POLISI YAKABIDHIWA VITABU NA HANS SEDEL FOUNDATION

     3

Naibu Mwakilishi wa Shirika la Hans Sedel Kanda ya Afrika Mashariki Konrad Teichert akizungumza katika hafla fupi ya Makabidhiano ya nakala 10600 za vitabu vya Haki na ulinzi wa mtoto, Fahamu misingi ya amani na usalama katika familia pamoja na stika 4000 za kupambana na rushwa.Kulia ni Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja pamoja na Mkuu wa huduma za Polisi Jamii Naibu Kamishna Michael Kamhanda. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi) 1
Naibu Mwakilishi wa Shirika la Hans Sedel Kanda ya Afrika Mashariki Konrad akimkabidhi moja ya stika za kupamba na rushwa  Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja wakati wa hafla fupi ya Makabidhiano ya nakala 10600 za vitabu vya Haki na ulinzi wa mtoto, Fahamu misingi ya amani na usalama katika familia pamoja na stika 4000 za kupambana na rushwa zilizochapishwa na shirika hilo.Kulia ni Mkuu wa huduma za Polisi Jamii Naibu Kamishna Michael Kamhanda.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
 2
Naibu Mwakilishi wa Shirika la Hans Sedel Kanda ya Afrika Mashariki Konrad akimkabidhi moja ya kitabu cha Haki na ulinzi wa mtoto  Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja wakati wa hafla fupi ya Makabidhiano ya nakala 10600 za vitabu vya Haki na ulinzi wa mtoto, Fahamu misingi ya amani na usalama katika familia pamoja na stika 4000 za kupambana na rushwa zilizochapishwa na shirika hilo kwa lengo la kulisaidia jeshi la Polisi katika kupambana na uhalifu jijini Dar es Salaam jana.Kulia ni Mkuu wa huduma za Polisi Jamii Naibu Kamishna Michael Kamhanda. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
………………………………………………………………………………
Na Tamimu Adam, Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi limekabidhiwa zaidi ya nakala 10600 za vitabu vya Polisi jamii na  ulinzi shirikishi kutoka shirika la Hans Sidel Foundation    ambavyo vitatumika katika kuendelea kuhamasisha dhana ya Polisi jamii na ulinzi shirikishi pamoja na kuendeleza mpango wa kufikisha elimu ya usalama hadi ngazi ya familia.
Nakala za vitabu zilizokabidhiwa ni  kitabu cha Haki na Ulinzi wa mtoto, nakla 5300 na kitabu cha fahamu misingi ya amani na usalama  katika familia nakala 5300 pamoja na stika 4000 za kupambana na rushwa.
 Vitabu hivyo vilikabidhiwa na Mwakilishi wa shirika la Hans Sidel Bw. Konrad Teichert  na kupokelewa na Kamishina wa Opereheni na Mafunzo (CP) Paul Chagonja kwa niaba ya Jeshi la Polisi katika hafla fupi iliyofanyika jana Makao makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es salaam.
Chagonja alisema kuwa vitabu hivyo vimefika wakati muafaka ambapo Jeshi la Polisi linaendelea na mpango wake wa kufikisha elimu ya usalama hadi ngazi ya familia pamoja na mapambano dhidi ya rushwa ambayo kila mmoja anatakiwa kuwajibika ili kutokomeza rushwa hapa nchini.
Aliongeza kuwa vitabu hivyo  vinalenga katika kuimarisha ulinzi shirikishi na kuwawezesha  kila mmoja katika familia kuwezeshwa na kujengewa uwezo katika kubaini na kuzuia fursa za kutendeka kwa uhalifu au vurugu ndani ya jamii.
Kwa upande wake Mwakilishi wa shirika la Hans Sidel Bw. Konrad Teichert alisema wataendelea kushirikiana na jeshi la Polisi katika kusaidia kufanikisha maboresho ya jeshi hilo pamoja na kuendelea kufanya mafunzo ya kuwajengea uwezo Maofisa na Askari wa Jeshi la Polisi.
Naye Mkuu wa Ufuatiliaji na tathimini wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishina wa Polisi, (DCP) Omar Rashid alishukuru shirika la Hans Sidel kwa ushirikiano walioutoa katika kusaidia kuchapisha vitabu hivyo na kuendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo , maofisa, wakaguzi na askari, ambapo jumla ya wahitimu 17 walitunukiwa vyeti vya mafuzo hayo.

Comments