Wednesday, December 09, 2015

WAFANYAKAZI HOSPITALI YA MUHIMBILI WAFANYA USAFI

VE1Baadhi ya Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakifanya usafi leo nje ya jengo la Kibasila akiwamo Mwenyekiti wa Khoja Shia Ithnashery Jamaat ya jijini Dar es Salaam, Dewji Azim (katikati).
VE2Kushoto ni Mwanasheria wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Veronica Hillary, Mkuu wa Idara ya Upasuaji,  Dk Julieth Magandi, Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk John Kimario na Mwenyekiti wa Khoja Shia Ithnashery Jamaat ya jijini Dar es Salaam, Dewji Azim wakifanya usafi leo Desemba 9 ambayo ni siku ya kuadhimisha Uhuru wa Tanzania. Usafi huo umefanyika katika Jengo la Kibasila.
VE3Mkurugenzi wa Upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk John Kimario akisomba takataka ikiwa ni sehemu ya kutekeleza agizo la Rais John Pombe Magufuli kwamba leo Desemba 9, siku ya Uhuru watu wote wajumuike kufanya usafi.
VE4
VE5Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha (wa pili kulia) akishiriki kufanya usafi katika hospitali hiyo leo Desemba 9, 2015.
VE6Mkuu wa Idara ya Sheria, Veronica Hillary, Ofisa Uhusiano Msaidizi, John Stephen, Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk John Kimario na Mkuu wa Idara ya Upasuaji, Dk Julieth Magandi wakijumuika pamoja kufanya usafi leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ikiwa ni kuitikia agizo la Rais John Pombe Magufuli la kufanya usafi leo Desemba 9, siku ya Uhuru.
VE7Mwenyekiti wa Khoja Shia Ithnashery Jamaat ya jijini Dar es Salaam, Dewji Azim akifanya usafi leo katika hospitali hiyo.

No comments: