Wednesday, October 09, 2013

Watuhimiwa wawili wa Uwizi,Mmoja akiwa na Kitambulisho cha Idara ya Usalama wa Taifa Wakamatwa kwenye Hoteli ya Picolo,Kawe jijini Dar es Salaam

 Mtuhumiwa wa Uwizi aliejitambulisha kwa jina la Juma Hamis huku akiwa na Kitambulisho cha Kazi cha Idara ya Usalama wa Taifa chenye jina la Kenedy Magige,akiwa amewekwa chini ya Ulinzi mara baada ya kunaswa Usiku huu kwenye Hoteli ya Picolo,Kawe jijini Dar es Salaam,
  Kava ya nje ya Kitambulisho hicho kinaonekana namna hii.
 Kitambulisho alichonashwa nacho Mtuhumiwa huyo kinaosomeka namna hii.
 Kitambulisho hicho kinavyoonekana kwa nyuma.
 Picha juu Mtuhumiwa wa Uwizi aliejitambulisha kwa jina la Juma Hamis huku akiwa na Kitambulisho cha Kazi cha Idara ya Usalama wa Taifa chenye jina la Kenedy Magige.
  Mtuhumiwa mwenza wa Tukio hilo la Wizi,aliejitambulisha kwa jina la Takula Manyenga mwenye umri wa Miaka 28,akidhibitiwa kwa kufungwa kamba mara baada ya kukamatwa Usiku huu kwenye Hoteli ya Picolo,Kawe jijini Dar es Salaam.
  Gari walilokuwa wakilitumia Watuhumiwa hao.
 Askari Polisi wakiendelea na Ukaguzi ndani ya Gari hilo,ambapo ndani ya Gari hilo kulikutwa na Simu zaidi ya kumi ambazo zilichukuliwa na Polisi hao.

 Wakipelekwa kwenye Gari la Polisi tayari kwa safari ya kwenda Kituoni
  Watuhumiwa wote wawili wakipakiwa ndani ya Gari la Polisi kutoka katika Kituo cha Kawe,Jijini Dar es Salaam.
Msafara wa kuelekea kituoni ukianza
---
Wu atwawili wanaotuhumiwa kuwa ni wezi a.k.a Wapigaji/Matapeli wamekamatwa Usiku huu kwenye hoteli ya Picolo, Kawe jijini Dar es Salaam.

Watu hao ambao wamekamatwa ni Bw. Takula Mayenga mkazi wa Mbezi Temboni na Bw. Juma Hamis ambaye ni mkazi wa Tabata wakiwa na nyaraka tofauti ikiwemo kitambulisho cha Idara ya Usalama wa Taifa, kadi za benki pamoja na simu zaidi ya kumi,wakiwa katika harakati za kumtapeli mwanadada mmoja aliejitambulisha kwa jina la Rebecca ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo cha Biashara cha CBE, Mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaa.

Akisimulia tukio dada huyo ambaye alipatwa na tukio hilo la kutapeliwa Ijumaa ya wiki iliyopita alisema kuwa, ilikuwa ni Ijumaa iliyopita wakiwa wamekaa katika fukwe wakipunga upepo ndipo alipokuja tapeli huyo na kukaa nao na baadae aliwawekea madawa ya kulevya na kuondoka na dada huyo kwenda kumtupa baharini.

JINSI YA MAJAMBAZI/MATAPELI HAO WALIVYOKAMATWA;



Baada ya kuwa wamefanya tukio Ijumaa ya wiki iliyopita la kumteka mwanadada na kumuibia vitu vyake vyote na kisha kumtelekeza katika fukwe za bahari beach, na wao kuondoka. Mwanadada huyo aliokolewa na ndugu zake na kukutwa akiwa salama ila keshaibiwa vitu vingi sana ikiwemo siku. Jukumu lililochukuliwa ni kwenda katika mtandao wa tigo na kurejesha simu kadi yake na baada ya hapo waliomba namba ya mwisho na kufanikiwa kupata namba ya huko tapeli. Wanadada hao huku wakishirikiana na familia kwa ujumla walichukua jukumu tena la kumpiga ile namba na kupokea kaka ambaye wao walisema wamekosea namba na walikuwa wakimtaka mtu mwingine.



Jambazi hilo lilipoona namba niya sauti ya mwanadada lilianza kumtongoza na kuomba miadi bila kujua lilikuwa mtegoni. Mtego uliiva zaidi baada ya jamaa kupewa miadi ya kukutana hoteli ya Piccolo na mwanadada aliyekuwa akiongea nae kwenye simu. Jamaa bila kujua anaingia katika mikono ya Polisi na wananchi wenye hasira kali alijongea mpaka hotelini pale na kukutana na mwanadada ambaye aliyejitambulisha kuwa ndiye waliyeongea nae kwenye simu.



Mtuhumiwa kwa ukarimu wake alimuagizia mgeni wake kinywaji na kuanza maongezi, ndipo mtuhumiwa huyo kuwekwa chini ya ulinzi na kutaka kukimbia huku mfukoni mwake akitoa kitambulisho cha Idara ya Usalama wa Taifa na kukitupa na kuokotwa na wananchi waliofika

No comments: