Wednesday, September 23, 2015

BI. SAMIA SULUHU AMNADI DK. MAGUFULI WILAYA ZA KORONGWE NA LUSHOTO

Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana mjini Korogwe, Mkoa wa Tanga.
Mgombea mwenza nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wasanii na wananchi wengine alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi jana  Mjini Korogwe ambapo alifanya mkutano wa kampeni.
Mgombea mwenza nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwapokea baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na CCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana Korogwe. Jumla ya wanachama 25 walijiunga na CCM katika mkutano huo.
Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana mjini Korogwe, Mkoa wa Tanga.
Baadhi ya wasanii waigizaji, Wema Sepetu (kulia) na Bibi Mwenda wakizungumza na WanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza kuwashawishi waichague CCM kutokana na mazuri mengi iliyowafanyia wasanii.
Mgombea mwenza nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimtambulisha na kumuombea kura mgombea ubunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba (katikati) katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea mwenza uliofanyika Lushoto Jimbo la Mlalo. Kulia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Lushoto, Shaban Shekilindi.
Mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Mjini, Mary Pius Chatanda akizungumza na wanaCCM na wananchi wa jimbo hilo walipojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza jana viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi.

Mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Mjini, Mary Pius Chatanda akizungumza na wanaCCM na wananchi wa jimbo hilo walipojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza jana viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi kunadi sera za CCM, huku mgongoni akiwa amebandika kipeperushi cha mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Profesa 'Maji Marefu' akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea mwenza uliofanyika Korogwe Mjini jana.
Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana mjini Korogwe, Mkoa wa Tanga.

Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Kwagunda, Salehe Abdullah (kushoto) akizungumza mara baada ya kujiunga na CCM jana kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza na kukikimbia chama chake cha CHADEMA.
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanaCCM na wananchi wa jimbo la Korongwe Mjini walipojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea huyo jana kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi.
Baadhi ya wananchi wakiwa wamemsimamisha njiani mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan eneo la Mombo ili asikilize kilio na changamoto zao kabla ya kuendelea na safari kwenda kuhutubia mkutano wa kampeni Wilaya ya Lushoto.

Sehemu ya wananchi  na wanaCCM wakiwa wamemsimamisha njiani mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan eneo la Soko la Soni Lushoto ili asikilize kilio na changamoto zao hasa akinamama kabla ya kuendelea na safari kwenda kuhutubia mkutano wa kampeni Wilaya ya Lushoto.

Post a Comment