Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akisisitiza jambo kuhusu mgomo
uliopangwa kufanywa na wadau wa usafirishaji nchini wakati
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jana jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akifafanua sheria namba 30 ya
mwaka 1973 ya usalama barabarani iliyofanyiwa marekebisho mwaka
2001 inayohusu kiwango cha mwisho cha uzito wa magari, kulia ni
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam Kamishna
Suleiman Kova akifuatilia kwa makini.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam Kamishna Suleiman
Kova akieleza jinsi Jeshi la Polisi lilivyojipanga kulinda usalama ili
watumiaji wa barabara wasiweze kupata usumbufu huku akisisitiza
kuwa kabla ya Jeshi la polisi kuchukua hatua za kisheria ni vema vyombo
vinavyosimamia usafirishaji vikachukua hatuaKushoto ni Waziri wa Ujenzi
Dkt. John Magufuli.
Baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Ujenzi na Waandishi wa Habari
wakifuatilia kwa makini maelezo toka kwa Waziri wa Ujenzi Dkt.
John Magufuli.Picha Zote na Eliphace Marwa
Comments