Saturday, September 26, 2015

MAMA SAMIA APIGA KAMPENI MOROGORO

Msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan ukiwasili mkoani Morogoro jana Septemba 25, 2015 ukitokea mkoani Dodoma.Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, MamaSamia Suluhu Hassan akimsalimia Katibu wa CCM mkoa wa Morgoro Rojas Rumuli wakati wa mapokezi yake, alipowasili mkoani Morogoro kufanya mikutano ya kameni katika mkoa huo jana.Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimsalimia mgombea Ubunge Jimbo la  Gairo, Ahmed Shabby wakati alipowasili mkoani Morogoro, kufanya mikutano ya kampeni mkoani humo.Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwapungua mkono wananchi waliofika kumlaki alipowasili mkoani Morogoro jana. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa na wapili ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro, Inocen KarogeresiMgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Gairo A, kuhutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Gairo mkoani Morogoro.Baadhi ya wananchi wakiwa na mabango kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika jimbo la Gairo jana.Katibu wa CCM, mkoa wa Morogoro, Rojas Romuli akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika viwanja vya shule ya msingi Gairo A katika jimbo la Gairo mkoani MorogoroMgombea Ubunge jimbo la Gairo Sadik Ahmed Shabiby akihutubia wananchi atika mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofanyika jana katika jimbo hio mkoani Morogoro.Umati wa wananchi ukiwa umefurika kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Gairo A, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Gairo mkoani Morogoro.Mwananchi akionyesha bango la kumfagilia Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika jimbo la Gairo mkoani MorogoroMbunge wa Afrika Mashariki, Angela Kizigha akimvalisha kanga za CCM, Bibi Fatuma Farijala, baada ya kuona mavazi yake yamechakaa, akiwa mmoja wa wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika katika jimbo la Gairo mkoani Morogoro janaWananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassa alipohutubia mkuano wa kampeni jana katika jimbo la gairo mkoani Morogoro.
Post a Comment