Tuesday, October 01, 2013

TAASISI YA WANAWAKE NA MAENDELEO (WAMA) – SAIDIENI WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI


 Meneja wa  Mradi wa Pamoja Tuwalee kutoka Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) , Gloria  Minja  akizungumza jambo wakati wa majadiliano ya kutengeneza ujumbe utakaohamasisha , Serikali , jamii na sekta binafsi ili  waweze kusaidia watoto  waishio katika mazingira hatarishi  kuwapatia elimu , chakula na  malazi  leo  jijini Dares Salaam.
 Kaimu  Katibu Mtendaji wa  Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) , Tabu  Likoko  akifungua  majadiliano ya kutengeneza ujumbe utakaohamasisha , Serikali , jamii na sekta binafsi ili  waweze kusaidia watoto  waishio katika mazingira hatarishi kuwapatia elimu , chakula na  malazi  leo  jijini Dares Salaam.Kushoto ni mjumbe wa majadiliano hayo kutoka WAMA ,Julius Jacob


Mjumbe wa majadiliano ya  kutengeneza ujumbe wa  kuwatambua na kuwahudumia  watoto waishio katika mazingira  hatarishi, Peter  Mabwe  akichambua  ujumbe   wenye kauli mbiu ‘ Pamoja Tuwalee’  inayosimamiwa  na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)   leo  jijini Dares Salaam.   

Mjumbe wa majadiliano ya  kutengeneza ujumbe wa  kuwatambua na kuwahudumia  watoto waishio katika mazingira  hatarishi , Asha Mtwangi  akichambua   ujumbe   wenye kauli mbiu ‘ Pamoja Tuwalee’  inayosimamiwa  na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)   leo  jijini Dares Salaam.  
Mtaalamu  wa masuala ya ushauri katika mitaala, uandishi na uhariri , Victor  Msinde  (katikati )akichangia  mada  juu  ya   majadiliano ya kutengeneza ujumbe utakaohamasisha , Serikali , jamii na sekta binafsi ili  waweze kusaidia watoto  waishio katika mazingira hatarishi kuwapatia elimu , chakula na  malazi  leo  jijini Dares Salaam.Picha zote Eleuteri Mangi –MAELEZO.---
 
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
 
SEKTA binafsi na taasisi mbalimbali zimeshauriwa  kufadhili katika kuwasaidia watoto wanaoshi katika mazingira magumu badala ya kusaidaia matamasha pekee ikiwa ni hatua mojawapo ya  ya kuwapatia maisha bora , ikiwemo kupunguza umasikini  na tatizo hilo.
 

 
Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja wa  Mradi wa Pamoja Tuwalee kutoka Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) , Gloria  Minja wakati wa majadiliano ya kutengeneza ujumbe utakaohamasisha , Serikali , jamii na sekta binafsi ili  waweze kusaidia watoto hao.
 

 
“Tuzinaomba sekta binafsi  ikiwa ni moja wa wadau katika kusaidia watoto waishio katika mazingira magumu katika malengo yao walijiwekea kupitia kipengele cha Uwajibikaji katika jamii (yaani corporate social responsibilities) kubadili mtanzamo wa kusaidia matamasha pekee ,bali waanze kufanya hivyo kwa watoto hawa ili nao waweze kusoma ,kutibiwa na kupata malazi,” alisema Gloria.
 

 
 Alisema ikiwa sekta hizo zitatekeleza wajibu huo,watoto hao wataweza kupata fursa ya kusoma , kupata kazi na kuajiriwa katika maeneo mbalimbali ili waweze kuendesha maisha yao.
 

 
 Gloria aliongeza kuwa mbali sekta hiyo , Serikali na   kila mwanajamii  wanawajibu  kutenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao , kwa kufanya hivyo kutasaidia  kuwawezesha kupata mahitaji muhimu  na kupunguza  tatizo la umaskini  nchini.
 

 
 Akizungumzia  kuhusu ujumbe uliokuwa unatengenezwa na wadau hao kutoka sekta binafsi na Serikali alisema lengo lake litakuwa ni kutoa ushawishi kwa jamii nzima  ili iweze kuwatambua na kuwahudumia watoto hao.
 

 
 Aidha  alisema   ujumbe huo  utatumika  kuhamasisha katika kampeni ya utetezi  kwa watoto hao ili  Serikali, Jamii na sekta binafsi zitambue  kuwa jukumu la kuwalea watoto hao ni la pande zote.
 

 
 Akifungua  majadiliano hayo Kaimu  Katibu Mtendaji wa  WAMA , Tabu  Likoko  alisema  kuwa  taasisi hiyo  inafanya kazi ya kusaidia elimu kwa watoto wa kike, yatima na uwezeshaji kwa wanawake.
 

 
Mradi huo wa Pamoja Tuwalee unatekelezwa katika mikoa  ya  Morogoro,Pwani, Dares Salaam na Zanzibar kwa kipindi cha muda wa miaka mitatu,ambapo ulianza kutekelezwa mwaka 2011 hadi mwaka 2013 na WAMA  kwa ushirikiano wa fhi360 chini ufadhili wa Shirika  la Misaada la Marekani(USAID).

No comments: