Wednesday, December 09, 2015

BAYPORT YAMUUNGA MKONO DR MAGUFULI KWA VITENDO, YAPAKA RANGI, YAFAGIA SHULE YA MSINGI HEKIMA


Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, akipaka rangi katika ukuta wa shule ya Msingi Hekima, iliyopo Tandale, wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo mchana. Picha zote kwa Hisani ya Bayport Financial Services.

Meneja wa Oparasheni wa Bayport Financial Serviices, Charles Mgeta, akizungumza na waandishi wa habari juu ya taasisi yao kuamua kufanya usafi, kutunza mazingira na kuipaka rangi shule ya msingi Hekima, iliyopo Kata ya Tandale, Wilaya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, kushoto mwenye kofia na miwani akishiriki kufanya usafi katika shule ya Msingi Hekima, iliyopo Tandale, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam, asubuhi.

Wafanyakazi wa Bayport, walimu na wanafunzi wakijiandaa kufanya usafi mbele ya jengo la shule ya Hekima, kabla ya kuanza kupakwa rangi.

Mchambuzi wa Miradi wa Bayport Financial Services, Joseph Munga, kulia akishiriki kupaka rangi katika shule hiyo ya msingi Hekima.
………………………………………………………………………………….
TAASISI ya
Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na utoaji wa mikopo, jana
imemuunga mkono kwa vitendo Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr John Pombe Magufuli
kwa kufanya usafi, kutunza mazingira na kupaka rangi shule ya Msingi Hekima,
iliyopo Kata ya Tandale, wilaya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, huku wakianza
kwanza kusafisha eneo la Makao Makuu ya ofisi yao, kabla ya kuelekea hapo. 
Tukio hilo
liliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Bayport, John Mbaga, pamoja na zaidi
ya wafanyakazi 80 kwenye taasisi hiyo inayotoa mikopo ya fedha kwa watumishi wa
umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi, bila kusahau wajasiriamali katika mradi
wao wa mikopo ya viwanja vilivyopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. 
Shughuli
hiyo Ilianza mishale ya saa tatu asubuhi ambapo Mkurugenzi huyo na wafanyakazi
wa Bayport walianza kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya shule hiyo,
pamoja na upakaji wa rangi katika baadhi ya madarasa katika shule hiyo yenye
wanafunzi zaidi 1900, ukiacha idadi kubwa ya wanafunzi wa darasa la kwanza
watakaonza shule mapema mwakani.
Wafanyakazi wa Bayport Financial Services wakiendelea na usafi katika shule ya msingi Hekima.

Akizungumza
katika tukio hilo leo asubuhi, Mkurugenzi wa Bayport Financial Servivces, John Mbaga,
alisema kwamba wameamua kuchagua shule ya Tandale kwa sababu inahitaji kuungwa
mkono kutokana na eneo iliyopo pamoja na changamoto mbalimbali za kimaisha. 
Alisema
baada ya rais kuagiza kwamba Sikukuu ya Uhuru 9 Desemba iendane na kazi ya
kufanya usafi na utunzaji wa mazingira, Bayport iliamua kwenda mbali zaidi kwa
kuhakikisha kwamba wanaipaka rangi shule hiyo ili ionekane safi, tofauti na
ilivyokuwa awali.
Usafi ukiendelea shuleni hapo
Usafi ukiendelea
“Tunamuunga
mkono Dr Magufuli na serikali yake kwa vitendo, hivyo si usafi tu, ila
tumeirudisha shule ya Msingi Hekima kwenye upya wake, huku tukiamini kuwa
tutaendelea kujikita zaidi katika mambo ya kijamii, hususan katika suala zima
la elimu kwa kusaidia kila kilichokuwa ndani ya uwezo wetu” alisema Mbaga.
 
Naye Meneja
Masoko na Mawasiliano wa Bayport, Ngula Cheyo, alisema kwamba wamefurahia
kushirikiana na walimu na wanafunzi wa shule ya Msingi Hekima kufanya nao usafi
na kutunza mazingira ya eneo la shule hiyo inayotumiwa na watoto wengi kutoka
kwenye Kata hiyo ya Tandale. 
“Bayport ni
taasisi ya Watanzania wote, wakiwamo watumishi wa umma na wafanyakazi wa
kampuni binafsi, hivyo naamini itaendelea kutoa huduma bora zenye kuwakwamua
wateja wetu,” alisema Cheyo.
 
Naye Mwalimu
Mkuu wa shule ya Msingi Hekima, Hussein Mohamed, aliishukuru Bayport kwa
kujitolea kurudisha upya wa shule yao kwa kuamua kuipaka rangi, pamoja na
kushirikiana nao katika 9 Desemba kufanya usafi, jambo ambalo ni muhimu ili
kujiepusha na magonjwa ya miripuko, ukiwamo ugonjwa wa Kipindupindu.
 
“Hatuna cha
kuwalipa Bayport kwa kujitolea kwao kwetu, hivyo tunawaombea kwa Mungu, ingawa
tunazidi kuwaomba waendelee kuwa karibu na sisi kwa kutusaidia mambo mbalimbali
ili tufanikishe kwa vitendo kuwapatia watoto wetu elimu bora ili kuwaandalia
maisha bora wanafunzi hawa ambao licha ya changamoto kadhaa zinazotukabili, ila
ufaulu wao umekuwa ni mkubwa, jambo linalotutia moyo,” alisema Mohamed.
Bayport ni
moja ya taasisi zinazofanya juhudi kubwa kuwakwamua wateja wao, wakiwamo
watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi kwa kupewa mikopo isiyokuwa
na amana wala dhamana, huku huduma hizo zikipatikana kwa urahisi kutokana na
kuenea kwa matawi zaidi ya 80 katika wilaya na mikoa mbalimbali ya Tanzania
Bara.

No comments: