Friday, May 31, 2013

REDD'S MISS LINDI 2013 KUPATIKA USIKU WA LEO

Washiriki wa Redd’s Miss Lindi 2013 katika picha ya pamoja ndani ya ufukwe wa Lindi Beach Resort
Redd’s Miss Lindi 2013 atajulikana Usiku wa leo 31 may,2013 ndani ya ukumbi wa Lindi Beach Resort. 

Jumla ya Warembo Kumi watachuana Vikali kugombania taji hilo. wanyange hao wako kambini Hotelini hapo kwa mazoezi makali huku wakiongozwa na Redd’s Miss Lindi 2012.

Mratibu wa Mashindano hayo Ndugu Justine alisema Mwaka huu wamejiandaa vizuri na warembo wako katika hali nzuri ya kiafya kambini hapo na Pia anataraji show itakuwa ya Kihistoria kwa jinsi maandalizi yalivyo andaliwa, hivyo amewataka wadau kujitokeza kwa wingi.
Viingilio vimetajwa kuwa viti vya kawaida siku hiyo vitakuwa Tsh 10,000/= na VIP itakuwa 15,000/= na tiketi zitaanza kuuzwa siku hiyo hiyo ya tarehe 31/05/2013 majira ya asubuhi Hivyo wahi tiketi yako mapema ili ushuhudie show ya kihistoria katika mambo ya urembo katika mji wa Lindi.

MREMBO WA REDD'S MISS TABATA 2013 KUPATIKANA LEO

Shindano la kumtafuta Miss Tabata 2013 linafanyika leo katika ukumbi wa Dar West Park Tabata. Warembo 20 watachuana kutaka kumrithi Noela Michael ambaye anashikilia taji hilo kwa sasa. Noela pia ndiye anashikiria taji la Miss Ilala.

Mbali ya kuwakilisha Miss Tabata kwenye shindano la Miss Ilala baadaye mwaka huu, mshindi huyo pia atazawadiwa Sh.600,000 pamoja na king’amuzi kutoka Multichoice ambacho kimelipiwa tayari kwa miezi mitatu kikiwa na thamani ya  Sh.400,000.

Mshindi pili atapata Sh. 300,000,  wa nne Sh.200,000 na wa tano  atazawadiwa Sh.150,000. Warembo wengine watakaofanikiwa kuingia 10 bora, watazawadiwa Sh.100,000 kila mmoja wakati waliosalia watapata kifuta jasho cha Sh.50,000 kila mmoja.

Warembo wanaoshiriki kinyang’anyiro hicho mwaka huu ni Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma Kibogoti (20), Upendo Dickson Lema (22), Hidaya David Mwenda (22), Aneth Ndumbaro (19),  Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Musa Kitereja (19),  Rehema Kihinja (20),  Pasilida Mandali (21), Brath Chambia (23), Joaniter Kabunga (21), Recho Mushi (20),Caroline Sadiki (20) na  Suzan Daniel (18).

Wadhamini wa shindano hilo ni Dodoma Wine, Redd’s Original, Nipashe, Vayle Springs, Multichoice, Fredito Entertainment, Integrated Communications Limited, CXC Africa, Brake Point na Saluti5.

Miss Tabata 2013 imeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.

MATOKEO YA KIDATO CHA SITA { ACSEEE } 2013


MATOKEO YA KIDATO CHA SITA { ACSEEE } 2013

BONYEZA LINK HAPO CHINI KUANGALIA MATOKEO


f Matokeo ya kidato cha sita (ACSEE) 2013 - Link 1
f Matokeo ya kidato cha sita (ACSEE) 2013 - Link 2

KINANA, NAPE WAENDELEA KUMWAGA CHECHE MKOANI NJOMBE

Mkuu wa Wilaya ya Makete,Mh Josephine Matiro akimuongoza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake,mapema leo mchana alipokuwa akikagua uhai wa mashina ya chama hicho katika kijiji cha Tandala,Wilaya ya Makete mkoani Njombe.Kinana na ujumbe wake wako ziarani mkoani Njombe katika kuimarisha shughuli za chama,kuangalia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi wa CCM na pia kuzungumza na Wananchi kuhusiana na matatizo yao mbalimbali yanayowakabili .
Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi Ndugu Abdulrahman  Kinana akizungumza na Wananchi wa kata ya Iniho mapema leo jioni ndani ya wilaya ya Makete mkoani Njombe,Kinana alizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara mambo mbalimbali ikiwemo na kuwahakikishia wananchi kuwa Serikali itaendelea kutekekeleza miradi yake yote iliyoahidi ikiwemo ya barabara,maji na umeme,aidha aliwataka wananchi kubeza baadhi ya vyama vya siasa vinanvyoeneza chuki kwa watanzania na kuindosha amani iliyopo.Kinana akiwa sambamba na ujumbe wake ameyazungumza hayo wilayani Makete katika kijiji cha Ukwama ikiwa siku ya nne ya ziara yake mkoani Njombe kutembelea mashina ya chama hicho pamoja na kufanya mikutano ya hadhara kueleza serikali ilichotekeleza.
Katibu  wa Itikadi na Uenezi Taifa  Nape Nnauye  akimtambulisha aliyekuwa mwanachama wa CHADEMA, Keffa Lupiana pichani kushoto kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye kata ya Iniho,Wilaya  ya Makete mkoani Njombe.
Mbunge wa Jimbo la Makete na Naibu Waziri wa Maji Dkt.Binilith Mahenge akieleza mambo mbalimbali ya kimaendeleo yaliyofanywa jimboni  mwake katika kutekeleza Ilani ya CCM kwenye mkutano wa .
 
 Sehemu ya Wananchi wakishangilia jambo wakati ndugu Kinana alipokuwa akizunngumza nao kwenye mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa shule ya msingi ya ukwama mapema leo jioni ndani ya wilaya ya Makete mkoani Njombe .
 
  Sehemu ya Wananchi wakiwa kwenye uwanja wa kata ya Ukwama wakimsubiri Ndugu Kinana  azungumze nao mapema leo jioni ndani ya wilaya ya Makete mkoani Njombe.
Ndugu Kinana akisalimiana akisalimiana Chifu wa kabila la Wakinga,Godfrey Mwemusi Sanga,mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye uwanja wa ukwama,wilaya ya Makete mkoani Njombe,shoto ni Katibu  wa Itikadi na Uenezi Taifa  Nape Nnauye 
 Sehemu ya hali ya hewa ya Wilaya ya Makete kama ionekavyo jioni ya leo. Picha na JIACHIE BLOG.

TANGAZO LA KIFO CHA MZEE MAKWAIA

Marehemu Felician M. Makwaia
Ndugu, CHRISTOPHER MAKWAIA (MK) Anasikitia kutangaza kifo cha Baba yake mzazi Mzee Felician M. Makwaia, kilichotokea jana May 30, 2013 huko Bombay nchini India alikokuwa amekwenda kwa matibabu baada ya 
kupambana kwa muda mrefu na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.

Mipango ya kusafirisha mwili kuurejeshwa nyumbani kwa mazishi inafanyika. Msiba upo nyumbani kwa marehemu Sinza Mori,Jijini Dar es Salaam.

Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo.
Tutaendelea kuwafahamisha hatua kwa hatua ya kiatakachoendelea katika msiba huu mzito.

Kwa mawasilian0 ya aina yoyote piga simu namba
0659 528446

BWANA ALITOA , NA BWANA AMETWAA
JINA LAKE NA LIHIMIDIWE

AMIN

Rais Kikwete awapandisha vyeo maafisa wa Polisi Kuwa Makamishna na Manaibu Kamishna

BAJETI 2013/14 YA JUMUIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI (EAC) YASOMWA LEO UGANDA

 Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Africa Mashariki kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya (EAC) ambaye pia ni Waziri wa Africa Mashariki kutoka Uganda, Shem Bageine (mwenye mkoba wa bajeti)  akiwa na Mawaziri wenzake kutoka Rwanda, Burundi, Tanzania pamoja na Katibu Mkuu wa EAC, Dk. Richard Sezibera  na Naibu Katibu Mkuu anaeshughulika na masuala ya Fedha na Utawala. Leo Bajeti ya Fedha ya mwaka 2013/14 ya Jumuia hiyo imesomwa Bungeni nchini Uganda.
 Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Africa Mashariki kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya (EAC) ambaye pia ni Waziri wa Africa Mashariki kutoka Uganda, Shem Bageine akisoma Bajeti ya Jumuia hiyo leo
Kikao cha Bunge la Jum,uia ya Afrika ya Mashariki kikiendelea nchini Uganda leo.

SOMA MATOKEO MAPYA YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012 HAPA

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa-QT.
--

f

Matokeo ya kidato cha nne (CSEE) 2012 - KIUNGANISHI CHA 1


f

Matokeo ya kidato cha nne (CSEE) 2012 - KIUNGANISHI CHA 2


f

Matokeo ya kidato cha nne (CSEE) 2012 - KIUNGANISHI CHA 3


f

Matokeo ya kidato cha nne (CSEE) 2012 - KIUNGANISHI CHA 4

Thursday, May 30, 2013

Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NHC

 Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NHC wakifuatilia kwa karibu mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiendelea jijini Tanga kwenye Hoteli ya Tanga Beach Resort. Mkutano huo ulitanguliwa na Semina ya Manunuzi ya Watendaji wa NHC iliyofanyika kati ya May 22 na 25.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Hamad Abdallah akizungumza na wajumbe wa  kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NHC kilichofanyika Hoteli ya Tanga Beach Resort
Wajumbe wa kikao hicho cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NHC wakifuatilia kwa karibu mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiendelea jijini Tanga kwenye Hoteli ya Tanga Beach Resort
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Goodluck Ole Medeye akifungua   kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NHC kilichofanyika Hoteli ya Tanga Beach Resort.
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NHC wakifuatilia kwa karibu mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiendelea jijini Tanga kwenye Hoteli ya Tanga Beach Resort.

Wajumbe wa kikao hicho cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NHC wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Hoteli ya Tanga Beach Resort.
 Wajumbe wakijadiliana

Wednesday, May 29, 2013

NHC bungeni Dodoma

Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Raymond Mndolwa wa Tawala na Uendeshaji wa Mikoa na Hamad Abdallah wa Usimamizi wa Miliki wakitafakari jambo nje ya ukumbi wa Bunge kabla ya kuingia ndani ambapo bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Meneja wa NHC mkoa wa Dodoma, Itandula Gambalagi na Hamad Abdallah, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki na Raymond Mndolwa wa Tawala na Uendeshaji wa Mikoa pamoja na Meneja Huduma kwa Jamii wa NHC, Muungano Kasibi Saguya wakitafakari jambo nje ya ukumbi wa Bunge kabla ya kuingia ndani ambapo bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
 

Katibu Mkuu wa Chama cha Wapangaji Tanzania (TTA), Ndumey Mukama, akizungumza jambo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Profesa Anna Tibaijuka, wanaoshuhudia ni Muungano Saguya na Hermes Mutagwaba wa NHC.

Tuesday, May 28, 2013

SHIRIKA LA NYUMBA LAINGIA MIKATABA NA BENKI TANO LEO KWA AJILI YA MIKOPO YA NYUMBA KWA WATEJA


CEO wa DCB Edmund  Mkwawa (kushoto) akisani makubaliano na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Felix Maagi baada ya kuingia makubaliano ya mkopo wa nyumba kwenye hafla iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa BancABC, Boni Nyoni (kushoto) akipeana mkono na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Felix Maagi baada ya kuingia makubaliano ya mkopo wa nyumba kwenye hafla iliyofanyika leo jijini Dar es SalaamCEO wa MGen Tanzania Charles Sumbwe akibadilisha faili na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Felix Maagi baada ya kuingia makubaliano ya mkopo wa nyumba kwenye hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. 

Viongozi wa benki za DCI, NIC, CRDB, BancABC na MGen Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kutia saini makubaliano

Viongozi wa mabenki na shirika la Nyumba wakiwa kwenye picha ya pamoja

Wadau wakifuatilia kwa makini jinsi mambo yanavyokwenda
BENKI nne za jijini Dar es Salaam, zimesaini makubaliano na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ajili ya kuwakopesha wananchi fedha za kununulia nyumba zinazojengwa na shirika hilo.
Makubaliano hayo yalisainiwa jijini Dar es Salaam leo kati ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NHC, Felix Maagi na viongozi wakuu wa benki hizo.

Benki zilizosaini makubaliano hayo ni DCB, ABC, NIC pamoja na Benki ya CRDB.
Akizungumza wakati wa makubaliano hayo, Maagi alisema yamefanyika kama sehemu ya mwendelezo wa taasisi za fedha kushirikiana na NHC kuwafanya wananchi wamiliki nyumba.
“Kama mtakumbuka, mwaka juzi tulisaini makubaliano na mabenki manane kwa ajili ya kuwasaidia wananchi kuweza kumiliki nyumba.

“Kwa faida ya wale ambao hawakuwapo wakati tunasaini makubaliano ya kwanza, ni kwamba tulisaini na Benki za Azania, BOA, CBA, Exim, KCB, NBC, NMB na Benki ya Stanbic.
“Kwa maana hiyo, kitendo cha kusaini makubaliano na mabenki haya manne leo ni mwendelezo wa utaratibu wetu wa kushirikiana na taasisi za fedha katika kuwakomboa wananchi, hasa hasa katika umiliki wa nyumba,” alisema Maagi.     

Kwa mujibu wa Maagi, lengo la shirika hilo ni kuwafanya wananchi waachane na tabia ya upangaji, badala yake wawe na uwezo wa kumiliki nyumba zinazojengwa na kuuzwa na shirika hilo kupitia mikopo inayotolewa na benki mbalimbali.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Bima ya MGen Tanzania, Charles Sumbwe, ambaye kampuni yake imesaini mkataba na NHC kwa ajili ya kuwadhamini wananchi wa kipato cha chini ili nao waweze kumiliki nyumba, alisema kampuni yake imelazimika kusaini mkataba huo, baada ya kuguswa na tatizo la wananchi wengi kutokuwa na uwezo wa kumiliki nyumba.
“Moja ya majukumu ya kampuni yetu ni kuwasaidia wananchi, kwa hiyo, tumeamua kujitosa katika kuwadhamini wananchi wenye uwezo mdogo kifedha ili nao waweze kumiliki nyumba kama ilivyo kwa wenye nazo,” alisema Sumbwe