Thursday, September 10, 2015

MWIGULU AZINDUA KAMPENI ZA UBUNGE WILAYA YA ITILIMA

Mwigulu Nchemba akiwa amaembatana na Mgombea Ubunge Jimbo la Bariadi Mashariki wilaya mpya ya Itilima Ndg.Njalu wakiwasili kwenye viwanja vya Laini kwaajili ya Mkutano wa kampeni wa Chama cha Mapinduzi wilayani humo.
Wananchi wakisukumana kuhakikisha kila mmoja anashikana mkono na Comrade Mwigulu Nchemba ambaye ni Mbunge mtarajiwa wa Jimbo la Iramba.
Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombe Ubunge wilaya ya Itilima Ndg.Njalu mapema hii leo wakati wa mkutano wa kampeni.
Mwigulu NChemba akizungumzia uchapa kazi wa Ndg.Njalu ambaye mbali ya kuwa ni Mbunge Mtarajiwa wa Jimbo la Bariadi Mashariki,Pia ni MNEC wa chama cha Mapinduzi kutoka jimbo  hilo.
Njalu anasifika kwa kushiriki kazi za Maendeleo ya WIlaya ya Itilima ikiwamo ujenzi wa shule,Maabara na Vituo vya Afya mbalimbali ndani ya wilaya hiyo.
Ndug.Njalu ambaye ni Mbunge mtarajiwa wa Itilima akiahidi kwa Wananchi wake kuwa atakuwa MCHAKA KAZI ndani ya nje ya Itilima,ameahidi kuhakikisha anaboresha Elimu na AFya,Barabara na Upatikanaji wa marisho ya Wafugaji.
Hisia za Wananchi wa  Itilima Mkoa wa Simiyu kwa Mbunge wao Mtarajiwa.
Wananchi wakishangilia Ufunguzi wa Kampeni wa Wilaya ya Itilima uliofanyika hii leo.
Sehemu ya Mamia ya Wananchi wa Itilima wakishangilia Uteuzi wa Ndg,Njau kuwa mgombea Ubunge jimbo lao ambalo kwa muda mrefu limekuwa likishikiriwa na Mbunge wa UDP Mh.Cheyo.
Mwigulu Nchemba na Mgombea Ubunge wa wilaya ya Itimia Ndg.Njalu wakiondoka kwenye viwanja wa Laini mara baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni kuelekea kilele chake cha tar.25/10/2015.
Picha na Sanga Festo Jr

No comments: