Saturday, December 19, 2015

CHINA YASAIDIA VITANDA 60 VYA KUJIFUNGULIA WAKINA MAMA KWA MKOA WA LINDI


 Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing akizungumza kabla ya kukabidhi vitanda 60 vya kujifungulia wakina mama katika mkoa wa Lindi, kushoto ni mkalimani wake Ndugu Mu Lin.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) ambapo alisema Serikali ya China pamoja na watu wake wamekuwa marafiki wa kweli kwa Tanzania na wamekuwa wakitoa misaada mingi bila kutoa masharti.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB)
akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Kassim Majaliwa (MB) ambapo aliishukuru  Serikali ya China pamoja na
watu wake kwa msaada wa vitanda 60 vya kujifungulia ambavyo vitasaidia kuokoa maisha ya Mama na Mtoto katika mkoa wa .
  Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing akiangalia baadhi ya vitanda ambavyo vimekabidhiwa kwa mkoa wa Lindi kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye hospitali ya mkoa wa Lindi Sokoine.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiangalia vitanda hivyo vya kujifungulia wakina mama akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Taasisi ya kukuza Urafiki wa Tanzania na China  Ndugu Joseph Kulwa Kahama.
 Bi. Ziada Maulid akitoa shukrani zake mbele ya Balozi wa China nchini  Dk. Lu Youqing mara baada ya ya Balozi huyo kukabidhi vitanda 60 vya kujifungulia wakina mama.
 Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama wakiwasili katika kata ya Kiwalala, jimbo la Mtama tayari kwa kukabidhi vifaa vya matibabu katika Zahanati ya Mauhumbika.
 Wakazi wa kijiji cha Mahumbika wakiwa wamejitokeza kwa wingi kushuhudia makabidhiano ya vifaa vya matibabu katika Zahanati yao.
  Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing akihutubia wakazi wa Mahumbika ambapo pamoja na kuahidi misaada zaidi ikiwemo kwenye matatizo ya maji, Balozi pia aliahidi kusaidia vijana wanaomaliza Chuo Kikuu kwenda kujiendeleza nchini China.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitoa salaam za shukrani kwa Serikali ya China kwa msaada wa vifaa vya tiba vilivyogharimu zaidi ya milioni 20.

No comments: