Tuesday, October 08, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MIRADI YA UKARABATI WA VITUO VYA KUPOZA UMEME NA UJENZI WA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME MKOA WA KILIMANJARO


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Moshi Vijijini, mara baada ya kuwasili kwenye Kituo cha kusambaza umeme cha Makuyuni Wilaya ya Moshi Vijijini Tarafa ya Himo Mkoa wa Kilimanjaro leo kwa ajili ya kuzindua rasmi miradi ya ukarabati wa Vituo vya Kupoza Umeme na Ujenzi wa Njia ya kusafirisha Umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka Jiwe la msingi, katika uzinduzi rasmi Miradi ya ukarabati wa Vituo vya Kupoza Umeme na Ujenzi wa Njia ya kusafirisha Umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika leo, Oktoba 7, 2013 katika Kituo cha kupoza umeme cha Makuyuni Wilaya ya Moshi Vijijini Tarafa ya Himo Mkoa wa Kilimanjaro. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo na nyuma yao ni Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Miradi ya ukarabati wa Vituo vya Kupoza Umeme na Ujenzi wa Njia ya kusafirisha Umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika leo, Oktoba 7, 2013 katika Kituo cha kupoza umeme cha Makuyuni Wilaya ya Moshi Vijijini Tarafa ya Himo Mkoa wa Kilimanjaro. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Felician Mramba, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (kushoto kwa Makamu) ni Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na baadhi ya viongozi wakitembelea kukagua mitambi ya kusambaza umeme ya Kiyungi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Felician Mramba, wakati alipotembelea kukagua Kituo cha kusambaza Umeme cha Kiyungi, mkoani Kilimanjaro.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya mtambo wa kisasa wa kusambaza umeme uliopo katika kituo cha Makuyuni  Wilaya ya Moshi Vijijini Tarafa ya Himo Mkoa wa Kilimanjaro, wakati alipofika kituoni hapo kuzindua rasmi Miradi ya ukarabati wa Vituo vya Kupoza Umeme na Ujenzi wa Njia ya kusafirisha Umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro, leo.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas gama, akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nishati na Madidi, Prof. Muhongo, aliyemkaribisha Makamu wa Rais, kuzingumza.
 Picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.
 Picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco baada ya uzinduzi huo.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

No comments: