Balozi wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani Zuriel Oduwole Alipokutana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete


 Balozi wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel  Oduwole (kushoto) akipokelewa na Msaidizi wa Rais katika masuala ya jamii Mwanahamisi   Kitogo  (kulia) kwenye ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA)  mara baada ya   kuitembelea ofisi hiyo  hivi karibuni jijini Dares Salaam.
 Mke wa Rais  Mama Salma Kikwete ( kulia) akisalimiana na  Balozi wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel  Oduwole (kushoto) kwenye ofisi za Taasisi ya Wanawake na  Maendeleo(WAMA)  mara baada  kuitembelea  ofisi hiyo hivi karibuni  jijini Dares Salaam.
 Mke wa Rais  Mama Salma Kikwete akimwonesha   tisheti yenye nembo ya   Taasisi ya Wanawake na  Maendeleo(WAMA)   Balozi wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel   mara  baada  kuitembelea ofisi hiyo   hivi karibuni   jijini Dares Salaam.
  Mke wa Rais  Mama Salma Kikwete akimvalisha  tisheti yenye nembo ya   Taasisi ya Wanawake na  Maendeleo(WAMA)   Balozi wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel  Oduwole ikiwa ni ishara ya kumteua kuwa balozi wa WAMA,  alipoitembelea ofisi hiyo hivi karibuni   jijini Dares Salaam. Kulia  ni  Mkurugenzi wa uboreshaji  afya – WAMA Dk. Sarah  Maongezi .
 Mke wa Rais  Mama Salma Kikwete akimwonesha   khanga iliyobuniwa na  Taasisi ya Wanawake na  Maendeleo(WAMA)   Balozi wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel yenye maandishi  ya ‘mtoto wa mwenzio ni mwanao mkinge na ukimwi’  kwenye ofisi za mara  baada  kuitembelea ofisi hiyo   jana jioni  jijini Dares Salaam.
 Mke wa Rais  Mama Salma   Kikwete akimuonyesha Balozi wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel  Oduwole kinyago kinachoonyesha umoja wa watanzania wakati balozi huo alipozitembelea ofisi za WAMA  hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais  Mama Salma Kikwete akisisitiza  jambo kwa   Balozi wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel  Oduwole,  kwenye ofisi za Taasisi ya Wanawake na  Maendeleo(WAMA)  mara  baada  kuitembelea  jana jioni  jijini Dares Salaam.
 Mke wa Rais  Mama Salma Kikwete ( kulia) akizungumza na  mama mzazi wa Balozi wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel  Oduwole, Partricia   Oduwole (kushoto) kwenye ofisi za Taasisi ya Wanawake na  Maendeleo(WAMA)  mara baada  kuitembelea  ofisi hiyo hivi karibuni jijini   jijini Dares Salaam. Aliyebebwa ni Ismachiah  mdogo wake na Zuriel.
Mke wa Rais  Mama Salma Kikwete ( kushoto ) akiwa na  Balozi wa kuwatetea watoto wa kike kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel  Oduwole,  kwenye ofisi za Taasisi ya Wanawake na  Maendeleo(WAMA)  mara  baada  kuitembelea  ofisi hiyo hivi karibuni  jijini Dares Salaam.Picha na Magreth Kinabo – Maelezo
----
 Na Magreth Kinabo-MAELEZO
MKE  wa  Rais Mama Salma Kikwete , ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya  Wanawake na Maendeleo (WAMA) amemtunuku  Balozi wa kuwatetea  watoto wa kike katika masuala ya elimu kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel  Oduwole kuwa  mwanachama (balozi) wa  heshima  wa  taasisi  hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Mama Kikwete mara baada ya Zuriel  kuitembelea ofisi  ya WAMA  iliyoko Ikulu jijini Dares Salaam na kufanya mazungumzo  kuhusu  shughuli  inazozifanya .

Mama Kikwete  alimwezea  Zuriel  jinsi taasisi yake inavyofanya  kazi  mbalimbali ikiwemo  ya kuhakikisha watoto  wa kike yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi wanapata elimu ili waweze kuajiriwa na kujiajiri  ikiwa ni hatua ya kuendeleza maisha yao ya baade na kutimiza ndoto zao.

Kwa mujibu wa  baba wa Zuriel,  Ademola Oduwole alisema mtoto  wake pia  amekuwa akihamasisha wasichana kubadili mtazamo wa  Bara la Afrika  kwa kuwa  huko Marekani watu hawalijuwi bara hilo na wanadhani  ni bara la njaa .  

“Amezindua mradi wa dreaming up dreaming big’ lengo lake ni kuwahamasisha watoto wa kike kuwa na ndoto za kuendelea,” alisema  Oduwole.

 Oduwole   aliongeza kuwa  Zuriel anapenda kuhamasisha kuhusu suala la elimu kwa kuwa ndio njia ya kufikia malengo ya milinea.

 Alisema Zuriel   ameshatembelea nchi  Nigeria,Malawi na Tanzania ambapo alifika Shule ya Msingi ya Olympio na Shule ya Sekondari ya Jangwani na  Shule ya Sekondari  ya wasichana  ya  Marian.Pia ameshafanya mahojiano na marais wanane wa Afrika , ambao ni   wa Tanzania, Mauritius, Kenya,Nigeria, Cape Verde,Sudan ya Kusini na Liberia.

Kwa upande wake Mama   Kikwete alifurahishwa   na juhudi za Zuriel na kumtaka kuendelea kufanya mambo makubwa   katika  kutimiza ndoto zake.

Naye Zuriel   alishukuru kwa ukarimu alioupata kwa Watanzania na ameaihidi kuitangaza Tanzania na WAMA   mahali popote  duniani.

Zuriel alikuwepo nchini kwa kipindi cha siku sita kuanzia jumapili iliyopita  akiwa na  wazazi wake na wadogo zake Azaliah Arielle na Ismachiah,  amerejea Marekani   mwishoni mwa wiki hii.

Comments