Saturday, September 26, 2015

LOWASSA NDANI YA MJI WA MERERANI, SIMANJIRO MKOANI MANYARA

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Mererani, katika Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye uwanja wa Machinjioni, Simanjiro Mkoani Manyara.Sehemu ya Wananchi wa Mji wa Mererani, Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara wakionyesha furaha yao mbele ya Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati akiwahutubia katika Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye uwanja wa Machinjioni, Mererani.
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akivishwa vazi maalum la jamii ya watu wa Kimasai, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye uwanja wa Machinjioni, Mji wa Mererani, Simanjiro Mkoani Manyara.
Meneja wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, John Mrema akizungumza na Wananchi wa Mji wa Mererani, Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara. 
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akipokea kadi za wanachama wa CCM walioamua kurudisha kadi na kujiunga na UKAWA, wakati wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye uwanja wa Machinjioni, Mji wa Mererani, Simanjiro Mkoani Manyara.
Post a Comment