Friday, March 24, 2023

Halotel yatoa Msaada wa vifaa vya Usafi Manispaa ya Mjini Zanzibar

Kampuni ya Mawasiliano ya simu Halotel kupitia imekabidhi vifaa mbalimbali vya kufanyia Usafi kwa Manispaa ya Mjini Zanzibar, ikiwa ni moja ya msaada wa kuhakikisha Mji wa Zanzibar unatunzwa kwa usafi na kukuza shughuli za kitalii na uchumi wa mji huo ikiwa ni sambamba na kuadhimisha miaka miwili ya Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Dkt Hussein Ali Mwinyi.

Kampuni ya Halotel inayo sera ya kurejesha Kwa jamii.Sera hiyo imejikita katika kuhahakikisha kuwa wajibu wa kushirikiana na taasisi binafsi na za serikali katika kuboresha ustawi wa jamii, ilikuchochea maendeleo ya Taifa na watanzania kwa ujumla katika sekta mbalimbali ikiwemo afya na elimu.

Akizungumza wakati wa tukio la makabidhiano ya vifaa hivyo katika viwanja vya Malindi Zanzibar, Naibu Mkurugenzi wa Huduma za Halopesa, Magesa Wandwi, alisema kampuni hiyo na sera ya kurejesha sehemu ya faida kwa jamii, taasisi binafsi na za serikali kuimarisha ustawi wa jamii.

“Tumeamua kutoa vifaa vya usafi na mabango ya elimu kwa wananchi juu ya wajibu wa ushirikiano katika kutunza mazingira na kuuweka mji katika hali nzuri kuvutia watalii na wenyeji. Hatua hii ni sehemu ya kampuni yateu na kuwaunga mkono kazi nzuri zinazofanywa na uongozi wa awamu ya nane chini ya Rais Dr. Mwinyi, ambae anaonekana kwa moyo wa dhati kutaka kuweka mji wa Zanzibar katika hali ya kupendeza na kuwa kivutio kikuu cha wageni wanaoingia hapa nchini,”alisema Magesa.

Aidha Magesa aliongeza kuwa “Nina matumaini kuwa vifaa hivyo vitatuzwa na vitawekwa katika sehemu zote zinazostahili kwa matumizi sahihi ili vitumike katika matumizi yaliyokusudiwa”.

Akipokea vifaa hivyo wakati wa makabidhiano yaliyofanyika katika viwanja vya Malindi Zanzibar Mkuu wa Wilaya ya Manispaa ya Mjini Mhe Rashid Simai Msaraka ameihakikishia kampuni ya Halotel kuwa Manispaa ya Mjini itatengeneza mkakati madhubuti wa usafi wa mji kupitia vifaa hivyo.

“Kwa muda mrefu Manispaa hii imekuwa ikitafuta mbinu ya kukabiliana na changamoto ya uchafu lakini kupitia msaada huu kutoka kampuni simu ya Halotel, umetufaa sana na baraza litahakikisha linawashughulikia wale wote wanaotupa taka hovyo katika maeneo mbalimbali ya mji.”

“Napenda kutumia fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza kampuni ya Halotel kwa kuliona hili na kutuunga mkono kwa kutuletea vifaa hivi muhimu, ninawaagiza watendaji wa manispaa hii kutimiza wajibu wenu ili mji uwe safi. Ninaiomba jamii pia kutambua kuwa suala la usafi si la manispaa pekee bali ni watu wote, hivyo baraza lina haki ya kumshughulikia kila atakayekwenda kinyume na utunzaji mazingira.” Alisisitiza Mh. Msaraka.

Zaidi ya shilingi Milioni 54 kutoka Kampuni ya Halotel zimetumika kwaajiliya kunua vifaa vya kusafishia mji ikiwemo 4 wheel Dustbin za lita 660, jumla 10, 2 wheel Dustbin za lita 240 zikiwa 50, mabwela suti 100, fagio 100, reki 100, toroli50, Shovel 50, glovu 100, bibs 100.

Halotel inaendelea kusambaza miundo mbinu ya Mawasiliano na kuboresha huduma hii ili kuwafikia watanzania wote kama ilivyokuwa dhima ya serikali kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia wananchi katika maeneo yote.

Katika kuboresha huduma hii ya Mawasiliano Kwa wateja wetu, Kwa mwaka 2022 kampuni imeongeza minara mipya zaidi ya kumi na saba (17) ya masafa ya 4G ambayo ni kwa Upande wa Unguja na kwa kisiwa cha Pemba, inayowawezesha kupata huduma bora za intaneti.
Naibu Mkurugenzi wa Halopesa Magesa Wandwi (kulia katikati) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mjini Iliyopo Zanzibar Mh. Rashid Simai Msaraka ( kushoto katikati) moja ya vifaa vya usafi kama ishara wakati wa tukio la makabidhiano ya vifaa vya Usafi vilivyogharimu zaidi ya Shilingi Milioni 54 katika eneo la viwanja vya Malindi Zanzibar. Pamoja nao ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Mjini (wa tatu kulia mbele) baadhi ya wafanyakazi wa Halotel na wawakulishi kutoka vikundi mbalimbali vya usafi wa Manispaa ya Mjini Zanzibar.
Vifaa vya usafi vilivyotolewa kwa Manispaa ya Mjini iliyoko Zanzibar kwaajili ya usafi.

NAIBU WAZIRI MIZENGO PINDA ATAKA MABADILIKO MAKUBWA NHC

  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Hamad Abdallah Hamad  akitoa ufafanusi wa jambo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Geofrey Mizengo Pinda leo hii Kambarage House Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Geofrey Mizengo Pinda akitia saini kitabu cha wageni leo hii Kambarage House Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuwasili.
 

Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Shirika la Nyumba la Taifa, Fatma Chillo akifafanua hoja kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Geofrey Mizengo Pinda wakati wa mkutano na Naibu Waziri  Kambarage House Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Geofrey Mizengo Pinda akizungumza na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo Kambarage House Jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Geofrey Mizengo Pinda ametaka kuwapo mabadiliko makubwa katika nyanja zote za utoaji huduma kwa Watumishi wa Shirika la Nyumba la Taifa ili waweze kuleta tija kubwa kwa Shirika na Taifa kwa ujumla.

Naibu Waziri Pinda aliyasema hayo baada ya kufanya ziara ya siku moja kufahamu kazi zinazofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na kuzungumza na Wafanyakazi wa Makao Makuu kwa niaba ya Wafanyakazi wote wa Shirika.

“Nichukue nafasi hii kuwapongezeni kwa kazi kubwa mnazozifanya kawa maendeleo ya Taifa, lakini niwachagize kuwa tunataka mabadiliko makubwa ya utoaji huduma ndani ya Shirika la Nyumba la Taifa kwa kila mmoja kufanya kazi apaswayo, mpendane, mheshimiane na mthaminiane na sisi kama Serikali tutawaunga mkono kama mlezi wenu,”amesema.

Ameutaka uongozi wa Shirika hilo kuutumia ujuzi wa Mkurugenzi Mkuu ambaye ameteuliwa akitokea katika uongozi kwenye taasisi ya sekta binafsi ili Shirika liweze kukua kwa kasi kibiashara kama linavyotakiwa.

“Fanyeni sensa ya kutambua nyumba zenu nchi nzima na mpitie mikataba yenu na wapangaji kuwe na utafiti wa mahitaji ya nyumba maeneo mbalimbali nchini kuna wapangaji wenu wanawapangisha watu wengine kwa fedha nyingi huku wakilipa NHC fedha kidogo, hili siyo jambo jema,”amesema.

Ametaka kuongezwa kasi ya kudai kodi kwa wadaiwa sugu wa Shirika hilo na kwa zile taasisi za Serikali ambazo nazo ni wadaiwa sugu orodha yao iwasilishwe Wizara ya Ardhi ili kusudi Wizara isaidie kudai kupitia kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Amependekeza pia uanzishwaji wa vijiji vya mfano vyenye kuleta tija lakini vyenye kuwasaidia Watanzania waliopo pembezoni mwa nchi pamoja na kwamba Shirika linaendeshwa kibiashara.

Ameelekeza ushirikishwaji wa Wafanyakazi wote kwa Menejimenti inapoamua kuyabuni mawazo ya maendeleo “Mimi nataka ustawi wa watumishi pia muwape malengo, watekeleze majukumu yao wanayotakiwa kuyatekeleza, lakini pia wapewe motisha ya kutosha ili kuwa na tija kwa nchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Hamad Abdallah alielezea umuhimu wa Serikali kulisaidia Shirika ili kuhakikisha kwamba Watanzania wengi zaidi wanapata makazi bora.

“Kadri idadi ya watu inavyozidi kuongezeka, uhitaji wa makazi unaongezeka pia. Idadi ya Watanzania inaongezeka kwa asilimia 3.1 kila mwaka ambayo inapelekea kuzidi kwa upungufu wa nyumba za makazi nchini. Hadi sasa kuna uhitaji wa nyumba milioni tatu na laki nane za makazi nchini,amesema Hamad.

Hamad amesema kuwa miaka ijayo asilimia 48 ya Watanzania wote watakuwa wanaishi mijini hivyo kuna haja kubwa ya kuongeza idadi ya makazi katika miji na nchini kwa ujumla.

Amesema kuwa Serikali haina budi kuunga mkono juhudi za Shirika katika uendelezaji wa miliki kwani kwa kupitia utekelezaji wa shughuli tofauti za Shirika kuna manufaa tofauti kama vile upatikanaji wa ajira kwa Watanzania, kuongezeka kwa pato la Shirika kupitia uuzaji na upangishaji wa nyumba na taasisi nyinginezo kama vila Tanesco na Mamlaka za maji na pia inachangia kwa kiasi kikubwa katika uendelezaji wa viwanda nchini kwani ujenzi wa nyumba unajumuisha matumizi ya  bidhaa za  ujenzi kama vile nondo, mabati, saruji n.k

“Riba kubwa zinazotozwa na mabenki pindi wananchi wanapochukua mikopo ya ujenzi asilimia 14 hadi 20 pamoja uwezo mdogo wa kiuchumi wa Watanzania wengi ni mojawapo kati ya changamoto zinazozuiya ukuaji wa sekta ya nyumba,alisema Hamad.

Alieleza kwamba idadi kubwa ya Watanzania wana vipato vidogo hivyo, riba ya asilimia 14 hadi 20 ni kubwa kwao pindi wanapochukua mikopo benki.

Pia hakusita kueleza jinsi Shirika lilivyomudu kuwapatia wanunuzi wake mikopo ya nyumba kwa riba ya asilimia 9 kwa Watanzania wanaonunua nyumba Iyumbu, Dodoma.