Semina ya mafunzo ya siku nne kwa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za wilaya na mikoa nchini kote, ambavyo ilianza jana mjini Dodoma kwa kufunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, leo imeendelea kupamba moto kwa mada mbalimbali, katika ukumbi wa sekreterieti ndani ya Jumba la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Pichani, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akitoa maneno ya utangulizi kabla ya mada kuanza kutolewa. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Zakiah Meghji na Katibu wa NEC, Itukadi na Uenezi Nape Nnauye.
Washiriki wakiwa kwenye semina hiyo leo asubuhi
Washiriki wakifuatilia mada kwenye semina hiyo asubuhi hii
Washiriki wakifuatilia mada
Washiriki wakifurahia mada motomoto
Washiriki kutoka Dar es Salaam, wakifuatilia kwa makini mada (kushoto) ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Abilah Mihewa
Nape akitoa angalizo kuboresha usikivu wa mada kwenye semina hiyo
Maofisa wa Chama kutoka Makao Makuu ya CCM wakiwa kwenye semina hiyo. (wacheki pande za kulia) Imetayarishwa na theNkoromo Blog
Comments