Thursday, September 10, 2015

NITABORESHA MASLAHI YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA-MAGUFULI

Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli ukiwasilia katika mkutano wa hadhara wa kampeni, Korogwe vijijini.
MGOMBEA urais kwa teketi ya CCM, Dk.John Magufuli akifafanua jambo kwa
msisitizo huku akibainisha kuwa iwapo atachaguliwa kwenye uchaguzi mkuu
mwaka huu, basi Serikali yake itahakikisha inaboresha maslahi ya
watumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini kutokana na kutambua
mchango wao katika kulinda amani ya nchi yetu. 
Dkt Magufuli alisema kuwa anataka kuona watumishi wa jeshi hilo wanakuwa na mishahara

mizuri na hiyo itawezesha kufanya kazi ya ulinzi na usalama wa nchi kwa
ufanisi zaidi huku akitumia nafasi hiyo kuomba Watanzania kudumisha
amani ya nchi kwani ikipotea hakutakuwa na maendeleo ya aina yoyote.Dk.Magufuli alitoa kauli hiyo jana katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Korogwe,
Mkinga na Lushoto ikiwa ni sehemu ya mikutano ya kuomba ridhaa ya
kuchaguliwa kuwa rais ambapo alisema anatambua kazi nzuri inayofanywa na
vyombo vya ulinzi na usalama na kuongeza kuwa serikali yake itaboresha
maslahi ya wanajeshi wa majeshi yote Nchini .
PICHA NA MICHUZI JR-LUSHOTO,TANGA
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Bumbuli
wakiwaaga wananchi wa Bumbuli waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa
kampeni uliofanyika mjini humo jioni ya jana.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa
Lushoto kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jitegemee.
  Lushoto ikiwa imefurika watu tayari kumsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasili kwenye mkutano wa
hadhara  katika uwanja wa Togotwe-Mponde wilayani Bumbuli kuwahutubia
wananchi na kuwaomba ridhaa ya kuwaongoza katika awamu ya tano.

  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa ubunge
jimbo la Bumbuli Ndugu January Makamba kwenye mkutano wa kampeni
uliofanyika kwenye viwanja vya Togotwe.
Mgombea Ubunge jimbo la Bumbuli Ndugu January Makamba akisisitiza jambo kwa
Wananchi wake katika jimbo la Bumbuli jioni ya jana kwenye mkutano wa
kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Togotwe.
 Wakazi wa Jimbo la Bumbuli wakifuatilia kwa makini mkutano wa Mgombea wa Urais
kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya 
jana.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa
kata ya Magoma wakati akiwa njiani kuelekea Korogwe mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa
Mashewa wilayani Korogwe kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo
aliwaambia wananchi hao kuwa serikali yake itakuwa ya kuchapa kazi kwa
maendeleo ya wananchi na nchi kwa jumla.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM pamoja na kumnadi mgombea Ubunge wa
Jimbo la Korogwe Vijijini Ndugu Stephen Ngonyani kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kwamazandu, Korogwe Vijijini.
Bangozzzz
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea ubunge
wa Jimbo la Korogwe mjini  Mary Chatanda Ilani ya uchaguzi ya CCM
kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya chuo cha ualimu Korogwe.
Mwenyekiti wa Wazazi CCM Taifa,Ndugu Bulembo akimkaribisha mgombea Urais wa CCM
Dkt John Pombe Magufuli kuwahutubia wananchi katika uwanja wa Togotwe-Mponde wilayani humo.
Wakazi wa Bumbuli waliojitokeza kwa wingi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa kampeni wa CCM jioni ya jana,
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa
Bumbuli kwenye viwanja vya Togotwe ambapo aliwaahidi kuwajengea barabara ya lami pamoja na kufuatilia suala la kiwanda cha Chai cha Mponde.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa
Bumbuli kwenye viwanja vya Togotwe ambapo aliwaahidi kuwajengea barabara
ya lami pamoja na kufuatilia suala la kiwanda cha Chai cha Mponde.
Wananchi wakifuatilia mkutano.
  Mgombea Ubunge jimbo la Bumbuli Mhe. January Makamba akifafanua jambo mbele ya umati wa wananchi  wa
Jimbo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya
Togotwe.
Wananchi wa Lushoto mjini wakishangilia jambo mara baada ya kumsikia Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia .
Post a Comment