Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi kwenye uwanja wa Samora Manispaa ya Iringa wakati alipokuwa akiwaomba kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
Dk. Magufuli amesema “Nipeni kura za ndiyo bila kubagua vyama vyenu kwa kuwa nitakuwa rais wa Watanzania wote wakati nikitekeleza majukumu ya kuwatumikia watanzania katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Hata wale wa CHADEMA huwa mnasema (Peoples Power) mpeni Magufuli hiyo Power ili awe rais wa Watanzania wote” .
Dk. John Pombe Magufuli akizungumza zaidi na wananchi wa Manispaa hiyo amesema Rais Jakaya Kikwete amefanya kazi kubwa katika kujenga mahusiano ya Kidiplomasia na mataifa mbalimbali ndiyo maana Tanzania ina mahusiano mazuri na nchi nyingi duniani zikiwemo nchi jirani, Amesema kwamba mara atakapochaguliwa na kuwa kiongozi wa Tanzania atahakikisha anadumisha mahusiano hayo na kuifanya Tanzania kupiga hatua katika maendeleo ya Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa
Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa leo
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli wa tatu kutoka kulia, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Abdallah Bulembo na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwa pamoja na wasanii wa Bongo Movie wakinyanyua mikono yao juu kama ishara ya Umoja ni Ushindi katika mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika mjini Iringa leo hii
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli wa tatu kutoka kulia, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kulia na wasanii wa Bongo Movie wakicheza muziki wakati wa mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza jambo huku wasanii wa Bongo Movie wakisikiliza wakati wakiwa jukwaani.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya wasanii wa Bongo Movie Mike, Rich Richie na Dude wakipiga Push Ups huku Mwimbaji Stara Thomas akiwahesabia.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimpigia debe mgombea ubunge wa jimbo la Iringa mjini Ndugu Fredrick Mwakalebela na wabunge wa viti maalum wa mkoa huo.
Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
Baadhi ya vijana wakiwa wamejichora rangi zinazowakilisha Chama cha Mapinduzi CCM wakiwa katika mkutano huo.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi ilani ya Uchaguzi mgombea ubunge wa jimbo la Iringa mjini Ndugu Fredrick Mwakalebela.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli hayupo pichani akiwanadi madiwani wa Manispaaa ya Iringa.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwapigia debe baadhi ya wagombea ubunge wa viti maalum mkoa wa Iringa, kulia ni Fredrick Mwakalebela.
Mgombea Ubunge jimbo la Iringa mjini Ndugu Fredrick Mwakalebela akiomba kura kwa wananchi katika mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.
Msanii wa Bongo Movie Jacob Steven akizungumza na wananchi katika mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akihutubia katika mkutano huo kwenye uwanja wa Samora na kumpigia debe Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea Ubunge jimbo la Isimani Mh. William Lukuvi akimpigia debe Dk. John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akiruka juu juu kuashiria ukakamavu wakati alipokuwa akimuombea kura mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akicheza muziki na Mgombea Ubunge jimbo la Iringa mjini Ndugu Fredrick Mwakalebela kabla ya Dk John Pombe Magufuli kuhutubia.
Katibu wa CCM mkoa wa Iringa akizungumza jambo na Kamanda wa vijana mkoa wa Iringa Bw Salim Asas Abri huku Nape Nnauye akifurahia.
Bw Salim Asas Abri Kamanda wa vijana mkoa wa Iringa akiteta jambo na Mh. William Lukuvi.
Mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini Ndugu Fredrick Mwakalebela akicheza muziki na baadhi ya waliokuwa wagembea ubunge wa jimbo hilo ndani ya Chama wa tatu kutoka kulia ni Balozi Mahiga.
Mh Temba na Chege wakifanya vitu vyao jukwaani.
Mwana FA aka Binamu akighani jukwaani.
Baadhi ya wana CCM wakishangilia wakati Dk. John Pombe Magufuli hayupo pichani alipokuwa akihutubia mjini Iringa leo.
Kundi la TOT nalo likaburudisha kwa nyimbo zake za hamasa.
Mgombea ubunge wa jimbo la Kilolo Mh. Venance Mwamoto akiwaomba kura wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika Ilula.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba ya Dk. John Pombe Magufuli.
Mcheza ngoma huyu alitoa mpya kwa kuweka kinu tumboni mwake na wenzake wakaendelea kutwanga unga wa muhogo.
Wakifurahia vipipirushi vyenye picha na Dk. John Pombe Magufuli huku wakisikiliza sera.
Comments