Thursday, August 24, 2017

KAMATI YA MAWASILIANO NA UJENZI YA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR YAVUTIWA NA UTENDAJI WA NHC

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza na ujumbe wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliofika katika Shirika la Nyumba la Taifa kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya ujenzi, teknolojia mpya na mikakati ianayowezesha kufanyika kazi kwa kasi zaidi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza na ujumbe wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliofika katika Shirika la Nyumba la Taifa kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya ujenzi, teknolojia mpya na mikakati ianayowezesha kufanyika kazi kwa kasi zaidi. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, ambaye ni mwakilishi wa Jimbo la kwa Mtipura, Mhe:Hamza Hassan Juma. Katika Maelezo yake Mheshimiwa Hamza Juma alipongeza utendaji wa kasi wa NHC na kusema ndicho kitu kikubwa kilichowavutia kama Wazanzibari kufika NHC kujifunza na kuchukua fursa hiyo kulipongeza Shirika kwa mchango wake mkubwa wa kuliasisi Shirika la ZHC.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, ambaye ni mwakilishi wa Jimbo la kwa Mtipura, Mhe:Hamza Hassan Juma, akizungumza wakati ujumbe wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar hiyo ulipofika katika Shirika la Nyumba la Taifa kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya ujenzi, teknolojia mpya na mikakati ianayowezesha kufanyika kazi kwa kasi zaidi. 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, ambaye ni mwakilishi wa Jimbo la kwa Mtipura, Mhe:Hamza Hassan Juma, akizungumza wakati ujumbe wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar hiyo ulipofika katika Shirika la Nyumba la Taifa kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya ujenzi, teknolojia mpya na mikakati ianayowezesha kufanyika kazi kwa kasi zaidi. 
Baadhi ya Watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa wakifuatilia kwa karibu maelezo yaliyokuwa yakitolewa katika mkutano huo jana mchana.
Wajumbe wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia maelezo katika mkutano huo.
Wajumbe wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia maelezo katika mkutano huo.
Baadhi ya Watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa na wengine kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na vyombo vya habari wakifuatilia kwa karibu maelezo yaliyokuwa yakitolewa katika mkutano huo jana mchana.
Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Issack Peter akitoa maelezo ya miradi kwa ujumbe wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliofika katika Shirika la Nyumba la Taifa kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya ujenzi, teknolojia mpya na mikakati ianayowezesha kufanyika kazi kwa kasi zaidi.
Wajumbe wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia maelezo katika mkutano huo.
Baadhi ya Watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa na wengine kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na vyombo vya habari wakifuatilia kwa karibu maelezo yaliyokuwa yakitolewa katika mkutano huo jana mchana.
Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Issack Peter akitoa maelezo ya miradi kwa ujumbe wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliofika katika Shirika la Nyumba la Taifa kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya ujenzi, teknolojia mpya na mikakati ianayowezesha kufanyika kazi kwa kasi zaidi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, ambaye ni mwakilishi wa Jimbo la kwa Mtipura, Mhe:Hamza Hassan Juma, akizungumza na vyombo vya habari nje ya mutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza na vyombo vya habari wakati Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliofika katika Shirika la Nyumba la Taifa kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya ujenzi, teknolojia mpya na mikakati ianayowezesha kufanyika kazi kwa kasi zaidi.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza na vyombo vya habari wakati Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliofika katika Shirika la Nyumba la Taifa kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya ujenzi, teknolojia mpya na mikakati ianayowezesha kufanyika kazi kwa kasi zaidi.

Wednesday, August 23, 2017

WAJUMBE WA CPA TAWI LA TANZANIA WAKUTANA NA WAJUMBE WA CPA TAWI LA CANADA JIJINI DAR ES SALAAM

   Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya  Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Tanzania Dkt Raphael Chegeni (katikati) akiongoza kikao wakati Wajumbe wa Kamati hiyo walipokutana na Wajumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada  katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam mapema leo.
 Mwenyekiti  wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada  Mhe. Yasmin Ratansi (wa kwanza kushoto) akisisitiza jambo wakati Wajumbe wa Chama hicho kutoka Canada walipokutana na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya  Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Tanzania katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam mapema leo.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Mhe. Yasmin Ratansi akimkabidhi  zawadi Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya  Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Tanzania Dkt Raphael Chegeni mara baada ya Wajumbe wa pande zote mbili kuzungumza mapema leo katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati Tendaji ya  Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Tanzania katika picha ya pamoja na Wajumbe wa   Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada mara baada ya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
        (Picha na Ofisi ya Bunge)

DKT. PALLANGYO AONGOZA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI ZIARA KATIKA MIRADI YA GESI LINDI

Msimamizi wa Uzalishaji na Ujenzi katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Said Ngongoki akielezea jinsi uzalishaji unavyofanyika kiwandani hapo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti mara walipofanya ziara kiwandani hapo
Meneja Rasilimaliwatu kutoka katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Msafiri Figa ( wa kwanza kulia) akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika eneo la uzalishaji la kiwanda hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) akibadilishana mawazo na mwakilishi kutoka Idara ya Biashara katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Emily Wu (kulia) katika eneo la uzalishaji la kiwanda hicho.
Mtaalam kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Dominick Ngunyali (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya jinsi gesi inavyopokelewa katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika eneo la kupokelea gesi hiyo
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mbele kulia) akiongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwenye ziara katika eneo la Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani.
Meneja Rasilimaliwatu kutoka katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Msafiri Figa (kushoto) akielezea jinsi udongo wa aina mbalimbali unavyochanganywa katika hatua za awali za maandalizi ya utengenezaji wa vigae (tiles) kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akitoa maelekezo kwa Mhandisi wa Mitambo katika Kituo za Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi cha Somangafungu kilichopo mkoani Lindi, Edwin Konyani katika ziara hiyo.
Msimamizi wa Bomba la Gesi Upande wa Umeme katika Kituo cha Kupokea Gesi kutoka Songosongo na Madimba Joseph Msafiri (katikati) akielezea jinsi  gesi inavyopokelewa katika kituo hicho kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika ziara hiyo.
Sehemu ya Kituo cha Kupokea Gesi kutoka Songosongo na Madimba kilichopo Somangafungu mkoani Lindi.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ameongoza Kamati y Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika maeneo mbalimbali yenye miradi ya gesi katika mkoa wa Lindi lengo likiwa ni kuona utekelezaji wa miradi hiyo. 

Kati ya maeneo waliyotembelea ni pamoja na Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa kutumia Gesi Asilia cha Somangafungu, Makutano ya Bomba la Gesi Asilia (Somangafungu) mkoani Lindi pamoja na eneo linalotarajiwa kujengwa Mitambo ya Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG) lililoko katika Manispaa ya Lindi.

RAZA AMWAGA ZAWADI MICHEZO YA MASKULI MIKOA


Mwenyekiti wa ZAT ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mhe. Mohammedraza Hassanali akimkabidhi kalkuleta Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Omar Ali Bhai kwa ajili ya washindi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa skuli za mikoa yote ya Unguja na Pemba inayotarajiwa kuanza Septemba 12, 2017 katika uwanja wa Amaan Mjni Unguja. 
Mkurugenzi Idara ya Michezo na Utamaduni Hassan Khairalla Tawakal akitoa shukurani kwa Mhe. Raza kwa msaada alioutoa kuwazawadia washindi wa michuano ya mpira wa miguu kwa skuli za mikoa ya Zanzibar itakayofanyika mwezi ujao mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.
Mkurugenzi Idara ya Michezo na Utamaduni katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Hassan Khairalla Tawakal, akimtambulisha Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi wa wizara hiyo Omar Ali Bhai kwa Mwenyekiti wa kampuni ya ZAT Mhe. Mohammedraza Hassanali.

Na Salum Vuai, MAELEZO

MKURUGENZI wa kampuni ya usafiri wa anga na huduma za viwanja vya ndege Zanzibar (ZAT) Mohammedraza Hassanali, ametoa wito kwa kampuni na taasisi mbalimbali kuunga mkono juhudi za serikali kuimarisha michezo maskulini.

Akizungungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vitu mbalimbali kwa ajili ya zawadi za washindi kwenye mashindano ya mpira wa miguu mikoa ya Unguja na Pemba iliyofanyika nyumbani kwake Kibweni, Raza alisema ni wajibu wa kila Mzanzibari kusaidia sekta ya michezo.

Alifahamisha kuwa, iwapo wafanyabiashara wa Zanzibar wataunganisha nguvu kwa lengo la kuinua michezo kuanzia ngazi ya skuli ambako ndiko kwenye msingi wa vipaji vizuri, nchi hii itafika mbali kimichezo na kulitangaza vyema jina la Zanzibar. 

“Hii ninchi yetu sote, tuna wajibu kusaidia juhudi za serikali, na nimpongeze Mhe. Rais kwa kuteua Mkurugenzi makini na mwenye jitihada kuongoza Idara ya Michezo na Utamaduni,” alieleza Raza.

Raza ambaye pia ni Mwakilishi wa jimbo la Uzini, alisema hatachoka kutoa msukumo katika sekta ya michezo na misaada mingine ya kijamii, na vitu hivyo alivyotoa ni kutimiza ahadi yake aliyoitoa kabla mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Katika hafla hiyo, Mkurugenzi huyo alikabidhi vityu mbalimbali kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Omar Ali Bai kwa ajili ya zawadi za washindi na washirikiwenmgine wa mashndano hayo yaliyopangwa kuanza Septemba 12, 2017 katika uwanja wa Amaan.

Mkurugenzi Bai aliyemuwakilisha Katibu Mkuu wa wizara yake Bi. Khadija Bakari Juma, akimshukuru Mhe. Raza, alisema kuwekeza katika michezo maskulini ni jambo muhimu kwa kuinua ufahamu wa wanafunzi masomoni.

Alisema dhana za watu wanaodhani mchezo inarejesha nyuma maendeleo ya masomo sio sahihi, kwani ushahidi duniani unaonesha wanafunzi wengine mahodari wamekuwa wakijikita kucheza michezo mbalimbali.

“Akili nzuri hutoka kwenye mwili wenye afya ambao kujengeka kwake kunatokana na mtu kujishughulisha katika michezo ambayo wataalamu wanasema ni sehemu bora kwa makuzi ya watoto”, alieleza.

Alimuahidi mfadhili huyo kwamba vitu vyote alivyovitoa vitafika kwa walengwa, huku akiwaomba wananchi wengine wenye uwezo, makampuni na wafanyabsiahara mbalimbali kushirikiana ili Zanzibar irejeshe hadhi yake michezoni ambayo kwa miaka ya karibuni imeonekana kutetereka.

Mapema, Mkurugenzi wa Idara ya Michezo na Utamaduni katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, alimshukuru Raza kwa moyo wake wa uzalendo, na kuwa tayari kutumia mali zake katika kujenga ustawi wa nchi.

Alisema kuwa Rais Dk. Shein amepania kwa dhati kuendeleza michezo kama anavyofanya katika mambo mengine, na akamsifu Raza kwa kuwa kiungo kizuri kati ya idara yake wanafunzi na watu wengine katika kuhakikisha michezo nchini inapiga hatua. 

Katika hafla hiyo, Raza alikabidhi kalkuleta za kisasa, madishi ya kuhifadhia chakula na kalamu huku akiahidi kufanya mambo mengine makubwa kwa ajili ya kuwashajiisha washiriki wa mashindano hayo ya mikoa sita ya Unguja na Pemba.

MAHUJAJI WA TANZANIA WAANZA KUWASILI SAUDI ARABIA


Baadhi ya mahujaji wakionekana Uwanja wa Ndege baada ya kuwasili nchini Saudi Arabia kwa ajili ya swala ya Hija.
Mahujaji kutoka Tanzania wakiwa wamewasili nchini Saudi Arabia.
Baadhi ya Waislamu wanaoendelea kuwasili nchini hapa wakionekana pichani.

Na Mwandishi Maalum, Riyadh, Saudi Arabia.
Mahujaji kutoka Tanzania wameanza kuwasili nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kutekeleza nguzo ya tano ya dini ya kiislamu ya kuhiji Makkah inayofanywa na watu mbalimbali duniani, wakiwamo Waislamu kutoka Tanzania.
Ibada ya Hijja mwaka huu inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Agosti hadi mwanzoni mwa mwezi Septemba, huku jumla ya mahujaji 977 kutoka Tanzania wameshawasili katika miji ya Madina na Jeddah. Mahujaji hao waliwasili katika viwanja vya ndege vya Madina na Jeddah na kupokelewa na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania.

Tanzania kwa mwaka huu inataraijiwa kupeleka mahujaji wapatao 2,700. Indonesia ndiyo nchi inayoongoza kwa kupeleka mahujaji wengi mwaka huu inatarajiwa kuwa na mahujaji wapatao 168,000. Mwaka huu Saudi Arabia inatarajiwa kupokea mahujaji zaidi ya 2,000,000 kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni.

Maendeleo ya miundombinu: Nguzo ya uwezeshaji katika kufikia uchumi imara


Mkurungezi Mtendaji wa Buzwagi Gold Mine Bw; Stewart Hamilton akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi wa Uwanja wa ndege wa Buzwagi na pembeni yake ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu ambao kwa kwa kiasi kikubwa ACACIA wamewekeza katika kuboresha uwanja huo.

Wananchi wa Kahama wakishuhudia uzinduzi wa safari za ndege za shirika la Precision Air katika uwanja wa ndege wa Buzwagi.

Mazingira mazuri ya kukuza uchumi yanahitaji miundombinu bora inayowezesha uchukuzi huku ikiboresha uzalishaji na ufanisi. Hivi karibuni, wakazi wa Kahama na Shinyanga watafurahia safari za ndege kati ya Kahama na Dar es Salam. Haya ni matokeo ya ushirikiano wa Acacia Mining ulioanza toka mwaka 2008, ilipoanza uzalishaji katika mgodi wake wa Buzwagi; huku wakiendelea kuwekeza katika kiwanja cha ndege cha Kahama, wakihakikisha kiwanja kinatunzwa na kufanya kazi. 

Ushirikiano wa karibu kati ya Mkuu wa Wilaya Mh. Fadhil Nkurlu na Mgodi umewezesha kuanzishwa kwa safari za ndege za moja kwa moja. Safari za shirika la ndege la Precision zitapunguza adha ya usafiri ya wakazi wa Kahama na Shinyanga waliotakiwa kusafiri hadi Mwanza ili kupata usafiri wa ndege kuelekea Dar es Salaam.

 ‘Hii itasaidia sana kuongeza ufanisi katika muda na fedha zinazotumika katika usafiri,’ alisema mfanyabiashara Bw. Charles Thomas akiongeza kuwa safari ya barabara hadi Mwanza ingeweza kuchukuwa hadi masaa 6. Kufuatia mafanikio ya safari ya majaribio mwezi uliyopita, Meneja Mahusiano wa Kampuni wa shirika la ndege la Precision, Bw. Hillary Mremi alisifia hali ya kiwanja akisema, ‘njia ya ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Buzwagi ipo katika hali nzuri na matunzo yake ni mazuri; hii ni nzuri kwa usalama wa abiria na ndege zetu. 


Tunashukuru Acacia kwa kuwekeza katika kuboresha, kiwanja kidogo cha Buzwagi; hatua iliyoturuhusu kuanza safari kuelekea Kahama, zitakazo anza 5 September, 2017, tukiwa na safari tatu kwa wiki, na safari zikiongezeka zikitegemea mahitaji ya wasafiri. Hatua ya kutatua shida ya miundombinu ni moja itakayoleta matokeo chanya kwa biashara mkoani Shinyanga kwa kupunguza gharama za kuendesha biashara; huku ikiongeza faida.

Japokuwa Acacia imefanya uwekezaji wenye tija katika kuendeleza na kurekebisha kiwanja hiki kidogo cha ndege, ni muhimu kukumbuka kwamba kiwanja hiki ni mali ya Serekali chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). Uwekezaji katika kiwanja hiki kidogo inaonyesha nia ya Acacia kuendelea kusaidia jamii na taasisi zinazozunguka migodi yake.

Monday, August 21, 2017

CHAKUA YAOMBA UCHANGIAJI WA SH.200 KWA ABIRIA WANAOSAFIRI KWENDA MIKOANI

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
CHAMA cha Kutetea Abiria (Chakua) kimewaomba abiria wanaongia katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani  cha ubungo kutoa sh. 200 kwa ajili ya kusaidia chama hicho.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam,Mratibu wa chama hicho, Monday Likwepa amesema kuwa chama kimekuwa na msaada mkubwa kwa abiria hivyo chama kinahitaji kujiendesha na wadau ni abiria kuchangia kiwango hicho.

Amesema kuwa kiwango hicho  walichopanga kitasaidia kuendesha shughuli za ofisi pamoja na kuweza kushughulika na matatizo ya abiria pale wanapopata usafiri.

Likwepa amesema kuwa abiria wamekuwa wakipata matatizo na kukimbilia chakua hivyo kwa utaratibu wa kuchangia wanawajibu kudai haki zao pale wanapopata usumbufu.

Aidha amesema kuwa wataendelea kutoa elimu zaidi juu ya uchangiaji wa fedha hiyo katika kituo cha ubungo ili wananchi wajue  uchangiaji huo na pamoja na faida zake.
Mratibu Mtendaji wa Chama  Cha Kutetea Abiria(Chakua), Monday Likwepa akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuchangia abiria  wanaosafiri katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo sh.200 kwa ajili kuendesha shughuli za utetezi wa abiria pale anapopatwa na tatizo.Kushoto ni Mratibu mtendaji wa Chakua, Elias Kalinga na kulia ni Mwenyekit wa wa Taifa wa Chakua, Hassan Mchanjawa.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

POLEPOLE AKUTANA NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI NCHINI, LEO JIJINI DAR ES SALAAM


Masaidizi wa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Petro Magoti akimpokea Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Inmi Petterson, alipowasili ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Katibu wa NEC, Itikadi na Uwenezi, Humphrey Polepole, leo. (Picha zote na Bashir Nkoromo)