Friday, October 30, 2009

Convocation ya Open University


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria, k. John Malecela (wapili kushoto) na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa, Tolly Mbwete (kushoto) katika mkutano wa wahitimu wa Chuo Kikuu Huria eneo la Biafra jijini Dar es salaam Oktoba 30, 2009. Kulia ni mkewe Tunu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Thursday, October 29, 2009

Balozi Mahiga apokea TUZO


Balozi wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Dkt Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Kamati ya Maadili na Masuala ya Kimataifa, na familia yake mara baada ya kutunukiwa Tuzo ya the Spirit of the United Nations" 2009" kulia kwa Balozi aliyeshika Tuzo ni Mke wake, Bibi Elizabeth Mahiga
Na Mwandishi Maalum
New York
Dkt Augustine Mahiga Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, amesema Tuzo aliyopewa imemwongezea ari na nguvu ya kujituma zaidi katika kutafuta amani, kutetea utu wa mwanadamu na haki za jamii na katika maeneo ambayo bado mambo hayo yanahitajika.

Ameyasema hayo wakati alipokuwa akitoa shukrani zake mara baada ya kutunukiwa tuzo ijulikanayo kama “The Spirit of the United Nations 2009” aliyotunukiwa mapema wiki hii jijini New York .

Kuhusu Tuzo hiyo aliyopewa, Balozi Augustine Mahiga mwanadiplomasia mzoefu katika Umoja wa Mataifa, anaielezea kuwa Tuzo hiyo kwamba, ni Tuzo ya Watanzania, Waafrika na wale wote wenye kuitakia dunia mema na kwamba yeye ni mpokeaji tu na mshikiliaji wa tuzo hiyo kwa niaba yao.

Akasema ataendelea kuzitafuta haki hizo za wanyonge kupitia Umoja wa Mataifa ambako anaamini kuwa mahali stahili kwa kuwa ndipo panapowakusanya kwa pamoja watu wenye fikra sawa na nia ya kuyafikia malengo mbalimbali yaliyowekwa na umoja huo.

“Umoja wa Mataifa ni chombo cha kilimwengu na cha kipekee ambapo nchi kubwa na ndogo zinakutana na kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano kama mataifa yaliyo sawa. Umoja wa Mataifa ni daraja linalounganisha tamaduni mbalimbali, rangi na imani katika kujenga utengamano , ushirikiano na maelewano ”

Tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwaka na Kamati ya Shirika la Maadili na Masuala ya Kimataifa , hutolewa kwa watu ambao msimamo na utendaji kazi wao katika Umoja wa Mataifa umekuwa ni kielelezo cha misingi na mwelekeo wa Umoja wa Mataifa.

Kamati ya Uteuzi ilieleza kuwa Balozi Mahiga amedhihirisha na kujitokeza kama mfano wa mtu anayeamini na kutekeleza misingi hiyo.
Tangu kuanza kutolewa kwa tuzo hiyo mwaka 2007, tayari imesha tolewa kwa mabalozi wawili wote wa Umoja wa Mataifa , wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na Taasisi zisizo za Kiserikali. Balozi Mahiga anakuwa Balozi wa kwanza kutoka Afrika kupata Tuzo hiyo.

Katika shukrani zake hizo, Balozi Mahiga akasisitiza kwamba Katiba ya Umoja wa Mataifa na Tamko la Haki za Binadamu, ni mihimili mikuu katika kukidhi nia ya mwanadamu katika kutafuta amani, maendeleo, haki, usawa na utu wa mwanadamu.

“ Hata wanao mkana Mungu hawawezi kuyapinga maadili haya ya msingi ambayo ni amani, haki za jamii, maendeleo ya mwanadamu na utu wa mtu, misingi ambayo Umoja wa Mataifa ndipo inaposimamia” akabainisha Balozi Mahiga.

Akawaeleza wageni waliohudhuria hafla hiyo kwamba katika miaka hiyo 17 akiwa mawana diplomasia ameshuhudia mambo mengi na ya kutisha yaliyomkumba mwanadamu.

Anayataja mambo hayo kuwa ni umaskini, vita na machafuko, watoto kulazimishwa kubeba silaha na kupigana , wanawake kudhalilishwa na mauaji ya halaiki na ya kimbari ya Rwanda.

“ Matukio haya ya kutisha niliyoyashuhudia katika utendaji wangu wa kazi, kwa njia moja yameniimarisha na kunifanya nielekeze nguvu zangu katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayomkabili mwanadamu kwa njia ya amani na kwa kutumia nguvu za pamoja za Kikanda, Umoja wa mataifa na watu wenye mapenzi mema.

Awali akitoa wasifu wa Balozi Augustine Mahiga , Mwenyekiti wa Taasisi iliyotoa Tuzo hiyo Bi Audrey Kitagawa, alimwelezea Balozi Mahiga kama mwanadiplomasia ambaye katika kipindi chake cha miaka 17 si tu amekuwa mstari wa mbele katika kutetea na kupigania haki za makundi mbalimbali ya jamii wakiwamo wakimbizi , wanawake na watoto lakini pia ameandika machapisho mbalimbali na kutoa mihadhara yenye mwongozo, ushauri na mapendekezo ya kukabiliana na madhira mbalimbali yanayomkabilia mwanadamu na dunia.

Miongoni mwa machapisho hayo ni Ushirikiano wa Kikanda na Utatuzi wa Migogoro ya Kivita, Upokonyaji wa Silaha na Maendeleo katika Afrika, Utatuzi wa migogoro na Usalama katika Afrika, Masuala ya wakimbizi , Haki za wanawake na watoto na ulinzi wa wananchi katika maeneo yenye vita na machafuko.

Karume arejea home toka majuu


Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraa la Mapinduzi Amani Abeid Karume na mkewe mama Shadya Karume wakiwa wameongozana mara baada ya kuteremka kwenye ndege ya shirika la ndege la British Airways wakitokea nchini Ufaransa aklikokwenda kuhudhuria mkutano wa Unesco ambao ulizungumzia kukuwa kwa elimu Duniani.

Rais Kikwete Azindua Mradi wa Umeme



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuzindua rasmi mradi wa umeme katika wilaya mpya ya Kilolo. Mradi huo unatekelezwa na wakala wa nishati vijijini (Rural Energy Agency) na unakadiriwa kugharimu Sh 1,665,600,000/-.

Tuesday, October 27, 2009

Day 51 on M-Net’s Big Brother Revolution



Day 51 on M-Net’s Big Brother Revolution sees the housemates relaxing as they come to terms with the fact that Biggie seems to have disappeared leaving the housemates with a note saying they’re on their own for now! Biggie also left behind a bright red telephone which connects the housemates to the Big Brother call centre but the operators are never available to take the call. How will the housemates cope without Biggie? Will Biggie be back? And will there be any new ‘housemates’ joining the game when Biggie returns? Tune in to Big Brother Revolution on DStv channel 198 or 199 and for more information, log on to www.mnetafrica.com/bigbrother.

Monday, October 26, 2009

Wachezaji wa Golf wanawake wa Tanzania


Wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya mchezo wa Golf, wakiwa wameshikilia makombe na ngao walizofanikiwa kizibeba baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa mashindano ya Afrika mashariki na Kati yaliofanyika Kampala , Uganda . Jumla ya nchi tano zilishiliki katika mashindano hayo ambazo ni Tanzania , Kenya , Zambia , Rwanda na wenyeji Uganda .

mambo ya uchaguzi serikali za mitaa


Uchaguzi katika Hospitali ya Serikali Segerea ulukiwa mzuri hakukuwa na shida yoyote ile, wapiga kura walifuata taratibu kama zilivyopangwa Picha ya mujydebubyz wa Foto Braza.

Day 49 on M-Net’s Big Brother Revolution


Day 49 on M-Net’s Big Brother Revolution saw the departure of Comrades-in-Arms Kristal ( Zimbabwe ) and Quinn ( South Africa ) plus performances from the energetic hip hop artist XOD. In addition, series presenter IK announced that the Comrades-in-Arms part of the series is over and housemates will once more play as individuals! With the series now past the halfway mark, the remaining ten housemates are in the hunt for the USD 200 000 grand prize as the tension and drama grows.

Visa 2 dance







TAMASHA ngoma za ubunifu linalofahamika kama Visa2 dance limemalizika, huku likiacha simulizi kwa watu wa mataifa mbalimbali hususani waliohudhuria.

vikundi tofautitofauti kutoka mataifa mbalimbali vimeshiriki tamasha hilo na kuonyesha mshikamano wa kipekee miongoni mwa wasanii na mashabiki wa ngoma hizo.

Mratibu wa tamasha hilo Aloyce Makonde amevitaja vikundi hivyo kuwa ni Kunja Dance Theatre na Jokajoka Dance (Kenya), FLUSSO dance Project na I'mperfect dancers (Italia),Dansgroep Amsterdam (Nertherland) Zufit Simon (Ujerumani) FACT (Afrika Kusini).

Vingine ni Jus De la vie (Sweeden) Aduga Community dance and Theatre Company ( Ethiopia) na Mionzi Dance Theatre, LumumbaTheatre Group na THT vya Tanzania.

Tamasha hilo limetanguliwa na warsha na mihadhara iliyoanza Jumatatu kwa wataalamu mbalimbali kuendesha mafunzo ya sanaa ya dansi ya ubunifu.
Warsha hizo zililenga utengenezaji wa jukwaa na matumizi ya taa, mavazi, historia ya dansi ya ubunifu, uhamasishaji na utawala wa sanaa dansi ya ubunifu.

Pia matumizi ya teknolojia kwenye dansi ya ubunifu ambazo zilitolewa na wataalamu wa humu nchini na nje ya nchi.

Makonde alisema: “ Visa 2 Dance ni tukio kubwa ambalo litatoa fursa kwa washiriki toka nchi mbalimbali kuonyesha umahiri wao kwa pamoja katika sanaa ya dansi.

“ Kupitia tukio hili wasanii wa Tanzania watapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kwenye uwanja wa sanaa wa kimataifa na watapata nafasi ya kujifunza na kubadilishana uzoefu.”

Makonde alisema kuwa tamasha la Visa 2 Dance linalenga kukuza vipaji miongoni mwa wasanii wa Tanzania na kuwapa uwezo wa kufikia malengo yao ya kisanii.

Baadhi ya malengo hayo ni pamoja na kuanzisha utaratibu wa kubadilishana uzoefu kupitia muziki, dansi na maigizo, kufungua mipaka ya kiutamaduni, kukuza mahusiano ya kimataifa na kuendeleza sanaa na utamaduni katika jamii ya Watanzania.

“ Mara ya kwanza tamasha hili lilifanyika mwaka jana na kushirikisha washiriki wa humu nchini. Mara ya pili lilifanyika mwaka jana ambapo idadi ya washiriki iliongezeka kufikia nchi 6 ambapo mwaka huu wan nchi 9 zilifanikiwa kushiriki tamasha hilo.
Imeandaliwa na Maimuna Kubegeya.

OBAMA AKITOKA KANISANI KUELEKEA IKULU


Sunday, October 25, 2009

Hebu cheki Rwasa alivyoibadilika



The former Burundian rebel leader, Mr Agathony Rwasa, who is now the general Director of National Social Security Institute (NSSI) in Burundi, received a certificate of attendance at the end of the 19th PPF members’ conference at Arusha International Conference Centre (AICC) last week. Presenting the certificate in Arusha regional commissioner, Mr Isdori Shirima who is flanked by (from right) PPF director general, Mr William Erio, chairman of PPF board of trustees, Mr Ramadhan Kijjah and board member whose name could not be obtained immediately. (Photo by A Correspondent)

Mama Nyoni atembelea THI


KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA NA STAWI WA JAMII MAMA BRANDINA NYONI AKISAINI KITABU CHA WAGENI MARA ALIPOWASILI KUTEMBELEA TAASISI YA MOYO TANZANIA MWISHONI MWA WIKI LENGO LA ZIARA HIYO NI KUJIONEA JINSI TAASISI HIYO INAVYOENDESHA KAZI ZAKE. SHOTO NI MWASISI WA TAASISI HIYO DR FERDINARD MASAU NA KULIA NI MGANGA MKUU KATIKA WIZARA YA AFYA DK DEO MTASIWA.

Friday, October 23, 2009

Mgamba avuna tuzo nyingine


Tanzanian Richard Mgamba (R) receives the Lorenzo Natali Journalism Prize for Africa from Mactar Silla, Chairman of the association of private producers and televisions of Africa , APPT, at a ceremony during the European Development days in Stockholm October 22 2009. Mgamba is awarded for his articles about albinos in Tanzania in The Guardian on Sunday. REUTERS/Bertil Ericson/Scanpix (SWEDEN MEDIA) SWEDEN OUT. NO COMMERCIAL OR EDITORIAL SALES IN SWEDEN

Kipawa wauziwa 'mbuzi kwenye gunia'






VURUGU ziliibuka jana kati ya wakazi wa Kipawa, uongozi wa Mamalaka ya Viwanja vya Ndege na Kamati ya malipo kwa wakazi wa Kipawa baada ya wakazi ya hao kuonyeshwa viwanja hewa wanavyotakiwa kuhamia.

Kamati ya malipo ya fidia kwa wakazi hao ilitangaza juzi kuwa jana ingefanya kazi ya kushughukia kesi za mirathi kwa wakzi hao pia kuwakabidhi viwanja wananchi ambao walikuwa hawajapata viwanja vyao.

Kazi ya kulipa fidai kwa wakazi hao wapatao 1,220 wa Kipawa ilianza Oktoba 15 mwaka huu lengo likiwa kuwalipa wakazi hoa ili waweze kuhama eneo hilo ambalo limechukuliwa na serikali kwa ajili ya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere.

Wakazi hao wapatao 300 walisafirishwa kutoka kwenye Bwalo la Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam hadi eneo la Pugu Mwakanga ambako walitarajia kwenda kukabidhiwa viwanja vyao wanavyotakiwa kuhamia mara baada ya kukamilisha utaratibu wa malipo ya fidia.

Tayari serikali imetoa notisi za siku 45 kwa wakazi hao na kwamba wanatakiwa kuwa wamaisha hama kupisha upanuzi huo wa uwanja wa Ndege pindi wanapokabidhiwa hundi zao.

Kabla ya kusafirisha kundi la watu hao mabishona makali kati ya maafisa kutoka mamlaka ya Viwanja vya Ndege na kamati ya malipo kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa walibishana kwa muda kuhusu utaratibu unaotakiwa kuitumika katika kuwakabidhi wananchi hao viwanja vyao.

Katika mabishano hayo Injiani Sechambo, William kutoka (TAA)aliwaambia wananchi hao utaratibu uliotakiwa kutumika kuwa wataanza kuwapeleka watu kwenye ameneo hayo kwa kufuata maeneo yalivyotengwa kutoka na kazi hiyo kufanywa na mthamani mmoja. Imeandikwa na Geofrey Nyang’oro.

Thursday, October 22, 2009

Chikawe azindua cheti kipya cha kuzaliwa


SERIKALI imebaini kuwa zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wanaoishi katika mikoa ambayo iko karibu na nchi jirani wanatumia vyeti vya kughushi kwa ajili ya shughuli zao mbalimbali.

Utafiti huo ambao umefanywa na wadau mbalimbali kwa kushirikiana na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA) ambapo wamebaini kuwa, wananchi hao wameghushi vyeti hivyo kwa ajili ya kupata hati ya kuzaliwa na vifo.

Akizungumza katika uzinduzi wa cheti kipya cha kuzaliwa chenye alama za usalama, uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alisema kuuwa, kutokana na hali hiyo serikali imejidhatiti kudhibiti hali hiyo.

Alisema mpaka sasa idadi ya watu wanaoishi na vyeti hivyo ni wengi, jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa wanakiuka sheria na taratibu za upatikanaji wa vyeti halali, kutokana na hali hiyo,wameandaa mkakati wa kuzunguka nchi nzima kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya matumizi ya vyeti bandia na kuwataka watafute vyeti halali kwa ajili ya shughuli zao.

“Tunajua kama kuna baadhi ya watu wanatumia vyeti bandia kwa ajili ya shughuli zao,ambavyo wamevipata kwa njia isiyo halali jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa wanavunja sheria,kutokana na hali hiyo tumeamua kubadilisha mfumo wa vyeti vya zamani na kutengeneza vya kisasa ambavyo vitatumia teknolojia na kompyuta ili kuwadhibiti watu wanaovighushi,”alisema Chikawe.

Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo vyeti vya zamani vitaendelea kutumika mpaka hapo watapopitisha sheria ya kuvibadilisha ili kila mmoja aweze kuwa na vyeti vya kisasa ambavyo ni vigumu kwa mwananchi wa kawaida kuvitengeneza.

Alisema kutokana na hali hiyo wananchi wenye tabia ya kughushi vyeti hiyo wametakiwa kuacha mara moja kwa sababu ni kos ala jinai ikiwa mtu atabainika maehusika katika zoezi zima la kughushi vyeti hivyo na kuchukulia hatua kaliza kisheria.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa RITA, Philip Saliboko alisema kuwa vyeti hivyo vipya vitaanza kutolewa leo katika ofisi za RITA zilizopo upanga jijini Dar es Salaam.

Wednesday, October 21, 2009

AG mpya aanza kazi kwa mkwara

Mwanasheria Mpya Jaji Frederick Mwita.
Seth Kamuhanda.



SIKU moja baada ya kuteuliwa na kisha kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali, Jaji Frederick Mwita Werema alisema atahakikisha kuwa taifa haliingii mikataba mibovu.

Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kuapishwa Ikulu jana, Werema alisema kwa msisitizo: "Rais aliyeniteua ndio anaujua msimamo wangu."

Werema aliyemrithi Johnson Mwanyika aliyestaafu kwa mujibu wa sheria, alisema kuwa atafanya kazi na kutekeleza wajibu wake mpya kulingana na kiapo alichokula mbele ya rais na Jamhiri ya Muungano wa Tanzania.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya kuapishwa, Mwanasheria Mkuu huyo alisema katika kutekeleza wajibu wake mpya hataki mashinikizo ya wanasiasa au mtu yoyote.

"Mashinikizo… Hayo yapo huwezi kufanya kazi bila hayo kuwepo; lakini aliyeniteua anajua msimamo wangu. ..Sitaki mashinikizo na sipendi kuhukumu bila ushahidi. Mnataka nirudie kiapo changu? Nawahakikishieni kuwa itafanya kazi kufuata kiapo changu," alisema Jaji Werema.

Alipoulizwa kuhusu kashfa ya kampuni ya Richmond (LLC) ambayo mtangulizi wake (Mwanyika) amehusishwa, Jaji Werema ambaye pia ni mtaalamu wa sheria za mikataba na biashara, alikata kulisemea hilo. Hata hivyo alisema hilo linafanyiwa kazi na wahusika.
Imeandikwa na Exuper Kachenje.

Rais Kikwete Mitambo ya IPTL kuwashwa

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAFANYABIASHARA na wawekezaji nchini katika kongamano la kujadili fursa za utalii nchini mjini Dar es Salaam, jana, Jumanne, Oktoba 20, 2009 walimwomba Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuingilia kati matatizo ya sasa ya mgawo wa umeme kwa kuruhusu kuwashwa kwa mitambo ya kuzalisha umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inapenda kufafanua kuwa tayari Mhe. Rais ameingilia kati kumaliza mgawo wa sasa wa umeme nchini.

Tokea majuzi, Mhe. Rais alikwishakutoa maagizo kwa Wizara ya Nishati na Madini, pamoja na Kampuni ya TANESCO, kuchukua hatua za kuhakikisha mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL inawashwa, haraka iwezekanavyo, na umeme unaanza kupatikana.

Kutokana na kuharibika kwa mitambo ya kuzalisha umeme ya Songas, Ubungo, mjini Dar es Salaam, na Kihansi, Mkoani Iringa, Gridi ya Taifa ina upungufu wa megawati 80, ikiwa ni megawati 20 ambazo kwa kawaida huzalishwa na Songas, na megawati 60 ambazo huzalishwa Kihansi.

IPTL kwa sasa haizalishi umeme. Lakini ina uwezo wa kuzalisha megawati 90 hadi 100. Hizi zinatosha kuziba pengo la sasa la megawati 80 katika Gridi ya Taifa, na kumaliza mgawo wa sasa wa umeme.

Ni kweli kwamba IPTL iko kwenye mchakato wa ufilisi ambao unaendelea sasa mahakamani, lakini Mhe. Rais Kikwete ameelekeza kuwa mchakato wa ufilisi mahakamani hauzii mitambo ya kampuni hiyo kuwashwa na kuzalisha umeme wakati malumbano ya kisheria yakiendelea kortini.

Katika kuhakikisha kuwa umeme unapatikana haraka iwezekanavyo, Mhe. Rais Kikwete ametoa maagizo mbalimbali kwa Wizara za Serikali kama ifuatavyo:

(a) Wizara ya Nishati na Umeme, kwa kushirikiana na TANESCO, imeagizwa kusimamisha masuala yote ya kiufundi ikiwa ni pamoja na upatikanaji haraka wa mafuta, ili umeme huo wa IPTL uanze kuzalishwa mara moja.

(b) Wizara ya Fedha na Uchumi imeagizwa kuhakikisha kuwa inatafuta fedha za kuwezesha ununuzi wa mafuta na mahitaji mengine muhimu, ili umeme uweze kuzalishwa.

(c) Wizara ya Katiba na Sheria imeagizwa kuhakikisha kuwa inasimamia masuala yote ya kisheria yanayohusu suala hilo

Katika kutekeleza maagizo hayo ya Mhe. Rais, jana, Jumanne, Oktoba 20, 2009, Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda, tayari aliitisha kikao maalum cha Mawaziri wa Nishati na Madini, Fedha na Uchumi, Katiba na Sheria, TANESCO na vyombo vingine husika katika suala hilo kujadili jinsi ya kuhakikisha kuwa umeme wa IPTL unawashwa haraka.

Kupatikana kwa umeme wa IPTL utawawezesha mafundi ambao kwa sasa wanahangaika kutengeneza mitambo ya Songas na Kihansi kuifanya kazi hiyo kwa utulivu zaidi.

Mhe. Rais Kikwete anaelewa fika matatizo yanayowapata wananchi kwa sababu ya mgawo wa sasa wa umeme, na madhara yake kwenye uchumi wa nchi. Lakini anapenda kuwahakikishia wananchi wote kuwa mgawo wa sasa wa umeme utakwisha katika siku chache zijazo.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

21 Oktoba, 2009

Balozi Dk.Augustine Mahiga Kupewa TUZO



Balozi Dk. Augustine Mahiga

Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Dkt. Augustine Mahiga atatunukiwa Tuzo ijulikanayo kama ‘ “The Spirit of the United Nations” kwa mwaka wa 2009.
Balozi Mahiga anakuwa mwana-diplomasia wa tatu kutunukiwa tuzo hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007.


Waandaji na watoaji wa tuzo hiyo ni Kamati ya Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya kiroho, maadili na mambo yanayo hususu ulimwengu katika ujumla wake (CSVGC-NY), ikishirikiana na taasisi nyingine isiyo ya kiserikali ya Umoja wa Mataifa inayo husika na masula ya mikutano na uhusiano.( CONGO)


Aidha kuanzia mwaka huu wa 2009 waandaji wa Tuzo hiyo ya “The spirit of the United nations”, wameamua iwe inatolewa kwa makundi matatu ambayo ni wana-diplomasia,wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, na wawakilishi wa taasisi zisizo za kiserikali ambazo zinauhusiano na Umoja wa Mataifa kupitia Kamati ya inayohusika na masuala ya Uchumi na Maendeleo ya Jamii (ECOSOC) au Idara ya Mawasiliano ya Umma (DPI)ya Umoja wa Mataifa.


Balozi Mahiga atatunukiwa tuzo hiyo Oktoba 26 katika wiki ambayo taasisi hiyo huadhimisha wiki ya kiroho, maadili na masuala yahusuyo ulimwengu. Maadhisho ya wiki hiyo yalizunduliwa rasmi mwezi Octoba mwaka 2007 kama sehemu ya kuendeleza utamaduni wa amani kama inavyotambuliwa ndani ya katiba ya Umoja wa Mataifa.


Kwa mara ya kwanza Taasisi hiyo ilimtunuku Tuzo hiyo mwaka 2007, Balozi Anwarul K. Chowdhury, (2007) aliyekuwa kwa wakati huo Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya nchi maskini na zinazoendelea, nchi zisizokuwa na bahari, na nchi zinazoendelea za visiwa vidogo.


Balozi wa Pili alikuwa ni Balozi wa Kudumu wa Ufilipino katika Umoja wa Mataifa, Hilario G. Dvide, Jr. aliyetunukiwa tuzo hiyo mwaka 2008.Watunukiwa wote hao waliteuliwa kupokea tuzo hiyo kutokana na juhudi zao za kutangaza na kuendeleza masuala kiroho na maadili katika Umoja wa Mataifa.


Wanaopatiwa tuzo hiyo ni watu ambao pamoja na sifa nyingine wanatakiwa wawe wameonyesha kwa vitendo dira na maadili ya kiroho ya Umoja wa Mataifa kama ilivyoainishwa katika katiba ya Umoja wa Mataifa na Tamko la haki za Binadamu kama msingi mkuu wa kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa.


Aidha anatakiwa awe ni mtu ambaye amefanya kazi katika Jumuia ya Umoja wa Mataifa kwa takribani miaka mitano mfululizo.

Tuesday, October 20, 2009

MCT yazindua jopo la wajuzi


Dk Peter Mwesige (Uganda)

Wangethi Mwangi (Kenya)

Profesa Palamagamba Kabudi


BARAZA la Habari Tanzania (MCT), jana lilizindua jopo la wajuzi la kwanza (Think Tank) lenye wajumbe sita ambao watahusika na uhuru wa kujieleza na masuala ya vyombo vya habari.

Mwenyekiti wa jopo hilo kwa miaka minne ijayo ambalo lilitambulishwa jana mbele ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini ni Profesa Issa Shivji.

Wajumbe ni Jenerali Ulimwengu, Profesa Robert White(Marekani), Profesa Palamagamba Kabudi, Dk Peter Mwesige (Uganda) na Wangethi Mwangi (Kenya).

Akizungumza wakati wa utambulisho wa jopo hilo jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa (MCT), Kajubi Mukajanga alisema kwa muda mrefu baraza hilo lilikuwa likifikiria jinsi ya kuboresha muelekeo wa vyombo vya habari hali iliyowalazimu kuunda jopo hilo chini wa wajuzi wa fani mbalimbali ili kuboresha taaluma ya habari.

“Kazi ya jopo hili ni kutafakari na kuandika machapisho, kukutana na watunga sera, kutembelea shule mbalimbali za uandishi wa habari pamoja na kuandika makala, ni wazi kuwa jopo hili litachangia fani hii kuingia katika kipindi kipya cha weredi wa tafakari mpya,” alisema Mukajanga na kuongeza;

“Kwa miezi 12 ya kwanza jopo hili litashughulikia na uhuru wa wahariri wa vyombo vya habari kwa sababu mwishi wa siku malengo ya vyombo vya habari ni kutoa habari kwa maslahi ya umma na sio kuandika habari kutokana na shinikizo la mmiliki au wanasiasa.”

Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa jopo hilo Profesa Palamagamba Kabudi alisema wamiliki wa vyombo vya habari hawatakiwi kuingilia utendaji wa kazi wa wahariri wao na kusisitiza kuwa wahariri wanatakiwa kupewa uhuru ili mradi hawakiuki maadili ya taaluma ya habari.

Akikinukuu kitabu kilichoandikwa na marehemu Mwalimu Julius Nyerere kinachoitwa ‘Uhuru na Umoja’, Profesa Kabudi alisema; “ Katikia kitabu hiki mwalimu alijaribu kuelezea umuhimu wa uhuru katika ngazi zote, hivyo hata mimi nasisitiza kuwa wahariri wana haki zote katika maamuzi ikiwa ni pamoja na habari gani itoke ipi isitoke.”

“Lakini uhuru huu lazima uzingatie haki za kimsingi za binadamu na kutokubali kuingiliwa katika utendaji wa kazi na mmiliki au mtu yeyote kutoka nje, lakini sio wamiliki tu wahariri pia hujikuta wanakosa uhuru kwa sababu ya wanasiasa, kutojiamini ambako huchangiwa na ukosefu wa elimu, watangazaji, kuogopa kufukuzwa kazi, wafanyabiashara pamoja na imani za kidini”

Alisema kuwa vyombo vingi vya habari kukosa sera ya kudumu, wamiliki wa vyombo vya habari kujali fedha kuliko kuelimisha umma, kuandika habari za kuwafurahisha wanasiasa ni moja ya sababu za kutoweka kwa uhuru wa wahariri.

“Kinachotakiwa hapa ni kuhakikisha wahariri na waandishi wanapata mafunzo ya mara kwa mara, kujali sera, wahariri kuwa huru katika ufanyaji wao wa kazi kutasaidia sana kuboresha taaluma hii” alisema Kabudi


Naye Mwenyekiti wa jopo hilo, Profesa Issa Shivji alisema uhuru wa mhariri wa chombo chochote cha habari ni kitu muhimu sana na kusisitiza kuwa uhuru wa vyombo vya habari hauwezi kuzungumziwa kama wahariri hawatakuwa na uhuru.

“Tatizo kubwa lipo kwa wamiliki kwani baadhi yao wamekuwa wakiingilia kazi za wahariri wao na kutokana na kuwa wahariri hawa pengine nao wanaogopa kufutwa kazi hujikuta wakifanya kazi bila uhuru kitu ambacho kinakuwa hakina maana halisi ya taaluma hii ya habari kwani lengo lake ni kuelimisha umma” alisema Shivji na kuongeza Imeandikwa na Fidelis Butahe, Picha za Mwananchi Communications.

Monday, October 19, 2009

Meneja Uwanja Uhuru afariki dunia



"Nimesema mlango huu ufungwe, nataka watu watumie mlango ule...inakuwa vipi watu wanapitia mlango huu...nyie vipi bwana mnataka tuharibiane kazi...," ni kauli ya mara kwa mara ya Charles Celestine Masanja wakati wa mechi ama shughuli ya kitaifa kwenye Uwanja wa Taifa na sasa Uhuru.

Sasa kauli hiyo ya Masanja, Meneja wa Uwanja wa Uhuru sasa haitasikika tena.

Masanja alifariki saa 9 za usiku wa kuamkia jana wakati akitoka kwenye shughuli zake ikiwemo kusimamia mapato ya uwanja baada ya mechi kati ya Simba na Ruvu JKT juzi.

Katika mechi ile ambayo ni ya mwisho kwake, alikuwa akipambana na watu wa milangoni waliokuwa wakiingiza watu na fedha kuingia mifuko mwao.

Wengi watamkumbuka kuwa si meneja wa kukaa ofisini, alikuwa akihaha huku na huko kuhakikisha usalama unakuwepo uwanjani wakati wote.

Taarifa zilizopatikana jana nyumbani kwake, Kimara Korogwe, zilisema kuwa Masanja amefariki katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikopelekwa baada ya kuteleza na kuanguka nje ya uzio wa nyumba yake.

Mdogo wa marehemu, Greyson Selestine aliliambia Mwananchi kuwa kaka yake alipatwa na mkasa huo wakati akirejea nyumbani majira ya saa 9 za usiku akitokea katika shughuli zake za kawaida ambapo pia jioni ya siku hiyo alishihudia mpambano wa ligi kuu kati ya Simba na Timu ya JKT Ruvu uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru. Habari iemdaliwa na
Sosthenes Nyoni na Sweetbert Lukonge

AFRICA SENDS KAONE & LIZ HOME!


Last night, Africa decided that Liz and Kaone’s time was up on the sixth eviction show of M-Net’s BIG BROTHER REVOLUTION (Sunday 18 October, live at 19:00 CAT).

The “Fabuliz” South African and the creative housemate from Botswana saw their 42-day stay in the BIG BROTHER REVOLUTION house come to an end as Africa chose to keep Edward & Emma in the house instead.

Earlier in the week, Head of House Quinn had replaced himself and Kristal, with Edward & Emma. When IK asked Quinn to share his decision with the housemates during the live Eviction show, he admitted that his decision to save himself and his Comrade in Arms was ‘a cliché’ and revealed that he had no specific reason for nominating Edward & Emma in their place.

Liz and Kaone emerged from the house looking happy, soaking up the adoration of the enthusiastic BIG BROTHER REVOLUTION studio audience. IK quizzed them about who they thought had nominated them, with Kaone declaring he had no idea because it was just a game. Liz said that she expected most of the housemates to have nominated her as she was a threat to everyone “except Kristal and maybe Emma”.

IK chatted to Kaone first about his time in the house, asking him about his love for fashion design, as he had spent a lot of time sewing and being creative. “I’ve been doing it a long time,” he said, “and I was just living my life in the house the same way I live it outside”. He was surprised when IK pointed out that he had had a number of disagreements in the house, but brushed them off as minor moments when other housemates crossed his boundaries.

Turning to the question of his love life, IK asked about Kaone’s feelings for Geraldine, as he had spent a lot of time in the house flirting with her. “We had a lot in common, but after chatting about it, we decided to remain as friends,” said Kaone. Then it was Molotov Cocktail time and when IK read out the details – that one housemate may not order anything extra for the grocery list and must only eat from the basic supplies for one week – Kaone named Geraldine, telling her that she shouldn’t order any more chocolate “because it’s bad for you!”

Liz was next on stage, with IK interrogating her about her love life in the house. When asked about Phil, she admitted she would have gotten into a relationship with him if she didn’t have a boyfriend outside the house. Some housemates were of the opinion that her boyfriend was a figment of her imagination, but when IK asked her if she really had a boyfriend, she said “he’s real.”

Asked about the clashes she had in the house, she said she felt she never really clashed with anyone. “I didn’t hate anyone – I didn’t like Yacob, but I didn’t hate anyone,” she said. IK asked her why she didn’t get along with Yacob and she answered because “he doesn’t like competition and I was his competition”. www.mnetafrica.com/bigbrother.

Siku ya afya ya akili duniani



Afisa Tawala katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Morogoro, Emmanuel Nzunda
akisoma risala wakati wa maadhimisho ya siku ya afya ya akili katika kituo
cha afya Sabasaba mjini Morogoro ambapo Manispaa hiyo ina wagonjwa wa akili
wapatao 622,



Wasanii wa kikundi cha Oldvai wakiwa wameungana na kutembelea mikono wakati
wakitoa burudani katika maadhimisho ya siku ya afya ya akili dunia
iliyofanyika katika kituo cha afya Sabasaba mjini Morogoro ambapo jumla ya
wagonjwa 622 wamebaini kukumbwa na ugonjwa huo katika Manispaa hiyo.

(Picha na Juma Mtanda).

Sunday, October 18, 2009

Rais Kikwete ateua Makatibu Wakuu Wapya

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mabadiliko katika safu ya maofisa waandamizi wa Serikali kwa kuteua Makatibu Wakuu wa Wizara wanne wapya, kuhamisha wengine wawili, na kuteua Katibu wa Rais mpya.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Oktoba 19, 2009, Ikulu, mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Philemon Luhanjo, imesema kuwa Mhe. Rais Kikwete amefanya mabadiliko hayo kufuatia kustaafu kwa baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara.

Aidha, taarifa inasema kuwa mabadiliko hayo yanaanza leo, Oktoba 19, 2009.

Taarifa hiyo imesema kuwa Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana David Kitundu Jairo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Jairo alikuwa Katibu wa Rais.

Bwana Jairo anachukua nafasi ya Bwana Arthur Mwakapungi ambaye amestaafu.

Katika taarifa yake, Bwana Luhanjo amesema kuwa pia Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana Sazi Salula kuwa Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Salula alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Taarifa hiyo pia imesema kuwa Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana Mbarak M. Abdulwakil aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Bwana Abdulwakil anachukua nafasi ya Bwana Patrick Rutabanzibwa ambaye anahamishiwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kama Katibu Mkuu. Ndugu Rutabanzibwa anachukua nafasi iliyoachwa na Bi. Salome Sijaona ambaye amestaafu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mhe. Rais Kikwete pia amemteua Bwana Christopher N. Sayi kuwa Katibu Mkuu wa Wizata ya Maji na Umwagiliaji.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Sayi alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo hiyo, na anachukua nafasi ya Bwana Wilson Mukama ambaye ameanza likizo ya kustaafu kwa mujibu wa sheria.

Bwana Luhanjo amesema katika taarifa yake kuwa vile vile Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana Sethi Kamuhanda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kamuhanda alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Anachukua nafasi Dkt. Florence Turuka ambaye anahamishiwa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kama Katibu Mkuu. Bwana Turuka anachukua nafasi ya Dkt. Naomi Katunzi, ambaye anamaliza mkataba wake wa utumishi wa Serikali mwezi ujao, Novemba, 2009.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi pia inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Prosper Mbena kuwa Katibu wa Rais. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mbena alikuwa Msaidizi wa Katibu wa Baraza la Mawaziri, na anachukua nafasi ya Bwana Jairo.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

19 Oktoba, 2009

Kunduchi Beach Hotel & Resort Kudhamini Miss East Africa 2009!!



Cefora kulia na Selemawit washiriki kutoka Eritrea.
Kunduchi Beach Hotel & Resort itadhamini mashindano ya kimataifa ya Miss East Africa 2009 yatakayo fanyika mwezi Desemba mwaka huu jijini Dare s salaam, Tanzania.
Kwa udhamini huo, Kunduchi Beach Hotel & Resort ndiyo inakuwa OFFICIAL RESIDENCE ya Miss East Africa 2009 ambapo
warembo wote kutoka Nchi 14 zinazoshiriki mashindano hayo watafikia na kuishi katika hoteli hiyo ya kifahali iliyo kandokando ya ufukwe wa bahari ya hindi.
“Tunapenda kushukuru uongozi wa Kunduchi Beach Hotel & Resort kwa kudhamini mashindano yetu ya mwaka huu ampapo sasa wasichana wetu tatafikia katika hiyo ambayo ni moja ya hoteli za kuvutia barani Afrika”
Mashindano ya MISS EAST AFRICA 2009 yamepangwa kufanyika tarehe 18 mwezi Desemba mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es salaam.
Mashindano hayo yatashirikisha warembo 28 kutoka Nchi 14 zilizo katika ukanda wa Afrika mashariki ambazo ni pamoja na wenyeji TANZANIA, KENYA, UGANDA, RWANDA na BURUNDI. Zingine ni ETHIOPIA, ERITREA, DJIBOUTI, SOMALIA, pamoja na visiwa vya MAURITIUS, MADAGASCAR, COMOROS, RE UNION na SEYCHELLES.
Taji la Miss East Africa kwa sasa linashikiliwa na mrembo Claudia Niyonzima wa Burundi aliyeshinda mashindano hayo mwaka jana jijini Bujumbura.
Tunapenda pia kuwakumbusha watu wote kwamba ile bahati nasibu ya MISS EAST AFRICA ya kusaidia yatima bado inaendelea na unaweza kujishindia zawadi mbalimbali kwa kununua tiketi za bahati nasibu hiyo kupitia kwa wauzaji wa magazeti kote Nchini au kwa kutuma neno “SHINDA” kwa sms kwenda namba 15567 kupitia simu za mkononi.
Zawadi ya juu kabisa katika bahati nasibu hiyo ni gari aina ya Range Rover Sport kutoka kampuni ya CMC Automobile Ltd.
“Tunapenda kuwahakikishia wapenzi wa fani ya urembo kwamba mashindano ya MISS EAST AFRICA mwaka huu yatakuwa ya kuvutia sana na yenye ushindani mkubwa kwa vile kila Nchi imekusudia kuleta warembo bora na wenye viwango vya juu katika fani hiyo”
Kwa ujumla maandalizi kwa ajili ya mashindano hayo yanakwenda vizuri;
Aidha, kampuni ya AKO Catering services ndiyo itakayo toa huduma ya chakula na vinywaji ndani ya ukumbi wa Mlimani City siku ya fainali ya mashindano ya Miss East Africa 2009.
“Tumeamua kuitumia kampuni ya AKO catering services kwa huduma hiyo ili kuhakikisha kwamba watu wote siku hiyo wanapata huduma bora kabisa ukumbini hapo. AKO ndiyo kampuni bora hapa Nchini kwa shughuri za chakula na vinywaji”
Fainali za mashindano ya MISS EAST AFRICA 2009 zinasubiliwa kwa hamu na wapenzi wa fani hiyo barani Afrika na inatarajiwa kwamba watu wapatao millioni 200 wataangalia mashindano hayo kupitia katika Television barani Afrika.
Kituo cha East Africa Television ndiyo official TV station ya mashindano ya MISS EAST AFRICA.

Wahasibu wakihitimu masomo yao







Hii ilikuwa jana pale Waziri Mustafa Mkulo alipokuwa akiwatunuku ndugu zetu hawa wahasibu wa ngazi mbalimbali wanaotambuliwa na bodi ya taifa ya wahasibu Tanzania, kwa upana wao sasa wanatambuliwa na bodi, Katika picha nyingine wanaonekana wasanii wakitumbuiza katika hafla hiyo iliyofanyika Mhasibu House jijini Dar

Thursday, October 15, 2009

Cassian mshindi Bongo Star Search 2009


Mashabiki wakiwa wamekolezwa na burdani.

PAschal Cassian akifanya vituuzz.

Jaji Mkuu wa shindano Madame Ritta akiwa na Master J

Kelvin Mbati

Mheshimiwa Zitto hakuachwa nyuma

MKOA wa Mwanza umezidi kung'ara kupitia sanaa mchini baada ya mshiriki kutoka mkoani humo, Pascal Cassian kuibuka mshindi katika shindano la kusaka vipaji vya waimbaji chipukizi maarufu kama Bongo Star Search ambalo fainali zake zilifikia tamati juzi usiku kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Kabla ya ushindi huo, tayari Mwanza ilikuwa imetwaa mara mbili mfululizo taji la urembo maarufu kama 'Miss Tanzania 2009' baada mwanadada Miriam Gerald kuibuka mshindi.

Hata kabla ya kutangazwa mshindi Casian alionekana kuuteka umati mkubwa wa watu waliojitokeza kushuhudia fainali hizo kiasi cha kuwafanya wainuke kila wakati katika viti vyao na kwenda kuungana naye hasa pale alipoimba kibao cha 'Shebeneza' chenye asili ya Afrika Kusini.

Kutokana na ushindi huo, Cassian aliweza kutia kibindoni fedha taslimu shilingi milioni 25 kutoka kwa waandaaji wa shindano Kampuni ya Benchmark Production .

Mbali na zawadi hiyo kutoka kwa waandaaji, mshindi huyo pia alikabidhiwa shilingi 1,500,000 baada ya kuibuka mtunzi bora wa wimbo wa ukimwi sambamba na kitita kingine cha 500,000 kutoka duka la mavazi la Mariedo Botique ambalo pia lilidhamini shindano hilo.

Katika fainali hizo zilizohusisha washiriki watano, Peter Msechu mshiriki kutoka Kigoma aliibuka mshindi wa pili na kupata kitita cha shilingi milioni 5 taslimu pamoja na ofa ya mavazi kutoka duka la Mariedo huku mshiriki kutoka Dar es Salaam Kelvin Mbati akikamata nafasi ya tatu na kukabidhiwa zawadi ya sh 500,000 pamoja na ofa ya mavazi kutoka duka la Shear Illusion.

Mshiriki kutoka Tanga, Jackson George alishika nafasi ya nne na kupata zawadi ya vocha yenye thamani ya shilingi 200,000 pamoja na ofa ya mavazi kutoka duka la Mariedo wakati mshiriki pekee wa kike aliyeingia katika hatua ya fainali, Beatrice William kutoka Mwanza alishika nafasi ya tano na kupata zawadi ya ofa ya mavazi kutoka Mariedo.

Mbali ya zawadi hizo, duka la mavazi la Marriedo pia liliwazawadia washiriki wote watano walioingia hatua ya fainali sh 500,000 kila mmoja.

Mara baada ya kutangazwa mshindi na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Simu ya Vodacom, Ephraim Mafuru, Casian aliwashukuru Watanzania kwa kumpigia kura na wadhamini Benchmark na Vodacom kwa kumwezesha kutwaa taji hilo. Habari imendikwa na
Sosthenes Nyoni.

Wednesday, October 14, 2009

mbio za mwenge zafika tamati


Kiongozi wa Mbio za mwenge mwaka huu Kheir Ahmada Mwawalo akimkabidhi Rais Kikwete nakala ya risala ya mwenge na taarifa za risala mbalimbali zilizosomwa wakati wa mbio za mwenge mwaka huu katika kilele cha sherehe hizo zilizofanyika Butiama mkano Mara leo mchana

Kiongozi wa mbio za ,mwenge mwaka huu 2009 Kheir Ahmada Mwawalo akiukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika kilele cha sherehe za mbio hizo zilizofanyika Butiama, mkoani Mara leo mchana.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mwenge wa Uhuru Waziri wa Kazi Vijana na maendelo ya ajira Profesa Juma Kapuya katika viwanja vya Butiama wakati wa kilele cha mbio za mwenge zilkizofanyika kijijinji hapo leo mchana.(picha zote na freddy Maro)

Mwenge wa Butiama




Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Kheri Ahmada Mwawalo kutoka mkoa wa mjini Magharibi akiuwasha mwenge wa Mwitongo uliopo nyumbani kwa hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kijijini cha Butiama wilayani Musoma mkoa wa Mara . Tangu kuwashwa kwa mwenge wa Uhuru mwaka 1961, mwenge wa Mwitongo huwa unawashwa kila mwaka na unajizima wenyewe baada ya mafuta kuisha.