Sunday, October 20, 2013

JULIUS NYAISANGAH 'UNCLE J' AFARIKI DUNIA


HABARI zilizotufikia kutoka mkoani Morogoro ni kwamba Mtangazaji Mkongwe nchini, Julius Nyaisangah 'Uncle J' ameaga dunia. Mpaka mauti yanamfika, Marehemu Nyaisangah alikuwa Mhariri Mtendaji wa Abood Media iliyopo mkoani Morogoro. Marehemu aliwahi pia kufanya kazi katika kituo cha Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na katika Kituo cha Redio One ambapo alikuwa Mkurugenzi. Mpaka sasa chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika japo marehemu alikuwa akiugua kwa muda mrefu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!  Taarifa zaidi zitawajia baadaye. SOURCE: GLOBALPUBLISHERS

1 comment:

emu-three said...

R.I.P Uncle J. Nyaisanga

🔴🔴TABORA ZOO YAENDELEA KUNG'ARA KAMA KITOVU CHA ELIMU, BURUDANI NA UTALII WA NDANI

Na Mwandishi wetu, Tabora. Bustani ya Wanyamapori Tabora (Tabora Zoo) imeendelea kujipambanua kama kivutio muhimu cha elimu na burudani jiji...