Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw. Jackson Mmbando (katikati)
akiongea na wanahabari (hawapo pichani)…
Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw. Jackson Mmbando akimkabidhi
cheti mshindi wa tatu wa nyumba ya Airtel Bi. Husnat John
aliyeibuka mshindi kupitia promosheni ya Airtel inayofahamika kwa jina
la Airtel Yatosha, shinda nyumba 3. Kati ni Meneja Uhusiano wa Airtel Bi, Aneth Muga. Na wa kwanza kushoto ni mtoto
wa mshindi huyo Eksher Abby.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw. Jackson Mmbando akimkabidhi
cheti mshindi wa tatu wa nyumba ya Airtel Bi. Husnat John
aliyeibuka mshindi kupitia promosheni ya Airtel inayofahamika kwa jina
la Airtel Yatosha, shinda nyumba 3. Kati ni Meneja Uhusiano wa Airtel Bi, Aneth Muga. Na wa kwanza kushoto ni mtoto
wa mshindi huyo Eksher Abby.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw. Jackson Mmbando (katikati)
akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kabla ya kumkabidhi cheti mshindi wa
tatu wa nyumba ya Airtel Bi. Husnat John
(kushoto) aliyeibuka mshindi kupitia promosheni ya Airtel inayofahamika kwa
jina la Airtel Yatosha, shinda nyumba 3. Kulia ni Meneja Uhusiano wa
Airtel Bi, Aneth Muga.
Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga akizungumza juu ya
vifurushi vya Airtel Yatosha Baba Lao iliyoboreshwa ili kumuwezesha mteja wa
Airtel kupata dakika 61 kupiga mitandao yote, kutuma ujumbe mfupi wa maneno
bila kikomo pamoja na 1.5 GB kwa bei ile ile ya shilingi 999 tu.
MSHINDI WA NYUMBA YA TATU AIRTEL YATOSHA APOKEA CHETI CHA
USHINDI
• Vifurushi vya
yatosha vyaongezwa muda wa kupiga mitandao yote dk 61, 1.5 GB na sms bila
kikomo
Dar es Salaam October 15, 2013: Mshindi wa nyumba ya tatu ya
Airtel Yatosha, Bi. Husnat Anthony leo amekabidhiwa rasmi cheti chake cha
ushindi ikiwa ni uthibitisho maalum wa
ushindi wake.
Mshindi huyo anakuwa ni mshindi wa tatu kuibuka na nyumba
kupitia promosheni ya Airtel yatosha shinda nyumba tatu baada ya nyumba ya
kwanza na ya pili kuchukuliwa na Sylvanus Juma pamoja na Agnes Lyimo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa cheti chake,
Bi. Husnat alisema “Kweli sikutegemea kama ipo siku naweza nikamiliki nyumba
yangu mwenyewe, na hata nilipopigiwa simu sikuamini ila Namshukuru sana Mungu
kwa kuniwezesha kuwa mshindi wa nyumba ya Airtel Yatosha”
“Pia nawashukuru sana Airtel kwa zawadi hii na nimeamini
kweli Airtel yatosha na inasaidia kupunguza makali ya maisha kwa watanzania,”
alisisitiza Bi. Husnat.
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson
Mmbando alisema Airtel inayo furaha kumpata mshindi mwingine wa nyumba na
haitoacha kutoa huduma bora na zenye manufaa kwa wateja wake nchi nzima na kwa
sababu hiyo bado inazidi kuboresha huduma zake na kuzifanya ziwe za kisasa
zaidi.
“Airtel hatujaishia tu kwenye utoaji wa nyumba bado
tunaendelea kuboresha huduma zetu na kuhakikisha wateja wetu wananufaika zaidi
na huduma tunazotoa” Alisema Mmbando.
Airtel imeboresha zaidi huduma zake na sasa hivi ukijiunga
na kifurushi cha siku cha 999 unaweza kupata dakika 61, kutuma ujmbe
mfupi wa maneno bila kikomo pamoja na 1.5 GB kwa ajili ya
matumizi ya Internet.
Kujiunga na vifurushi mbalimbali vya Airtel mteja anapaswa
kupiga *149*99# na kuchagua 1 au 2 kisha aweze kujiunga na kifurushi chochote
cha Wiki, Siku au Mwenzi.
Airtel kupitia promosheni ya Airtel yatosha imetoa zawadi ya
pesa taslimu shilingi milioni 90 kwa wateja wake na nyumba tatu zenye thamani
ya milioni 65 kwa kila moja tayari zilishapata washindi.
Comments