Wednesday, October 02, 2013

Sheikh Ponda Afikishwa Mahakamani Ombi lake latiwa shitaka moja kati ya matatu yanayomkabili Sheikh Ponda


  Ulinzi ukiwa umeimarishwa mahakamani leo wakati kesi hiyo ikiendelea katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro
 Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini Sheikh Issa Ponda akishuka kwenye basi la Magereza tayari Kuingia Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro ambapo Mahakama Ilikuwa inatoa Maamuzi kuhusu Kufutiwa shitaka moja kati ya matatu yanayomkabili Sheikh Ponda.Mahakama Imetupilia Mbali Ombi hilo na kesi itaendelea Kusikilizwa katika Mahamama hiyo. Kesi hiyo imeahiriswa Mpaka tarehe 7 November mwaka huu ambapo mahakama itaanza kusikiliza Mashahidi wa kesi hiyo. Sheikh Ponda Amerudiswa Rumande.
   Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini Sheikh Issa Ponda akiingia katika viwanja vya mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Morogoro.
  Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini Sheikh Ponda akiwa mahakamani akimsubiri Hakimu tayari kusikiliza Kesi yake katika Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Morogoro.
 Mke wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini sheikh Ponda akiwa mahakamani. Picha Zote na Habari na Audiface Jackson

No comments:

KIKWETE ATEULIWA KUWA MWAKILISHI WA NGAZI YA JUU WA MWENYEKITI WA KAMISHENI YA AU

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Mhe. Mahmoud Ali Youssouf, amemteua Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Ki...