Monday, December 31, 2012

KOCHA MPYA MFARANSA MPYA WA SIMBA ATUA DAR

Katibu wa Simba, Evodius Mtawala (kushoto) akiongozana na kocha mpya wa klabu hiyo, Patrcik Liewig baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam mchana huu. 

Mtawala na Liewig

Liewig, Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Ufundi, Dani Manembe na Mtawala

Anazungumza na Waandishi

Anapanda kibasi

Ndani ya kibasi

Wanachama waliokuja kumlaki PIcha zote za http://bongostaz.blogspot.com

Rais Jakaya Kikwete atangaza matokeo ya sensa,Watanzania waongezeka kutoka watu 34.4 milioni hadi 44.9


Rais Jakaya Kikwete atangaza matokeo ya sensa ya watu na makazi, Watanzania waongezeka kutoka watu milioni 34.4 hadi kufikia watu milioni 44.9. Tanzania bara kuna watu 43.6 milioni na Zanzibar watu 1.3milioni.Kwa habari zaidi ungana nasi baadaye.

RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MZEE MOHAMED ABOUD

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib  Bilali, Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Iddi, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika mazishi ya Marehemu Mohamed Aboud Mohamed, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, katika Makaburi ya Ngazija jijini Dar es salam  Desemba 29, 2012.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiweka mchanga kaburini wakati wa mazishi ya Marehemu Mohamed Aboud Mohamed, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, katika Makaburi ya Ngazija jijini Dar es salam ,Desemba 29, 2012.

PICHA NA IKULU

BABA WA PINDA ALAZWA MUHIMBILI

POLE BABA: Waziri Mkuu Mizengo Pinda akmjulia hali jana jioni, Baba yake mzazi Mzee Savere Kayanza Pinda ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili   kitengo cha Moi, Dar es Salaam. Mzee Mizengo yupo hospitalini hapo baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na tatizo la nyonga. Kulia kwa waziri mkuu ni Muguzi wa zamu, Edna Mhina  na kushoto kwa waziri mkuu ni  Donatila Kwelukila ambaye ni Ofisa uguzi chumba cha wagonjwa mahututi  MOI, (Picha na Chris Mfinanga)

ISSA KWISSA MWAIFUGE AFUNGA NDOA

 

  Issa Kwisa Mwaifuge, akiwa na mkewe Binti mrembo aliyewahi kushiriki shindano kubwa la Miss Tanzania, 2004, Verdiana Kamugisha, ambao kwa pamoja wameamua kumeremeta siku ya jana na kufunga ndoa yao katika Kanisa la Lutheran lililopo Sinza jijini Dar es Salaam. Na hapa ni wakati wakiwa katika sherehe ya ndoa yao inayoendelea muda huu katika Ukumbi wa Msasani Makuni. Picha Zote na www.sufianimafoto.blogspot.com
 Bwana Harusi, Issa Kwisa (kushoto) akisebeneka na Suleiman Semunyu, aliyekuwa akipokea zawadi ya keki kwa niaba ya ITV.

IJUMAA YA MWISHO KWA MWAKA 2012 SKYLIGHT BAND YAVUMBUA KIPAJI KIPYA NI MSHINDI WA PILI WA EBSS 2012 SALMA YUSUF


Sam Machozi a..k.a Sam Mapenzi akiongozaji waimbaji wenzake Aneth Kushaba (kushoto) sambamba na Sony Masamba wakitoa burudani ya aina yake Ijumaa ya mwisho kwa mwaka 2012 katika kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam. (Picha na Mo Blog).
Sura mpya ya SKYLIGHT Band ikifanya yake Jukwaani katika show ya mwisho ya Band hiyo kwa Mwaka 2012 iliyofanyika Ijumaa ya tarehe 28 mwezi huu katika kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam. Si mwingine ni Binti mdogo mwenye kipaji cha aina yake mshindi wa pili katika shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 Salma Yusuf sambamba na Meneja wa Band hiyo Aneth Kushaba AK 47 wakiwapa raha mashabiki wa bendi hiyo.

 
Chezea Salma Yusuf wewe ulizoe kumuona kwenye TV wakati wa EBSS 2012 njoo umuone Live Ijumaa akitambulishwa rasmi kwa mashabiki wa SKYLIGHT BAND.
 
Vijana Watanashati wakipata Ukodak…Single Ladies mpooooo??? Kazi kwenu.
 
SKYLIGHT BAND ilipata ugeni kutoka The B Band ya Banana Zorro. Pichani ni Aneth Kushaba AK 47 akishow love na baadhi ya wasanii wa The B BAND.
 
Mdau King Kif akishow Love na Aunty Ezekiel a.k.a Mrs. Demonte pamoja na rafiki yake katika usiku wa SKYLIGHT BAND.
 
Kati ya Vijana hawa wawili walikuwa wakisheherekea siku yao ya kuzaliwa ndani ya Kiota cha Thai Village na SKYLIGHT BAND.
S
 
Wadau wakishow Love.

TSN Board Appoints Nderumaki Acting ME


By Staff Reporter
THE Board of Directors of Tanzania Standard (Newspapers) Limited (TSN) has appointed Mr Gabriel Nderumaki (pictured), the company’s Acting Managing Editor effective December, 24, this year.
According to a statement issued by the company yesterday, Mr Nderumaki takes over from Mr Mkumbwa Ally, after expiry of his contract with the company on December 15.
The new acting Managing Editor has been with TSN for over 20 years and served in senior editorial positions including Sports Editor, News Editor and Business Editor.
“I am ready for the new challenge and looking forward to getting maximum co-operation from readers, government, private sector and all other stakeholders,” Mr Nderumaki.
He pledged that under his leadership, TSN who are the publisher of Daily News, Sunday News, Habari Leo, Habari Leo  Jumapili and SpotiLeo, will continue to publish well researched educative and informative, as opposed to unreasonable sensational articles.
“We will continue to publish informative stories in support of the government’s initiatives to improve the lives of Tanzanians and when necessary provide constructive criticism, as opposed to unreasonable sensational articles.
 
“To investors and those in the private sector, we will continue writing balanced and educational stories about their role in national development,” he said.
TSN is a registered company and has been in the newspapers industry for more than 70 years. The company is currently wholly owned by the government

RAILA ODINGA ATUA JIJINI DAR KIMYAKIMYA

Katika…
Katika kuonyesha kuwa Dk. John Magufuli na Raila Odinga ni maswahiba kwa taarifa nilizozinyaka na ni za uhakika ni kuwa, Mh. Raila Odinga yupo nchini Tanzania kumtembelea rafiki yake kipenzi Mh. Dk. John P. Magufuli ambapo nimebahatika kupata baadhi ya picha kama mnavyoziona hapo juu. Na inavyoonyesha ziara hii ni ya kimyakimya. Pichani juu, Raila Odinga akikaribishwa na mwenyeji wake, Dk Magufuli katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam siku mbili zilizopita.

Saturday, December 29, 2012

Zitto Kabwe:Utajiri wa Gesi Asilia: Tuwasikilize Watanzania wa Mtwara na Lindi. Tusipuuze

 Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA,Mh Zitto Kabwe
---
Maandamano ya amani yaliyofanyika mjini Mtwara siku ya alhamis wiki hii yameibua hoja mbali mbali kutoka kwa viongozi, wananchi, vyombo vya habari na mjadala wa siku nzima kwenye mitandao ya kijamii hasa facebook, twitter na JamiiForums. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ameita waandamanaji wapuuzi na Waziri wa Nishati na Madini amewaita watu hatari na wahaini. CHADEMA tumetoa kauli kupitia kwa Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba udhaifu wa utendaji serikalini ndio chanzo cha maandamano haya.

Lakini kuna tatizo kubwa zaidi ambalo linaonekana siyo katika sekta hii tu bali pia katika sekta nyingine ambapo tunaona matokeo yake katika maisha ya watu wetu na naweza kusema ni dalili za kushindikana kwa sera za CCM. Sera hizi ndizo ambazo zimelifikisha taifa hili hadi hapa. Kama hadi wananchi wa Mtwara ambako kwa muda mrefu imekuwa ni ngombe ya CCM wanaanza kuhoji matokeo ya sera za chama tawala basi ni dalili kuwa Watanzania wamefungua macho yao na wanaona.

Wanaona katika nishati, wanaona katika utawala bora, wanaona katia elimu (kuanzia ya msingi hadi ya juu kabisa!), wanaona katika afya, wanaona katika utendaji wa jeshi la polisi wanaona katika madini. Sera za CCM zimeshindwa. Zimeshindwa kuinua maisha yao na zinaonekana kuendelea kushindwa.

Mtwara na Lindi wanataka nini?
Watu wa Mtwara wanataka gesi isiondoke Mtwara na badala yake viwanda na mitambo ijengwe Mtwara kisha kama ni umeme au mbolea isafirishwe kupelekwa sehemu nyingine ya nchi. Watu wa Mtwara hawasemi kwamba Gesi yote na mazao yake vibaki Mtwara na Lindi. Wanasema umeme uzalishwe Mtwara usambazwe nchi nzima. Mbolea izalishwe Mtwara na kusambazwa nchi nzima. Wanataka Bandari ya Mtwara iboreshwe na kuhudumia mikoa ya Kusini. Watu wa Mtwara hawasemi kwamba mapato yote ya Gesi yatumike Mtwara tu la hasha.

Sio dhambi hata kidogo kwa watu wa Mtwara kudai masuala haya. Watu wa Mtwara wamefanya maandamano kwa amani kabisa bila kuharibu mali na kutoa maoni yao. Kwanini tuwasute na kuwasusubika kwa madai yao haya? Kwa nini tusiwasikilize? Kosa lao nini kudai viwanda ili wapate ajira? Tumesahau kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara ni mikoa masikini kabisa nchini? Tumesahau kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara ilitumika kwa ukombozi wa kusini mwa Afrika kiasi cha kuwa katika hatari kabisa? Tumesahau ‘sacrifice’ ya watu wa Mtwara na Lindi dhidi ya usalama wa nchi yetu? Tumesahau kuwa Korosho imekuwa zao kubwa la biashara na linaloingiza mapato mengi sana ya Fedha za kigeni? Waziri Muhongo anasema Mtwara warudishe Fedha za Mkonge na Kahawa. Mbona hataji fedha za Korosho? Mwaka 2011 Korosho ilikuwa zao la pili kwa kuingiza fedha nyingi za kigeni baada ya Tumbaku.

Lakini tujiulize, watu wa Mtwara na Lindi walifadi fedha za Mkonge? Walifaidi fedha za Kahawa? Wamefaidi fedha zao za Korosho? Tumesahau hata Reli iliyoachwa na Mkoloni ya Nachingwea – Mtwara iling’olewa na Serikali huru ya Tanzania?

Tujiulize zaidi, hivi watu wa Nzega wamefaidika vipi na Mgodi wa Resolute pale Lusu? Mgodi umefungwa ukiwa umezalisha na kuuaza dhahabu ya thamani ya dola za marekani 3.3 bilioni. Hivi katika uhai wa mgodi huu Serikali Kuu imekusanya kodi kiasi gani? Halmashauri ya Wilaya ya Nzega imepata ushuru kiasi gani? Watu wa Mtwara wanayaona haya yaliyotokea Nzega na yanayotokea Tarime, Biharamulo, Kahama na Geita. Watu wa Mtwara wana Haki kuandamana kuzuia haya yaliyotokea wenzao yasiwatokee wao kwenye Gesi asilia.

Mtwara na Lindi wanakosea wapi?
Madai yao halali na mimi binafsi na chama changu tunayaunga mkono. Lakini kuna mahala lazima waelimishwe.

Watu wa Mtwara pia wanapaswa kuelewa kuwa juhudi zao zisiwatenganishe na Watanzania wengine kwani bado utajiri wa Taifa unafadisha kikundi cha Watanzania wachache sana. Watu wa Mtwara wanahitaji kuungana na watu wa Mara, watu wa Mwanza, watu wa Shinyanga na watu wa Kagera kudai utajiri wa nchi utumike kwa maendeleo ya watu badala ya kunufaisha kundi dogo la watu. Watu wa Mtwara wanapaswa kuunganisha nguvu na Watanzania wengine kuzuia uporaji wa rasilimali ya nchi dhidi ya kizazi kijacho. Watu wa Mtwara wasijitenge wakawa peke yao na Gesi yao. Nguvu ya mnyonge ni umoja.

Serikali isiyosikia
Serikali ina hoja kuhusu kujenga Bomba la Gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa gharama nafuu. Umeme unaotumiwa na asilimia 14 tu ya Watanzania. Kwa kuwa hii asilimia 14 ndio wenye sauti basi watu wa Mtwara wataonekana hawana hoja kabisa. Lakini Serikali imejiuliza mara mbilimbili kuhusu mradi huu wa Bomba? Tunaambiwa na Wataalamu kwamba kuna uwezekano mkubwa mwakani gesi asilia ya kiasi cha futi za ujazo trillioni 20 itakuwa imegunduliwa katika Kitalu namba 7( block 7) ambacho kipo mkoani Dar es Salaam katika Wilaya ya Temeke. Iwapo gesi nyingi hivi itakuwa hapa Dar karibu kabisa na mitambo ya kuzalisha umeme, mradi huu wa Bomba unaojengwa kwa trillioni za shilingi utakuwa na maana tena? Huu mkopo utakuwa na tija?

Serikali imewaambia watu wa Mtwara gharama za kuleta bomba Dar dhidi ya gharama za kujenga mtambo wa kuzalisha umeme Mtwara na kuusafirisha umeme kwenda maeneo mengine ya Tanzania? Serikali imeangalia faida ya kujenga gridi nyingine badala ya kuwa na gridi moja tu yenye kushikwa na bwawa la Mtera? Leo bwawa la Mtera lisipozalisha hata megawati moja hata Dar es Salaam izalishe megawati alfu kumi umeme hautakuwapo maana uti wa mgongo wa gridi ni Mtera! Kwa nini tusiwe na gridi nyingine yenye uti wa mgongo Lindi au Mtwara?

Tuwasikilize watu wa Mtwara
Watanzania sio mabwege tena. Kuwaita watu wa Mtwara ni wahaini, wapuuzi au watu hatari haisaidii kujenga Taifa moja lenye watu huru. Serikali na wadau wote wa sekta ya Gesi likiwemo Bunge washirikiane na watu wa Mtwara kuhusu miradi ya gesi asilia. Tuwe na Azimio la Mtwara, tamko la kuelekeza namna bora ya kutumia utajiri wetu wa Gesi bila kuathiri umoja wa Taifa letu.

Ujio wa Sera, Maono na Uongozi Mbadala
Sasa hivi wananchi wa Mtwara kama wananchi wa sehemu nyingine wanahitaji maono mbadala, uongozi mbadala, sera mbadala na mwelekeo mbadala wa kitaifa ambao utaangalia mahitaji yao, utazingatia raslimali zilizopo na utaunganisha utendaji wa sekta mbalimbali katika kutengeneza mfumo wa kiutawala na kiuchumi ambao utaliinua taifa zima.

Ni kwa sababu hiyo naamini chama changu ni jibu sahihi kwa matamanio na kiu ya wananchi wa Mtwara na sehemu nyingine nchini. Ikumbukwe kuwa katika Ilani yetu ya Uchaguzi ya 2010 tulielewa haja ya kuangalia mikoa hii ya Kusini kwa namna ya pekee na kuipa mwelekeo wa kipekee katika sera.  Bado tuna makusudio hayo tunapoelekea 2015 na tukishika Dola wananchi wa Mtwara na sehemu nyingine zote zilizoachwa pembezoni mwa mafanikio wajue kuwa wamepata rafiki na mshirika wa karibu wa kushirikiana nao kuleta maendeleo.

Siyo katika suala la gesi tu bali katika nishati, maji, elimu, miundombinu, kilimo, ufugaji, uvuvi, utalii. Mtwara kama ilivyo mikoa mingine ina raslimali za kutosha kuweza kuwainua wananchi wake kimaisha, na zaidi ya yote kutoa mchango mkubwa wa kiuchumi. Hili ambalo ni kweli kwa Mtwara ni kweli kwa mikoa mingine kama Kigoma, Manyara, Katavi, Lindi n.k

Mrembo wa Unique Model 2012 apatikana

Mwanamitindo
wa mwaka 2012 Catherine Masumbiga (katikati) amepatikana jana usiku
kwenye shindano lililofanyika kwenye Klabu ya New Maisha
jijini Dar es Salaam akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa pili
Cesilia Michael (kushoto) na mshindi watatu Amina Ayubu.
Washiriki waliongia tano bora.
Washiriki waliongia tano bora.
Majaji wa shindano hilo kutoka kushoto ni Gymkhana Hilal kutoka Paka Wear , Asia Idarous na Martine Kadinda.
Unique Model Talent of the year 2012 Vestina Charles akionyesha uwezowake wa kucheza jukwaani.
Wakitumbuiza mashabiki mapema kabla ya kuingia kuonyesha mavazi ya aina mbalimbali.
Washiriki 12 wa shindano hilo wakiwa wamejipanga tayari kusubiri kutangazwa mshindi.

BREAKING NEWZZ: TELA LA LORI LATEKETEA KWA MOTO KIBAMBA


Tela la lori linateketea kibamba nje kidogo ya jiji la dar es salam.kwa habari zaidi endelea kufuatilia issamichuzi.blogspot.com

Friday, December 28, 2012

WANANCHI MTWARA WAFANYA MAANDAMANO MAKUBWA KUPINGA GESI KUSAFIRISHWA KWENDA DAR




Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Mtwara Mjini wakiwa kwenye maandamano makubwa waliyoyafanya mapema leo kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar!








Wakazi hao wakiwa na mabango yao yenye jumbe mbalimbali kama uonavyo pichani








Waandamanaji wakiwa wamekusanyika kwenye moja ya uwanja mjni Mtwara mapema leo wakipinga gesi kusafirishwa kwenda jijini Dar! 

  Mmoja wa wakazi wa mji wa Mtwara mjini akiwa amebeba bango lake
Baadhi ya askari wakiwa kwenye gari yao wakiangalia usalama wa hapa na pale kufuati maandamano makubwa yalliyofanya na wakazi wa Mkoa wa Mtwara, mapema leo wakipinga gesi kusafirishwa kwenda jijini Dar!