Monday, October 21, 2013

Simba ilivyotibua starehe za yanga kwa kulazimisha sare ya 3-3


 Kikosi cha kwanza lilichoanza cha Simba.
 Kikosi cha Yanga cha kwanza kilichoongoza mabao 3-0 hadi dk45 za kwanza.
Amisi Tambwe (kushoto) akimiliki mpira huku akisongwa na wachezaji wa Yanga Hamis Kiiza(kulia) na David Luhende.
 Mashabiki wa Yanga wakifurahi baada ya kuongoza mabao3-0 dk45 za kwanza dhidi ya Simba.
Mashabiki wa Simba ilikuwa zamu yao dk45 za mwisho kufurahi mabao 3 ya haraka baada ya kasi ya Vijana wao.
Kocha Mkuu wa Simba Abdallah Kibaden,(kushoto) na Msaidizi wake Jamhuri Kihwelo na Meneja Niko Nyagawa(katikati) hawaamini kilichotokea katika dk45 za kwanza.
 Kocha Mkuu wa Simba Abdallah Kibaden,Msaidizi wake Jamhuri Kihwelo(kulia) hali ngumu kabla ya mapumziko.
Wachezaji Gilbert Kaze (kulia) aliyefunga bao la 3 akiwaongoza wezake kushangilia kwenye Jukwaa la Yanga.
  Mchezaji Gilbert Kaze AKISUJUDI baada ya kuipatia timu yake bao la 3 na kufanya sare dhidi ya Yanga.
 Kocha Msaidizi Jamhuri Kihweloakinywa maji baada ya Vijana wake kufanya kweli.
 Mmoja wa mashabiki wa Simba alizimika baada ya Simba kukomboa mabao 2 kabla ya la 3
 Kocha Mkuu wa Simba Abdallah Kibaden akiwaangalia vijana wake (hawaonekani pichani) baada ya kuwachosha Wazee wa Yanga na kufuta uteja.
Mwamuzi Israel Nkongo akimuonesha kadi ya njano mchezaji Betram Mwombeki kwa madai ya kutumia nguvu. Pamoja hiyo Athuman Idd Chuji alitumia nguvu sana dhidi ya Ramadhan Singano Mess wa Simba akatolewa nje kwa maumivu lakini Nkongo alipeta rafu za Simba aliziona za Yanga hakuziona.
 Mashabiki wa Yanga waliongoza kwa kuzimia japo timu yao iliongoza dk 45 za mwanzo kulikuwa na jambo gani?.
 Mshabiki akibebwa na Msalaba Mwekundu.
 Mshabiki wa Yanga Bonge la Mama hoi je kulikuwa na nini?.
  Kocha Msaidizi Jamhuri Kihweloakinywa maji baada ya Vijana wake kufanya kweli.
 Mipira mitano ya Yanga ilifunikwa na kuwekewa Ulinzi mkali na mheshimiwa huyu katikati ya Uwanja wa Taifa kabla mchezo kuanza.
Umati wa Mashabiki,Wepenzi wakiwa nje ya Uwanja wa Taifa Dar es Salaam wakijiandaa kuingia Uwanjani kushuhudia mpambano wa Simba na Yanga. 
Baadhi ya watu walikamatwa kwa madai ya kuuza tiketi za mchezo wa Simba na Yanga. PICHA ZOTE ZA MROKI MROKI

No comments: