”

Tuhuma dhidi ya Chenge za kujilimbikizia fedha hizo, ziliibuliwa na gazeti la The Guardian la Uingereza, ambalo lilieleza kuanza kwa uchunguzi dhidi ya waziri huyo baada ya wachunguzi kukuta na zaidi ya dola za Marekani milioni moja (sh bilioni moja za kibongo).

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai nchini humo ya Serious Fraud Office (SFO), inatarajia kuanza upya kufanya uchunguzi kuhusu fedha hizo, ili kuangalia iwapo zina uhusiano wowote na zile zinazoaminika kutolewa kwa njia ya rushwa wakati Tanzania iliponunua rada ya kijeshi kutoka nchini humo kwa paundi za Uingereza milioni 28, ambazo ni sawa na Sh 70 bilioni, mwaka 2002.

Sunday, April 13, 2008

Baraza jipya la mawaziri Kenya


Baraza jipya la mawaziri lililotangazwa jioni hii ni hili hapa

Office of the President

Ministry of State for Provincial Administration and Internal Security
Minister: Prof George Saitoti
Assistant Ministers: Simon Lesirma and Joshua Orwa Ojode

Ministry of State for Defence
Minister: Yusuf Haji
Assistant Ministers: David Musila and Joseph Nkaisserry

Office of the Vice President
Vice President and Minister for Home Affairs: Stephen Kalonzo Musyoka
Assistant Minister: Lorna Laboso

Ministry of State for Immigration and Registration of Persons
Minister: Gerald Otieno Kajwang’
Assistant Minister: Francis Baya

Ministry of State for National Heritage & Culture:
Minister: William ole Ntimama
Assistant Minister: Joel Onyancha Omagwa

Office of the Prime Minister:
Prime Minister: Raila Amollo Odinga
Assistant Minister: Alfred Khang’ati

Ministry of State for Planning, National Development and Vision 2030:
Minister: Wycliffe Ambetsa Oparanya
Assistant Minister: Peter Kenneth

Ministry of State for Public Service:
Minister: Dalmas Anyango Otieno
Assistant Minister: Aden Ahmed Sugow

Office of Deputy Prime Minister and Ministry of Trade:
Deputy PM and Minister for Trade: Uhuru Kenyatta
Assistant Minister: James Omingo Magara

Office of the Deputy Prime Minister and Ministry of Local Government
Deputy PM and Minister for Local Government: Wycliffe Musalia Mudavadi
Assistant Minister: Robison Njeru Githae

Ministry of East African Community
Minister: Amason Kingi Jeffah
Assistant Minister: Peter Munya

Ministry of Foreign Affairs
Minister: Moses Wetangula
Assistant Minister: Richard Momoima Onyonka

Ministry of Finance
Minister: Amos Kimunya
Assistant Minister: Dr. Oburu Oginga

Ministry of Justice, National Cohesion and Constitutional Affairs
Minister: Martha Karua
Assistant Minister: William Cheptumo Kipkorir

Ministry of Nairobi Metropolitan Development
Minister: Mutula Kilonzo
Assistant Minister: Elizabeth Ongoro Masha

Ministry of Roads
Minister: Kipkalya Kones
Assistant Ministers: Wilfred Machage and Lee Kinyanjui

Ministry of Public Works
Minister: Chris Obure
Assistant Minister: Dickson Wathika Mwangi

Ministry of Transport
Minister: Chirau Ali Makwere
Assistant Minister: John Harun Mwau

Ministry of Water and Irrigation
Minister: Charity Kaluki Ngilu
Assistant Minister: Mwangi Kiunjuri

Ministry of Regional Development Authorities
Minister: Fredrick Omulo Gumo
Assistant Minister: Judah Katoo ole Metito

Ministry of Information & Communications
Minister: Samuel Poghisio
Assistant Ministers: George Munyasa Khaniri and Dhadho Godhana

Ministry of Energy
Minister: Kiraitu Murungi
Assistant Ministers: Charles Keter and Maalim Mohamud Mohamed

Ministry of Lands
Minister: Aggrey James Orengo
Assistant Ministers: Silvester Wakoli Bifwoli and Samwel Gonzi Rai

Ministry of Environment and Mineral Resources
Minister: John Michuki
Assistant Ministers: Ramadhan Seif Kajembe and Jackson Kiplagati Kiptanui

Ministry of Forestry and Wildlife
Minister: Noah Wekesa
Assistant Minister: Josphat Koli Nanok

Ministry of Tourism
Minister: Mohamed Najib Balala
Assistant Minister: Cecily Mtito Mbarire

Ministry of Agriculture
Minister: William Samoei Ruto
Assistant Ministers: Japhet Kareke Mbiuki and Gideon Musyoka Ndambuki

Ministry of Livestock Development
Minister: Mohamed Abdi Kuti
Assistant Minister: Bare Aden Duale

Ministry of Fisheries Development
Minister: Paul Nyongesa Otuoma
Assistant Minister: Mohamed Abu Abuchiaba

Ministry of Development of Northern Kenya and other Arid Lands
Minister: Ibrahim Elmi Mohamed
Assistant Minister: Hussein Tarry Sasura

Ministry of Cooperatives Development
Minister: Joseph Nyagah
Assistant Minister: Linah Jebii Kilimo

Ministry of Industrialisation
Minister: Henry Kiprono Kosgey
Assistant Minister: Ndiritu Murithi

Ministry of Housing
Minister: Peter Soita Shitanda
Assistant Minister: Bishop Margaret Wanjiru Kariuki

Ministry of Special Programmes
Minister: Dr. Naomi Namsi Shabani
Assistant Minister: Mohamed Muhamud Ali

Ministry of Gender and Children Affairs
Minister: Esther Murugi Mathenge
Assistant Minister Atanas Manyala Keya

Ministry of Public Health and Sanitation
Minister: Beth Wambui Mugo
Assistant Minister: Dr. James Ondicho Gesami

Ministry of Medical Services
Minister: Prof. Peter Anyang’ Nyong’o
Assistant Minister: Danson Buya Mungatana

Ministry of Labour
Minister: John Kiyonga Munyes
Assistant Minister: Sospeter Ojamaa Ojamong’

Ministry of Youth and Sports
Minister: Dr. Helen Jepkemoi Sambili
Assistant Ministers: Wavinya Ndeti and Kabando wa Kabando

Ministry of Education
Minister: Samson Kegeo Ongeri
Assistant Ministers: Prof. Patrick Ayiecho Olweny and Andrew Calist Mwatela

Ministry of Higher Education, Science and Technology
Minister: Dr. Sally Jepngetich Kosgey
Assistant Ministers: Kilemi Mweria and Asman Abongotum Kamama

Office of the Attorney General
Attorney General: Amos Wako

Mwenge wa Olympiki



Tanzanian Vice President Ali Mohammed Shein holds the Olympic torch in Dar es Salaam April 13, 2008. The Indian Ocean port hosted the Tanzanian leg of the Olympic torch relay this weekend. REUTERS



Under-Secretary-General of the United Nations and Executive Director of the United Nations Human Settlements Programme Tibaijuka holds the Olympic torch in Dar es Salaam

Kipigo kikali


E bwaana watu wakiibiwa siku hizi hawana subira hutafuta tairi matofali na kila kitu ili mradi kuhakikisha wanaangamiza yule aliyepora, tabia hii imeenea sana na wakati mwingine huwakumba watu wasio na hatia na huuawa, je msomaji unafikiriaje, huyu jamaa alikutwa pale IFM anachomoa mali za watu amepigwa gadi basi. Picha ya mdau Deus Mhagale.

Friday, April 11, 2008

mkataba wa TICTS wa kifisadi



Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabuza Serikari, Ludovick Utouh akitoka nje ya ukumbi
wa bunge Dodoma mara baada ya ripoti za hesabu za serikari za mitaa na hesabu za
serikari kuu za mwaka ulioishia tarehe 30 june 2007 kuwasilishwa jana bungeni. Picha
na Edwin Mjwahuzi.

Na Ramadhan Semtawa aliyepo Dodoma

RIPOTI ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali hadi Juni 2007 imetoka kwa kuanisha ufisadi katika ofisi mbalimbali za umma, na kuonyesha mkataba mpya kati ya Kampuni ya Kupakua Shehena za Kontena Bandarini (TICTS) na Mamlaka ya Bandari (TPA), haukufuata taratibu za kisheria.

Hatua ya mkabata huo wa TICTS kuhusishwa na ufisadi ndani ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambaye kisheria ndiye mkaguzi wa hesabu za umma, kunazidi kuthibitisha taarifa za siku nyingi kwamba, mchakato mzima wa kuongezea mkataba wa awamu ya pili kwa Kampuni hiyo umetawaliwa na ufisadi kutokana na kutofuata taratibu za zabuni.

Akisoma ripoti hiyo mjini hapa jana CAG, Ludovick Utouh, alisema maoni ya ofisi ni kwamba hatua ya kuongeza mkataba kwa TICTS kabla ya kumalizika wa awali imekiuka taratibu za Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004, ambayo inahuisisha pia zabuni. Kwa taarifa zaidi soma Mwananchi.

Thursday, April 10, 2008

Kazi ya Jeshi kugangamala



Hebu mcheki huyu mdada alivyorusha mguu hewani, hakika kaiva ipasavyo, hii ilikuwa majuzi hapo jirani ya nchi yetu Kenya wakati askari wapya walipopass out hakika wameiva hebu nambie, hapo mwananchi mkaidi utaona ndani. Picha kwa niaba ya gazeti la Nation la Kenya

Mshindi ya Bongo Star Search


Jamani Misoji oooh Misoji ni Misoji tuu eti kashinda Bongo Star Search mengi yamesemwa na yataendelea kusemwa lakini historia imeshajiandika huyu ndo mshindi hebu mcheki hapa alivyopendeza na outfit yake

Wednesday, April 09, 2008

Wabunge wapya



Mbunge wa Kiteto,Mh Benedict Ole Nangoro akila kiapo cha uaminifu bungeni Dodoma jana mjini Dodoma baada ya kushinda uchaguzi katika jimbo jilo hivi karibuni.. Mbunge wa kuteuliwa, Al- Shaymaa Kwegyir akila kiapo kuwa mbunge mbele ya spika wa bunge la jamhuri wa Tanzania, Mh Samwel Sitta,mjini Dodoma jana.Picha Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu


Mbunge wa kuteuliwa, Al- Shaymaa Kwegyir akiapa kuwa mbunge mbele ya spika wa bunge, Samwel Sitta, mjini Dodoma leo
Picha za Edwin Mjwahuzi

Sunday, April 06, 2008

Serikali yawapigia magoti wafanyakazi TRL

* Yaikopesha zaidi ya Sh3.6 bn kuongeza mishahara
* Wafanyakazi sasa kulipwa mishahara mipya





HATIMAYE Serikali imeingilia kati mgomo wa wafanyakazi wa Kampuni ya Reli nchini (TRL), uliosababisha kusitishwa kwa huduma za usafirishaji wa reli ya kati baada ya kuikopesha kampuni hiyo kiasi cha Sh 3.6 bilioni kwa ajili ya kuongeza mishahara ya wafanyakazi wake.

Uamuzi huo wa serikali, umewafurahisha wafanyakazi hao na kutangaza kusitisha mgomo wao mara moja na kurudi kazini baada ya madai yao ya kutaka kulipwa mshahara wa Sh 160,000 kwa kima cha chini kupatiwa ufumbuzi.

Akizungumza na wafanyakazi hao kwenye makao makuu ya kituo cha reli cha kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema serikali imelikopesha zaidi ya Sh3.6 bilioni ili liweze kuwalipa wafanyakazi hao mishahara hiyo mipya kwa kipindi cha miezi mitano.

Mwandishi Mkongwe afariki dunia



Marehemu John Mndolwa

MWANDISHI Mwandamizi na Mratibu waHabari na Matukio wa televisheni yaITV na Radio One, John Mndolwa (46),amefariki dunia leo alfajiri majira ya saa 10 baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kwa mujibu wa habari zilizotolewa naMkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One, Joyce Mhaville, marehemu Mndolwa alilazwa hospitali ya Kairuki kwa wiki moja. Kifo chake kimesababishwa na shinikizo la damu.

Mndolwa ambaye alizaliwa Novemba 9,1962 mkoani Tanga alianza kazi za uandishi mwaka 1980 katika Idara ya Habari ya Radio Tanzania (RTD) na aliajiriwa na ITV na Radio One Julai 1994.
Mipango ya mazishi inaendelea kufanyika. soma zaidi habari hii ya kuhuzunisha kwa kwenda lukwangule.blogspot.com

Mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu - AMINA/AMEN

Friday, April 04, 2008

Maiti iliyogombewa Dar yazikwa


Na Jackson Odoyo wa Mwananchi

HATIMAYE mwili wa marehemu Paul Goliama (40) umezikwa na ndugu zake ambao ni waumini wa dini ya Kikristo badala ya waumini wa Kiislamu katika makaburi ya Sinza, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi jana, Shemeji wa marehemu, Ibrahim Msumari, alisema mazishi ya marehemu Goliama yalifanyika jana majira ya saa 8:00 mchana katika makaburi ya Sinza, jijini Dar es Salaam kwa amani na utulivu.

Msumari alisema baada ya kutoka katika eneo la mazishi, watu wote walielekea nyumbani kwa marehemu walipoweka matanga ili kuungana na ndugu jamaa na marafiki wa familia ya marehemu.

Machi 28, ulizuka mzozo mkubwa wa kugombea maiti hiyo baina ya waumini wa dini hizo huku kila upande ukidai kuwa ndiye mwenye haki ya kuizika maiti hiyo.

Mzozo wa huo ulidumu kwa zaidi ya saa tano katika Kanisa la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Jimbo la Kinondoni Usharika wa Sinza muda mfupi baada ya mwili wa marehemu kupelekwa kanisani hapo kuombewa sala za mwisho kabla ya mazishi.

Baada ya jitihata na busara za Mchungaji wa Kanisa hilo, Tuheri Tuheri pamoja na Imamu wa Msikiti wa Safwa za kujaribu kusuluhisha mzozo huo zilishindikana, Jeshi la Polisi iliamua kuuchukua mwili huo na kuurudisha katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam mpaka mahakama itakapotoa maamuzi kuhusu dini ambayo ilistahili kumzika marehemu.


Machi 31, ndugu wa marehemu waliamua kwenda kufungua kesi katika Mahaka ya Kinondoni kudai kuuzika mwili huo ambapo juzi mahakama ilitoa uamuzi kuwa mwili huo uzikwe na ndugu zake.

Sababu kubwa iliyosababisha ya mwili huo kugombewa na dini mbili ni kutokana na marehemu kubadili dini mwaka 2004 kutoka Ukristo kwenda Uislamu na hatimaye mwaka 2006 akabadili tena toka Uslamu kurudi Ukristo.

migodi yafuguliwa Mererani

Na Mussa Juma wa Mwananchi Mererani

SERIKALI imeruhusu shughuli za uchimbaji kuendelea katika migodi ya madini ya
Tanzanite ya Mererani wilayani Simanjiro katika maeneo ya kitalu C
kinachomilikiwa na wawekezaji wa Tanzanite One na kitalu D baada ya kufungwa
kutokana na maafa yaliyotokana mafuriko ya maji na kuuwa zaidi ya wachimbaji 64.

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Henry Shikifu alitangaza uamuzi huo jana wakati
akizungumza na waandishi wa habari na wachimbaji katika kikao kilichofanyika kituo
cha polisi katika machimbo ya Tanzanite Mererani.

Katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa pia na Naibu waziri wa Nishati na madini,
Adam Malima, Shekifu hata hivyo alisema uchimbaji wa migodi katika eneo la kitalu
B utaendelea kufungwa hadi hapo kamati ya maafa itakaporidhika na kuopolewa miili
ya wachimbaji wadogo wote waliofariki na kukamilika kwa zoezi ya kuboresha migodi
mingine katika kitalu hicho.

Uamuzi huo, wa kufunguwa migodi ya kitalu C na D na kuendelea kuifunga migodi ya
kitalu B ambayo ndiyo imeathirika sana na maafa hayo kunatokana na mapendekezo ya
Rais Jakaya Kikwete alipotembelea migodi hiyo na kuitaka kamati ya maafa ya
kufanyatathimini na kuhakikisha katika kipindi cha siku tatu wanafungua migodi
hiyo.

Awali serikali ilitangaza kusitisha zoezi hilo Jumapili iliyopita kupitia kwa
Waziri wa Madini na Nishati William Ngeleja ili kupisha zoezi la kuopoa miili ya
wachimbaji waliokufa kwa mafuriko hayo.

Katika agizo lake Waziri Ngeleja alisema wanafunga migodi ili wachimbaji wote
waelekeze nguvu zao katika zoezi la kuokoa miili na maisha ya wenzao waliokumbwa
na maafa.

matata ya Mererani




Pichani juu mmoja wa waokoaji Alfonce Silayo (kushoto) akimwelza mmiliki wa mgodi Fred Mbwambo (kulia) hali ilivyo ndani ya mgodi na jinsi zoezi la kutoa miili iliyoonekana jana jioni ilivyokuwa gumu , picha inayofuata sehemu ya umati wa wachimbaji wadogo wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete alipozungumza nao jana wakati Rais alipotembelea eneo hilo la maafa
na chini kabisa Catapilar za kampuni ya TanzaniteOne zikiwa kazini kutengeneza upaya mtaro wa maji na kuziba sehemu yam taro huo iliyobomoka na kuleta maafa kwa wachimbaji. Picha kutoka kwa mdau Athumani Khamis wa Daily News.

Posted: 06:43, Tuesday, April 1, 2008

Tuesday, April 01, 2008

Kwa waliopita Tabora Boyz



P

Picha hizi nimezifuma kwa Mdau Issa Michuzi iliwakililishwa kwake na mdau mmoja hivi karibuni, shule hii ni maalumu ya kijeshi. Aliyeiwakilisha kwa michuzi ni alisoma pale mwaka 1997-1999. Mimi nilikuwapo kule mwaka 1993-95.

Picha hizi imetukumbusha mengi wadau mambo ya A and B coy, unyuka, afande Majambo, dada zetu wa warsaw,redo, kuengua, nguchiro, nguna, bweni la A-level la SINA aka 'Sleeping Is Not Allowed', Mwl. Mkumba, Mwl. Mwombeki bila kusahau Afande Peter, Afande Warioba, Afande Chacha na wengineo.