Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abass Kandoro wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Songwe mkoani humo jana Sept 20,2015 kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu mteule wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini Mchungaji Kenan Salim Pannja zilizofanyika katika Uwanja wa michezo Tukuyu Mkoani Mbeya.
Wasanii wa kwaya ya Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo kuu la kusini wakitoa burudani wakati wa sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu Kenen Salim Panja iliyofanyika jana Sept 20,2015 katika Uwanja wa michezo Tukuyu Mkoani Mbeya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na kumpongeza Askofu mteule wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini Mchungaji Kenan Salim Panja wakati wa sherehe ya kuwekwa wakfu iliyofanyika jana Sept 20,2015 katika Uwanja wa michezo Tukuyu Mkoani Mbeya.
Comments