Friday, June 30, 2017

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ANNA MGHWIRA ,ASHUHUDIA MAGARI 103 YAKIWA NA SHEHENA YA MAHINDI NJIA PANDA YA HIMO


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akiwa ameongozana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro wakiwemo Kamanda wa Polisi ,Hamis Issah na Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba wakitembelea maeneo ambayo yameshikiliwa magari yaliyobeba shehena ya Mahindi .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizunbgumza na baadhi ya wafanyabaishara wa Mahindi ambao magari yao yanashikiliwa eneo la Njia Panda mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya Wafanyabiashara ambao Mahindi yao yanashikiliwa katika eneo la Njia Panda mkoani Kilimanjaro wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira alipofika eneo hilo kwa lengo la kuzungumza nao.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiangalia magari yaliyobeba shehena ya Mahindi yanayoshikiliwa katika eneo la Njia Panda ya Himo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizungumza na baadhi ya madereva na Wafanyabaisahara ambao Mahindi yao yanashikiliwa eneo la Njia Panda ya Himo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akitizama Malori yenye Shehena ya Mahindi yakiwa yamehifadhiwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo nyuma ya vituo vya Mafuta .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiongozana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issa wakiodoka katika eneo hilo baada ya kuangalia malori yanayoshikiliwa yakiwa na shehena ya Mahindi.
Baadhi ya Magari yakiwa yameegeshwa katika maeneo tofauti tofauti yakiwa na shehena ya Mahindi.
ENEO la njia Panda linalounganisha barabara za Moshi/Arusha,Tanga/Dar es Salaam na ile ya Holili mpakani mwa nchi jirani ya Kenya linatajwa kama kituo kikuu cha Malori yanayosafirisha Nafaka kwenda nchi jirani ya Kenya.
Uchunguzi uliofanywa na Globu ya Jamii umebaini kuwepo kwa maeneo yasiyo rasmi ya kuegesha Malori hayo ,mengine yakiwa na Matela yake ,ambako shughuli za kupakua mahindi na kupakia katika Magari Madogo aina ya fuso zinazotoka nchi jirani ya Kenya hufanyika.
Maeneo mengine yanayotajwa kuwepo na Magulio  ya Mahindi ni katika sehemu za maegesho ya magari  zilizopo katika  vituo mbalimbali vya kuuza Mafuta ,pamoja na baadhi ya nyumba za wageni ambazo zimegeuzwa Maghala ya kuhifadhia Mahindi.
Magari zaidi ya 103 yanashikiiwa katika maeneo ya Njia Panda na Himo yakiwa yamebeba Shehena ya Mahindi tayari kusafirishwa huku baadhi ya madereva wakiyatelekeza Malori yao kwa siku ya tano sasa na kwenda kusiko julikana .
Hatua iliwasukuma Wafanyabiashara wa Mahindi pamoja na Madereva kufika ofisi za Mkuu wa mkoa kuwasilisha malalamiko yao juu ya kukamatwa kwa Malori hayo yakiwa Njia Panda badala ya mpakani kama alivyo agiza Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa.
Wakizungumza nje ya jingo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Wafanyabiashara hao ,Laurance Kanyota,Nuru Madai na Mariam Ramadhan walisema wameshangazwa na hatua ya jeshi la Polisi kushikilia magari yao yalikuwa na Mahindi yakisafirishwa kuelekea mikoa ya Arusha na Moshi.
“Magari yetu yapo pale Sheli Maount Meru,yalitokea Tunduma kwenda Arusha,yalipofika pale siku ya Jumamosi madereva walienda kula siku kuu ya Idd,jana (Juzi) asubuhi  Matandiboi wakapiga simu kwamba tumezungukwa na Polisi ,tukaenda pale tukaonana na OCD tukaliza kwanini mnatushikia magari ambayo yako Njia Panda yanayoenda Arusha au Moshi ,wakajibu tumetumwa kushika magari yote ya Mahindi.”alisema Mfanyabiashara Mariam.
Alisema alimuelewa Waziri Mkuu katika agizo lake kwamba magari yaliyopo mpakani ndio yashikiliwe  na si kama lilivyofanya jeshi la Polisi kukamata magari yaliyokuwa Njia Panda kuelekea Moshi na Arusha huku wakimuomba Waziri Mkuu kutoa ufafanuzi  kwa wasaidizi wake juu ya agizo lake.
Mfanyabiashara Kanyota alisema amekuwa akifanya biashara ya kusafirisha mazao kwa njia halali ikiwa ni pamoja na ulipaji wa kodi lakini anashangazwa na hatua ya kuzuiliwa kwa  Mahindi yake ambayo amekuwa akinunua na kuyauza katika viwanda vya kutengeneza unga kwa ajili ya Chakula.
“Tulikua tunaomba Mkuu wa mkoa ajue kwamba sisi ni wafanyabiashara tunaolipa kodi halali ya serikali atusaidie tufikishe mazao yetu sehemu yanapotakiwa kufika ,Mahindi yangu yanatoka Mbeya ,mkulima aiyeniletea mimi kama Dalali ametoka Tunduma.”alisema Kanyota.
Kauli ya Serikali ya mkoa wa Kilimanjaro.
Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Kilimanjaro imepigiria msumari katika Agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la kutaifisha Mahindi pamoja na gari litakalokutwa kuanzia June 26 mwka huu likiwa limebeba na kusafirisha Mahindi kwenda nje  ya nchi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro Anna Mghwira  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa alisema jana ofisini kwake mbele ya waandishi wa habari kuwa magari 103 yaliyokamatwa Himo na Njia Panda yatahesabiwa kama sehemu ya uhujumu uchumi na kwamba yatataifishwa .
“Magari yaliyokamatwa kule Siha ,tayari tulikwisha amua kwamba yatapelekwa Nationa Milling(Ghala la chakula la taifa) Arusha ,lakini haya ya Himo ,Waziri Mkuu Alisha agiza kwamba kuanzia tarehe 26 ,magari yote yatakayokamatwa ,Bidhaa pamoja na magari yenyewe yatahesabiwa kuwa ni sehemu ya uhujumu Uchumi ,kwa hiyo yatataifishwa.”alisema Mghwira.
Mghwira alisema baada ya mfululizo wa vikao vya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro juu swala zima la uuzaji na usafirishaji wa chakula nje ya nchi,kamati imefanyia kazi tamko la Waziri Mkuu kutaka kujiridhisha vya kutosha juu ya hali ya chakula iliyopo Kilimanjaro na mikoa ya jirani.
“Uogozi wa mkoa wa Kilimanjaro unapenda kuwatangazia wananchi wote,hususani Wafanyabiashara wa Sukari na Nafaka za Mpunga,Mchele ,Mahindi na Unga wa Mahindi ya kuwa ni marufuku kwa mfanyabiashara yoyote au mwananchi yoyote kusafirisha bidhaa hizo kwenda nje ya nchi bila kibali cha serikali”alisema Mkuu huyo wa Mkoa .
Alisema kukiuka agizo hilo ni kuhujumu uchumi wa nchi  kama ilivyo ainishwa kwenye kifungu cha 3 cha jedwali la kwanza la sheria ya uhujumu Uchumi sura ya 200 ya sheria za Tanzania na pia ni kukiuka agizo la Waziri Mkuu,kupitia waraka wake alioutoa  Mei 30,2017,uliozuia utokaji  wa vyakula na sukari kwenda nchi jirani .
Alisema kwa kukiuka sheria hiyo kunaweza kusababisha upungufu wa chakula kwenye baadhi ya maeneo nchini na kusababisha Mamlaka ya Mapato hapa nchini (TRA)  kukosa takwimu muhimu wa bidhaa zinazosafirishwa nje
“Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro imejiridhisha kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakisafirisha sukari  na nafaka hizo nyakati za usiku na hiki ndicho kinaleteleza kukosa takwimu muhimu kwa kupitia njia ambazo si rasmi kwa kushirikiana na baadhi ya askari polisi ambao sio waaminifu.
Wakati wa baraza la Idd lilifanyika kitaifa katika msikiti wa Riadha mjini Moshi,Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa alitangaza kupiga marufuku usafirishaji wa Mahindi kwenda nchi jirani na kwamba atakaye kiuka utaratibu huo atahukuliwa hatua kali za kisheria

WAHALIFU WANNE WAUWAWA KATIKA MAPAMBANO NA POLISI KIBITI


12
MKUU WA OPERESHENI ZA POLISI, NAIBU KAMISHNA DCP LIBERATUS SABAS, AKIONYESHA BUNDUKI AINA YA SMG ZILIZOPATIKANA JUZI USIKU WAKATI WA MAPAMBANO YA KURUSHIANA RISASI  BAINA YA WAHALIFU NA POLISI KATIKA KIJIJI CHA PAGAE WILAYANI KIBITI MKOANI PWANI. BUNDUKI 2 AINA YA SMG ZILIPATIKANA PAMOJA NA MAGAZINI 2 NA RISASI 17. PICHA NA HASSAN MNDEME-JESHI LA POLISI.
……………………..

Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua wahalifu wanne wanaosadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji  katika mapambano yaliyodumu kwa zaidi ya nusu saa katika kijiji cha Pagae wilayani Kibiti mkoani Pwani.

Akielezea tukio hilo Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi juni 29 majira ya saa tatu usiku kwenye barabara ya vumbi itokayo Pagae kuelekea Nyambunda ambapo Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita ambapo wahalifu hao baada ya kuona gari la Polisi walikimbilia vichakani na kuanza kuwarushia risasi Polisi.

Sabas alisema baada ya hali hiyo kutokea Askari nao kwa ujasiri walijibu  na mapambano hayo yalidumu kwa zaidi ya nusu saa ambapo Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu wanne kwa risasi ambao baadaye walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali.

“Katika tukio hilo tumefanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao na hii ni dalili kuwa tunaendelea vizuri na oparesheni yetu ambayo inashirikisha vyombo vingine vya ulinzi na Usalama katika wilaya hizi tatu za Mkuranga, Kibiti, na Rufiji” Alisema Sabas.

Aidha Sabas ametoa wito kwa wahalifu wengine kuacha mara moja kufanya vitendo hivyo kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanya jitihada zote za kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanakuwa salama na wananchi wanaishi katika hali ya amani na usalama.

Vilevile amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana wahalifu wengine ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwa usalama ambapo kwa ambaye atakayetoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa wahalifu hao kiasi cha shilingi milioni kumi kitatolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro

MKUTANO WA KITAIFA WA WADAU WA ELIMU NA CHAMA CHA WALIMU WAFANYIKA JIJINI DAR


Mwakilishi kutoka Mtandao wa Kodi Tanzania (TTJC), Grace Masalakulangwa akiwasilisha ripoti ya utafiti ya One Billion Question iliyotafitiwa na shirika la ISCEJIE katika Mkutano uliowakutanisha wadau wa Elimu na Wenyeviti wa Chama cha Walimu ngazi ya mikoa ya Tanzania Bara  iliyofanyika jijini  Dar es Salaam. 
Afisa Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Alistidia Kamugisha akifungua mkutano na kuwaelezea malengo ya mkutano huo wa siku mbili kwa wadau wa elimu na Chama cha Walimu Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET), Cathleen Sekwao akitoa mada kuhusu umuhimu wa ukusanyaji wa rasilimali za ndani na kuwekeza katika kuboresha sekta ya elimu hususani kwa mtoto wa kike na maslahi ya walimu katika mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU).
Meneja Mradi wa Elimu kutoka shirika la ActionAid Tanzania Ndugu Karoli Kadeghe akiwasilisha changamoto zinazoikabili elimu msingi hapa nchini ikiwa ni pamoja na upungufu wa vyumba vya madarasa, upungufu wa walimu kwenye mkutano uliowakutanisha wadau wa elimu pamoja baadhi ya viongozi wa Chama cha Walimu ngazi ya mikoa ya Tanzania Bara  iliyofanyika jijini  Dar es Salaam. 
  Baadhi ya wadau wa elimu nchini Tanzania wakichangia mada kwenye mkutano uliowakutanisha ili kujadili kodi na ubora wa elimu hapa nchini Tanzania  kwenye mkutano uliofanyika jijini Dar 

Shirika la ActionAid-Tanzania, Mtandao wa Elimu Tanzania, Shirika la Maendeleo ya Elimu Singida-MEDO na Mtandao wa Asasi za Kiraia-KINGONET  kwa pamoja wanatekeleza mradi wa uhamasishaji utoaji elimu bora kupitia rasilmali zetu wenyewe ( PROMOTING QUALITY EDUCATION THROUGH PROGRESSIVE DOMESTIC RESOURCE MOBILIZATION) unaotekelezwa huko Kilwa na Singida Vijijini kwa ngazi ya wilaya kwa kufanya kazi na kamati za shule na klabu za haki za watoto shuleni. Kitaifa MRADI Huo unalenga kufanya  utetezi wa mabadiliko ya kisera na sheria  hasa suala la ulipaji kodi, ukusanyaji kodi kwa haki (tax Justice), uzibaji wa mianya ya uvujaji wa kodi  ili makusanyo yaongezeke na yagharimie huduma bora kwa wananchi wa Tanzania hususani kuboresha utoaji wa Elimu bora Nchini.

Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania Bi. Cathleen Sekwao akifungua mkutano huo aligusia pia kuhusu “utoaji wa huduma za jamii hapa nchini unakabiliwa na ufinyu wa fedha, wote tu mashahidi kuwa hadi kufikia mwezi Machi, 2017 serikali ilikuwa imetoa asilimia 34 tu ya bajeti yote ya 2016/2017. Jambo hili lina madhara makubwa katika utoaji wa huduma za jamii hasa elimu msingi yenye ubora  hasakwa mtoto wa kike”.
Aliongelea pia serikali kushindwa kutoa asilimia mia moja ya fedha za kutekeleza bajeti ya 2016/2017 tafiti zinaonyesha kuwa Tanzania inapoteza fedha nyingi kupitia misamaha ya kodi.

Meneja Mradi wa Elimu kutoka shirika la ActionAid Tanzania Ndugu Karoli Kadeghe aliwasilisha changamoto zinazoikabili elimu msingi hapa nchini ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa vyumba vya madarasa, Upungufu wa ofisi za walimu, Upungufu wa vyoo vya wanafunzi,Uwiano usiokubalika kitaratibu wa mwalimu na wanafunzi, Shule nyingine kukosa kabisa walimu wa kike.

 Upungufu wa nyumba za walimu, fedha za ruzuku zisizotosheleza, utegemezi wa bajeti ya nchi za nje unaoathiri pia bajeti ya elimu na kusababisha Serikali kushindwa kugharimia kiufanisi utoaji wa elimu, mgawanyo wa ruzuku usiozingatia mahitaji halisi ya wenye uhitaji maalumu, jinsia na mahitaji ya kijiografia na pia shule changa na zile ambazo ni kongwe, Kuwa na mipango ya kibaguzi-Shule inayofanya vizuri ndiyo inapewa fedha(payment for results- P4R) kutoka mpango wa BRN bila kujali mizania ya usawa wa mazingira kati ya shule na shule, Kukosekana kwa mafunzo kazini kwa walimu, Kutopandishwa madaraja walimu, Kutolipwa kwa wakati stahiki za walimu wanaohamishwa/kustaafu mfano pesa ya usafiri.

Mratibu wa Inter Faith Standing Committee Bi. Grace Masalakulangwa aliwasilisha kuhusu Utafiti wa Ripoti ya “1 Billion Question” iliyojikita kubaini upotevu wa kodi katika sekta ya madini au uziduaji katika wilaya za Kilwa, Tarime na Geita. Utafiti huo umebaini serikali inapoteza takribani dola bilioni 1.83 sawa na Tsh trilioni 4.09 kwa mwaka kupitia misamaha ya kodi, uhamishaji wa fedha nje ya nchi bila kufuata utaratibu, kushindwa kutoza kodi sekta isiyo rasmi na aina nyingine za ukwepaji kodi.

Washiriki mbalimbali wakichangia katika mkutano huo, walishauri serikali kuboresha ukusanyaji wa kodi na utengaji wa bajeti katika sekta ya maendeleo hususani sekta ya elimu. Baadhi ya washiriki walichangia pia kukosekana kwa ufanisi na maendeleo yenye tija katika sekta ya Elimu kutokana na usimamizi mbovu wa elimu, serikali kushindwa kuwekeza katika elimu, kuwepo kwa wizara mbili zinazosimamia elimu na muda mwingine kuingiliana kwa majukumu pamoja na kutozingatiwa katika maslahi ya walimu.  

Thursday, June 29, 2017

KANALI LUBINGA AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA CCM TAWI LA UINGEREZA (UK), LEO
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akimkaribisha Ofisini kwake, Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza (UK), Kangoma Kapinga, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Mwenyekiti huyo ambaye alifuatana na Katibu wa CCM wa tawi hilo Leybab Mdegela alifanya mazungumzo na Kanali Lubinga ikiwemo haja ya kuimarishwa matawi ya CCM yaliyopo nchi za nje.
Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza Kangoma Kapinga akisaini kitabu cha wageni Ofisini kwa Kanali Ngemela (katikati), kabla ya mazungumzo yao kuanza. Kushoto ni Katibu wa CCM Tawi la Uingereza Leybab Mdegela.
Katibu wa CCM Tawi la Uingereza Lebab Mdegela akisaini Kitabu cha wageni. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza Kangoma Kapinga na Katikati ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.
Katibu wa CCM Tawi la Uingereza Lebab Mdegela akisaini Kitabu cha wageni. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza Kangoma Kapinga na Katikati ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akifafanua jambo wakati akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza Kangoma Kapinga (kulia), katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Katibu wa CCM wa tawi hilo Laybab Mdegela. PICHA: BASHIR NKOROMO-CCM Blog.

Wednesday, June 28, 2017

17 Big Bets for a Better World” launched in Tanzania


Ruge Mutahaba, Co-founder Clouds Media Group (right) speaking during the panel discussion on solutions for ‘off-grid societies’ during the launch of the book ’17 Big Bets for a Better World’. Also in the panel is, Chief Executive Officer of Benjamin Mkapa Foundation, Dr Ellen Mkondya- Senkoro (left) and Executive Director of the Dalberg Group, James Mwangi (middle) moderating the panel discussion
Executive Director of the Dalberg Group, James Mwangi (middle) moderating the panel discussion on solutions for ‘off-grid societies’ during the launch of the book ’17 Big Bets for a Better World’. Also in the panel is, Chief Executive Officer of Benjamin Mkapa Foundation, Dr Ellen Mkondya- Senkoro (left) and Ruge Mutahaba, Co-founder Clouds Media Group.
Guests following the panel discussion on solutions for ‘off-grid societies’ during the launch of the book ’17 Big Bets for a Better World’. 


150+ business leaders engage in panel discussion on solutions for ‘off-grid societies’. 

Dar es Salaam, Tanzania: Dalberg Group, The Africa List and the CEO Roundtable hosted an Iftar dinner to celebrate Dalberg’s 10 years in Africa by launching the book “17 Big Bets for a Better World”. The purpose of the launch was to kick off a discussion on Tanzania’s future and the role that the private sector plays in building the economy while addressing issues that affect Tanzanians. 

The event was attended by more than 150 business leaders in Tanzania representing a diverse range of sectors including finance and banking, telecoms, agribusiness and manufacturing. Reflecting on the launch in the Tanzanian context, Dalberg Group’s Executive Director - James Mwangi - remarked, “The book presents 17 bold and innovative ideas to reduce global poverty and improve lives. It tackles the types of questions that Dalberg has been addressing in Tanzania and the rest of Africa for the past decade. The private sector is a major driving force in developing our economies and a key partner in the type of work we do – working on the most pressing development challenges.” 

In the book, some of the world’s most renowned thought leaders detail how we collectively can reach the global goals (Sustainable Development Goals) set forth by the UN last year. From a bank president and a Nobel Peace Prize winner to an artist and Michelin-chef, contributors include Amina Mohammed – current Deputy Secretary-General of the United Nations and a former Minister of Environment of Nigeria, Ashish J. Thakkar – the founder of the Mara Group and Mara Foundation, James Mwangi – Managing Director and CEO of Equity Bank among others. 

The book presents fresh and credible solutions to the challenges humanity faces through 17 transformational ideas for positive change. Reviews of 17 Big Bets Ban Ki-moon, Secretary General, United Nations. 

“The Sustainable Development Goals embody the aspirations of people everywhere for lives of peace, prosperity and dignity on a healthy planet. To uphold our core promise to leave no one behind, we need action from everyone, everywhere. The United Nations looks forward to working with all partners to mobilize the leadership and investments that will turn this transformative vision into tangible progress.” 

Muhammed Yunus, Nobel Peace Prize Laureate “What drives the world forward is transformative and game-changing solutions and innovations. Leveraging the big bets of global thinkers, this book is an important contribution to the new Global Goals.” 

To further the discussion on Big Bets in the Tanzanian context, James Mwangi, spoke about a new concept called “off-grid societies” and why solutions must be created for serving them. 

“In the past, “off-grid” has been used to refer to those without energy access, but we need to look beyond that to define off-grid societies as those that do not have access to 20th century infrastructure, such as roads, bank branches, hospitals, and schools. Finding solutions to reach these unconnected populations is extremely important if we are to achieve truly inclusive growth. Creating effective solutions for off-grid societies often requires us to devise new business models and leapfrog technologies that require formal infrastructure, such as phone networks or roads, to function. These are challenges that could unlock a huge amount of growth in Tanzania, but that need the private sector’s leaders to get behind.” 

The off-grid societies discussion focused on five key sectors that were well represented in the audience: Finance, Retail, Energy, Healthcare and Finance. After the main session, participants were invited to engage further in coming up with off-grid solutions and big bet ideas for Tanzania.

Monday, June 26, 2017

DKT SHEIN AONGOZA BARAZA LA EIDD EL FITRI MJINI UNGUJA,ZANZIBAR


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wananchi mbali mbali baada ya Swala ya Eidd Fitri iliyoswaliwa leo katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja katika kusherekekea kumalizika kwa Mfungo wa MweziMtukufu wa Ramadhan.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wananchi mbali mbali baada ya Swala ya ElIdd Fitri iliyoswaliwa leo katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja katika kusherekekea kumalizika kwa Mfungo wa MweziMtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
 Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga   alipokuwa akitoa khutba baada ya Swala ya El Idd elfitri iliyoswaliwa katika Uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja katika kusherehekea Sikukuu ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan aliyohudhuriwa na Viongozi  wa Kitaifa na Waislamu mbali mbali wa Mkoa wa Mjini Magharibi  leo.
 Waislamu wanawake wakiwa katika Swala ya Eid  el fitri iliyoongozwa na Sheikh Fadhil Soraga katika Uwanja wa Maisara Suleiman Mjni Unguja leo katika Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo  Viongozi  wa Kitaifa na Waislamu mbali mbali walihudhuria [Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
 Baadhi ya waislamu wanaume waliohudhuria katika swala ya EId elfitri wakimsikiliza  Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar  Sheikh Fadhil Soraga aklipokuwa akitoa khutba ya Swala ya El Idd elfitri iliyoswaliwa katika Uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja katika kusherehekea Sikukuu ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MKOANI KILIMANJARO


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira mara baada ya kuwasili Mkoani hapo kwa ajili ya kuhudhuria ibada ya Eid Elfitr itakayo fanyika Kitaifa mjini Moshi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Thursday, June 22, 2017

OFISI YA MANISPAA YA ILALA YAHAMIA KWA MUDA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA KUWAHUDUMIA WANANCHI KATIKA KUADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akizungumza na mmoja wa wazee waliofika kupatiwa huduma katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo ofisi nzima ya Manispaa hiyo imehamia viwanjani hapo kwa ajili ya kuhudumia watu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma katika wilaya hiyo.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala , Edward Mpogolo akiwa na Naibu Meya wa Manispaa hiyo Omary Kumbilamoto wakitoa huduma kwa wadau waliofika kutaka msaada juu ya mambo yanayowakabili . Ofisi za Manispaa hiyo zimahamia hapo kwa muda kwa ajili ya kuhudumia watu, ikiwa ni sehemu ya mahadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma katika wilaya hiyo.
Mkurugenzi  wa Manispaa ya Ilala Msongela Palela akimuhudumia mmoja wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliofika katika viwanja vya mnazi mmoja.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wakilishi wa kampuni ya kuuza vifaa vya kuzimia moto inayojulikana kwa jina la Zima Moto  
 Afisa mkaguzi  Msaidiz wa jeshi la Zima Moto , akitoa maelezo kwa  Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema wakati wa maonyesho ya wiki ya utumishi wa Umma yaliyofanyika katika Viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akizungumza na baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Ilala ambo wanatoa huduma kwa wananchi katika Viwanja vya mnazi mmoja