Thursday, September 17, 2015

NDOA YA UKAWA VUNJO YAVUNJIKA…MADIWANI CHADEMA WAAPA KUMMALIZA MBATIA

X1

Na Richard Makore.
‘NDOA’ ya vyama viwili vilivyopo chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Chadema na NCCR-Mageuzi ipo hatarini kasambaratika katika jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro baada ya kila kimoja kusimamisha wagombea udiwani katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Kufuatia hatua hiyo, wagombea wa udiwani wa Chadema wametangaza kutomuunga mkono, mgombea wa ubunge katika jimbo hilo, James Mbatia na wapo tayari kuwaelekeza wanachama wao kupigia kura chama tofauti na kwa mgombea mwingine.
Wagombea hao wamesema wamegundua mpango mkakati wa NCCR MAGEUZI wa kukifuta chama cha CHADEMA jimboni humo kwa kutumia mbinu chafu za kuwanunua baadhi ya wagombea na viongozi wa chadema vunjo.
Chini ya makubaliano ya Ukawa, vyama hivyo vimekubaliana kusimamisha mgombea mmoja kwa kila kata, jimbo pamoja na ngazi ya urais.
Vyama vinavyounda Ukawa ni NLD, NCCR-Mageuzi, Chadema na Cuf ambavyo kwa pamoja vimekubaliana kusimamisha mgombea mmoja na wengine kumuunga mkono kwa kumpigia kampeni.
X2
Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye Hotel ya Keys mjini moshi madiwani hao na uongozi wa Chadema Vunjo wamefanya vikao vingi na wenzao wa NCCR-Mageuzi ili kuachiana baadhi ya kata lakini imeshindikana na badala yake kumekuwa na mkakati wa kukidhoofisha chama hicho jimbo la vunjo.
Alisema baada ya kushindikiana kwa sasa watafanya kampeni zao wenyewe na kwamba suala la Ukawa ikiwamo kumnadi Mbati majukwaani nan je ya majukwaa wanaliweka pembeni na itambulike kwamba hakuna maridhiano yoyote baina ya vyama hivyo jimbo la Vunjo.
walifafanua kuwa NCCR-Mageuzi kinataka kuwaachia Chadema kata nne ili wao wachukue kata 12  pamoja na nafasi ya ubunge hatua ambayo walisema hawakubaliani nalo kwa kuwa ukweli chama chenye nguvu kwenye jimbo la Vunjo ni chadema.
unnamed
 kwa upande wake Katibu wa Chadema jimbo la Vunjo, Emanuel Mlaki alikiri kuwapo mgogoro huo ambao mpaka sasa haujapatiwa ufumbuzi na leo wamelazimika kufikisha maazimio yao kwa mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro bwana Filemon Ndesamburo ambapo nae amebariki maazimio hayo.
Mlaki alisema Chadema na NCCR-Mageuzi walikubaliana kumsimamisha, James Mbatia kugombea ubunge jimbo la Vunjo, lakini ameshangaa kuona ngazi ya udiwani kumejitokeza utata.
Alisema NCCR-Mageuzi imeamua kusimamisha wagombea udiwani katika kata zote 16 za jimbo hilo na Chadema nao wameweka wagombea katika kata 14.
Kwa mujibu wa Mlaki, Chadema kinataka kiachiwe kata 10 ili kisimamishe wagombea udiwani, lakini NCCR-Mageuzi kimekataa ombi hilo huku kikisitiza kuwaachie kata tatu.
“Tumeendelea kutafuta maridhiano kwa muda mrefu, lakini naona hakuna malengo ya Ukawa ya kupata ushindi hayatafanikiwa,” alisema
Alikiri kwamba kuwapo mgogoro huo kutawaathiri Chadema kwa kiasi kikubwa na kwamba kunaweza kutoa nafasi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia mgombea wake Bwana Innocent Melleck Shirima kushinda kirahisi.
Post a Comment