Thursday, October 31, 2013

Mahakama ya Rufaa yasikiliza maombi ya ‘Babu Seya’ na ‘Papii Kocha’


 Nguza Vicking ‘Babu Seya’ akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza ‘Papii’ wakiwa na nyuso za furaha wakati wakitoka katika Mahakama ya Rufaa baada ya majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania kusikiliza maombi yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia hukumu iliyoitoa mwaka 2010.
 Nyuso za matumaini…….
bofya
 Johnson  Nguza ‘Papii’ akibusu mkono wake baada ya kuibusu ardhi mara baada ya kutoka mahakamani.
 Papii akinyoosha mkono juu kama ishara ya kumshukuru mungu.
 Waandishi wa habari wakiwa chini wakati wa harakani za kuchukua matukio mahakamani hapo.
 Nguza Vicking ‘Babu Seya’ akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza wakati wakitoka mahakamani.
 Nguza Vicking ‘Babu Seya’ akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza au Papii wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo.  
 Watu waliohudhuria mahakama hapo wakifuatilia kesi hiyo.
 Nguza Vicking ‘Babu Seya’ akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza au Papii wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo.  
 Mahakamani.
Nguza Vicking ‘Babu Seya’ akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza wakiteta jambo na wakili wao, Mabere Marando.

Picture
Nguza Vicking na mwanaye Johnson Nguza katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania jijini Dar es Salaam leo, kabla ya kuanza kusikilizwa kwa rufaa ya kesi yao. (Picha: Francis Dande)
Na HAPPINESS KATABAZI, Tanzania Daima

MWANAMUKIZI wa muziki wa dansi nchini Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanae Johnson Nguza 'Papi Kocha Mtoto wa Mfalme', wameiomba Mahakama ya Rufaa nchini iifanyie upya hukumu yake iliyoitoa Februali mwaka 2010 ambayo iliwahukumu kifungo cha maisha kwasababu hukumu hiyo ina utetelezi wa wazi wa kisheria.

Ombi hilo Na.5/2010 liliwasilishwa kwa niaba yao na wakili wao Mabere Marando jana mbele ya jopo lilelile lilotoa hukumu ya awali ya Februali 2010  ambalo linaongozwa na Jaji Nataria Kimaro, Salum Massati na Mbarouk .S.Mbarouk.

Wakili Marando alidai kwa mujibu wa kanuni ya 66 ya Mahakama ya Rufaa ya mwaka 2009  inatoa mamlaka kwa mahakama ya rufaa kufanya mapitio ya hukumu inazozitoa  hivyo wateja wake wamewasilisha ombi hilo la mapitio kwasababu wanaamini  mahakama yake ilikosea wazi wazi kisheria katika hukumu yake ya Februali 2010 na kwa mujibu wa kanuni hiyo inatoa mamlaka kwa mahakama hiyo kufanya mapitio ya hukumu yake.

Wakili Marando alieleza kuwa ombi lake amelileta chini ya kifungu cha 3 aya A ya Kanuni ya Mahakama ya Rufaa ya mwaka 2009 ,   ikisomwa pamoja na Ibara 13 (3) (6)(a) ya Katiba ya nchi, litaja  moja ya utelezi wa wazi wazi wa kisheria uliofanywa na mahakama hiyo, ni kwamba katika hukumu hiyo  kuna baadhi ya aya inasomeka kuwa majaji hao walikubaliana na hoja yake iliyodai kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakati inasikiliza kesi hiyo, ilikosoea kufuata utaratibu wa kurekodi ushahidi wa watoto waliokuja kutoa ushahidi katika kesi hiyo na kwamba mahakama ya rufaa ikasema licha ya taratibu za kurekodi ushahidi wa watoto kukiukwa, mahakama yake iliona kuna ushahidi unaounga mkono na kwamba mahakama ya rufaa ilitumia ushahidi wa kuunga mkono ndiyo walioutumia kuwatia hatiani waomba rufaa kwa adhabu ya kifungo cha maisha.

“Waheshimiwa majaji kwasababu jopo lenu katika hukumu yake lilikiri wazi wazi  kuwa mahakama ya kisutu ilikosoea kurekodi ushahidi wa watoto wa dogo ambao walidai walitendewa vibaya na waomba rufaa(Nguza na Papii), na sheria za nchi zipo wazi kabisa zina sema endapo mahakama itabaini kuwa mahakama ya chini ilikiuka taratibu za kurekodi ushahidi wa watoto wa dogo, basi ushahidi ule wa watoto wa dogo uliotumika katika mahakama ya chini kuwatia hatiani washitakiwa, ushahidi huo wa watoto unafutwa na waomba rufaa au washitakiwa wanaachiriwa na pia maamuzi ya kesi mbalimbali yaliyokwisha kutolewa na mahakama hii;

“Nafahamu ni kazi ngumu sana  kuwashawishi nyie majaji kubadili uamuzi wenu mlioutoa katika hukumu ya Februali 2010 ambapo mliwatia hatiani wateja wangu, ila kwa uterezi huo wa kisheria niliouanisha unaonyesha katika hukumu yenu mlikubaliana na hoja yangu kuwa Mahakama ya Kisutu ilikosea kurekodi ushahidi watoto wadogo ,naamini mtatumia busara zenu na kufuata sheria inayosema wazi wazi kuwa endapo utaratibu wa kurekodi ushahidi wa mtoto utakiukwa basi ushahidi huo utafutwa na wateja wangu wataachiliwa huru, basi leo naiomba mahakama hii iwaachirie huru wateja wangu’ alidai Marando.

Kwa upande wao mawakili wa upande wa mjibu maombi (DPP),Angaza Mwipopo,Jackson Mlati, Imaculata Banzi na Joseph Pande waliomba mahakama hiyo itupilie mbali ombi hilo kwasababu sababu zote alizozitoa jana ni sababu ambazo alizitoa wakati wa usikilizwaji wa rufaa na ziliamliwa katika hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo Februali mwaka 2010.

Jackson alidai kama Marando anaona hukumu ya mwaka 2010 ilikuwa na dosari , basi angeomba mahakama hiyo impangie jopo la majaji watano wa kusikiliza ombi na siyo ombi lake kuja kusikilizwa na jopo la maji watatu wale wale waliotoa hukumu ile ambayo Marando anadai ina dosari.

“Hoja za Marando ni za kirufaa, na hoja zake zote anazotaka kuonyesha hukumu ya mahakama hii ina dosari zilishaamriwa na mahakama hii wakati ikisiliza rufaa ya wateja wake mwaka 2010 na tunamtaka Marando aelewe kuwa hakuna maamuzi yasiyonamwisho hivyo sisi tunaomba ombi la Marando linalotaka mahakama hii ifanyiwe mapitio hukumu yake halina msingi”alidai wakili  Jackson.

Aidha Jaji Kimaro alisema amesikiliza hoja za pande zote mbili akaamuru waomba rufaa warejeshwe gerezani na kwamba mahakama itatoa tarehe ya kutoa uamuzi wake kuhusu maombi hayo kwa pande zote mbili.

Aliyekuwa Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Addy Lyamuya, aliyekuwa jaji wa Mahakama Kuu Thomas Mihayo na jopo hilo la majaji wa tatu linaloundwa na Jaji Kimaro ,Massati na Mbarouk liliwatia hatiani kwa makosa ya kuwabaka watoto wadogo na likawahukumu kifungo cha maisha gerezani na hadi sasa wameishakaa gerezani kwa miaka kumi.

Mahakama ya Rufaa, Februali mwaka 2010 ,ilirekebisha hukumu ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Kisutu ambapo iliwaachiria huru waomba rufaa wawili katika kesi hiyo  ambao ni watoto wa Nguza Vicking, Nguza Mbangu na Francis Nguza waliachiwa huru, huku Viking na Papi Kocha wakiendelea kutumikia kifungo chao hadi sasa.

Hata hivyo jana mahakama hiyo ilifurika wanamuziki, mashabiki, ndugu wa washitakiwa na wengine walilazimika kukaa sakafuni ambao walikuja kusikiliza kesi hiyo.

No comments: