SHEREHE YA KUWAAGA RASMI, BALOZI CHABAKA KILUMANGA NA KAMISHNA MKUU WA UHAMIAJI, BWANA SYLVESTER AMBOKILE


 Kwenye picha ya pamoja na Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe (kulia), Mama Joyce Kallaghe (Kushoto), Wafanyakazi wa Ubalozi, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki waliofika kwenye sherehe hiyo ya kuwaaga rasmi.

Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, siku ya Ijumaa 18 Octoba 2013 uliwaaga rasmi maofisa wake wawili ambao wameteuliwa rasmi na Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. MHE. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kuiwakilisha nchi katika nafasi tofauti. Maofisa hao wa kwanza ni Mheshimiwa Balozi Chabaka Kilumanga, ambaye alikuwa Naibu Balozi katika Ubalozi huo wa Tanzania - London, ambaye hivi sasa ameteuliwa na Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano, Tanzania kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Comoro

Ofisa mwingine ambaye ameagwa rasmi katika sherehe hiyo fupi iliyofanyika Ubalozini hapo ni Bwana Syslevster Ambokile, ambaye nae pia ameteuliwa na Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete  kuwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, kabla ya kuteuliwa kwake Bwana S. Ambokile alikuwa msaidizi wa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Tanzania. 
 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe, akimkabidhi Zawadi za pongezi Balozi Chabaka Kilumanga, zawadi ambayo imetoka kwa Maofisa na Wafanyakazi wa Ubalozi huo katika sherehe fupi ya kuwaaga rasmi ambayo iliyofanyika hapo Ubalozini.
 Mheshimiwa Balozi Kallaghe, akimkabidhi Zawadi za pongezi, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Bwana Sylvester Ambokile
 Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Chabaka Kilumanga, akiongea na baadhi ya Wafanyakazi wa Ubalozi, katika sherehe fupi ya kuwaaga rasmi iliyofanyika siku ya Ijumaa tarehe 18 Octoba 2013.
Pichani, Maofisa wa Ubalozi, watoto wa maofisa hao, ndugu, jamaa na marafiki waliofika kushuhudia sherehe za kuwaaga rasmi, Mheshimiwa Balozi Kilumanga na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Bwana S. Ambokile.

Comments