Monday, March 31, 2014

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (katikati), Andrew Chenge (kulia) na James Mbatia wakiteta jambo bungeni mjini Dodoma leo Machi 31, 2014.

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Anne Makinda ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akibadilishana mawazo na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Kificho ndani ya bunge leo.…
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (katikati), Andrew Chenge (kulia) na James Mbatia wakiteta jambo bungeni mjini Dodoma leo Machi 31, 2014.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Anne Makinda ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akibadilishana mawazo na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Kificho ndani ya bunge leo.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
2 (2)Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Tundu Lissu akitanga Kamati ya Uongozi kutoa ratiba itakayoongoza shughuli za Bunge hilo leo mjini Dodoma
3 (3)Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Zakia Meghji(kushoto) na Christopher Ole Sendeka(kulia) wakijadiliana leo mjini Dodoma kabla ya kuelekea katika Kamati zao kwa ajili ya kuanza kupitia rasimu ya Katiba mpya. 5 (1)Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Anne Makinda (kushoto) na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Namelok Moringe Sokoine (kulia) wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma kabla ya kuelekea katika vikao vya Kamati mbalimbali za kupitia vifungu mbalimbali rasimu ya Katiba mpya zoezi ambalo  limeanza leo .8bWajumbe wa Bunge Maalum la Katiba James Lembeli (kushoto) na Mchungaji Peter Msigwa (kulia) wakijadiliana leo mjini Dodoma kabla ya kuelekea katika Kamati zao kwa ajili ya kuanza kupitia rasimu ya Katiba mpya. 9Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta akiondoka katika ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirisha kikao cha Bunge leo mjini Dodoma ambao wajumbe wameelekea katika Kamati zao mbalimbali kupitia vifungu vya rasimu ya Katiba Mpya.
Picha na Tiganya Vincent-Dodoma.

ANGALIA MAJINA YA WALIMU WALIOBADILISHWA VITUO VYA KAZI


AJALI MBAYA SANA 14 WAFA, WAOKOAJI NAO WAZOLEWA WAFA WAFIKIA 21


Watu 21 wamefariki dunia katika ajali mbaya imetokea Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani ikihusisha magari 3 na wengine 11 kujeruhiwa.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Ulrich Matei, alisema ajali hiyo imetokea katika Barabara Kuu ya Dar es Salaam-Lindi, eneo la Ikwiriri, wilayani humo.
Awali ajali hiyo ilihusisha magari mawili, Toyota Hiace (T 948 CUX), iliyokuwa ikitokea Ikwiriri kuelekea Rufiji ambalo lilikwenda kukwaruzana na Lori(T 132 AFJ) kwa nyumba, ambalo lilikuwa limeharibika na kusimama barbarani.
Alisema baada ya kulikwaruza roli hilo, mlango wa Hiace uling'oka na kubaki kwenye roli ambapo gari hiyo lilipoteza mwelekeo na kwenda kugongana uso kwa uso na gari nyingine aina ya Canter(T 774 CJW) na kupinduka.
"Katika ajali hii, watu 14 walifariki dunia papo hapo, wakati polisi na baadhi ya wananchi wakiendelea kuwaokoa majeruhi ili wakimbizwe hospitali, likatokea basi la kampuni ya Mining (President)( T 242 BXA), kuwakanyaga watu waliokuwa wakitoa msaada na kuwaua ndio maana idadi ya waliokufa imefikia 21.
"Basi hili lilikuwa linatoka Lindi kuelekea Dar es Salaam...polisi walifanya jitihada za kulisimamisha lakini dereva wake alikataa kusimama na kwenda kukanyaga watu lakini tayari tumemkamata, majeruhi mmoja amehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam," alisema Kamanda Matei.
Kamanda Matei alisema, basi hilo linashikiliwa polisi ambapo uchunguzi ukikamilika, dereva wake atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka.
Aliwataja waliokufa ni Sixtus Ally Mtanga(32) na Nassoro Mohamed Kajani(20) wakazi wa Ikwiriri, Juma Said Kitambulilo(30) na Salum Goma Makonde (50), Ustaadhi Kalilambwe(34) na Shafil Kip (30), Wasabi Sabil(45), Ramadhani Ally (23)wote wakazi wa Mbagala.
Shabani Bakari(30) Kondakta wa Hiace, mkazi wa Kibiti, Masud Abulal (27), mkazi wa Mkuranga, Ammi Mpemba (30)na Madadi Hassan Mangasongo (45) wakazi wa Jaribu na Japhet Ponsian (24), mkazi wa Dar es Salaam.
Pia yupo Said Ally China (21) mkazi wa Kimanzichana, mkazi wa Jaribu, Abdalahaman Yusuph Kihemke(45), mkazi wa Kongowe na Fikiri Said Sauze, mkazi wa Vikindu.
Wengine ni Nywari Mshigani mkazi wa Dar es Salaam, Hassan Wasabi (18), mkazi wa Kibiti na Seleman Mcharazi (47) mwingine aliyejulikana kwa jina moja la Mustafa, wote wakazi wa Mbagala na maiti ya mwanamke haijafahamika jina lake.
Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Frank Sixmundi (31), dereva wa gari la Maliasili Kibiti ambaye alifika eneo ili kutoa msaada kwa majeruhi ambaye ameumia kichwani, Mohamed Salehe (49) na Charles Rogasani (23), wote wakazi wa Kibiti na Mohamed Mengine (42), mkazi wa Dar es Salaam.
Wengine ni Mniko Magige Mango (54) na Abdalah Issa (25) wakazi wa Mkuranga, Khalid Salum (32), mkazi wa Dar es Salaam, Ahmad Yusuph (23), mkazi wa Kigamboni na Shomari Yusuph (42), mkazi wa Mburahati. Majeruhi wamelazwa katika hospitali za Ikwiriri, Misheni ya Mchukwi na wengine hospitali ya Taifa Muhimbili.

UZINDUZI MAALUMU WA SHINDANO LA SCHOOLAR INVESTMENT CHALLENGE 2014 (UDBS)


Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila (kushoto) akizungumza na viongozi wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), mara baada ya uzinduzi wa Shindano la linalohusu uelimishaji wa umuhimu wa kuweka akiba kwa uwekezaji kwa wanavyuo walio katika taasisi za elimu ya juu nchini. Kutoka (kulia) ni  Mkuu wa Idara ya Uhasibu Dkt. Henry Chalu,  Ofisa Mtendaji Mkuu, Moremi Marwa na Mkuu wa Shule Kuu ya Biashara, Dkt. Wineaster Anderson.
   Mgeni Rasmi Alexander  Mwinamila akizungumza na Ofisa Mtendaji Mkuu, Moremi Marwa  (kushoto) mara baada ya kuzindua mpango huo Chuo Kikuu Ukumbi wa Nyerere Theatre II, Dar es Salaam
                                                       Hotoba ya mgeni rasmi
                         Baadhi ya wanafunzi waliohudhulia uzinduzi huo wakisikiliza hutoba ya mgeni rasmi
    Wanafunzi na wageni mbalimbali wakisikiliza kwa makini hutoba na maelezo kuhusu mpango huo.

Mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mathayo Mang'unda Torongey akiendelea na mikutano ya Kampeni Jimboni Chalinze.

DSC_0216
Ally Bananga, mgombea wa Chadema Mathayo torongey na viogozi wengine wakiwa katika kampeni Jimbo la Chalinze.
IMG_20140327_173115
Mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ndugu Mathayo Mang'unda Torongey akiendelea na mikutano ya Kampeni Jimboni Chalinze, Ijumaa Machi 28, 2014,
SOMA ZAIDI

RIDHIWANI KIKWETE AENDELEA NA KAMPENI CHALINZE

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akizungumza na Baadhi ya Viongozi wa Dini kwenye Kijiji cha Mkange,Kata ya Mkange wakati alipopita kuwasalimia na kuwaomba ridhaa ya kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Jana Machi 30,2014.Picha zote na Othman Michuzi.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Sam wa Ukweli akitoa Burudani kwa wananchi wa Kijiji cha Java,Kata ya Mkange jana Machi 30,2014.
Shangwe kwa wananchi wa Kijiji cha Java,Kata ya Mkange.
Wananchi wa Kijiji cha Java,Kata ya Mkange wakifatilia kwa makini Mkutano wa Kampeni za CCM.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akisalimiana kwa furaha na wakinamama wa Kijiji cha Java,Kata ya Mkange jana Machi 30,2014.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akimsikiliza kwa Makini Mzee Hussein Mwindadi ambaye ni Baba wa Diwani wa Kata ya Mkange.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akitaniana na Mzee Nassor Samnamwanja wa Kijiji cha Mkange, Kata ya Mkange jana Machi 30,2014.
Wakazi wa Kijiji cha Manda Mazingara wakiwa wameshika mabango ya Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati walipokuwa wakimkaribisha Kijijini kwao.
Kikundi cha Kwaya ya Kijiji cha Manda Mazingara kikitoa Burudani.
wakisikiliza jambo kwa Makini.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Manda Mazingara,Ibrahim Rajab Mahede akizungumza wakati wa kutoa taarifa ya Kijiji kwa Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete.
Diwani wa Kata ya Mkange, Abdallah Mwendadi akiwasalimia wananchi wake wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM katika Kijiji cha Manda Mazingara jana Machi 30,2014.
Meneja wa Kampeni wa CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Steven Kazidi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Manda Mazingara jana Machi 30,2014.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akinadi sera zake kwa wananchi wa Kijiji cha Manda Mazingara wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika jana Machi 30,2014.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akimsalimia Mzee Salum Ramadhan Satajiri.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akionyeshwa maendeleo ua ujenzi wa Msikiti (haupo pichani) na Sheikh Yahya Abdullah Imam wa Msikiti huo.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akizungumza machache na wananchi wa kijiji cha Chamakuru,aliposimama kuwasalimia akiwa safarini kwenye Kijiji cha Miono.
Wananchi wa Kijiji cha Manda Mazinga wakifatilia kwa makini Mkutano wa Kampeni za CCM zilizofanyika jana Machi 30, 2014.