Tuesday, August 31, 2010

Mkapa ayawakia mataifa ya Magharibi


Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa (kushoto) akimsikiliza Katibu Mtendaji wa African Forum Dk John Tesha mara baada ya kumaliza mkutano wa marais wastaafu na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam jana uliokuwa unaelezea mikakati ya maboresho ya ardhi barani Afrika.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa (kushoto) akitoa ufafaunuzi jana jijini Dar es salaam kwa wanahabari mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Marais wastaafu wa Afrika uliokuwa unajadili juu ya maboresho katika sekta ya ardhi barani Afrika. Kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es Salaam.

Pingamizi la Chadema latinga kwa JK


Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, akiwa ameshika nakala ya pingamizi dhidi ya mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete, wakidai mgombea huyo amekiuka kanuni za sheria ya gharama za uchaguzi baada ya kuiwasilisha kwa msajili wa vyama vya siasa jana jijini Dar es Salaam. Picha na Zacharia Osanga

**********************************************************************
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeteketeza azma yake ya kumwekea pingamizi mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.

Taarifa zimeeleza kuwa chama hicho kiliwasilisha pingamizi hilo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini jana saa 7:30 mchana.

Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika, ndiye aliyewasilisha pingamizi hilo.

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa alipoulizwa hakutaka kukubali au kukataa kuliona pingamizi hilo na akasema atazungumzia suala hilo leo.

Awali Chadema ilipanga kuweka pingamizi hilo la kutaka Kikwete azuiwe kugombea urais, Agosti 27 mwaka huu, lakini, ilisitisha kwa kile ilichoeleza kuwa inasubiri mambo mengi zaidi ambayo wangeyaingiza kwenye pingamizi hilo.

Chama hicho awali kilitaka kuweka pingamizi hilo kwa kile kilichoeleza kuwa Rais Kikwete amekiuka Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa kutangaza nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi kwenye kampeni.

"Tulishindwa kupeleka pingamizi hilo jana kwa sababu tumesikia kwamba huku anakoendelea na kampeni zake, mgombea huyo ameendelea kufanya makosa mengine ambayo tutataka tuyaingize kwenye pingamizi hilo," alisema Mnyika mwishoni mwa wiki. Habari hii imeandikwa na Geofrey Nyang’oro. SOURCE: MWANANCHI.

Monday, August 30, 2010

Kampeni za mzee Ndessa


Umati mkubwa wa wafuasi wa Chadema na Wananchi wa Jimbo la Moshi mjini waliofurika viwanja vya Manyema katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni wa mgombea Ubunge wa chama hicho,Philemon Ndesamburo

Mgombea Ubunge Jimbo la Moshi mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Philemon Ndesamburo akihutubia wananchi wa Jimbo hilo waliojitokeza wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho juzi katika viwanja vya Manyema.

Sunday, August 29, 2010

Madee afunika Mbeyaa


Mwanamuziki nguli wa kikundi cha muziki wa kizazi kipya cha Tip Top Connection chenye maskani yake mitaa ya Manzese jijini Dar es Salaam, Madee akiimba wakati wa uzinduzi wa huduma ya Tigo Pesa katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mwishoni mwa wiki. Picha kwa hisani ya Tigo.

Oliver Mtukudzi ndani ya bongo



Mkongwe wa muziki kutoka Zimbabwe, Oliver Mtukudzi maarufu ‘Tuku’ akifanya onyesho la muziki usiku wa kuamkia jana jijini Dar es Salaam. Onyesho hilo lililoanza Ijumaa usiku na kumalizika jana liliandaliwa na wananchi wa Zimbabwe wanaoishi hapa nchi na kudhaminiwa na makapuni mbalimbali ikiwemo Mwananchi Communications Ltd. Kushoto ni mpiga tumba, Namatayi Mabariki Chipanza. Picha na Salhim Shao

Friday, August 27, 2010

Kenya waidhinisha katiba mpya


Mbwembwe za kijeshi
Rais Mwai Kibaki akiapa.
Mashirika ya haki za binadamu yameilaumu serikali ya Kenya kwa kumruhusu Rais Omar Hassan al-Bashir kuitembelea Kenya ambako atahudhuria sherehe ya nchi hiyo ya kuidhinisha katiba mpya.Kiongozi huyo anatakiwa na Mahakama ya Kimataifa (ICC) kwa mashtaka 10 ya uhalifu, ikiwemo uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari yanayodaiwa kufanyika huko Darfur.

Yeye ni kiongozi wa kwanza aliye madarakani kutuhumiwa na mahakama hiyo ya the Hague. Kenya ni moja ya nchi zilizotia saini mkataba wa mahakama ya ICC ujulikanao kama sheria ya Rome unaoitaka kisheria kumkamata na kumkabidhi kwa mahakama hiyo.

Hata hivyo, uamuzi wa mara mbili uliofanywa na Umoja wa Afrika, uliwaamuru wanachama wake wasimkamate Rais huyo wa Sudan, hata hivyo ulikosea tu kusema kama kuna hatua itakayochukuliwa dhidi ya nchi yoyote itakayokiuka maagizo hayo na kutii amri ya ICC.

Shirika rasmi la habari nchini Sudan (SUNA) limesema katika taarifa fupi kuwa Rais Bashir atasafiri kwenda Nairobi akifuatana na mshauri wake Mustafa Ismail, waziri wa mashauri ya kigeni Ali Karti na mkurugenzi mtendaji wa idara ya ujasusi Muhammad Atta Al-Mawla.

Hii ni ziara yake ya pili katika moja ya nchi wanachama zilizotia saini mkataba wa Rome baada ya kuzuru Chad mwezi uliopita. Licha ya ziara hiyo alipuuza mwaliko wa kuhudhuria mkutano wa kilele wa nchi wanachama wa IGAD mjini Nairobi mwaka huu.

Shirika la Human Rights Watch limesema kuwa ziara yake itaweka doa sherehe za kuidhinisha katiba iliyosubiriwa kwa hamu kwa kumpokea kiongozi huyo.source BBC.

Tuesday, August 24, 2010

Ufisadi misaada ya wahisani wapatiwa dawa


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi,Ramadhan Khijjah akioyesha kwa wadau mbalimbali chapisho linaloelezea jinsi ya kupata taarifa kwa njia ya tovuti zinatoa ufafanuzi wa Mfumo wa Usimamizi wa Misaada ( Aid Management Platform System) inayotolewa na wahisani mbalimbali kwa Tanzania. Mfumo huo utawawezesha wadau mbalimbali kupata taarifa sahihi ya misaada yote inayotolewa na wahisani kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania.picha ya Maelezo

CUF yapata pigo wagombea wawili wafa


Wagombea wawili wa Chama cha Wananchi (CUF) wamefariki dunia jana visiwani Zanzibar katika matukio tofauti.Waliofariki dunia ni alikuwa Mwakilishi wa Jimbo la Kojani (CUF), Omar Ali Jadi (55) Mkoa wa Kaskazini Pemba na Mwalimu Shani Hamada Shani ambaye ni mgombea wa udiwani wa chama hicho katika Jimbo la Kikwajuni. Jadi alikuwa akiugua ugonjwa wa kisukari na kwamba alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo. Shani alifariki dunia baada ya kugongwa na gari wakati akielekea kuchukua fomu katika Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC), eneo la Maisara.Habari ya Salma Said, Zanzibar. SOURCE: CUF

Tendwa aongeza siku 10 fomu za Gharama za Uchaguzi



MSAJILI wa Vyama vya Siasa, John Tendwa amevitaka vyama vya siasa ambavyo vimeshindwa kupata nakala za fomu ya Gharama za Uchaguzi kuchukua fomu hizo na kuzijaza ndani ya siku kumi, kabla ya kuzikagua na kuweka pingamizi kwa wagombea ambao wameshindwa kuzijaza.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa malalamiko ya baadhi ya vyama kikiwemo Chadema, kudai kukosa nakala hiyo ambayo inaweza kuwasababishia wagombea wao kuwekewa pingamizi kwenye Uchaguzi Mkuu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Tendwa alisema kuwa malalamiko hayo yapo kwenye vyama vingi, jambo ambalo limemfanya aongeze siku kumi kwa ajili ya kuzijaza na kuwasilisha ofisini kwake au ofisi ya mkurugenzi wa Wilaya (DED).

“Nimeongeza siku kumi, kuanzia leo hadi Septemba 6 mwaka huu kwa vyama vya siasa kuchukua fomu hizo na kuzijaza, kwa sababu malalamiko haya hayapo kwa Chadema peke yake bali ni vyama vingi, jambo ambalo limenifanya niongeze siku ya kuzichukua na kuzijaza, hivyo basi wagombea au vyama wanapaswa kuzingatia suala hilo,”alisema Tendwa.

Aliongeza kutokana na hali hiyo vyama vya siasa vinapaswa kuwathibitisha wagombea wake kwenye fomu hizo ili kusiwe na sababu ya kuwekewa pingamizi kwa wagombea walioshindwa kufanya hivyo, jambo ambalo linaweza kuongeza malalamiko mengine kwenye uchaguzi.

Alisema kuwa wagombea ambao wamepita bila ya kupingwa kwenye majimbo yao pia wanapaswa kujaza fomu hizo kwa sababu ya kuthibitisha uhalali wake kwenye vyama na kuzikabidhi kwenye ofisi za DED, ikiwa watashindwa kufanya hivyo wataweza kuwekewa pingamizi na ofisi yake au wagombea wenzake.


Kwa mujibu wa Tendwa, wagombea ambao watashindwa kufanya hivyo wataweza kuwekewa pingamizi la kutokushiriki kwenye uchaguzi mkuu na ofisi yake ikiwa ni pamoja na kufuata utaratibu uliowekwa ndani ya sheria ya gharama ya uchaguzi hivyo basi vyama vya siasa vinapaswa kufuata utaratibu huo.

Alisema, awali fomu hizo alizigawa kwenye mkutano wa mwisho wa kujadili sheria ya gharama za uchaguzi, ambapo baadhi ya vyama vilishindwa kuhudhuria mkutano huo, badala yake wanaamua kulalamikia suala hilo.


“Baadhi ya vyama vya siasa vimezoea malalamiko, ukiwaita kwenye mikutano wanashindwa kuhudhuria badala yake wanaamua kulalamika kana kwamba wameonewa, sasa basi muda niliotoa umetosha, wasipojaza sheria itachukua mkondo wake,”alibainisha.

WAKATI huohuo Mussa Mkama na Lilian Mazula wanaripoti kuwa chama cha NCCR Mageuzi kimesema sheria ya gharama za uchaguzi inapingana na sheria mama ya uchaguzi ya mwaka 1985, kifungu cha (1) sehemu ya 40(ii).
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya ofisi ya chama hicho jana jijini Dar es salaam, mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia alisema kitendo hicho ni hatari kwani kinaweza kusababisha machafuko nchini.
“Uzembe wa ofisi moja ya serikali kutunga sheria kwa nia mbaya isiwe chanzo cha Watanzania kuingia katika vurugu, zisizo na sababu ya msingi” alisema Mbatia na kuongeza kuwa
“Sheria mpya ya gharama ya uchaguzi iliyotungwa mwaka jana, kupitishwa mwaka huu na kusainiwa kwa mbwembwe na rais Jakaya Kikwete katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam kusudio siyo kwa maslahi ya Taifa, bali kwa maslahi binafsi”.
Alisema zoezi hilo la kutunga sheria hiyo kwa makusudi ni batili hivyo msajili wa vyama vya siasa John Tendwa awaache TAKUKURU wafanye kazi yake kwa sababu yeye ameshindwa kuandaa mazingira mazuri ya uchaguzi.
“Kutokana na sheria hiyo bado Tendwa anabolonga kazi yake anaonekana ajiamini na kitu anachokifanya, sheria hiyo mama inasema mgombea anatakiwa aweke pingamizi ndani ya masaa 24, lakini yeye anatoa siku saba huko ni kuvunja sheria” alisema Mbatia.
Hata hivyo Mbatia alisema kitendo cha msajili huyo kuvifanya vyama vya siasa kama wakala wa ofisi yake kwa kutaka vyama vyote vitoe kopi ya fomu hizo na kuzisambaza hadi ngazi ya vitongoji, huku ni kazi ya ofisi yake si utaratibu mzuri.
“Msajili kama alitaka vyama viwe wakala wa ofisi yake aseme tuzungumze, lakini siyo atupe fomu original alafu tuzitoe kopi mitaani, huo ni upungufu anatakiwa aombe radhi” alisema Mbatia kwa msisitizo.
Aidha alisema kutokana na mapungufu hayo tayari uchaguzi umeshaharibika asikae na kusema kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni huru na wahaki, kwa kuwa na mapungufu mengi katika sheria hiyo ambayo hivi sasa inakwenda hovyo hovyo.
“Serikali iliyoko madarakani pamoja na ofisi yake ya msajili imeshindwa kuandaa mazingira bora ya uchaguzi utakaokuwa huru na haki,ambao kwa mara ya kwanza Watanzani wangejivunia kilicho bora” alisema Mbatia.
Hata hivyo Mbatia aliwataka wagombea wa vyama vyote waliowekewa pingamizi na ofisi ya msajili wasiwe na wasiwasi kwa sababu sheria mbili zinapokinzana, mahakama huwa inaangalia sheria mama, amabayo katika uchaguzi ni ya mwaka 1985.
“Pingamizi la msajili wa vyama halina maana yoyote kwa sheria mama, hivyo wagombea endeleeni kufanya kazi zenu kama kawaida” alisema Mbatia. Taarifa hii imeandikwa na Patricia Kimelemeta: SOURCE: MWANANCHI

Monday, August 23, 2010

Pengo: Wanasiasa wengine wapumbavu



BAADHI ya waanasiasa nchini wameelezwa kuwa wana tabia za kipumbavu ambazo hazina tofauti na zile za wanasiasa nchini Ruanda ambao kwa upumbavu wao waliweza kusababisha maafa ya mauaji ya halaiki mwaka 1994.

Askofu mkuu Kanisa Katoliki jimbo kuu la Dar-es-Salaam Mwadhama Policarp Kadinali Pengo alilazimika kutumia kauli hiyo mwishoni mwa wiki mjini Dodoma kutokana na kile alichokisema kuna baadhi ya wanasiasa ambao kwa makusudi wamekuwa wakiwazuia viongozi wa dini kuhubiri habari njema.

Kadinali Pengo ambaye alikuwa akizungumza na halaiki katika kilele cha maadhimisho ya mwaka wa mapadri nchini alisema kuwa kitendo cha baadhi ya viongozi wa dini kuhusihwa katika matukio maovu mfano Mapadri ambao kwa kushirikiana na wanasisa dhalimu waliweza kujihusisha katika mauaji ya halaiki, si sahihi maana si viongozi wote wa dini wenye tabia chafu kama hiyo.

Alisema kauli mbaya dhidi ya viongozi wa dini zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa zimekuwa zikitolewa makusudi kwa malengo ya kuwafanya wananchi wasiwe na imani na viongozi wao wa dini vivyo hivyo kuwafanya viongozi wa dini wakate tamaa na kuacha kuhubiri kuhusu habari njema hasa kukemea maovu yanaweza kujitokeza miongoni mwa jamiii ambayo kwa namna moja au nyingine yangeweza kusababisha maafa kwa taifa.

Alisema endapo viongozi wa dini watayasikia maneno na kauli za baadhi ya wanasiasa aliyewaita wapumbavu watakuwa hawana tena thamani katika jamii endapo watashindwa kuwapuuza wanasiasa hao na kuendelea na changamoto ya kuleta tumaini jipya kwa jumuiya ya maskini.

“Nyinyi (mapadri) msidanyanyike, kwa sababu hata hao mapadri walioshiriki katika mauaji ya halaiki nchini Ruanda walivutwa na wanasiasa wapumbavu ambao walifikiri wanaweza kutwaaa nchi kirahisi kwa mbinu ile chafu,......”,

“Hatuwezi kukataa kuwa kuna mapadri sasa wapo magerezani wamehukumiwa kwa kujihusisha na mauaji hayo ya halaiki, hili lisitukatishe tamaa sisi tukihitajika kufanya utume kwa kuhubiri habari njema, waache wanasiasa waende zao maana wanasiasa wapumbavu sio wapo tu nchini Rwanda, tunao hata hapa Tanzania, kusema mapadri wasisikilizwe ni kukosa akili,”alisema Pengo. Picha na Habari za Israel Mgussi, Dodoma.

MAmbo ya utawala bora hayo


Waziri Sofia Simba akibadilishana mawazo na IGP Said Mwema mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa nane wa wakuu wa kupambana na rushwa katika nchi zilizopo kusini mwa janga la Sahara leo uliofanyika katika hoteli ya Ngurdoto Jijini Arusha(Picha na Moses Mashalla)

Sunday, August 22, 2010

Mgombea aahidi kujenga Machinga Complex



Mgombea Ubunge Jimbo la Moshi mjini kwa tiketi ya CCM, Justine Salakana akihutubia mkutano wa uzinduzi wa kampeni uliofanyika juzi viwanja vya Manyema. (picha na Dionis Nyato).

JK aanguka jukwaaani


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeanza kampeni za uchaguzi mwaka huu kwa vikwazo baada ya mgombea wake wa urais, Jakaya Kikwete kuanguka jukwaani.

Tukio hilo lilitokea jana mchana wakati mgombea huyo anayetetea nafasi yake ya urais akizindua kampeni hizo za CCM katika viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Saalam.

Rais Kikwete aliwasili katika viwanja hivyo saa 7:45 mchana akifuatana na Mgombea Mwenza, Dk Mohamed Gharib Bilal na kupanda katika jukwaa kuu kuungana na viongozi kadhaa wa CCM na serikali akiwa na furaha.
Rais Kikwete alianza kuhutubia saa 9:07 alasiri akitaja mambo mbalimbali yaliyotekelezwa na CCM katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Hata hivyo, dakika 16 baada ya kuanza kuhutubia umati wa wanaCCM waliofurika katika viwanja hivyo alinza kuishiwa nguvu na kasha kupepesuka, lakini walinzi wake walimdaka na kumpa msaada kwa kumdoa jukwaani.

Rais aliondolewa jukwaani na kupelekwa kwenye gari maalum la wagonjwa lililokuwepo uwanjani hapo kwa ajili ya kupatiwa huduma ya kwanza.

Baada ya dakika 14 baadaye alirejea jukwaani akiwa uso wake ukiwa unaonyesha kuchoka ambako aliendelea na hotuba yake kwa dakika tano kabla ya kwenda kuketi meza kuu kwa dakika mbili na kasha kuondoka katika viwanja hivyo.

Akiwa amesindikizwa na walinzi zaidi ya watano kurudi jukwaani, Kikwete alisema,"CCM oyee. Jamani nimefungulia ila niliishia kwenye suala la rushwa.''

Kitendo hicho cha rais Kikwete kukata ghafla hotuba yake kwa mara ya pili kiliwashtua mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo na kusababisha baadhi yao kuanza kulia.

Umati wa watu hao wakiwa wengi wamevaa nguyo za rangi ya kijani na njano ambayo ni rangi ya CCM ulingubikwa na vilio na kelele huku kila mmoja akizungumza maneno yake.

Tukio hilo lilishuhudiwa na familia yake akiwamo mkewe mama Salma, baadhi ya watoto wake, mama Salma Kikwete na marais wastaafu na viongozi wa serikali na chama.

Mama Salma Kikwete alishtuka baada ya tukio hilo, huku baadhi ya watoto wake wakilia.

Baadhi ya viongozi waliokuwepo hao ni marais wastaafu Benjamin Mkapa, Ali Hassan Mwinyi na Rais wa Zanzibar, Aman Abeid Karume.

Wengine ni mke wa Baba wa Taifa Marehemu Julius Nyerere, Maria Nyerere, Mke wa Marehemu Karusme, Mama Shadya Karume, Edward Lowassa, Salim Ahmed Salim, Ali Mohamed Shein na Shamsi Vuai Nahodha.

Mara baada ya Kiwete kuondoka kwenye viwanja hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, John Chiligati alitangaza kuwa hotuba aliyoitoa mgombea huyo, imefungua rasmi kampeni za chama hicho.

''Jamani Rais Kikwete ndio ameshafungua rasmi kampeni za CCM, kwa hiyo huko mikoani na hapa Dar es Salaam watu waanze kampeni. Rais Kikwete amepata tatizo kidogo ila limekwisha, lakini burudani bado zipo. Mnaopenda burudani endeleeni kuwepo katika viwanja hivi, wapo Ze Comedy hapa,'' alisema Chiligati.

Kuanguka kwa mgombea huyo kuligeuza shangwe zilizotawala uwanjani hapo tangu asubuhi kutawaliwa na vilio.

Gazeti hili lilishuhudia zaidi ya watu 15 waliovalia sare za CCM wakianguka chini na kupoteza fahamu huku mmoja wao ambaye alikuwa amevaa kanzu, akinusurika kupigwa kwa kile walichomhisi wenzake kuwa ni mchawi.

Mtu huyo ambaye alikuwa amevaa nguo nyeusi na kilemba cheupe, alianza kuzongwa na wananchi alipoanza kunyanyuka alipokuwa amekaa kiwanjani hapo baada ya kumwona Rais Kikwete akidondoka.

Hata hivyo, aliokolewa na askari polisi waliokuwa karibu na eneo hilo na kumpeleka katika Kituo Kidogo cha Polisi Jangwani kilichopo mita 100 kutoka katika eneo hilo.

Baadhi ya watu waliopoteza fahamu kutokana na mshtuko wa tukio hilo walipelekwa katika vituo vya msalaba mwekundu vilivyokuwa vikitoa huduma ya kwanza uwanjani hapo.

''Jamani siwezi kujizuia inauma sana,'' alisikika mwanachama mmoja akisema kabla kuanguka na kupotesa fahamu.

Tukio hilo lilionekana kama limewatia uchungu wanachama wa CCM kwani baada ya rais Kikwete kuondoka hakuna mwanachama aliyetaka kubaki katika viwanja hivyo licha ya burudani ya vikundi na wasanii mbalimbali iliyokuwepo.

Kikwete alifika uwanjani hapo akitokea ofisi ndogo za CCM-Lumumba akisindikizwa na msafara wa pikipiki zaidi ya 200, magari na watembea kwa miguu waliokuwa wakiimba nyimbo za kumsifu mgombea wao.

Hili ni tukio la nne kwa Rais Kikwete kupatwa na mkasa wa aina hiyo, wakati akiwa jukwaani akihutubia.

Tukio la kwanza lilitokea kwenye viwanja hivyo hivyo vya Jangwani Oktoba 30, 2005, wakati anahitimisha kampaeni za chama hicho. Siku hiyo Kikwete akiwa mgombea wa CCM alionekana aliishiwa nguvu ghafla na kudondoka, kasha kundolewa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Baadaye ilitolewa taarifa kwamba, uchunguzwa na daktari umenyekana kuwa ni mzima na kwamba hali hiyo ilisababishwa na uchovu ulitokana na pilika nyingi za kampeni na wakati huo huo alikuwa anafunga kwa kuwa ulikuwa ni mwezi Mtukufu wa Waislamu.
Tukio la pili, ilikuwa Oktoba 4, mwaka jana wakati akihutubia mamia ya watu katika maadhimisho ya miaka 100 ya Kanisa la African Inland (AIC) kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusiana na tukio hilo, vilieleza kwamba Rais Jakaya Kikwete aliishiwa nguvu jukwaani kisha kubebwa wasaidizi wake kumpeleka katika chumba maalumu kwa ajili ya kupatiwa huduma ya kwanza. Taarifa zaidi soma www.mwananchi.co.tz

Wednesday, August 18, 2010

Mambo ya Yanga na Simba hayo


Baadhi ya mashabiki wa timu za watani wa jadi Simba na Yanga wakinunua bendera katika maandalizi ya mchuano huo ulifanyika jana jioni jijini Dar es Salaam.Picha na Venance Nestory

Meryl na Yacob nusura wachapane makonde



JUMBA la Big Brother Africa All Staes jana iligeuka uwanja wa vita baada ya Meryl na Yacob kuzozana kwa maneno makali kabla ya washiriki wenzao hawajaamua kuwaingilia na kumtaka Yacob amuombe msamaha Meryl.

Yacob ambaye bila woga na mbele ya Mwisho ambaye inasemeka ana uhusiano na Meryl alisikika akisema kuwa mshiriki huyo alitaka kufanya mapenzi na Munya, kitu ambacho kilimkasirisha.

Yacob ambaye awali alilizungumza suala hilo alipokuwa na Kaone na Uti, alidai kuwa Munya alimwacha na kumchukua Tatiana. Meryl alikasirika na kumfuata Yacob.

Mshiriki huyo alisikika akimweleza Yacob kuwa ana uhusiano na watu wengi sana kumshinda yeye hivyo ana uwezo wa kuwaweka nyuma yake na kuwabeba, pia ameshacheza sana na wanaume, hivyo hawezi kumweleza chochote.

Maneno hayo yaliwafanya washiriki wengine kubaki kimya. Baadaye Sheila aliamua kumuuliza swali Yacob, "Hiyo ni tabia yake kuwataka wanaume wa aina yoyote?". Imeandaliwa na Herieth Makwetta.

IGP na majadiliano ya amani na usalama


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP) Saidi Mwema (kushoto) akijadiliana na Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Ulinzi ya Ultimate, Zainul Dossa wakati wa semina kuhusu amani, usalama na utulivu iliyofanyika katika ukumbi wa maafisa wa polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam . IGP alikutana na wakurugenzi wa makampuni yote ya ulinzi nchini kijadiliana kuhusu amani, usalama na utulivu haswa wakati huu tunapoelekea uchaguzi mkuu oktoba, 2010. Picha na Hassan Mndeme- Jeshi la Polisi.

Dk Shein azugumza na wabunge


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na wananachama wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi wa Zanzibar, baada ya kuwahutubia kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika jana katika ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Zanzibar.

Makamu wa Rais Dk Shein, akiwahutubia Wagombea wa Viti vya Ubunge, Uwakilishi na Udiwani pamoja na Wananchi mbalimbali katika ukumbi wa salama Hoteli ya Bwawani Zanzibar jana.


Wagombea wa Viti vya Ubunge, Uwakilishi, Udiwani pamoja na Wananchi mbalimbali wa Zanzibar, kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Wakimsikiliza Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein, alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa Hadhara katika ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Zanzibar jana. Picha na Amour Nassor VPO.

Monday, August 16, 2010

Wapewa Tuzo ya taifa ya Ugunduzi Dar


Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msolla akimtunuku cheti cha mshindi wa kwanza Prof. Mathew Luhanga wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kufuatia Taasisi ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kushika nafasi ya kwanza leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya kutoa tuzo za taifa za ugunduzi na ubunifu na kutoa Mwega kwa ajili ya utafiti mwaka 2010.



Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msolla akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni ishirini Prof. Mathew Luhanga wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kufuatia Taasisi ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kushika nafasi ya kwanza leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya kutoa tuzo za taifa za ugunduzi na ubunifu na kutoa Mwega kwa ajili ya utafiti mwaka 2010.

Thursday, August 12, 2010

Mungai, Mwakalebela waburuzwa kortini



TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Iringa imewafikisha mahakamani aliyekuwa Mbunge wa Mufindi Kaskazini, Joseph Mungai na Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela kwa tuhuma za kutoa rushwa wakati wa mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM.

Katika mchakato huo, Mungai alikuwa anawania ubunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini na Mwakalebela alikuwa akiwania ubunge katika Jimbo la Iringa Mjini.

Mungai ambaye aliangushwa katika kura hizo za maoni baada ya kupata kura 3,430 akiongozwa na Mahmud Mgimwa, jana alifikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Iringa kujibu mashtaka 15.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, Mary Senape, Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Prisca Mpela alisema Mungai na wenzake wawili wanatuhumiwa kufanya kosa hilo Agosti 8 mwaka huu, katika Kata ya Ihalimba, wilayani Mufindi.

Aliwataja washakiwa wengine kuwa ni Katibu wake Moses Masas (38) na Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Mufindi, Fides Cholela (39).

Mpela alisema washtakiwa hao kwa pamoja, walitoa rushwa kinyume na Sheria ya Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15(1)(b) kinachokwenda sambamba na Sheria ya Gharama za Uchaguzi namba 6 ya mwaka mwaka 2010 kifungu namba 21 (1) (a) na kifungu cha 24(8).

Aliendelea kudai mahakamani hapo kuwa kwa pamoja watuhumiwa hao waliwapa rushwa wanachama 15 wa CCM, kila mmoja kwa wakati wake ili kuwashawishi.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa wanachama hao ambao ni viongozi wa ngazi mbalimbali katika Kata Ihalimba na vitongoji vyake, walipewa fedha taslimu kwa viwango tofauti kuanzia Sh 2,000 na 20,000.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka huyo, kwa pamoja washtakiwa hao walifanya kikao katika Kata ya Ihalimba, kilichojumuisha viongozi wa CCM kutoka matawi matano ya kata hiyo.

Aliendelea kuieleza Mahakama kuwa baada ya kikao hicho kumalizika, walipatiwa fedha hizo kwa lengo la kuwashawishi kumchagua Mungai katika kura za maoni zilizofanyika hivi karibuni.

Makosa hayo 15 yanayomkabili Mungai na wenzake, yanajumuisha kitendo cha kumpa rushwa kila mmoja kati ya wajumbe 15 wanaotajwa kwenye mashtaka hayo.

Mpela aliwataja wajumbe hao kuwa ni Obadia Mtokoma, mwenyekiti wa Kijiji cha Vikula ambaye aliyepewa Sh 10,000, Katibu wa Fedha na Uchumi wa Kijiji cha Vikula, Konjeta Kiyeyeu alipatiwa Sh 10, 000, Katibu Kata wa CCM wa Ihalimba, Aldo Lugus alipewa Sh 10,000 na Katibu wa Fedha wa kata hiyo aliyepatiwa kiasi cha Sh 10,000.
Habari imendikwa na Tumaini Msowoya na Hakimu Mwafongo wa MWANANCHI kutoka Iringa.

Ramadhan kareem


Mwezi waonekana hivyo leo Waislamu Tanzania wanaungana na wenzao duniani kote kuanza Mwezi mtukufu wa Ramadhan ambapo Waislam watakuwa wakishiriki Funga ya Mwezi Mtukufu. Blogu hii inawatakia Mwezi Mtukufu na Mungu awajalie nyote mtakao funga Funga njema. Ramadhan Karim

Wednesday, August 11, 2010

Mdau aingia uwanjani


Mdau John Stephen Mwanahabari wa siku nyingi na mwanataaluma wa habari aliyebobea kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino ameingia katika kijiji chetu cha mablogu na sasa anapatikana kwa kubonya hapabaadaye katika mtandao wake

Precision Air yaleta ndege mpya!!



SHIRIKA la Ndege la Precision linalotoa huduma bora Tanzania, limetangaza kuleta ndege yake mpya ya sita aina ya ATR42-500 itakayowasili Agosti 26 mwaka huu kutoka Toulouse, Ufaransa, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza programu ya kutoa huduma za kisasa zaidi. Mkurugenzi Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air, Alfonse Kioko, aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa, ndege hiyo mpya itakayopachikwa jina la Bukoba, itafuatiwa na nyingine ya saba itakayoingia Septemba 15 mwaka huu.
Mwaka 2006, Precision na ATR ya Ufaransa walisaini mkataba wa dola za Marekani milioni 129 ili kutoa ndege saba mpya. Ndege ya kwanza kati ya hizo iliwasili Machi 2008. Tangu wakati huo, Precision imepokea ndege tano aina ya ATR 72-500 na kufanya iwe na ndege tano mpya mpaka sasa. Pia ina ndege nyingine tatu za zamani. Kioko alisema baada ya ndege hiyo yenye namba 5H-PWF kuwasili, wataizindua Dar es Salaam Agosti 27.
Alisema ina vifaa vya kisasa vya burudani kwa ajili ya wasafiri kuangalia sinema na kusikiliza muziki wakiwa safarini. Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 70. Mkurugenzi huyo pia alitangaza kwamba tangu kuanza mwaka mpya wa fedha, idadi ya abiria wapya imeongezeka kwa asilimia 12 kulinganisha na mwaka jana. Pia mizigo ya biashara imeongezeka licha ya kudorora kwa uchumi duniani.
Akizungumza katika mkutano huo, Meneja Masoko wa Precision, Emillian Rwejuna alisema kampuni hiyo inatarajia kupata ndege ya Boeing 737, kati ya Oktoba na Novemba mwaka huu. Rwejuna alisema kupatikana kwa ndege hiyo kutapanua wigo wa huduma za safari.
Ndege hiyo ya tatu aina ya Boeing 737 itaboresha safari za Johannesburg, Afrika Kusini, na pia katika miji ya Kinshasa na Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Precision Air hivi sasa inafanya safari katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Tabora, Musoma, Shinyanga, Kigoma, Kilimanjaro, Zanzibar, Mtwara na Arusha. Pia ina safari za Nairobi na Mombasa, Kenya na Entebbe, Uganda. Taarifa ya Precision Air

Monday, August 09, 2010

Lil Kim, Juma nature wafunika fiesta jipanguse 2010




Lil Kim baada ya kupiga songi zake kadhaa, alimuita msanii Juma Nature jukwaani na kuanza kuimba nae,ama kwa haki kuliibuka makelele na mayowe ya shangwe ile mbaya uwanjani hapa usiku huu. Picha zote za Silvan Kiwale na Michael Momburi

REDD’S FASHION PARTY 2010 & fiesta jipanguse 2010 ilivyofana.


Lil Kim akiwahamasisha wakazi wa jiji la Dar waliofurika usiku huu ndani ya viwanja vya Lidaz Club katika tamasha la Fiesta Jipanguse, tamasha ambalo mdhamini wake mkuu ni kampuni ya bia ya Serengeti a.k.a Mfalme wa raha kamili .


Alaji alaji alaji mpaka chini….pichani ni Warembo wakiwa wamepandwa na mzuka na wimbo huo ambao umeshika chati sana kwa sasa hapa nchini.Picha zote kwa hisani ya Mo Blog.

Sunday, August 08, 2010

Jk :Sihitaji kura za wafanyakazi



Mwanachama wa Chama cha Chadema akiwa amevalia fulana ya CCM yenye picha ya Rais Kikwete jana katika mkutano wa chama hicho jijini dar es salaam na kuandikwa maandishi yasemayo 'Kikwete: Sihitaji kura za wafanyakazi'. Picha ya Said Powa

Thursday, August 05, 2010

Mambo ya Polisi na mihanjo yao


Mkuu wa Wilaya ya Chato Bi. Khadija Nyembo akikagua gwaride maalum lililoandaliwa na askari wa Wilaya hiyo kwa ajili ya kumkaribisha Kamishna wa Polisi anayeshughulikia Operesheni Paul Chagonja wakati wa ziara yake ya ukaguzi Mkoani Kagera.

Askari wa Wilaya ya Muleba wakiwa wamejipanga katika mtindo wa kuhami Kituo wakati wanaonyesha zoezi hilo kwa Kamishna wa Operesheni, Paul Chagonja katika ziara ya ukaguzi wa maeneo mbalimbali ya Polisi Mkoani Kagera.

Kamishna wa Operesheni, Paul Chagonja akisalimiana na wanakijiji wa Kagoma, Wilayani Muleba, Mkoani Kagera mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa uhamasihaji wa Ulinzi Shirikishi kiujijini hapo.

Mjomba akikamua Nanenane Moro


Msanii wa muziki Mrisho Mpoto akitumbuiza baadhi ya wananchi waliokuwa wakitembelea banda la Wizara ya Fedha juzi katika maonyesho ya Nanenane kanda ya kati yanayoendelea mkoani Dodoma.
Picha na Masoud Masasi.

Mrema: Vunjo wamenileta mtetea



MWENYEKITI wa Taifa wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema jana alitembea umbali wa zaidi ya kilometa 10 kwa miguu kuudhihirishia umma kuwa yuko fiti alipokwenda kuchukua fomu za kugombea Ubunge Jimbo la Vunjo, huku akifurahia wanaCCM kumletea mgombea ambaye yeye alimwita mtetea na yeye (Mrema) ni jogoo atakayempanda mtetea huyo.

Mrema akifuatana na mgombea Urais wa TLP,Mutamwega Mganywa walitembea kwa miguu kutokea kijiji cha Chekereni kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi mji mdogo wa Himo huku akisindikizwa na mamia ya wanachama wa TLP.

Wanachama hao wakiwa wamevalia fulana za njano zenye nembo ya TLP na maneno "Vunjo hatudanganyiki" walikuwa wakishangilia huku vijana waliokuwa wakiendesha pikipiki zaidi ya 40 wakifanya vituko mbalimbali kama ishara ya kushangilia.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara baada ya kukabidhiwa fomu hizo,Mrema aliwapongeza wanachama wa CCM wa Jimbo la Vunjo kwa kuamuangusha Mbunge aliyemaliza muda wake, Aloyce Kimaro katika kura za maoni.

“Wana-CCM Vunjo ni watu wazuri sana hongereni sana kwa sababu kitu kikubwa mlichokifanya ni kumuondoa Kimaro kwa sababu anapesa nyingi na angenisumbua sana lakini mmeniletea Mtetea na mimi ni Jogoo”alitamba Mrema.

Katika mchakato wa kura za maoni,wakili na mwanasheria wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Chrispin Meela aliongoza kwa kupata kura 7,732 dhidi ya Kimaro aliyepata kura 3,207 na hivyo kushindwa kutetea kiti chake.

Huku akitumia misemo ya Kiswahili kufikisha ujumbe wake wakati akiwaomba wananchi wa Jimbo hilo wasimsaliti, Mrema aliwaambia wananchi hao siku zote hajawahi kuwaomba samaki wakampa Nyoka na anaamini hawatamsaliti.

Mrema alisema ameamua kugombea Ubunge Jimbo la Vunjo kwa kuwa anasukumwa na dhamira ya dhati ya kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi ikiwamo kuongeza uzalishaji wa kahawa bora na kutatua kero ya maji mji wa Himo.

Lakini Mgombea aliwaomba wananchi hao wamuwezeshe kuwa Mbunge kwani ana siri nzito ya namna alivyokamata vigogo wakiwa wanatorosha dhahabu nje ya nchi na mahali pekee anataka kutoboa siri hiyo ni Bungeni.

Mrema alisema aipokamata dhahabu hiyo yenye thamani ya sh175 Milioni kwa wakati huo, alimwita Inspekta Jenerali na kumuuliza wawachukulie hatua gani watuhumiwa hao lakini mkuu huyo wa polisi akashikwa na kigugumizi.

“Nikamwendea Rais wangu Mpendwa Mwinyi (Ali Hassan) nikamwambia Mheshimiwa Rais tuwafanyeje hawa watuhumiwa naye nikaona anashikwa na kigugumizi na hivi sasa wanatanua huko Kariakoo,”alidai Mrema.

Wednesday, August 04, 2010

UN Secretary-General's statement on United Republic of Tanzania


United Nations Secretary-General Ban Ki Moon.
The Secretary-General congratulates the people of the United Republic of Tanzania, particularly of Zanzibar, for the peaceful holding of their recent referendum in Zanzibar. He also welcomes the inter-party agreement between the two main political parties, Chama Cha Mapinduzi and Civic United Front, that led to the referendum, aimed at paving the way for a long term reconciliation. The Secretary-General is encouraged by the determination of the people of Zanzibar to build a peaceful and united future, and reiterates the readiness of the United Nations to assist them.

'Helikopta ya Dk Slaa' yapata hitilafu


Dk. Willibrod Slaa katika msafara uliompokea mjini Songea

'''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chadema, Dk. Willbrod Slaa, jana alipanda jukwaani saa 12.04 na kumaliza saa 12.30 jioni, huku akieleza kuwa kuchelewa kwake kumetokana na Helkopta yake kupata hitilafu akitokea mjini Songea, hali iliyomlazimu kukodi ndege ya dharura ili aweze kuwafikia wananchi hao waliokuwa wakimsubiri tangu saa 9 mchana.

Alisema umasikini wa wakazi wa mikoa ya kusini, Lindi, Mtwara na Ruvuma unatokana na wakazi hao kuikumbatia CCM, na kwamba ni wajibu wao kupima hali zao za maisha miaka 40 tangu Tanzania ipate uhuru huku CCM kikiwa chama pekee kilichotawala.

“CCM ndiyo iliyowafikisha hapo mlipo, miaka 40 tangu uhuru bado hali ya maisha ya watu wa kusini ni duni, barabara ni moja tu ya lami, ukiacha hiyo utang’atwa na nyoka maporini” alibeza mgombea huyo.

Baadhi ya wasikilizaji wakiongea na mwandishi wa habari hizi walimsifu Dk. Slaa kwa hotuba yake ya ushawishi, huku wengine wakimdhihaki kwa madai kuwa pweza aliyeitabiria Hispania kutwaa kombe la dunia pia amemtabiria Dk. Slaa kuwa rais.

“Dk. Slaa kwangu namuona ni mtu anayekerwa na matatizo ya watanzania maana hata hotuba yake imeweka wazi na kuchambua matatizo yetu……pweza amemtabiria kuwa rais” alisema Joshua George

Wakenya wajitokeza kwa wingi kura ya katiba


Kenya's Prime Minister Raila Amollo Odinga casts his ballot on August 4, 2010 at Old Kibera Primary School where he went to cast his vote in the ongoing constitutional referendum. Kenyans voted Wednesday on a proposed constitution to make their institutions more democratic amid tight security aimed at preventing a repeat of deadly post-election violence in 2007-8. AFP / PHOTO

**************************************************************************************************
WANANCHI wa Kenya, jana walijitokeza kwa wingi kupiga kura ya maoni (maamuzi) itakayoamua kama nchi hiyo iwe au isiwe na katiba mpya.

Kwa muda wa miaka 20 sasa, kumekuwepo na shikinizo la kutaka kuundwa kwa katiba mpya ili kukidhi mahitaji ya kizazi kipya nchini Kenya, hasa kwa kuzingatia kuwa katiba ya sasa iliundwa mara tu baada ya uhuru wa nchi hiyo.

Kuanzia saa kumi za usiku wa kuamkia jana tayari kulikuwa na mistari mirefu ya wapigakura katika vituo vya kupigia kura, vya maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi.

Wakenya 12,470, 443 waliojiandikisha kupiga kura, wanatarajiwa kubadilisha historia ya nchi hiyo ikiwa watapiga kura ya ndio kutaka mabadiliko ya katiba.

Kenya nzima ina vituo vya kupigia kura 27,000 na ina majimbo 210.

Ikiwa zaidi ya asilimia 50 ya wapigakura watasema ndio, ina maana ya kuwa kutakuwa na mabadiliko makubwa katika muundo mzima wa serikali na uendeshaji wake.

Rais Mwai Kibaki, aliwataka Wakenya kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

"Kura hii si ya Kibaki, ni kura yenu nyinyi Wakenya kwa maisha yenu," alisema kiongozi huyo wa Kenya.

Mke wa Dk Slaa ahamia Chadema


ALIYEKUWA mgombea wa Ubunge wa jimbo la Hanang,kupitia CCM, Rose Kamili leo anatarajia kurejesha kadi ya CCM na kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wilayani Hanang mkoani Manyara.

Kamili ambaye ni Diwani wa CCM tangu mwaka 1994 katika kata ya Basotu, alitangaza uamuzi huo, juzi mara baada ya kutangazwa matokeo ya Ubunge ambapo, yalionesha ameshindwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Mary Nagu.

Kamili ambaye ni mke wa Dk Slaa, mgombea wa Urais wa Chadema mwaka huu, alisema ameamua kujiondoa CCM kutokana na kutoridhishwa na mwenendo ya chama hicho hasa katika kampeni za ubunge.

"napenda kutangaza wazi kuwa mimi siwezi kumuunga mkono Nagu katika kampeni za ubunge na natarajia kurejesha kadi ya CCM kesho(leo)"alisema Kamili.

Kamili alisema ameamua kujiondoa CCM kutokaa na kutoridhishwa na uchaguzi huo, hasa kutokana na kitendo cha Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Michael Sakra kupiga kampeni wilaya nzima ashindwe.

"katibu amekuwa akiwaita viongozi wote wa CCM na kuwaagiza kuhakikisha Nagu anashinda wametumia fedha na hila nyingi hivyo nimeona basi mchango ambao nimeutoa CCM kwa zaidi a miaka 20 unatosha"alisema Kamili

Hata hivyo, alisema uamuzi wa kugombea ubunge au kutogombea atautangaza lakini anaimani chadema ina mgombea mwingine mzuri katika jimbo hilo.

Uamuzi wa kamili kujiunga na chadema utakuwa ni pigo kubwa kwa CCM Hanang na hasa kutokana na nguvu kubwa aliyokuwa nayo katika wilaya hiyo. Imeandikwa na Mussa Juma, Arusha: SOURCE MWANANCHI

Sunday, August 01, 2010

Dk Slaa atisha Kigoma


Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Deomkrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, akihutubiakatika mkutano wa hadhara wa kuomba udhamini, uliofanyika mjini Kigoma jana. (Picha na Joseph Senga)

Rais aongoza kura za maoni CCM



Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo, Jumapili, Agosti Mosi, 2010, alikuwa miongoni mwa maelfu kwa maelfu ya wanachama wa CCM nchi nzima ambao wamepiga kura ya maoni ndani ya chama hicho.
Kikwete, akifuatana na Mama Salma Kikwete, amepiga kura yake ya maoni katika kijiji cha kwao cha Msoga, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani ambako ameandikishwa kama mpiga kura.
Kura ya maoni ya CCM inalenga kuchagua nani wana-CCM wanaamini anafaa kuwa mgombea nafasi ya ubunge na udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kupitia chama hicho katika majimbo na kata mbali mbali nchini.
Mheshimiwa Kikwete amewasili kwenye Kituo cha Kupigia Kura cha Ofisi ya CCM ya tawi la Kijiji cha Msoga majira ya saa nane mchana na kujiunga na wapiga kura wengine kwa ajili ya zoezi hilo muhimu kwa Chama cha Mapinduzi.
Mara baada ya kupiga kura yake, Rais Kikwete amerejea Dar es Salaam.