Monday, March 19, 2012

Rais Jakaya Kikwete Amwapisha Meja Jenerali Samwel Ndomba Kuwa Mkuu Mpya wa JKT

Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi miongozo ya kazi mkuu mpya wa JKT meja Jenerali Samwel Ndomba wakati wa hafla ya kumuapisha iliyofanyika leo asubuhi ikulu jijini Dar es Salaam.

Amiri Jeshi mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(Katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange(kushoto) na Mkuu mpya wa JKT Meja Jenerali Samwel Ndomba muda mfupi baada ya hafla ya kumuapisha iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Picha na Freddy Maro-IKULU

Dk Mwakyembe yuko fiti!!

Naibu Waziri wa Ujenzi Dk Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ofisini kwake kuhusiana na maendeleo ya Afya yake nakusema kwamba yeye sasa yuko fiti kiafya, na ameripoti ofisini rasmi leo hii alipoulizwa maswali kutoka kwa waandishi wa habari akasema mambo yote anaichia serikali kupitia tume maalumu iliyoundwa kufutilia suala la ugonjwa wake. (PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)

Dr Mwakyembe akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari mbalimbali leo ofisini kwake

Wednesday, March 07, 2012

CRDB Bank -Customer Information

Greetings.

Kindly note BOT has issued circular recently to commercial Banks, the circular requires clients to update particulars of their accounts.

The forms for updation of customers information can be found in CRDB Bank’s website under resources centre. The dully filled forms can be mailed in a scanned format to customer-hotline@crdbbank.com or send directly to respective branch before 14/03/2012.

I look foward to receiving maximum cooperation and timely filling of the forms.

NB; I have attached the Customer KYC Update Forms with this email and please you may share this information with other Tanzanians.

Regards,

Crispin S

RM-Tanzanite Account

President Kikwete presents Country Assesment Report to APRM team of experts


President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete presents the Tanzania Country Assessment Report to an APRM (Africa Peer Review Mechanism) Lead Panelist Barrister Mr. Akere Muna. during a function held at State House Gardens in Dar es Salaam, this morning. (photo by Freddy Maro).

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi(CCM) Nape Nnauye Akutana na Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha Masuala ya Afrika wa Uingereza

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimfafanulia jambo Balozi Msaidizi wa Uingereza Hapa nchini, Susie Kitchens wakati wa mazungumzo yake na Mkugenzi wa Kitengo cha Masuala ya Afrika wa Uingereza Nick Pyle (hayupo pichani) aliyemtembelea katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba mjini Dar es Salaam.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimkaribisha Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha Masuala ya Afrika wa Uingereza Nick Pyle aliyemtembelea katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi Msaidizi wa Uingereza hapa nchini, Susie Kitchens
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha Masuala ya Afrika wa Uingereza Nick Pyle (kushoto) aliyemtembelea katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba mjini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi Msaidizi wa Uingereza hapa nchini, Susie Kitchens

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha Masuala ya Afrika wa Uingereza Nick Pyle (Wapili kushoto) baada ya mazungumzo yao leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi Msaidizi wa Uingereza hapa nchini, Susie Kitchens