Thursday, December 24, 2015

NSSF KUKABIDHI DARAJA LA KIGAMBONI JANUARI 2016




Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi John Msemo akimuonesha Waziri muunganiko wa barabara zinazoingia katika daraja hilo. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni wakati waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, ambapo ujenzi wake utakamilika mwishoni mwa mwezi Januari mwakani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau (katikati) wakati alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Mradi ujenzi wa Daraja hilo. Mhandisi Kareem Mataka. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau (wa pili kulia), akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia), alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, ambalo ujenzi wake utakamilika Januari Mwakani. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau wakati alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo ambalo ujenzi wake utakamilika Januari Mwakani. 

Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau wakati ziara yake Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau akifafanua jambo.
Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza wakati alipofanya ziara katika Daraja la Kigamboni.
Sehemu ya Daraja la Kigamboni.
Waziri akipata maelezo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni.




WAZIRI wa Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama amelitaka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kuhakikisha linakabidhi daraja la Kigamboni ifikapo Januari, 2016.

Pia ametoa fursa kwa shirika hilo na mengine nchini kama yataweza kuja na mradi wa ujenzi wa daraja kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar.

Hayo alibainisha jana jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa daraja hilo, ambalo linatarajiwa kukamilika mwakani.

Alisema ujenzi wa daraja hilo, umegharimu kiasi cha Dola za Marekani 143.5, ambapo serikali imetoa asilimia 40, huku NSSF ikitoa asilimia 60 ya fedha zote.“Tunaliomba shirika hili, lihakikishe linaheshimu nha kuzingatia muda uliotoa katika kukabidhi daraja hilo mwakani licha ya kujitokeza ujenzi mwingine wa barabara ya Kilomita moja,”alisema.

Alisema shirika hilo linapaswa kulikabidhi daraja ifikapo Januari 30 au kabla ya muda huo, kwani ukamilifu wake utapunguza adha ya foleni na kukuza sekta ya uchumi inayotarajiwa kukuwa kwa kasi.

Katika hatua nyingine, Mhagama alisema endapo mradi ukiwa katika ubora na viwango vinavyotakiwa utadumu kwa muda mrefu na kuisaidia Seriali katika kukuza uchumi.

“Miradi ya namna itasaisdia kukuza uchumi wa ndani na nje ya nchi, pia inatufundisha kujifunza ili kujua kwamba tunaweza kuhimili miradi mingine mikubwa zaidi ya huu,”alisema.

Kuhusu daraja la kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar, alisema uwezekano wa kujengwa upo endapo mashirika yakijitokeza na mradi huo. “Kila kitu kinawezekana, hivyo kama Shirika litajitokeza serikali ipo tayari kwa kila kitu kuunga mkono mkakati watakao kuja nao,”alisema.

Naye Mkurungenzi wa NNSF, Dk.Ramadhan Dau alisema ujenzi wa daraja hilo umekuwa wa kasi licha ya matatizo yaliyojitokeza, hivyo Watanzania watarajie Januari mwakani kulitumia.

“Bado kuna sehemu nyingine ambazo tutamalizia ila hadi Januari litakuwa limekamilika kwa asilimia 100, hivyo tunaipongeza serikali kwa ushirikiano uliotuonyesha,”alisema

No comments: