Dar es Salaam – Mchezaji wa klabu ya Yanga, Pacome Zouzoua, amepata faraja ya kipekee baada ya kutembelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam.
Rais Samia alikuwa hospitalini hapo kwa ajili ya kumjulia hali Sheikh Rashid Hamad Othman, lakini alipojulishwa kuwa Pacome amelazwa katika chumba jirani akipatiwa matibabu kufuatia majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya JKT Tanzania, alitumia fursa hiyo kumtembelea na kumpa pole.
Hatua hiyo imeonesha moyo wa upendo na kujali kwa viongozi wakuu wa Taifa kwa wanamichezo, ikisisitiza nafasi muhimu ambayo michezo inaendelea kuwa nayo katika kuunganisha Watanzania.
Mashabiki wa soka nchini wanaendelea kumuombea Pacome apone haraka na kurejea uwanjani kuendelea kuonesha kipaji chake na kuiburudisha Yanga pamoja na wapenzi wa soka kwa ujumla.
Tunamtakia Pacome Zouzoua nafuu ya haraka na kurejea uwanjani akiwa imara zaidi. 💚⚽


No comments:
Post a Comment