Godwin Gongwe na Ruge Mutahaba waliokaa katikati
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa mtangazaji wa Redio Tanzania, ITV na Redio One na Redio Aboud, marehemu Julius Nyaisanga, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita huko mjini Morogoro kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu. Marehemu Nyaisanya ameagwa leo katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni na anasafirishwa leo hii kuelekea Tarime kwa ajili ya maziko.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi akisalimiana na Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal
Menyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi, akizungumza machache....
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda (kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, wakati wa shughuli hiyo Viwanja vya Leaders.
Leah Nyaisanga, ambaye ni mke wa marehemu wa aliyewahi kuwa mtangazaji wa Redio Tanzania, ITV na Redio One na Redio Aboud, marehemu Julius Nyaisanga, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu mumewe, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita huko mjini Morogoro kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu, wakati wa shughuli za kuagwa mwili huo zilizofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni na anasafirishwa leo hii kuelekea Tarime kwa ajili ya maziko.Msafara wa Magari ambao moja wapo (la mbele) likiwa limebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Julius Nyaisanga ukiingia kwenye viwanja vya leaders muda huu kwaajili ya wakazi wa jiji la Dar kuweza kutoa heshima zao za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga kabla ya Kusafirisha Kwao Tarime Mkoani Mara
Baadhi ya Ndugu, Jamaa na marafiki wakibeba jeneza lenye Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga Kwaajili ya kupeleka sehemu husika tayari kwa kutoa heshima za mwisho kwa wakazi wa jiji la Dar waliofika katika viwanja vya leaders muda huu
Sehemu Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga litakapowekwa kwaajili ya wakazi wa jiji la dar kuweza kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Tarime Mkoani Mara.
Baadhi ya wakazi wa jiji la dar waliojitokeza katika viwanja vya leaders muda huu
Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar wakisubiria Kutoa Heshima zao za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga Kabla haujasafirishwa kupelekwa Kwao Tarime Mkoani Mara.
No comments:
Post a Comment