Tuesday, October 15, 2013

Mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro akipelekwa katika wodi baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi mbili jana alfajiri huko Kibamba, Dar es Salaam


Mwandishi na mtangazaji wa ITV, Ufoo Saro akiwa hospitali ya taifa ya muhimbili
 Wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wakimpeleka katika wodi mwandishi na mtangazaji wa ITV, Ufoo Saro aliyejeruhiwa kwa risasi na mpenzi wake.Picha na Emmanuel Herman na Mroki Mroki
----
Mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro amejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi mbili jana alfajiri huko Kibamba, Dar es Salaam.

Katika tukio hilo linalodaiwa kufanywa na mzazi mwenzake, Anthery Mushi ambaye alijiua baadaye, pia anadaiwa kumuua mama yake Ufoo, Anastazia Saro.Ufoo alipigwa risasi moja tumboni na kutokea kwenye mbavu na nyingine ilipita kifuani hadi kwenye ziwa lake la kulia na kutokea kwenye mkono wa kulia.
 
Baada ya tukio hilo, Ufoo alipelekwa katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alifanyiwa upasuaji.Kwa habari zaidi bofya na Endelea..........

No comments:

RAIS SAMIA ASHIRIKI NA KUTUNUKU TUZO ZA WASANII WA KOMEDI TANZANIA 2025

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki kama mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Wasa...