MISS UNIVERSE TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA LEO

Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2013 Betty Boniface Omara amekabidhiwa bendera leo na waziri wa mali asili na utalii mheshimiwa Kagasheki.
Zoezi hili limefanyika katika ukumbi wa mkutano wa wizara hiyo tayari kwa safari yake ya kwenda kwenye mashindano ya Miss Universe yatakayofanyika Moscow nchini Urusi mapema mwezi Novemba.
Akimkabidhi bendera huku akimpongeza waziri Kagasheki pia amemtakia mafanikio mema huko aendako.
Betty pia aliwaahidi watanzania kuwa mbali na kurudi na ushindi lakini pia ataenda kuitangazia dunia kuacha kutumia nakshi(Mapambo) yanayotumia pembe za ndovu ili kumaliza tatizo la ujangili nchini.
Zoezi la kukabidhiwa bendera lilifanyika likishuhudiwa na Mkurugenzi wa Kitaifa Miss Universe Tanzania Maria Sarungi Tsehai.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania 2013 yamedhaminiwa na hifadhi ya Taifa Tanapa na Mrembo Betty Boniface ameshaanza kutangaza hifadhi hizi kwa njia mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi.

Comments