Wateja wa Vodacom sasa kutimka na Bodaboda



 Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa
---
Dar es Salaam 2013 … Katika kuhakikisha inaendelea kuthamini na kutambua mchango wa wateja wake kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua promosheni ya kuwawezesha wateja wake kujishindia pikipiki maarufu kama Bodaboda pamoja na fedha taslimu kila siku.

Ni takribani miezi sita sasa tangu kampuni hiyo iboreshe maisha ya maelfu ya Watanzania kwa kujishindia fedha taslim kupitia Promosheni ya MAHELA ambapo Valerian Mugisha ambaye alikuwa mwanafunzi wa chuo cha uwalimu Kasulu Kigoma aliibuka kidedea kwa kujinyakulia Shilingi milioni 100 ambazo kwa sasa zimebadilisha kabisa maisha yake.

Promosheni hiyo itakayo chezeshwa kwa siku 100 imepewa jina la Timka na Bodaboda itashuhudia pikipiki 430 zikitolewa kwa Watanzania Huku kila siku pikipiki tano zikitolewa na mshindi mwingine mmoja kuibuka na shilingi milioni 1 na  kila wiki kwa wiki 14 mshindi mwingine ataibuka na shilingi milioni 5.

Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Kelvin Twissa amesema Vodacom imeendelea kuwa chaguo la kwanza kwa mamilioni ya Watanzania, hivyo ni vyema kurudisha kile wanachokipata kwa wananchi wenyewe ili nao waweze kuboresha maisha yao.

“Vodacom imekuwa ikitoa misaada mingi ya kijamii kwa Watanzania na wote tunalitambua hilo, Kwa upande wetu sisi wa Masoko bado tunaendelea kuboresha maisha ya Watanzania kwa namna ya kipekee,” alisema Twissa na Kuongeza.

“Wote tunajua kuwa sasa Bodaboda ndio habari ya mjini, kulingana na mfumo wa maisha ya sasa tumetambua kuwa usafiri umeendelea kuwa changamoto kwa Watanzania wengi, na ili kutatua tatizo hili kwa Watanzania tumeamua kuwapatia usafiri rahisi wa kuwatoa sehemu moja kwenda nyingine,” alisema Twissa.

“Tumedhamiria kuendelea kuimarisha maisha ya Watanzania kwa njia mbalimbali katika Promosheni hii, Mshindi wa jumla atajinyakulia milioni 30 na katika muda wote wa Promosheni hii Watu watajinyakulia bodaboda tano kila siku na Shilingi milioni 1. Nawasihi wateja wa Vodacom na watanzania wengine kwa ujumla ambao hawajajiunga na Mtandao wetu wajiunge kwani huu ni wakati mwafaka kabisa nakuweza kushiriki kucheza kwa kutuma SMS kwa kuandika neno PROMO kwenda namba 15544 mara nyingi kadri wawezavyo na wataingia moja kwa moja kwenye droo hii.”

Mwisho…..

Comments