Saturday, October 19, 2013

IDADI YA WANAWAKE WABUNGE SADC IMEONGEZEKA

aNNE mAKINDA (KULIA) NA ANNA aBDALLAH
Gladness Mushi, Arusha

IDADI  ya wabunge wanawake  kwenye nchi wanachama wa mabunge ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC) imeongezeka ingawaje kwa Tanzania bado baadhi ya wanawake wanahofu kubwa ya kushiriki katika chaguzi mbalimbali kutokana na changamoto zilizopo kwenye jamii
Hayo yameelezwa  na Anna Makinda ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akiongea na vyombo vya habari mapema leo kuhusiana na mkutano  wa 34 wa jukwaa la Mabunge ya Nchi wanachama wa jumuiya  ya maendeleo kusini mwa Afrika unaotarajiwa kufunguliwa na Makamu wa Raisi dkt Gharib Bilali mapema jumapili ijayo.
Aidha Makinda alisema kuwa kuongezeka kwa wabunge wanawake katika mabunge ya SADC kunatokana na juhudi mablimbali ambazo zinafanywa na jumuiya hiyo hali ambayo nayo imefanya mabadiliko makubwa sana kwenye baadhi ya nchi.
Alisema kuwa pamoja na ongezeko kubwa la idadi ya wabunge wanawake katika jumuiya hiyo lakini kwa Tanzania bado baadhi ya wanawake wanauoga na hofu ya kushiriki katika chaguzi kuu jambo ambalo wanatakiwa kulipinga.
“hapa tunaona kuwa hii idadi ya wanawake ni kubwa katika jumuiya hii ya SADC lakini kupitia ongezeko hili ni muhimu sana kwa wanawake wa Tanzania nao wakahakikisha kuwa wanajitokeza kwenye chaguzi mbalimbali na kushiriki kwani uwezo wa wao kuwa wabunge upo na wasiogoope wala kujiwekea udhaifu wa changamoto”aliongeza Makinda
Wakati huo huo alidai kuwa wanawake wa Tanzania hawapaswi kukatishana tamaa wao kwa wao na badala yake wanatakiwa kupena moyo hasa pale wagombea wanawake wanapokutana na changamoto kubwa ambazo wakati mwingine zinasababisha baadhi yao kukimbia nafasi za uongozi
Awali akiongelea mkutano huo wa 34 alisema kuwa Nchi ya Tanzania imepewa nafasi ya kuwa mwenyeji mkuu wa mkutano huo ambao utaweza kuwashirikisha viongozi wa Mabunge mbalimbali kutoka SADC na hivyo kupitia mkutano huo wataweza lkujadili mambo mbalimbali
Makinda alisema kuwa mkutano huo utaaangalia vitu muhimu kwa nchi wananchama kama vile  vigezo vya kusimamia na kutathimini mwenendo wa chaguzi za nchi wanachama wa jumuiya hiyo.
“Kauli mbiu ya mkutano huu ni  vigezo vya kuendesha na kutathimini chaguzi kwa nchi za kusini  mwa Afrika hivyo basi hapa tutaweza kuangalia na kukagua hilo hivyo tutaweza kupata hata majibu ambayo yatasaidia nchi zetu”aliongeza Makinda.

No comments: