Wednesday, December 09, 2015

PB YASAFISHA SOKO LA FERI, YATOA VIFAA VYA USAFI, NI KATIKA KUUNGA MKONO UAMUZI WA RAIS MAGUFULI WA UHURU NI KAZI


Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Henry Bwogi, akizibua
chemba ya kupitisha maji taka kwenye zoni 3 ya soko la samaki la kimataifa Feri
jijini Dar es Salaam Desemba 9, 2015. TPB imeungana na watanzania katika kuunga
mkono agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwataka wananchi
kusherehekea sikukuu ya Uhuru wa Tanganyika kwa kufanya usafi ili kutekeleza
zana ya “Uhuru ni Kazi” badala ya kufanya sherehe na matamasha huku nchi
ikakabiliwa na ugonjwa wa Kipindupindu
 ………………………………………………………………………
Na
K-Vis Media/Khalfan Said)
KATIKA
kuunga mkono maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa wananchi
na taasisi za serikali kufanya usafi siku ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru
wa Tanganyika, Benki ya Posta Tanzania, TPB, nayo iliungana na wananchi hususan
eneo la soko la kimataifa la samaki Feri, katika kutekeleza agizo hilo.
Wakati
Mh. Rais alishirikiana na majirani zake, wavuvi na wachuuzi wa samaki pale nje
kidogo ya uzio wa Ikulu, hali ilikuwa hivyo hivyo kwenye maeneo mengi, ya nchi
ambapo katika eneo hilo la soko la Feri, TPB walipewa eneo la kufanyia usafi
kwenye zoni namba 1 na eneo la kuegeshea mitumbwi maarufu kama “Lebanon” ambapo
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bw. Henri Bwogi, aliwaongoza
wafanyakazi wa benki hiyo katika kufagia, kuzibua mitaro na chemba za maji
taka, hali kadhalika kupakia taka kwenye malori ya kubebea taka.
Katika
hatua nyingine Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bw. Bwogi, alikabidhi
vifaa vya kufanyia uasafi viliovyokuwa vikitumiwa na wafanyakazi wa benki hiyo
kwa uongozi wa soko ili waendelee na kazi ya usafi siku za usoni.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,
aliagiza sherehe za mwaka huu za Uhuru wa Tanganyika, zisherehekewe kwa kufanya
kazi ili kutekeleza zana ya “Uhuru ni Kazi” badala ya kufanya matamasha na shamra
shamra kwenye viwanja mbaklimbali nchini.

Nimefurahishwa sana na wananchi jinsi walivyojitokeza kwa wingi kwenye maeneo
mbaklimbali ya nchi katika kufanya usafi ili kuiweka nchi yetu safi na
kujikinga na maradhi kama Kipindupindu.” Rais Magufukli aliwaambia majirani
zake baada ya zoezi la kufanya usafi.
Naye
Kaimu Afisa Myendaji Mkuu wa TPB, Bw. Bwogi, alisema TPB kama taasisi ya
serikali iliamuru wafanyakazi wake, wafike kazini na kushiriki katika kufanya
usafi na sisi tumeona tuje kuungana na wenzetu wa feri ili kutekeleza maelekezo
ya Rais wetu.” Alisema.
 Mfanyakazi wa TPB, akizibua chemba katika kutekeleza zana ya Uhuru ni Kazi

No comments: