Thursday, December 17, 2015

WAZIRI KITWANGA AMUAGA NAIBU WAZIRI WA USALAMA WA RAIA WA CHINA UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM

32
Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang (kushoto) akimshukuru kwa kukaribishwa vizuri nchini pamoja na ushirikiano waliofanya baada ya kusaini kusaini Hati ya Makubaliano mwanzoni mwa wiki hii katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam.
33
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang (kushoto) wakati alipomsindikiza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumuaga kiongozi huyo wa China. Naibu Waziri huyo wa China na Waziri Kitwanga, mwanzoni mwa wiki hii walisaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya wizara hizo mbili. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil.
34
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akifurahi jambo na Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang (kushoto) wakati walipokuwa wanaagana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.. Naibu Waziri huyo wa China na Waziri Kitwanga, mwanzoni mwa wiki hii walisaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya wizara hizo mbili.
31
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akimuaga kwa kumpungia mkono Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang (kushoto ndani ya gari) wakati kiongozi huyo wa China akiwa anaondoka mara baada ya kumaliza ziara yake nchini. Juzi Waziri Kitwanga na Naibu waziri huyo wa China walisaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika masuala mbalimbali ya Ulinzi na Usalama wa Raia kati ya Wizara hizo mbili, katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa Waziri Kitwanga ni Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi, Kamishna Thobias Andengenye.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
Post a Comment